VITA DHIDI YA ULAWITI NA UBAKAJI KWA WATOTO KUNUSURU VIZAZI VYETU
UTANGULIZI Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazokumbwa na ongezeko la matukio ya ulawiti na ubakaji kwa watoto wa dogo tatizo hili linaongezeka kwa kasi sanaa .takwimu zinaonyesha kufikia aprill,2024 jumla yamatukio 799 ya ulawiti na ubakwaji kwa watoto wadogo yameibuliwa na kuwasilishwa katika mamlaka husika.
Idadi hii ni hatarishi sana kwakuwa idadi hii imekuwa mara mbili ya idadi ya mwaka 2016 matukio haya kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakileta madhara makubwa sana kwenye jamii ikiwa pamoja na kuwa haribu watoto kimwili na kisaikolojia inapelekea wanakosa amani na furaha kwenye maisha yao kila wanapokumbuka ukatili waliotendewa hii inapelekea baadhi yao kuchukua maamuzi magumu kama kujitoa uhai ili kukwepa fedheha hiyoo lakini pia matukio hayo yame eneza magonjwa kwa watoto kama vile UKIMWI na magonjwa mengine hivyo yana athiri mfumo mzima wa akiri ya mtoto na afya yake kwa ujumla.
Nipende kuipongeza serikali na taasisi mbalimbali ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikipambana sanaa kuwanusuru watoto na kuchukua hatua kali dhidi ya watenda matukio ya namna hii ingawa kadri siku zinavoenda matukio ya namna hii yanazidi kuongezeka kwa kasi sana . Napendekeza zitumike njia zifuatazo ambapo kwa mtazamo wangu kama zitafuatwa ilivyo matukio ya namna hii huenda ya kapungua kwa kasi sana na pengine kupotea kabisa kadri miaka inavozidi kwenda njia hizo ni,
Kuanzisha somo la utu na uzalendo mashuleni. Napendekeza mashuleni lianzishwe somo la utu na uzalendo ambapo wanafunzi waanze kujifunza tangu shule ya msingi hadi chuo kikuu katika somo la utu wanafunzi kuanzia darasa la awali waanze kujifunza kujari na kuthamini utu wa mtu kuwapenda wenzao kama wao wanavojipenda pamoja na kuheshimiana na zaidi wajengewe misingi ya kuwa na umoja na msimamo hii itapunguza roho ya ukatili kwa watu na hawatakuwa na uwezo wa kufanya ukatili wa namna hii wakikuzwa katika mazingira ya utu na kupitia somo la uzalendo wanafunzi wajifunze jinsi ya kudumisha amani kulipambania taifa lao dhidi ya matukio ya kikatili yoyote yale kila mmoja afunzwe kusimama kama silaha kwa matukio yoyote yale yanayoenda kinyume haki za binadamu na si kuiachia serikali na taasisi jukumu hili ambalo ni zito na gumu sana bila kufanya kazi kwa pamoja itatuwia ugumu sana kulimaliza ili kujenga taifa imara lenye haki na furaha.
Serikali pamoja na taasisi za haki za watoto zinapaswa kuanzisha programu maalumu walau ya dakika 30 programu hiyo iwekwe mahospitalini ambapo mama wajawazito wanapokuwa wanaenda kwenye mahudhurio ya kliniki wawe wanapewa semina fupi juu ya malezi bora ya watoto na namna yakuweka mazingira rafiki kwa watoto na mazungumzo ya mara kwa mara kwa watoto na kuwaasa wasiruhusu sehemu zao za siri zikaguswa na mtu yoyote Yule hii itafanya watoto kuwa wakweli na wakali endapo watataka kufanyiwa matukio hayo kwakuwa wanajua wazazi wao wako pamoja na hivyo itaongeza sana kujiamini kwao pamoja na kujua tatizo mapema na kulichukulia hatua tatizo hilo haraka ili kuepusha tatizo kuwa kubwa kiasi cha kushindwa kulitatua au kuchukua mda mrefu kupata utatuzi kunabaadhi ya matukio ya kikatili yanatokea na chanzo chake pia inakuwa ni wazazi kwa kuonyesha wazazi hawana mda wakukaa na kuzungumza na watoto wao pamoja na kujua hali zao na mienendo yao hivyo wazazi wapewe elimu ya juu ya malezi bora kwa watoto.
Serikali kuwaongeza jukumu wajumbe wa nyumba kumi la kupita kwenye nyumba zao walau mara mbili (2) kwa wiki kwenye nyumba zao kwanza kwenda kuongea na watoto juu ya haki zao na kusikiliza kero zao hii itaongeza kujiamini kwa watoto kwa kuona pia hata jamii inayo wazunguka iko karibu yao mara zote na inajali sana kuhusu wao hivyo itazidisha uchungu na hasira kwa watakao taka kujaribu kuwatendea ukatili wowote watalipotiwa haraka sana na endapo wajumbe watakapokuta kuna kero zozozte wazitatue haraka sana ili tatizo lisiendelee kuwa kubwa zaidi na pili kuzungumza na wazazi na kuwasisitiza namna bora ya kuwa karibu na watoto hii itajenga mazingira ya watoto kuwaona wazazi kama marafiki zao watakuwa huru kuzungumza changamoto zao zozote zile.
KUZUIA BAADHI YA MAUDHUI KUTOKA KWENYE KAZI ZA WASANII YANAYOENDA KINYUME NA TAMADUNI NA MAADILI YA MTANZANIA. Kuna baadhi ya kazi za wasanii mbalimbali kutoka ndani na nje ya mipaka ya Tanzania ambapo kazi hizo kama tamthiliya ,filamu pamoja na mziki maudhui yake yana momonyoa sana maadili ya mtanzania kwani kazi hizo zinaonyesha watu wamevalia mavazi yanayo onyesha robo tatu ya miili yao pamoja na kazi nyingine za sanaa kuonyesha maudhui za mapenzi ya jinsia moja hivyo kama watoto wanaona pia wanaamini kuwa ni jambo la kawaida na hivyo hata wakitendewa hawasemi kwani wanaona ni kitu cha kawaida hivyo inapelekea uchochezi wa matukio kama hayo dunia ya sasa imekuwa ni rahisi kuona mtoto anaimba nyimbo ya anasa ikiwa hata nyimbo ya taifa haijui kazi za sanaa zinanguvu kubwa ya kushawishi jamii kuwa chanya au hasi pia ziwepo .pamoja na hilo naziomba taasisi zipokee kazi zetu sisi wasanii na wadhidhamini ili zitoe elimu kwa ukubwa nina filamu inayoeleza ukatili wote wanaokumbana nao watoto kwa kuzingatia uhalisia imeshindwa kuchezeka kwakuwa nimeshindwa kulipia gharama za uchezwaji wake na imekosa wadhamini nina imani kwa pamoja tunaweza kutokomeza hili
Ni imani yangu kubwa kuwa endapo njia hizi zitafuatwa kikamilifu yawezekana tatizo hili kuanzia miaka mitano (5) ijayo likaanza kupungua kwa kasi napengine kupotea kabisa kwa pamoja tusimame imara kukemea ukatili dhidi ya watoto tunaweza kuutokomeza kabisa.
‘’TUJENGE MSINGI IMARA KWA WATOTO KWA TAIFA IMARA LA KESHO’’

Upvote
2