Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Kwa hiyo wewe ukienda TANESCO kutoa taarifa ya tatizo la umeme na ukamkuta mtu aliyekuibia jogoo lako naye kaja kuripoti tatizo hilohilo basi utamwachia? Kwamba kwa kumwachia basi tatizo la umeme litaisha?

Nimeyapenda hayo mawazo, simuachi, nafanya fujo pale Tanesco ili nifunguliwe kesi ya kufanya fujo katika eneo la watoa umeme! Au kama kituo cha polisi kipo karibu nasubiri ahudumiwe kisha naenda polisi kuwaambia nimemuona mwizi wangu akihudumiwa Tanesco na hivyo kutumia mtego wa Tanesco wamkamate kirahisi. Wewe mwenzangu ungafanyaje?
 
Nimeyapenda hayo mawazo, simuachi, nafanya fujo pale Tanesco ili nifunguliwe kesi ya kufanya fujo katika eneo la watoa umeme! Au kama kituo cha polisi kipo karibu nasubiri ahudumiwe kisha naenda polisi kuwaambia nimemuona mwizi wangu akihudumiwa Tanesco na hivyo kutumia mtego wa Tanesco wamkamate kirahisi. Wewe mwenzangu ungafanyaje?


Bahati mbaya mimi sio domokaya
 
Habari Comrades..

Hii ni meseji fupi sana kwako RC wa Dar Paul Makonda.

Kama kwenye listi ya majina ya watuhumiwa wa Madawa ya Kulevya uliyoitangaza jana halipo jina la Ridhiwan Kikwete.. acha kucheza na muda na akili za watu.

Tafuta shuguli nyingine ya kufanya, hii vita huiwezi.
 
Habari Comrades..

Hii ni meseji fupi sana kwako RC wa Dar Paul Makonda.

Kama kwenye listi ya majina ya watuhumiwa wa Madawa ya Kulevya uliyoitangaza jana halipo jina la Ridhiwan Kikwete.. acha kucheza na muda na akili za watu.

Tafuta shuguli nyingine ya kufanya, hii vita huiwezi.
Kila mtu ataadhibiwa kwa wakati wake.
 
Mnasikitisha sana vijana, jiulize japo kwa nini waziri mwenye dhamana kaamua kukaa kimya na kumuachia huyo madereva akibwabwaja hovyo

sio madereva sema Mh Makonda mkuu wa mkoa bwana. Jibu ndio upate wewe hapo makonda anadeal na Dar es salaam na sio Tanzania yote, pia kwan nn huyo waziri akae kimya kwa hili jambo???? swali nahis unalo hapo na michakato bado inaendelea tu. Tutajua tu kwa nn yupo kimya kwa kweli
 
Akomae, vita dhidi ya madawa ya kulevya ni kali sana.

Ndio maana hao akina MSUKUMA wamenyanyuka juu yake baada ya kuona maslahi yao yameguswa!
Ni kweli kabisa mkuu, halafu hii vita ikifanyika kwa haki, CCM ndio watakaoumbuka Zaidi.
 
Mwana CBE kumbe wewe ni kielelezo tosha cha vijana na wafuasi wa BILICANAS club walivo wachovu wa kufikiri, Makonda kamtaja mtu mmoja tu waupinzani leo mnakuja kusema anatka kuua upinzani hahahahahah duh Mungu wa nchi hii tunampa kazi kwelikweli inabidi aanze upya kupitia baadh ya bongo zao

Imeandikwa mpige mchungaji ili kondoo watawanyike. Na inajulikana vizuri hiyo ndiyo nia ya huyo bwege wenu anayejiona yeye ni Mungu.

Kama unajifanya hauelewi sina namna ya kukusaida labda rejea kitabu cha mithali ujifahamu mtu wa aina yako anatambulikaje mbele za Mungu. Imeandikwa heri kukutana na dumu aliyenyang'anywa watoto kuliko kukutana na kiumbe mwenye akili kama uliyonayo.

Tena ni vyema unafamu hapa hakuna hoja ya wanachama wangapi wa chama fulani ndiyo watajwe. Hapa issue ni ukweli wa jambo linalofanyika kwa kuzingatia sheria za nchi na siyo hivi vituko vinavyoendelea.
 
