Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Naomba na mabaharia wachunguzwe mana inasemekana wao ndio wanaingiza madawa .mana madawa yanaingia nchin kwa meli.na wao wanauza pia ndani na nje ya nchi.makonda ebu fatilia na hao watu kwa ukaribu zaid
 
Nadhani baada ya kumaliza kazi tutampa ubalozi marekani au france
 
Huo ni Mwandiko Wa Rais.....kwa anae juwa mwandiko wake.
 
Makonda kawa sahau wengine Wa chama chake ambao waliwahi kukamatwa china

Sent from my Infinix-X552 using JamiiForums mobile app
Sio hao tu wakina Ghraib na Salah wapo na yeye anajua wapo wapi ila anawalinda. Hawa ndiyo nawajua vizr ni wauza ngada wa kimataifa na ndiyo wafadhili wake
 
hapa

mi bado sielewi..kumtaja mtu bila ushahidi ni a waste of time. kwanza utamfanya awe makini zaidi ili usimkamate..next kama unajua anafanya hiyo biashara kwa nini usimtegee mtego ukamkamata na ushahidi umtie jela..somthing is hangingi there
SIASA Au ...........................................
yaani kumtaja mtu hadharani kisa kuna majirani wanakunyoshea vidole, wakati Tanzania ya leo ukifanikiwa tu kwa kuchachalika kwako mtaani utasikia MADAWA, akili ndipo ilipolalia.
 
Unaweza kuta huyu jamaa anatumika kama cover up ili jamaa wapitishe makontena yao bandarini...maana attention yote ipo kitaaa...bandari ipo wazi....
 
Utawala unaojidai unatetea wananchi unafiki tu
Hivi ni utawala gani kucha kutwa kupambana na wapinzani tu?
Nitoe mfano wa mbowe
Wamemuandana na club bilicanas wakati wapo vigogo kibao wanamiliki club kama hizo na wana madeni
Wameamua kumfata mpaka machame hotel yake wanataka kuiuza kimabavu
Wamemfata mpaka nyumbani kwake kwenye greenhouse yake wamempiga marufuku kule machame ni wawekezaji wangapi wamejenga kwenye mto pale mto uwau amuoni, weruweru jee kule mto namwi wawekezaji wamefyeka.misitu yote mtoni na kujenga green house za maua kwenye mito
Hawa wanaandamwa
tundu lissu
lema
zitto
madiwani wa chadema
Yaani huu utawala umejaa unafiki wa kuvaa ngozi ya kondoo kumbe chui
Hii serikali na utawala wa kidteta ni wa kupingwa na kila mtu
Vijana wamenyimwa mikopo na sera za kimabavu na kikoloni za serikali ya ccm
Mnajidai mnatetea na waombewe
Unawaambia wananchi kuwa wewe sio mpishi halafu unataka uombowe
Hadi shetani anaishangaa awamu hii
Kuchukua rambirambi za wahanga wa tetemeko ni haki kweli?
Nakemea huu utawala kwa jina la mungu
 
Akomae, vita dhidi ya madawa ya kulevya ni kali sana.

Ndio maana hao akina MSUKUMA wamenyanyuka juu yake baada ya kuona maslahi yao yameguswa!
Ubora huu unaouonyesha penye mada hii ya madawa zote nimekuwa nikikuelewa sana keep it up ndugu.
 
Juzi si ulikuwa unazungumza habari za vdagaa, Leo umekuja na habari za WAITWE KIMYA KIMYA!
Mkuu kutaja majina mazito for the sake of mazito haina mashiko kma ushahidi haupo..... nilitegemea aseme MANJI NI MTUHUMIWA kwa ushahidi A B C hivyo jalada lake lipo linasubiri kupelekwa mahakamani..... sio porojo za ''aje ofisini kwangu tujadiliane" thats not objective mkuu.

Mapapa nao waongelea ni wale wale wa list ya kikwete ambayo kitwanga alisema ushahidi upo kilichobaki ni kukamatwa tu ssa ile yenye mapapa aliosema kikwete kwanni wasikamate mpaka tena tuanze na list mpya ya makonda ambayo haina ushahidi zaidi ya kusema "waje kwa ajili ya mahojiano" afu mwisho wa siku wataachiwa tu kma kina TID sijui nyando tozi!!!

Kma tuko serious tuchukue list ya ikulu tuifanyie kazi maana ndio yenye ushahidi wa kutosha ili wanokamatwa tujue moja kwa moja wanaenda ndani sio kuhojiwa na kuachiwa tu afu kisifanyike chochote
 
Msukuma uduni wa elimu ndio unaomla,
siku zote alikuwa wapi kuhoji hayo kama si hofu imezingira, na huenda ni mtumiaji au muuzaji hawezi tu kulipuka bure, hiyo ni defense mechanism kama yumo asubiri kutajwa........
The saga Continue
Kwani Msukuma ni mkazi wa Dar au Makonda anamamlaka nchi nzima? Ngoja tuone mwisho wa haya maigizo.
 



