Video ya kwanza yenye Dakika Hamsini na Sita (56) na Sekunde Tisa (9), nimemaliza kuiangalia ila kuna baadhi ya vitu nimevigundua na vinanifanya nijiulize Masuali ya hapa na pale.
Nitataja vichache tu, kwanza:-
Mkuu wa Mkoa amewapa Wadau nafasi ya kuuliza Masuali lakini kuna baadhi ya Wadau waliouliza Masuali, hawakujibiwa ipasavyo, nikiwa na maana,
Wamejibiwa kwa mkato, kimkato. Moja la Suali ni la kumuhusu yeye mwenyewe binafsi kuhusiana na Nchi alizozizuru ni kama alienda kukutana na Magwiji wa Bwimbwi ili wayamalize juu kwa juu (kupunguza kasi), cha ajabu Mkuu wa Mkoa badala ya kujibu Suali, yeye anamwambia Muulizaji Suali,
"Utoto twende Suali lingine"
Huku akimpotezea Muulizaji Suali na kumchagua Mdau mwingine aulize Suali.
Hapana, hapa hakumtendea Haki Muulizaji Suali, labda tu kama angeweka Masharti kutokuulizwa Suali kuhusiana na yeye, hapo ningeelewa, lakini si kwa kuwapa Uhuru Wadau kuuliza Masuali kisha kutowajibu ipasavyo, inakuwa kama ni Dharau fulani vile.
Pili alipoulizwa kuhusu Masogange na kuhusiana na Biashara ya Bwimbwi,
Kwanza amepatwa na mshtuko, Pili hakupendezewa kuuulizwa lile Suali ingawa amejitahidi kuonesha ujasiri lakini kwa Mtu kama Mimi ambae nnao uwezo wa kumsoma Mtu nimeona kabisa pale kayumba, na kanywea kimtindo ingawa yeye Mwenyewe amejisifia ni Kidume wa kupambana na Changamoto yoyote ile ikiwemo ya KimaSuali.
Pili hapo hapo kwa Masogange kabla ya kumjibu Mdau Suali lake Kimkato, ilimchukua Muda kidogo na kufikia Kujikuna Taya, chini ya Kishavu karibu na Kidevu.
Hapa kwa upande wangu naona kuna namna fulani.
Sawa nampongeza kwa Kazi nzuri sana anayoifanya (kupambana na Madawa ya Kulevya), na sipingani nayo hata kidogo, na ninaifurahia sana, Maana mimi mwenyewe Watoto wangu bado wadogo sana, sasa niambie Mtoto wangu wa Kwanza atakapofika Umri wa Miaka Kumi na Kitu, na Ulimwengu wenyewe huu wa Madawa ya Kulevya si Mtihani wa hali ya juu. Sikatai, Malezi na Maadili wanayolelewa ni Meema ila kama ujuavyo Binaadam anabadilika pamoja na Maadili hayo hayo Mema.
Nikirudi tena kwa Mkuu wa Mkoa, pamoja na Pongezi nilizompa haina maana kwenye/penye Mapungufu nisiseme au nikae kimya, hapana ntatoa Sauti yangu.
Mapungufu kwenye hii Video nimeyaona.
Nikirudi tena kwenye Video yenyewe ,
Kuna vipande Sauti zimeondolewa/zimeminywa hii nafikiri kwasababu Maalum.
Maana nlikuwa na Shauku sana kuhusiana na huyo Mama anaewapeleka Wasichana wa Umri wa Kati Nchini CHINA na kuwalipa Ujira wa Dollars 7000 iwapo KAZI ikiingia salama