Vita vya Gaza: Marekani ina ‘matumaini’ kwamba Hamas itakubali pendekezo jipya la Israel la kusitisha mapigano

Vita vya Gaza: Marekani ina ‘matumaini’ kwamba Hamas itakubali pendekezo jipya la Israel la kusitisha mapigano

Malaria 2

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2023
Posts
6,846
Reaction score
10,288
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amesema ana matumaini kuwa Hamas itakubali pendekezo la hivi punde la Israel la kusitisha mapigano Gaza na kuwaachilia mateka.

Aliita pendekezo hilo kuwa la "ukarimu usio wa kawaida", wakati ujumbe wa Hamas ulipojadiliana na wapatanishi mjini Cairo.

Baada ya wiki kadhaa za mvutano, afisa mkuu wa Hamas alinukuliwa akisema "haina masuala makubwa" na pendekezo hilo.

Inaripotiwa kuwa inahusisha kauli mpya juu ya kurejesha utulivu kwa maana ya kukidhi matakwa ya Hamas ya kusitisha mapigano ya kudumu.

Serikali ya Israel inakabiliwa na shinikizo kubwa kutoka kwa washirika wake wa kimataifa na familia za mateka kuafikia makubaliano.

MY TAKE
kumbe HAMAS bado wananguvu? kibur hichi cha HAMAS ya kukataa suluhu na vita vya nchi 5 dhidi yake kimetokeawapi?

Israel ilianzisha kampeni ya kijeshi ya kuiangamiza Hamas kujibu mashambulizi ya kundi hilo kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba, ambapo takriban watu 1,200 waliuawa na wengine 253 walichukuliwa mateka.

Zaidi ya watu 34,480 wameuawa huko Gaza tangu wakati huo, kulingana na wizara ya afya ya eneo hilo inayosimamiwa na Hamas.
 
Oh!!, hatuwezi Fanya majadiliano na Hamas!!!!
20230604_005828.jpg
 
Sio kusitisha mapigano.... Israel anataka mateka waachiwe ili asitishe kipigo cha mbwa koko
 
Huo ni mtego wa kijinga sana Israeli anartaka awe. anasurverry gaza mara kwa mara na kuuwa watu kwa kutumia. Dron siku akiona hatta wastu wanajenga nbyumba ailipue ili asema hamasi magaidi wanajenga industrial military base. Hamasi sio wajinga hivyo
 
Sio kusitisha mapigano.... Israel anataka mateka waachiwe ili asitishe kipigo cha mbwa koko
Hahaha mbona unabadilisha mada Israel alisema hatofanya makubaliano na hamas hila anataka kuwafuta lakini sasa kila siku anahangaika kutafuta makubaliano baada ya kuona mambo magumu maana north Hezbollah anapga kila siku hakukaliki huku red sea houthi kazuia meli hazipiti uchumi wote hakuna kitu sasa hv anaishi kutegemea misaada kama serikali za nchi za Africa na hamas kashagundua jamaa pumzi imekata basi na yy analinga tu kila mapendekezo yakipelekwa wanakataa wanataka marekebisho
 
Comment nyingi ni za Kigaidi... wenzenu wanaombea kautulivu japo kadogo kama kalivyo sasa magaidi wanafurahia wanajiona wameshinda vita... okay wacha tutizame picha.. wenzenu huko wameteka Chuo now wanaomba chakula waletewe ndani maana njaa imewakamata kama wa Gaza.. unakuwa jeuri as if mwili wako hauhitaji msosi
 
Back
Top Bottom