Vita vya Kagera 1979: Kwanini Jeshi letu lilipitia mipaka ya Sudan badala ya kukatiza hapo kati kufika Kampala?


Askari wa Msumbiji waliokuwa wakitusaidia kupigana na Amini walifanya kazi kubwa sana kwenye kuungurumisha yale Ma BM 21 (Saba saba). Wale walikuwa hawalali ni kazi kazi
 
Mzee asante Kwa darasa nashauri ungeandika Uzi kuhusu Hii Vita ya Kagera ili tujifunze zaidi
 
Naomba nakala mwanajamvini
 
KUNA VITOTO VIJINGA SANA HUMU. SASA ALIYEKUWA VITANI ANAELEZA HALAFU KITOTO KILICHOVAA PAMPASI KINAJIFANYA KIJUAJI. HALAFU VITOTO VYA KIUME VISHOGA NDIO VINADAI VITA HAIKUWA NA UMUHIMU. UNAJUA HAVIJAWAHI KUCHUKULIWA DEMU. MWANAUME ALIYEPORWA DEMU WAKE NDIYE ANAJUA UMUHIMU WA KUMPAMBANIA. SASA VISHOGA HUWA HAVIPAMBANI NI VILAINI KWA KWELI.
MIMI NILKUWA JESHINI. KAZI YANGU ILIKUWA KUTAWANYA BISCUITS. ILE VITA WEWE HADITHIWA TU. WAKATI FULANI TULIKUWA TUNASHAMBULIWA LAKINI HATUKUWA TUNAJUA KUWA INFORMER ALIKUWA NI KABIBI KIZEE KAMOJA KANAJIFANYA KANAOKOTA KUNI. IDD AMIN ALIKUWA AMEJIPANGA KILA MAHALI. LAKINI TULIMCHARAZA MBAYA KABISA. MZEE KICHUGUU HEBU ENDELEA KUVIFUNDISHA HISTORIA HIVI VISHABIKI VYA FERGARSON (SIO MANJESTA)
 
Askari wa Msumbiji waliokuwa wakitusaidia kupigana na Amini walifanya kazi kubwa sana kwenye kuungurumisha yale Ma BM 21 (Saba saba). Wale walikuwa hawalali ni kazi kazi
Mwaka 1978 Msumbiji ilikuwa na miaka minne au mitano tu ya uhuru na ilikuwa bado inaitegemea sana sana Tanzania kiulilinzi katika kupambana na uvamizi kutoka Rhodesia na South Afrika. Kulikuwa na askari wengi wa Tanzania waliokuwa wakiisadia Serikali ya Samora dhidi ya mashambulizi hayo, na vile vile katika kufundisha jeshi lake. Msumbiji hawakuwa na jeshi la kuja kusaidia Tanzania hata la mtu mmoja tu.
 

Usikatae Kichuguu, Msumbiji walileta Askari wao kwetu kutusaidia vita vya Kagera na walikuja na uzoefu mkubwa wa uwanja wa mapambano, hiyo siyo siri mbona, ni fact
 
Usikatae Kichuguu, Msumbiji walileta Askari wao kwetu kutusaidia vita vya Kagera na walikuja na uzoefu mkubwa wa uwanja wa mapambano, hiyo siyo siri mbona, ni fact
Hii siyo kweli; ni hadithi za kufikirika tu. Msumbiji yenyewe bado ilikuwa inatutegea sisi wakati huo. Mwulize Echolima aliyekuwa msituni huko frontline akupe account ya moja kwa moja, siyo hizi stori za kuambiwa tu.
 
Usikatae Kichuguu, Msumbiji walileta Askari wao kwetu kutusaidia vita vya Kagera na walikuja na uzoefu mkubwa wa uwanja wa mapambano, hiyo siyo siri mbona, ni fact
Ninavyojua BM-21 Grad tuliipata kutoka USSR na naamini tulinunua, kama tungepewa taarifa zingekuwepo.
Vipi zile ndege za Mig-21 tulizopewa na Warusi na nyingine tulizonunua. Na zile zilizokamatwa pale kambi fulani ya Uganda ilipotekwa.
 
Hii siyo kweli; ni hadithi za kufikirika tu. Msumbiji yenyewe bado ilikuwa inatutegea sisi wakati huo. Mwulize Echolima aliyekuwa msituni huko frontline akupe account ya moja kwa moja, siyo hizi stori za kuambiwa tu.

Soma hii page kuhusu Ushiriki wa Msumbiji katika ile vita kutusaidia.

Msumbiji walileta Batallion nzima na zaidi, Takribani askari 800 kutusaidia

Invasion of Kagera - Wikipedia

Nimeongea na Askari waliokuwepo katika hiyo vita wamekiri uwepo wa askari wa Msumbiji

Na si Askari wa Msumbiji tu waliotusaidia vilikuwepo pia vikosi vya waasi vya waganda vilivyokuwa na makazi nchini, vikundi tiifu kwa obote navyo vilikuwa vinashirikiana nasi bega kwa bega.

Hilo wala siyo siri, hata ukigoogle juu ya hili jambo liko wazi sana, cheki. kwa mfano kwenye hiyo link ya wikipedia niliyoweka wanasema hivi.

