chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 20,834
- 26,217
Wadau salaam..
Baada ya Mh Tundu A. Lisu kuonyesha nia ya kuwania nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA Taifa tumeona mambo mengi na matamko mbalimbali, matamko mengi ambayo hayakutegemewa ni namna Lisu anvyopigwa vita na kukatishwa tamaa, Siyo ndani ya CHADEMA Tu Bali hata kwa Vyama vingine kama CCM nao wanaungana kumpinga Lisu kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA. Hii inafikirisha sana na kuzua Maswali mengi kwamba ni kitu gani haswa wanachohofia kutoka kwa Lisu, kwanini wasimuache awanie hiyo nafasi alafu Baada ya matokeo tuone itakavyokuwa?
Kwanini CCM wanataka Mbowe aendelee kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA pamoja na kuwa ameshakuwa mwenyekiti zaidi ya miaka 20 sasa ? CCM Wana maslahi gani na CHADEMA chini ya Uongozi wa Mbowe.
La mwisho lakini Siyo kwa umuhimu naomba Lisu apewe Ulinzi wa kutosha, maisha yake Yana thamani kuliko nafasi hizi za kisiasa.
Kila la kheri TAL.