Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Kwa nafasi ya mbowe hata siku 1 hawezi kuwa bwege kufanya biashara hiyo hata siku 1,ngoja tuone anaetafutwa hapa
 
Kwa Mbowe ni njia moja wapo ya kummaliza kiuchumi baada ya kutumia mbinu zote kugonga mwamba.

Unaposema tumewalazimisha kuwataja hivi unapimlazimisha kutaja MTU lazima uwe na MTU kichwani mwako.Taja Mwema au taka Mbowe hizi trend kana hakuna ukweli hivi mnarudishaje heshima ya MTU??

Kwa kuomba radhi kimya kimya??Tuache siasa kama ni vita si kwa kuchukia watu. Masogange amemtaja??Au bado??
 
Huyu Kijana hii sasa si kazi yake kwa kweli. Tunamsifia sana lakini yakimshinda mbele ya safari itakuwa aibu sana kwa Taifa. Wale wala Unga wa jana wakina TID ni size yake kabisa. Lakini anapoelekea ni suala la kitaifa ni kazi ya mawaziri husika na baraza la mawaziri. Ni sawa ninamuunga mkono lakini mbona protocali kwake inagoma. Nani yupo nyuma yake?. Ok Ngoja tusubiri.
Hujui alie nyuma yake??..
Kumbuka tu u RC hauipigiwi kura na wananchi.
 
Akazungumzie kuhusu Agness Masongange, pamoja na kumpangia nyumba. Achilia kutokukmkamata licha ya kuwa punda
Hiyo ya mahusiano yake na masogange ni personal issues,hawezi kujibu utumbo kama huo ila kama anajihusisha na biashara hiyo basi hilo ndo jambo la msingi
 
Whatever is excellent kwa anachokifanya makonda na alipo fikia hata leo akisema anaishia hapo still nitampa big up sanaaaa, wapo viongozi wengi wenye mamlaka wanaoweza kushuhulikia madawa yakule sio yeye tu na wao wafanye kwamuendelezo sio kumuachia mtu mmoja nakukaa pembeni heti tumuone atakapofikia, nachoamini MUNGU akiwa upande wake hakuna hata mmoja atakae mshinda, kaza buti makonda kwa hili la madawa umeukuna moyo wangu.
Mungu hawezi kuwa kwa mumiani kama makonda anayepanda kwenye migongo ya damu za watu ili apande
 
Wamemtafuta mbowe kila kona sasa wameamua kumbambikizia kesi za madawa ya kulevya ili kuua upinzani,makonda anatumiwa.
 
Makonda anakurupuka na kwa hili ni lazima sasa anajuta, hakujua kuwa yupo kwenye nyumba ya vioo alivyoanza kutupa mawe, hahaaahaa, aseme mfadhili wa mambo yake sasa.
ha ha ha ni papa gani aliyetajwa kakugusa?
 
Napenda sana vijana wenye shauku ya kuleta changes kama hawa. Imefika mahala tutingishe ukuta bila kuogopa coz there's rule of law and everyone is equal before the law. Sasa nashangaa vijana wanavyoogopa utadhani makonda amemgusa Mungu, hebu acheni uoga vijana wenzangu let's bring changes.
 
Back
Top Bottom