Mhh, amenyuti kama vile hasikii na haoni kinachoendelea. Au Makonda ndiye Waziri wa Mambo ya Ndani?
Lazima kuna sintofahamu huko wizara ya mambo ya ndani. Tukumbuke kuna ishu ya jina na vyeti hewa huenda ni namna ya kuonyesha hahitajiki tena. Muda utasema
 
Bro Siro, nakufamu toka ukiwa Uru seminary, K'njaro Boys, Tosamaganga, Udsm nk. Nakushauri usidhalilishe weledi wako wala taaluma yako Bro.
Siro kasoma Uru Seminary? Ile shule ilikua na vichwa sana. Kamaliza mwaka gani? Cyril Chami nae ni product ya kule
 
nina mashaka na uelewa wako.. siwezi kuendelea kubishana na wewe, nikupoteza muda wangu.. mkuu wa mkoa mwenyewe ameulizwa imebidi arekebishe
Ndo maana nilikwambia ulishindwa kujiongeza kujua huyo ni nani , mpaka unakuja kuuliza humu
 
Mimi naunga mkono harakati zote za kupambana na madawa ya kulevya pamoja na maovu mengine yote yanayoirudisha nyuma taifa letu. Hapa nina maana kuwa madawa ya kulevya ni moja tu ya matatizo tuliyonayo kama taifa. Mfano wa tatizo lingine ni RUSHWA. Vita dhidi ya madawa ya kulevya ni ngumu sawa vita dhidi ya rushwa. Kama kweli kuna nia ya dhati ya kupambana na maradhi haya katika taifa letu, ni lazima viongozi wafanye utafiti na uchambuzi wa kutosha kujua mizizi ya matatizo haya na jinsi ya kuyakata. Kwa maoni yangu, vita iliyoanzishwa na mheshimiwa Paul Makonda (RC) dhidi ya madawa ya kulevya yamevalishwa sura ya kisiasa zaidi hivyo kutia shaka kama kweli kuna nia ya dhati. Mkanganyiko unaotokana na "JINSI" vita hivi vinavyoendeshwa ni sawa na mkanganyiko uliopo kati ya "Public Interest" na "Interest of the Public". Ni kwanini mheshimiwa ameamua kutumia njia ya kutaja majina ya washukiwa kwenye vyombo vya habari badala ya kupeleka polisi kuwakamata na kuwahoji baada ya uchunguzi? Kwanini vita hii ya kitaifa inaendeshwa kana kwamba ni ya mkoa mmoja? Kwanini baadhi ya watu waliowahi kukamatwa au kutuhumiwa muda mrefu kujishughulisha na biashara ya madawa ya kulevya hawajakamatwa? Jambo lolote zuri likifanywa kwa njia isiyo sahihi haliwezi kufanikiwa!
 
Ni kweli kabisa mkuu, halafu hii vita ikifanyika kwa haki, CCM ndio watakaoumbuka Zaidi.

Usiweke siasa kwenye masuala kama haya CCM ndio inauza unga au? embu ushindani usiwepo bwana hauwezi jua? hapa tuangalie nani kahusika na sio chama bwana
 
Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kutaka majina ya Watu 65 wanaojihusisha na Biashara ya Dawa za kulevya, Kwa nyakati tofauti Bishop Gwajima na Yusuph Manji wamejaribu kueleza hisia zao na kutoa namna walivyojisikia juu ya hilo..
Niwaambie watanzania wenzangu kilichofanyika kinawahusu Wao kama wao na wala wasijitetetee kwa kuhusisha Dini wala Chama kubwa la Yanga..
Makonda ni mdogo kwao kiumri lakini ana mamlaka ya kufanya alichokifanya kama Kiongozi wa juu wa Mkoa ambao hao wote wanaishi katika Mkoa wake wa Dar es Salaam....
Kama kuna yeyote anahusika akamatwe bila kuangalia brand aliyonayo maana hata yeye haangalii jinsi Watanzania wanavyoumia sababu yake...
[emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji120] [emoji123]
 
Na what if mtu amekuwa suspected tu then ametajwa hadharani halafu baadaye ikabainika hana hatia? Inachukua muda sana kuijenga heshima but it takes only few seconds kuiharibu!
 
Back
Top Bottom