Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Uonevu,ubabe na udanganyifu pamoja na woga wa baadhi ya watu kwa binadamu wenzao ambavyo vimeoneshwa tangu mwanzo wa vita hivi hakuna shaka kutaleta mabadiliko ya maana kwa dunia nzima.
Kwa nje na kwa akili za kibinadamu kuna watu wanadhani Hamas na wenzao ndani ya Palestina wameshindwa.Kiundani vita hivi vitaondoa moja kwa moja fikra ya kumtegemea binadamu kutatua matatizo yako.Kila mmoja ataamua kujitetea kwa silaha aliyonayo mpaka mwisho wake bila kujali kiwango cha hasara atakachopata au kumsababishia adui yake.
Vitu visivyo vya kawaida ambavyo vimeonekana mubashara vimewafanya binadamu wasajili kwenye akili ushahidi mwingi.Si kawaida adui kuua mfululizo watoto na akinamama na kuwanyima chakula watu wengine bila adui huyo kushikwa mkono asiendelee na balaa hizo.
Kuanzia sasa hakuna atakayeamini kuwa kuna mataifa ya kidemokrasia ya kuamrisha mataifa mengine yafuate mifuomo yao.
Hakuna atakayekuwa tayari kutekeleza maazimio ya umoja wa mataifa wakati ameona maazimio yote yamekanyagwa na Israel na hakuna hatua iliyochukuliwa.
Hakutakuwa na taifa litakaloamini kuwa kuna jirani yake atamsaidia wakati wa shida anapovamiwa na adui yake.
Mlolongo wa mabadiliko wa tabia za binadamu huko mbele kutajenga zaidi imani ya kumtegemea Mwenyezi Mungu kuliko ilivyokuwa awali.
Kuna matukio chanya ambayo mpaka sasa hayajatokea lakini haitachukua muda mrefu sana yataonekana.Kuna mabalaa yatazikumba nchi ambazo zimeachia uonevu uendelee mbele ya macho yao mpaka zitadhoofika na hatimae tawala zao kuchukuliwa na watu waliokuwa hawakutegemewa kabisa .
Mfumo wa mapinduzi na kujiamini kupambana na wababe ambao umeonekana nchi za Afrika Magharibi utakuwa nidio mtindo wa nchi nyingi ambazo zilikuwa chini ya ukandamizaji wa mabeberu na wanayonyaji wa dunia.
Mwisho wa yote harakati za kuikomboa Palestina na kupomoroka kwa Israel zitapata kasi kutoka mikono ambayo haikufikiriwa kabisa.
Popote vita vya Gaza vitakapoishia basi Israel hatoweza kuitawala nchi pamoja na maeneo ya wapalestina na hatopata tena nguvu za kupambana na wapinzani wengine walio jirani naye kama ilivyokuwa mwanzoni.
Baadhi ya matukio chanya yaliyoanza kuonekana katika ukombozi wa kifikra ni kutambuliwa kwa taifa la Palestina na mataifa mengi japo wanajua mipaka ya taifa hilo imeshavurugwa na Israel.