 
@Mlolongo [QUOTE]
Unaweza ukanipa straight fact (sio porojo) kwamba kwa nini immediately after Kagera War uchumi wa TZ ulishuka mpaka negative 3% (rejea mahindi ya Yanga kutoka Marekani na mchele wa Thailand)
Unaweza kutaja sababu moja plain (usipige story) kwamba kwa nini Nyerere baada ya kuona vita inamshinda, aliamuru Migambo Wote wa mitaani wapelekwe frontline vitani kupigana vita... Wanajeshi walikua hawatoshi?
[/QUOTE]
Duh mpaka hapo tu inaonesha Vita vya Kagera ulihadithiwa kuwa mgambo waliokotezwa mitaani ukiwa na maana Mgambo sio Askari wa Akiba na ndio Infantry wanaotumika
Ina maana ni Tanzania tu uchumi ulianguka kwa sababu tulitumia unga wa yanga?
Nilivyoshuhudia Tanzania hatukupoteza askari wetu katika vita hivyo na wewe umehesabu siku zile Daraja la Kyaka lilipobomolewa
Tafuta uzi wa Echolima achana na hadithi za mitaani
 
Hiyo uliyoquote imeshaletwa hapa na tumeishaijadili; aliyeiandika hajui alichokuwa anaandika. Tanzania ilikuwa na batallion mbili kule Msumbiji ambazo siyo tu silisaidia katika vita ya Uhuru wa Msumbiji bali pia ndizo zilikuwa zinafundisha jeshi la Msumbiji baada ya uhuru; ndiyo maana mpaka leo bado jeshi letu linatoa amedali za Msumbiji kwa askari wake. Angalia nishani hizi:






Wakati wa vita sehemu kubwa ya askari wetu waliokuwa Msumbuji walirudishwa nyumbani kwa ajili ya vita hiyo. Haiwezekani Msumbiji walete Batallion nzima vitani halafu eti wote warudi nyumbani salama bila hata majeruhi hata mmoja, na wala hata batallion commander wao hajulikani, na vile vile haijulikani ilikuwa ni Batallion chini ya Brigade gani. Vita siyo swala la kukusanya wapiganaji tu, ni swala la uongozi wa kivita; makamanda ndio wanaomata sana kuliko idadi ya wapiganaji- huyu mwandishi wako hajasema ni nani alikuwa kamanda wa hao askari wa Musumbiji. Makamanda wote waliooongoza vita ile kwenye theater wanajulikana wote na vikosi walivyoongoza kuanzia mameja Generali walioongoza Divisions, Mabrigedia walioongoza Brigades na makanali na maluteni kanali wote waliiongoza batallions majina yao yanajulika wazi wazi na wala hakuna hakuna kamanda aliyetoka Msumbiji.

Hakuna kumbukumbuku zozote huko msumbiji zinazoonyesha askari wao kufa au kujeruhiwa kwenye vita ya Kagera. Msumbiji lilikuwa bado ni taifa changa sana lenye umri wa miaka minne tu tangu uhuru, usingeweza kulilinganisha na jeshi la Tanzania ambalo lilikuwa na umri wa miaka 15 na lilishapigana siyo tu huko huko Msumbiji bali pia Rhodesia.

Usifuate hizo habari za kupotosha; tuliokuwa karibu na vita ile tunakuambia ukweli. Mimi nilikuwa Brigade ya Magharibi na nilikuwa kitengo cha mawasiliano ambapo nilikuwa najua yote yaliyokuwa yanaendelea vitani. Tanzania jeshi letu lilipanuka haraka sana baada ya kuunganishwa Polisi, Magereza JKT na Mgambo na kuwa kubwa sana kiasi kuwa kuna askari wetu wengi hawakupelekwa kwa sababu idadi tuliyokuwa nayo huko frontline ilikuwa inatosha sana. Kwa hali hiyo hatukuhitaji masaada wa kutoka nje kabisa. Halafu hata hivyo diplomatically Nyerere asingekubali msaada huo kwa sababu alikuwa anataka OAU imkemee Amin, msaada huo wa kutoka nchi nyingine ungetia doa kabisa katika dhima yake ya kuonyesha kuwa Tanzania imevamamiwa na inajitetetea.
 
Well-Done Kichuguu Kama mwenye kuelewa ataelewa!!!!!
 

Information kuhusu uwepo wa askari wa msumbiji katika kutusaidia kupigana na Amini zipo kila mahali labda wewe ulikuwa huzijui, au hutaki tu kuzijua lakini fanya utafiti wako kwa kuuliza askari walikuwepo kwenye mapambano ambao walikuwa embedded nao watakueleza.

Kuhusu wewe kutojua wangapi walikufa na kiongozi wao ni nani hiyo haifanyi kuwa hawakuwepo.
Kwanza lazima ujue Nyerere hakupenda ijulikane kuwa tunasaidiwa na nchi yoyote huenda ndo maana hizo info ziliwekwa low profile.
But hata machapisho mbalimbali ya masuala ya conflicts zimeandikwa, usipokuwa mvivu ukizitafuta utauona tu huu ukweli.

Kuhusu Taifa changa kusaidia nchi nyingine hiyo siyo hoja.

Tanganyika ilikuwa Taifa Changa lakini ilipeleka askari kuisaidia Zanzibar kulinda mapinduzi yake mwaka 1964.

Uchanga siyo hoja, kinachomatter ni uzoefu wa mapambano na Msumbiji walikuwa na uzoefu mkubwa wa mapambano baada ya kupigana muda mrefu na wareno, Uzoefu wao ulitusaidia kumpiga Amini
 
Sasa wewe ulitegemea nchi iingie vitani halafu baada ya vita maisha yawe kama Ulaya. Ebu nenda Libya sasa hivi ukaone, hutaamini kama ni nchi iliyokuwa bora kipindi cha Ghadafi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…