Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Jambo hili ili liishe kwa uzuri ni vema mtuhumiwa akajitokeza mbele na kuwasuta watu(wabaya wake) kwa kumsingizia jambo.Hili la kuja kwa kuvizia kama Wafarisayo kuona nini kitajibiwa hakisaidii asilani.Hello there,come out here and do something for the sake of your dignity,if any boss!
 
Vyeti vyake vilishakaguliwa na Utawala wa Rais mstaafu Kikwete na Rais Magufuli ndiyo maana yuko kazini mpaka sasa.

Wenye vyeti fake au vya kuazima hawako kazini Leo hii.

Mwenye ukweli na ushahidi wa taarifa hizo zinazosambaa mitandao ni si afungue kesi Mahakamani na mawakili wakujitolea wako wengi tu watasimamia kesi bila malipo maana ni wazalendo wa nchi.

Nashangaa Mch Gwajima kujitapa madhabahuni kuwa ana miliki vyeti vya watu ofisini kwake ambao hawamuhusu wala si waajiriwa wake.
Hawamhusu?
Aa wewe....wacha maneno weka muziki @ cheti.
 
Namuongelea "Necha"
Huyu msanii kipenzi cha watanzania
hususan dar ambaye ukimuangalia basi utagundua ufanano na Peter Tosh yaani ni "BUSH DOCTOR" imekuwaje jina lake halikusomeka kwenye orodha ya Makonda???


MYTAKE:-
BANGI IHALALISHWE MISUGUANO KATIKA JAMII IPUNGUE.
 
Tanzania kesi kwa wanyonge tu mkulu alisema atatutetea kumbe weeee chamoto tunakiona
 
Cc hatuko interested, kama unataka kujua nenda kwa karani wa jaji anayoisikiliza hyo kesi utapata jibu.
 
Hapana kesi dhidi ya Mbowe haikufunguliwa kutokana na kukosa ushahidi wa tuhuma zilizotajwa labda tusubiri soon itakapofunguliwa kesi ya forgery,personification,fraud,Armed Robbery,criminal tresspass, threatening to kill & stealing dhidi ya Daud Albert Bashite.
 
Tanzania na Ethiopia ziliwahi tia sahihi makubaliano ya ndege za ethiopian airways kutumia uwanja wa ndege wa Dar es salaam kwa kutua na kuruka. Makubaliano yaliƴosainiwa kati ya Tanzania na Ethiopia ni kuruhusu meli za Ethiopia za shirika kubwa la meli za Ethiopia kutua na kushusha mizigo na kupakia bandari ya Dar kama ilivƴo Ethiopian airways.

Shirika la meli la ethiopia ni shirika kubwa la ƙimataifa kama ilivƴo ethiopian airways.lilianzishwa 1964 na liko fit ujio wao utaongeza uwingi wa meli na mizigo kwenye bandari ya Dar es salaaam.

=======

WAZIRI Mkuu wa Shirikisho la Kidemokrasia la Jamhuri ya Ethiopia, Hailemariam Dessalegn amemhakikishia Rais John Magufuli kuwa nchi yake ipo tayari kuimarisha na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano.

Alisema ushirikiano huo utasaidia kuleta manufaa makubwa zaidi kiuchumi na kukabiliana na umasikini wa wananchi wa nchi zote mbili.

Dessalegn alitoa kauli hiyo Ikulu, Dar es Salaam wakati akizungumza na wananchi wa Tanzania na Ethiopia kupitia vyombo vya habari muda mfupi baada ya kuwasili nchini kwa ziara rasmi ya kiserikali ya siku mbili, anayoifanya kwa mwaliko wa Rais Magufuli.

Miongoni mwa maeneo ambayo Waziri Mkuu Dessalegn amesema atatilia mkazo ni ushirikiano katika usafiri wa anga ambapo ameahidi kuwatuma wataalamu kutoka Shirika la Ndege la Ethiopia kuja nchini kushirikiana na wataalamu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) ili kuimarisha utendaji kazi na kuikuza ATCL.

