Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Kwa ufundi na subira za hali ya juu Hamas wameweza kuhimili kipigo kizito cha Israel na washirika wake mpaka umefika mwaka mmoja hapo Septema 7.
Uzito wa vita hivyo umeonekana na kila upande ambapo mpaka sasa kikwazo kikubwa ni waziri mkuu wa Israel,Benjamin Netanyahu ambaye anaona aibu kusitisha vita bila kufikiwa malengo aliyojiwekea na kuyatangaza mwanzoni mwa vita.
Kwa bahati mbaya Marekani imekuwa na sera za kumuendekeza waziri mkuu huyo bila kuona mbele kwamba maslahi anayoyafikiria Netanyahu itakuwa ni kuitumbukiza Marekani kwenye balaa kubwa.Unaweza ukauona msongo wa mawazo wa Marekani unapowasikilizawagombea uraisi wa nchi hiyo utakaofanyika mwezi Novemba mwaka huu.
Kila mmoja kati ya wagombea hao anajaribu kumpaka matope mwenzake kwamba si rafiki wa Israel. Hapo juzi Truma amesema akichaguliwa Kamalla Harris basi Israel itafutika.
Waziri wa Ulinzi wa Israel mwenyewe Yoav Gallant,mara kadhaa amekuwa akikosana na Netanyahu hadharani akiunga mkono kufikia makubaliano na Hamas akisema makubaliano hayo yataitua mzigo mkubwa nchi yake ya kiusalama kwenye mipaka yake yote.
Kwa upande wake Netanyahu amekuwa na tamaa za fisi kufikiria kila siku kwamba ataua kiongozi wa Hamas ili awatangazie wafuasi na wafadhili wake kwamba amepata mafanikio.Kwa kukimbilia huko ametangaza kifo cha Mohammed Deif ambaye mpaka leo hakuna uthibitisho wa kifo hicho.