Vita Janga la Corona, Rais Magufuli Aanza Kusifiwa Duniani!, Jarida la The Economist 'Lamsifu' JPM Kumtegemea Mungu!, Ni Uamuzi Sahihi?, Utatuokoa?

Paskali, kichwa cha habari haswa hilo neno walilotumie to "quackery" haliwezi kuwa sifa kwa aliyetajwa kwenye hiyo article.
 
Magufuli amekuwa shujaa kwenye mapambano dhidi ya corona.

Kilichomsaidia ni kumtanguliza Mungu kwenye haya mapambano.
Ningekabaliana na wewe kama ungeeleza baada ya kumtanguliza Mungu mbele tumefanya nini kama taifa. Je ni kiasi gani kimetengwa kwa NIMR na wataalam wetu wengine kufanya utafiti ya kupata tiba ya hii dawa? Ni vifaa gani tiba tumeanza kutengeneza wenyewe kwa ajili kupambana na hili janga? Binadamu pamoja na kumtegemea Mungu, tofauti na viumbe vingine tumepewa akili, na lazima tuitumie.
 
Nafasi ya DC kule Mtwara jana kateuliwa Dunstan Kyobya
 
Pascal Mayalla Jarida hilo linawezekana halina nia ya kumsifia Rais Magufuli moja kwa moja.

Mimi ni mpinzani wa ccm miaka yangu yote niliyoweza kuifahamu ila wakati mwingine ninatoka nje ya utaratibu wangu wa kuwachukui wana-CCM wote.....kwenye hili la CORONA njia anayotumia Mh.Rais Magufuli kupambana nayo naunga mkono 100% kumtanguliza Mungu na Kuchukua tahadhari zingine zote...

Wanasayansi wako chimbo kwenye maabara zao mpaka leo bado hawajatoka na jibu.
 
Wandugu, hapa nafanya tuu follow up ya Corona nikipitia kujikumbusha niliwahi kuandika nini au kusema nini kuhusu Corona na hiki kinacho endelea sasa. Corona is real tusifanye masihara, tujilinde kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.

Kila Jumamosi asubuhi kuanzia saa 1:30 hadi saa 3:00 asubuhi , Star TV, huwa ninakuwa live kwenye kipindi cha TV cha Jicho Letu Ndani ya Habari ambacho huwa kinatangwa live na Star TV kila siku za Jumamosi asubuhi, kwa Jumamosi ya kesho, mgeni wetu ni Waziri wa Habari, Dr. Harrison Mwakyembe tukijadili kuhusu athari za Corona kwenye sekta ya Habari, nini kifanyike.

Ukipata nafasi karibu utufuatilie.

P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…