“Shirika letu la ndege la Ethiopia ni shirika linaloendeshwa kwa faida barani Afrika, lina ndege 96 na linatarajia kununua ndege nyingine 42, ndege zake zinatua katika viwanja 92 duniani kote na viwanja 42 ndani ya Ethiopia.

“Hivyo nitawaleta viongozi wa shirika hili ili waje washirikiane na ATCL kuweka mkakati wa namna ya kuiendeleza ATCL na kuiwezesha kufanya kazi kwa faida,” alisema Waziri Mkuu Dessalegn.

Pia alisema Shirika la Ndege la Ethiopia kwa kushirikiana na ATCL litaufanya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam kuwa kituo chake cha mizigo na hivyo kuwezesha mizigo ya ukanda wa Afrika Mashariki na maeneo jirani kutumia uwanja huo kusafirisha mizigo yake duniani kote.

Rais Magufuli na Waziri Mkuu Dessalegn ambao kabla ya kuzungumza na wananchi walifanya mazungumzo rasmi, wamesema wamekubaliana kuwa Tanzania na Ethiopia zibadilishane uzoefu juu ya uzalishaji wa nishati ya umeme kwa kutumia maji.

Katika makubalino hayo Waziri Mkuu Dessalegn aliahidi kuwatuma wataalamu wa nchi yake kuja nchini kutoa uzoefu wa namna Ethiopia ilivyoweza kuzalisha kiasi kikubwa cha umeme kwa kutumia maji ukiwemo mradi mkubwa unaoendelea kujengwa uitwao Grand Ethiopian Renaissance Dam (GERD) ambao unatarajiwa kuzalisha megawati 6,470 za umeme.

Viongozi hao wamekubaliana kushirikia na kufanya mapinduzi ya kilimo na mifugo, hasa ikizingatiwa kuwa Ethiopia inaongoza kwa idadi kubwa ya ng’ombe barani Afrika na Tanzania inashika nafasi ya pili na kwamba juhudi hizo zitakwenda sambamba na kujenga viwanda vingi vitakavyoongeza thamani ya mazao.

“Naamini kuwa tukishirikiana katika kilimo na mifugo, tutaweza kutumia teknolojia za kisasa katika uzalishaji wa mazao ikiwemo ngozi na nyama na tutatumia mashirika yetu ya ndege kuyafikia masoko mbalimbali duniani na hivyo kukuza uchumi na kuwaongezea wakulima wetu kipato,” alisisitiza Rais Magufuli.

Aidha, viongozi hao wamekubaliana kushirikiana kwa kubalishana uzoefu juu ya namna sekta mbalimbali zitakavyoleta manufaa ya kiuchumi zikiwemo huduma za benki, madini na gesi, elimu na mawasiliano hususani simu.

Rais Magufuli alisema ziara ya Waziri Mkuu Dessalegn imekuwa ya manufaa makubwa kwa Tanzania na amesisitiza kuwa wakati umefika wa kukuza biashara kati ya nchi hizo ambazo kwa sasa thamani ya biashara kati yake ni Dola za Marekani milioni 2.24 tu.

Kabla ya kuzungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari, viongozi hao walishuhudia utiaji saini wa mikataba 3 ambayo ni mkataba wa mkakati wa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Ethiopia, Mkataba wa kuanzishwa Kamisheni ya Pamoja ya Kuduma kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Ethiopia na Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika sekta ya utalii kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Ethiopia.

Waziri Mkuu Dessalegn aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere asubuhi na kupokewa na mwenyeji wake Rais Magufuli aliyeongozana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa na akiwa uwanjani hapo alipigiwa mizinga 19, kukagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake na alishuhudia burudani ya ngoma za asili.

Mbali na kusaidia ufanisi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), makubaliano mengbine ni matumizi ya Bandari ya Dar es Salaam, kuendeleza kilimo, matumizi ya Mto Nile, sekta ya viwanda, mawasiliano, hati za kusafiria, utalii, elimu, madini, sekta ya michezo, ushirikiano wa majeshi na kuboresha mfumo wa kodi.