Kumekucha!!Ni siku nyingine tena,Mkuu wa Mkoa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa wa Dsm,ndugu Paul Makonda ataongea leo na waandishi wa habari kuhusu muendelezo wa vita ya madawa ya kulevya ktk jiji la Dsm.

Mkuu wa Mkoa atakuwa mubashara Azam Tv mara ifikapo saa 05:00 asubuhi leo hii.

Tetesi ni kuwa,mkutano huo unaweza kuwa ni kujibu tuhuma za kuwa anawakabili "dagaa" na wakati "mapapa" wa biashara hiyo wapo.Na majibu ya mkuu wa mkoa yatakuwa ni kuwataja hao mapapa na kuelezea hatua zitakazochukuliwa...

Tega usikie....(Stay Tuned)

=======
UPDATE:
=======

ORODHA KAMILI:

View attachment 468414
View attachment 468415
View attachment 468416
View attachment 468420
Ameanza kwa Kumshukuru Rais wa Jamuhuri.

Paul Makonda asema anataka wauzaji wa dawa za kulevya wajulikane hadharani na hakuna sababu ya kuficha.

Paul Makonda asema vita vya dawa za kulevya vilianza muda mrefu kwa kufutilia hali ilivyo mitaani.

'Kuna watu nilitaka nikutane nao polisi, kuna tofauti kati ya kukamatwa na kuitwa, unapoitwa unapewa nafasi ya kusikilizwa'-RC Makonda


'Kampeni hii dawa ya dawa za kulevya si ya kufanyika kimyakimya tunataka hata watoto wadogo wajue dawa hizi ni hatari kwa afya'-RC Makonda

'Asante kwa watu kama TID, nawapongeza kwa kukiri na kusema kuwa wanatambua namna walivyoingia na kuomba serikali kuwasaidia'-RC Makonda

'Tumemaliza awamu ya kwanza vita ya dawa za kulevya, sasa hii ni awamu ya pili ambayo itakuwa si nyepesi itakuwa na mawimbi mengi-Makonda

'Awamu ya 2 ya vita ya dawa za kulevya tunaianza leo na tunaianza tukiwa tumekamilika, nimekuwa kwenye operesheni usiku na mchana- Makonda

'Watu wanafanya biashara za dawa za kulevya na meli zinazokuja na mafuta'-RC Makonda

'Kuna mama kazi yake ni kusafirisha watoto wa kike ambao wanapewa dawa za kulevya, wawili wako jela China na amewatelekeza'-RC Makonda

'Tukiendelea kuvutanavutana tutapoteza lengo la kupambana na dawa za kulevya'-RC Makonda

'Tukishindwa vita hii ya dawa za kulevya, hajashindwa Makonda au Rais Magufuli tumeshindwa wote'-Rais Makonda

'Tuko na majina 65, nitahitaji kukutana nao ijumaa, wako wanaosemekana wanatumia, wako wanasemekana wanazo taarifa zitakazotusaidia-Makonda

'Nawashukuru wenyeviti wa mitaa wameanza kuleta majina ya watu ambao wanawasiwasi nao kuhusu dawa za kulevya'-RC Malone's

'Kila tunayemuita tunamfahamu kuliko mnavyofikiri kazi yetu ni kuwasikiliza'- RC Makonda

'Zile nyumba mnazozitilia shaka, hamuelewi hata kinachoendelea ni wajibu wetu wananchi kutoa taarifa na taarifa zitakuwa ni siri-RC Makonda

'Kuna ambao tuliwaita wako nje ya DSM, wapo waliotoa taarifa na watafika ila wapo waliokimbia tunawafuatilia na tutawapata wote'- RC Makonda

'Nawashukuru ndugu zangu walioko nchi mbalimbali kwa kunipigia simu na kunipa taarifa mbalimbali'-RC Makonda


ym taifa kwanza.png
ym taifa kwanza.png
ym taifa kwanza.png
 
Wakuu wote wa mikoa wapo kimyaaa wanaangalia makonda na baba wanavyocheza hili game! Lakini baba akishindwa kukinga kifua makonda ataishia kuumia. Hili game tamu sana nasubiri matokeo tu mie yangu macho
 
Kikwete alishutumiwa sana atate orodha ya wauza unga na inasemekana orodha aliacha Ikulu.

Kambi ya upinzani juzi bundeni wakitaka orodha hiyo,Hoja;huenda majina hayo 65 ikawa ni sehemu ya orodha JK aliyoacha Ikulu?
Hapana mkuu makonda kakataa kasema ile orodha ya ikulu yye haimuhusu kadai anafanyia kazi ya mkoa wake tu.

Hoja yako haina mashiko maana ya kikwete ilikuwa verified yenye uchunguzi na ushahidi wa kutosha unlike hii ya makonda yenye majina ya watu walioitwa KWA AJILI YA MAHOJIANO TU na wanaachiwa tu kurudi mitaani hivyo haipo effective.

HOJA: makonda afuate list ya kikwete hta asipowataja akamate awaweke ndani na afungue mashtaka full stop kuliko haya maigizo ya kila cku
 
Back
Top Bottom