Vita Kuu ya Tatu (WW3) ipo dhahiri mlangoni, Tuwe na akili ili tuishi

Vita Kuu ya Tatu (WW3) ipo dhahiri mlangoni, Tuwe na akili ili tuishi

Ukifuatilia magaidi na wapiganaji karibia wote wa misituni wanapewa chapuo ya misaada ya zana na kimafunzo kutoka kwa hayo mataifa unayoyaona ndo mkombozi wa dunia hii
SASA MTU ANATAKA VITA SI UNAMUUZIA SILAHA KUTOKANA NA UJINGA WAKE MATAIFA MAKUBWA MBONA WENYEWE KWAO HAMNA VITA WATU WAO WANAISHI SAFI KAMA MPUMBAVU ANATAKA VITA WEWE MUUZIE SILAHA ILI AENDE NA UJINGA WAKE.

HATA VIAZI MBEYA HAVINA DILI ILA UKIPELEKA DAR VINACHANGAMKIWA SANA
 
All out war ni ngumu Nuclear Bombs zina-act kama deterrent watu wanaogopa kulianzisha wakilianzisha na wale wanalianzisha....

Vita ni internally matabaka kugombania resources gap of classes zimezidi have and have nots; Bila a sustainable economic systems kutakuwa na chaos na tusipoangalia even anarchy...
 
Urusi ilipovamia Ukraine kutokana na uchokozi (indirect) wa US akishirikiana na NATO ilikuwa ndiyo curtain-raiser, Baadaye tukaona Vita ya Sudan na Juba vimepambamoto huku taarifa za madhila zikidhibitiwa kwa kiwango kikubwa na vyombo vya kimataifa na serikali za Afrika... Tumeona Afrika Kaskazini na Magharibi kumekubwa na mapinduzi ya kijeshi yanayosemwa kuratibiwa na Urusi....

Israel imeendeleza unyama mkubwa ulioanza kwa uchokozi wa kigaidi kutoka kundi la HAMAS. unyama huo umeenda kuathiri maisha ya watu WOTE wa Gaza Strip. Vita imeanza kusambaa Lebanon na sehemu za Jordan huku Syria ikiendelea kupokea vipigo mfululizo...

Tumeona pale DRC Afrika ya Kusini imepeleka majeshi yake (kwa kivuli cha SADC) kujipanga kuishambulia Rwanda (mshirika wa US) na hili lipo wazi kabisa.

Kaskazini mwa Msumbiji jirani na mpaka wa Tanzania eneo la Cabo Delgado vita imechachamaa kupambana na majahili wanaofadhiliwa na mataifa makubwa, haya mambo yanafichwa na serikali zetu kwa nguvu kubwa sana.

Houth imejipanga kupigana na imeweza kushambulia kila meli inayokatiza bahari nyeusi kutoka nchi zinazoiunga mkono Israel....

Ndugu zangu wabongo wenzangu, Vita Kuu ya Tatu ya Dunia ipo mlangoni kwa sababu maandalizi yote yamekamilika na sasa mataifa makubwa yameshaweka vikosi vyao sawa. Ukiangalia mwenendo wa China, Korea Kaskazini, Iran, NATO na kwingineko ni mwendo wa mazoezi na majaribio ya kijeshi kila kona... Hivyo tujipange kama nchi tujue tunaishije katikati ya ulimwengu huu wa kitimtim.

Tusisahau kujiwekea akiba ya chakula kama nchi
mchi gani ?? hiii hii iliyotupelekea mdoli bungeni
 
Tumechoka na tabiri zenu...
Kila siku vita vita

Mbuzi kashatoa session 6 kule
 
Kama mwaka 2001 kiranja mkuu alipigwa kwake na akiwa na nguvu na ushirika wa nguvu na hakuna upinzan kuliko sasa na vita havikutokea tusahau kuhusu ww3
 
Back
Top Bottom