Makubaliano hayo ni pamoja na nchi ya Ethiopia kuanza kufundisha lugha ya Kiswahili ambapo wataalamu wa lugha hiyo kutoka Tanzania watakwenda kufundisha katika moja ya vyuo vikuu kitakachochaguliwa kwa ajili hiyo.

Akizungumza baada ya kusainiwa mikataba hiyo pamoja na makubaliano, Rais John Magufuli alisema ujio wa kiongozi huyo utaleta manufaa katika nchi hizo mbili.

“Tumekubaliana kwenye elimu watachagua chuo kikuu kimoja kwa ajili ya kufundisha Kiswahili na mimi nimeahidi kutoa maprofesa kufundisha kwa sababu lugha hii ni ya Afrika,” alisema Rais Magufuli.

Alisema wamekubaliana Mto Nile utumike kwa manufaa ya nchi zote na kusiwe na nchi mmoja itakayodai Mto huo ni wake.

Rais Magufuli alisema katika suala la umeme, Ethiopia kwa kutumia mabwawa imeweza kuzalisha umeme unaouzwa kwa wananchi kwa bei nafuu huku akisema kuwa jambo hilo litatoa changamoto kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Alisema kupitia ziara hiyo Tanesco inapaswa kujifunza kutoka Ethiopia wanaozalisha umeme na kuuza kwa bei ya chini.

Rais alifahamisha kuwa, kwa sasa megawati moja inauzwa senti sita hadi saba na pia biashara ni ya ushindani. “Wenzetu wamejenga bwawa la megawati 1,870 na sasa wanajenga jingine ambalo litazalisha umeme wa megawati 6,400, sisi umeme wetu nchi nzima ni megawati 1,500, nimetamani kuwaambia watuletee umeme wote huo,” alisema Rais Magufuli.

Alisema Ethiopia imekubali kuanza kuleta umeme megawati 400 na baadaye wataongeza kutoka katika vyanzo vya mabwawa yao hayo ambapo kwa sasa wanasambaza hadi mpakani mwa nchi hiyo na Kenya.

Alisema kwa kuwa imepiga hatua katika kutumia vyanzo vya umeme na kupata umeme wa bei nafuu na wa uhakika, wamekubali kuleta wataalamu nchini kuangalia na kutoa mafunzo.

Rais Magufuli alisema Serikali ya Ethiopia imekubali kutoa ushirikiano wa kibiashara na mafunzo kwa ATCL.

“Shirika la Ndege la Ethiophia lina ndege nyingi, ni shirika kubwa na wanafanya vizuri Afrika na duniani, ushirikiano huu utasaidia katika kutoa mafunzo kwa shirika letu na pia matengenezo ya ndege,” alisema.

Rais Magufuli alisema Shirika hilo la Ndege la Ethiopia pia limekubali kujenga kituo kikuu cha mizigo kitakachojengwa Dar es Salaam na kitakuwa kikubwa katika Bara la Afrika na pia mizigo kuchukuliwa kupitia Bandari ya Dar es Salaam.

Alisema serikali hizo zimekubaliana katika sekta ya viwanda, kwa kuwa nchi hizo mbili zina mifugo mingi, kujenga uhusiano wa kibiashara katika kutumia maziwa, ngozi na nyama na kwamba sasa, nyama toka Tanzania inaweza kusafirishwa na kwenda kuuzwa Ethiopia.

Katika hati ya kusafiria, Rais Magufuli alisema inasababisha wafanyabiashara wengi katika nchi hizo kukwama katika shughuli zao hivyo wanaangalia namna ya kuiondoa.

“Viza inazuia biashara kati ya nchi hizi mbili, tunataka kuondoa viza hii ili wafanyabiashara, mabalozi wasiwekewe vizingiti wakija,” alisema Rais Magufuli.

Rais Magufuli alisema Ethiopia imekubalikuja kufungua ubalozi wao mjini Dodoma na amekubali kuwapatia eneo la kujenga ofisi na nyumba ya balozi.

