Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Philemon Mbowe ndiyo Freeman Aikaeli Mbowe?
Sleep Way ndiyo Slip Way ?
How Come?
Mmiliki Yatch Club? pale Yatch si ni club ya members kama ilivyo Saigon ya Kariakoo Dar es Salaam. Na je Makonda anajua wanachama wa Yatch club wana- influence kubwa hapa mjini DSm ktk kila sekta, je amejiridhisha kuwa taarifa kwa umma haiwezi kuja kumpatia tabu kisheria RC Makonda?
.....
 
kinondoni nzima imezima kuhusu mbowe jamaa anapendwa sana kama anasingiziwa dhambi kubwa sana
 
Apewe orodha iliyotoka China magerezani ya Watanzania waliokuwa wanangojea kunyongwa!!
Atwambie aliye watuma, quote. 2013 Ubarozi wa Tanzania China!!
 
Tulijua, serikali hii yenye kuwatafutia visa na namna ya kuvuruga vyama vya upinzani, haikosi safari hii wanataka kuivuruga chadema kwa kisingizio cha madawa ya kulevya. Hivi mbowe angekuwa anauza madawa ya kulevya, angeshimdwa kulipa madeni yake? Vipi yule mtoto was raisi aliyekutwa na madawa China, yupo kwenye orodha.
 
mwana una akili sana unastahili kuitwa great thinker sio hawa wanafiki kina pasco wanaosifia eti vita ya madawa ya kulevya wakati wenye akili tunaona mchezo unaofanyika uko vipi na utaisha vipi fuatilia comments utaona jinsi gani watanzania wengi ni wajinga na wapumbavu kupitiliza.
 
Huwa nasikiaga wanasema mwito, samasi nk, hivi vinaweza kufanyika kwa kupigiwa simu au kusema redioni!?
 
Wanaolengwa kudanganywa kwa huu usanii ni wajinga tuu.tulionauwezo wakupambanua mambo awawezi kutudanganya kitoto namna hii.
 
Kuna kosa kubwa sana linafanyika kwenye hii issue ya madawa.

Kwanza, Hawa watuhumiwa kwanini wanatajwa kabla hawajatiwa nguvuni?

Pili, inakuaje unamtuhumu mtu kwa issue nzito hivi halafu badala ya kumkamata unampa muda mrefu hivi about 48 hrs kuripoti polisi? Is this how to deal with drugs?

Kweli Ma-Don wa Drugs ambao hata kwa majina huwajui vizuri unawapa 48 hrs uraiani?

Naunga mkono mapambano dhidi ya Unga, lakini naona kuna something fishy which is going on..!

Isije ikawa lengo ni kuchafuana tu, Mlianza vizuri tukawaunga mkono, lakini naona tayari mmeanza kuingiza siasa zenu!
 
Kwa sababu katajwa Malaika wako Mbowe.?
Hao vijana wa ufipa wamechachanhanyikiwa baada ya DJ kutajwa...walisema serikali ina majina ya vigogo inaogopa kuwataja...Mbowe kaonekama ufipa hakukaliki
 
Acha uzuzu wewe!
Mbowe ni mmiliki wa Billicanas& Cassino na kwenye mahoteli makubwa matumizi ya madawa yapo juu so hata kama hafanyi yeye kama hotel yake imeorodheshwa basi atatoa ushirikiano kwa kamanda Sirro
Be quiet.
he!mbona umejipa ukiranja humu JF,unapata wapi mamlaka ya kumwambia mtu Be quite?
 
Hii sinema bana. Vita gani unatangaza mbinu zako kwa mpinzani? Vita ya madawa ya kulevya, halafu watuhumiwa wanapewa muda na uhuru wa kujisalimisha polisi kwa mahojiano; hapo hapo tunaambiwa utafuata msako nyumba hadi nyumba. Yaani Makonda na wenzie wanataka kutuaminisha kuwa hao jamaa waliotajwa ni wapumbavu kiasi cha kushindwa kutumia muda waliopewa kujipanga dhidi ya tuhuma hizi na uchunguzi? Kwamba tuamini hawa jamaa watakuwa convicted kwa maneno ya mateja?

Makonda pia kama kiongozi wa uma, anastahili kujieleza na kuchunguzwa tuhuma dhidi yake, kuhusu 'utajiri wake wa ghafla'. Haijalishi tuhuma hizo kazitoa nani, wala dhumuni lake; ni tuhuma za msingi, na zifanyiwe uchunguzi wa kina. Too bad sioni hili likifanyika, given ana kinga ya mkuu.

Anyway, faida pekee ya hii sinema ni kuwa tutasikia mengi kuhusu wengi. Hao jamaa waliotajwa, lazima watatafuta kulipa kisasi kwa kuchafuliwa. Pengine kuna watakaofuata mifano ya Nicky Barnes na Frank Lucas.

Binafsi naamini kama hii ni vita, siyo dhidi ya madawa. Kuna mchezo tu unafanyika hapa. Labda muda utatuambia.
 
Mkubwa serikali ipo...Unadhani kwa vile katajwa Mbowe atakuambia? Atapitia wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…