Wewe muunge mkono tu kama unayo nia njema...
Mkiwa vitani siku zote huwa lenu ni moja...kumshambulia adui na sio kuchukua mashambulizi ya adui dhidi ya askari mwenzenu na kuanza kumshambulia...hapo adui atakuwa amefanikiwa ktk mbinu yake ya kuwachonganisha na mkiendelea kuhitilafiana atawapiga.
Vita hii ya dawa za kulevya ni kubwa na tunapaswa kuunga mkono kwa kufumbia macho vitu vidogovidogo kwa mfano suala la masogange dhidi ya Makonda ni suala la kipuuzi na propaganda za hovyo kabisa na bahati mbaya muandishi wa habari anasimama kuuliza huo ujinga hii inaonesha kama jamii hatuko pamoja kuondoa tatizo la dawa za kulevya.
Yaani waandishi wa habari wanasimama na kuuliza propaganda bila kujua kuwa wanaziimarisha na kwa namna moja au nyingine wanamuunga mkono adui...are we serious?????
Nia njema nnayo, na namuunga Mkono, nawaunga Mkono wote wenye Nia ya kutokomeza, au naweza sema kupunguza Kasi ya Madawa ya Kulevya Bongo.
Lakini penye mapungufu tuseme ili Mistari inyooke/Twende sawa.
Kumbuka huyohuyo Masogange alishawahi kamatwa na Madawa ya Kulevya, na Vizibo ubaoni.
Na yeye Mkuu wa Mkoa hapo kwa Masogange kachemka mara mbili.
Suali la kwanza, alijibu "kujuana sio tatizo". Jibu unapata kwamba Wawili hawa wanafahamiana/wanajuana.
Suali la Pili, alishikwa na Kigugumizi cha ghafla na akawa mzito, na kama amenyong'onyea fulani, na kufikia mpaka kujikuna Taya yake. Pale Suali lilikuwa zito na lilimuingia haswa.
Hata kama tufanye ndio Propaganda, kwa hadhi yake pale mbele ya Waandishi alitakiwa ajibu kihadhi yake, sio kujibu kama vile yuko Kitaa, Skani, au Pande zozote zile ambazo za kujiachia, ukijibu Kisela sio Kesi. Ila si kwa pale