Aidha, alisema wamekubaliana pia kuendeleza sekta ya utalii, kwamba ndege za nchi hiyo zitakuwa zinakuja Tanzania katika vivutio mbalimbali vilivyopo.

Rais Magufuli alisema wamekubaliana pia kuendeleza sekta ya kilimo kwa kuwa ili kuwe na viwanda, lazima kuwe na kilimo bora.

Rais Magufuli alisema wamekubaliana kutoa mafunzo katika sekta ya mawasiliano ili kuboresha ukusanyaji wa mapato kwani Ethiopia imeimarisha mfumo wao.

Alisema wamekubaliana katika uwekezaji wa pamoja na kushirikiana katika mafunzo ya sekta ya madini, kodi na michezo hasa katika riadha na pia kushirikiana katika majeshi.

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Dessalegn alisema Tanzania ni nchi yenye mfano mzuri katika sekta ya kilimo. Alisema mabadiliko ya kuboresha sekta ya kilimo yaanzie kwa wakulima wadogo.

“Tujenge kilimo kwa Tanzania na pia kwa Ethiopia ili kuileta jamii pamoja na kushirikiana, katika kuleta mabadiliko ya kilimo; tuanzie na wakulima wadogo wadogo,” alisema.

Alisema amekuja Tanzania kwa sababu ni nchi yenye mambo mengi ya kujifunza katika nchi za Afrika, hivyo hakuona umuhimu wa kwenda nje ya Bara hili Waziri Mkuu huyo aliwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 5.43 na kupokelewa na Rais Magufuli pamoja na viongozi wengine, alipigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride.

Vipaumbele vya nchi hizi Pamoja na kuwa uchumi wa Ethiopia umeimarika zaidi kuliko Tanzania huku kukiwa na maendeleo makubwa, nchi zote mbili zipo katika orodha ya nchi zenye uchumi unakua kwa kasi barani Afrika.

Ikitoka katika janga la njaa miaka thelathini nyuma iliyoua raia wengi, nchi hiyo iliyotambulika kwa umaskini wa kukithiri, sasa imeimarika na kuwa moja wapo ya nchi yenye uchumi unaokua kwa kasi zaidi barani Afrika, huku udhibiti wa rushwa ukitajwa kuchochea maendeleo kwa kasi.

Nchi hiyo imo katika mkondo wa kuwa taifa lenye utajiri wa kati kufikia mwaka wa 2025, huku ikiwa na mafanikio makubwa katika sekta ya usafiri wa anga kutokana na Shirika la Ndege la Ethiopia kuwa na mafanikio makubwa barani Afrika.

Tanzania ambayo pia inakisiwa kufikia uchumi wa kati mwaka 2025, ipo katika mipango ya kufufua shirika lake la ndege, mipango iliyoanza baada ya kuingia madarakani kwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli.

Ingawa viwango vya umaskini vinatajwa kuwa bado ni vikubwa Ethiopia, Serikali ya nchi hiyo imeendelea kukabiliwa na changamoto kubwa katika kupambana na mfumuko wa bei za bidha muhimu, huku uzalendo wa taifa kwa viongozi na wananchi ukitajwa kuwa ni wa kiwango cha juu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia (WB) ya mwaka 2016, Tanzania na Ethiopia zimetajwa kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi barani Afrika zikiwa katika orodha ya nchi 10 bora barani humo.

Wakati Pato la Taifa (DGP) la nchi ya Ethiopia lilikua kutoka Dola za Marekani bilioni 7.325 mwaka 1981 hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 61.54 mwaka 2015, DGP ya Tanzania ilikua kutoka Dola Billioni 5.1 mwaka 1981 hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 48.197 mwaka 2015.

Taarifa za Benki ya Dunia zinaonesha kuwa wastani wa ukuaji wa uchumi kwa nchi ya Ethiopia umefikia wastani wa 8.9 mwaka 2017, tofauti na miaka saba iliyopita ambapo wastani ulikuwa asilimia 7.

Kwa upande wake, Tanzania imeweza kwenda kasi katika kukuza uchumi na kufikia wastani wa 7.1, kiwango ambacho kwa mujibu wa Benki ya Dunia kilitazamiwa kufikiwa mwaka 2019, lakini kimeweza kufikiwa miaka miwili kabla, na hivyo kuwa kichocheo cha kuelekea kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Mafanikio hayo makubwa kwa Ethiopia yanaweza kuwa yanachangiwa zaidi na Taifa hilo kuwa idadi kubwa zaidi ya nguvu kazi ukilinganisha na Tanzania.

Kwa takwimu hizo za Benki ya Dunia, tofauti ya uchumi baina ya mataifa hayo inapimwa kuanzia mwaka 1960 wakati Ethiopia ikiwa na watu milioni 22.671 huku Tanzania ikiwa na idadi ya watu milioni 10.1.

Takwimu za hivi karibuni za kiuchumi zilipimwa na benki hiyo mwaka 2015, wakati Ethiopia ikiwa na watu milioni 99.39 wakati Tanzania ikiwa na watu milioni 53.47.

Pamoja na tofauti katika baadhi ya maeneo ya uwekezaji, sera na vipaumbele vya uwekezaji baina ya mataifa hayo mawili ni kama zinaelekeana hasa kutokana na mataifa yote kuweka kipaumbele katika kuwekeza katika barabara na reli na hivyo, ujio wa Waziri Mkuu huyo unaweza kuongeza fursa za ushirikiano.

Waziri wa Fedha wa Ethiopia, Sufian Ahmed anasema Serikali yake itaendelea kuwekeza katika barabara na reli. Kipaumbele hicho kinafanana kwa karibu na kile cha Serikali ya Tanzania inayoendelea kuwekeza katika ujenzi wa barabara na ujenzi wa Reli ya Kati ya kisasa (Standard Gauge).

Wakati Tanzania imeanza mipango ya kuwa na treni ya umeme kutoka Dar es Salaama hadi Morogoro, tayari Ethiopia ujenzi wa reli hiyo katika mji mkuu wa Addis Ababa umekamilika na tayari treni za kutumia umeme zimezinduliwa.

Eneo lingine ambalo wafanyabiashara wanaweza kushirikiana katika kukuza sekta binafsi ni katika ujenzi wa majengo makubwa (nyumba), maeneo ya burudani na nyumba za wapangaji.

Chanzo: Habari leo
 
Akili za CCM bwana. Nichoree ramani ya Ethiopia

Tanzania na Ethiopia ziliwahi tia sahihi makuɓaliano ya nɗege za ethiopian airways kutumia uwanja wa nɗege wa ɗar es salaam kwa kutua na kuruka.Makuɓaliano yaliƴosainiwa kati ya tanzania na ethiopia ni kuruhusu meli za ethiopia za shirika kuɓwa la meli za ethiopia kutua na kushusha mizigo na kupakia ɓanɗari ƴa ɗar kama ilivƴo ethiopian airways.shirika la meli la ethiopia ni shirika kuɓwa la ƙimataifa kama ilivƴo ethiopian airways.lilianzishwa 1964 na liko fit ujio wao utaongeza uwingi wa meli na mizigo kwenye banɗari ya dar es salaaam.moɗerator usiunge hii habari na zingine ili kuwapa taarifa sahihi wachangiaji
 
Mkuu bado hujaeleweka kabisa.
Kwa mfano.
Tanzania tuna bandari na viwanja vya ndege, meli kutoka POPOTE duniani inaweza kuja kutia nanga kwenye bandari yetu na hapo watalipa Tozo au ushuru wa kushusha mizigo, na ndege hivyo hivyo zinaweza kutua ili kushusha Abiria, mizigo au kujaza mafuta.

Sasa embu tuambie sasa, mkataba wa Tanzania na Ethiopia uliotiwa juzi una kitu gani kipya au special?
Meli za Ethiopia zitatia nanga bure?
Ndege za Ethiopia zitatua bure?
 
Back
Top Bottom