Vita vya Kagera 1979: Kwanini Jeshi letu lilipitia mipaka ya Sudan badala ya kukatiza hapo kati kufika Kampala?

Kiuhalisia ile vita haikuwa na Ulazima

Watanzania walikufa wengi sana kuliko Waganda.

Ukikutana na wanaoijua ile vita vizuri watakueleza.
Kwanini mkuu?
 
Kuna watu wanaamini kuwa Tanzania ni nchi dhaifu sana; akili zakiwehu kabisa. Mkuu wa sasa wa jeshi la Uganda amesoma Monduli.

Sidhani kama ni makosa yao! Maybe ni vile wanashuhudia huo udhaifu wa jeshi “letu ?”
Imani yangu, mtoto hujifunza kwa Baba!

Heshima yako babu!
 

Ili silaha ifanye kazi yake haswaa bila hashki ni vyema impate mjuzi asilia (an experienced personel)kutimiza yanayohitajika!!

Kweli babu shule yako madhubuti!! Ubarikiwe!
 
Watanzania wafe wengi na washinde vita?hivi huo ujinga mnasomeaga wapi

Inawezekana!

Ukiumizwa sana (kimwili ama kiroho)mwisho wa siku “ubongo “ unakupa namna ya kujinasua! Ila uthubutu ndio dhamira njema zaidi!!

Heko kwa Mwalimu Nyerere kuwa the best “Motivator “ of all times!! Alijua namna ya kuziamsha ‘hari!’
 

Ila pia yawezekana Kanali Kotta nae pia ni “mwanafunzi” wao “hao”!

Najaribu tu kuelewa! [emoji120]
 

Kuna tatizo kati ya Tz na Msumbiji or may be I’m hallucinating mpaka leo!

Ila.....

Hapo kwenye hizo battalions, kuna uwezekano wowote tukapata “sensa “ ya watu/watanzania hasa upande wa vijana?! Kwamba waliojitolea (Askari wa ziada) ni wangapi na namba halisi ya vijana uraiani enzi hizo ni ngapi??
 
Ila pia yawezekana Kanali Kotta nae pia ni “mwanafunzi” wao “hao”!

Najaribu tu kuelewa! [emoji120]
Hapana; Kanali Kotta alikuwa amesomea Kanada, Israel na Urusi kabla hata Msumbiji haijapata uhuru wakati bado tuna uhusiano na Israel.
 
Sizijui ila rekodi hizo zipo, kwa sababu kulikuwa na utaratibu nadhani wa kila kijiji au kila kata kutoa idadi kadhaa ya vijana kutoka kwenye jeshi lao la Mgambo. Lakini rekodi hizo ukizitafuta jeshini utazipta; hazikufichwa; na hata list ya askari waliokufa vitani inajulikana.
 
Allah amlaze mahala pema peponi ndugu yetu Idi amin, bila kumsahau Ndugu yetu na kipenzi cha waafrika kwa ujumla Muammar Gaddafi, Allah amlaze mahala pema peponi!
 
Wamemaliza kulipa hilo deni,wamelipa kw miaka 35
 
hii habari ya uchumi haihusiani na wanajeshi kufa vitani. Unadhani wale mgambo walienda front line?!? jeshi linapokuwa vitani kuna kazi nyingi sana zinaendelea huku nyuma
 
Kuna mambo mengi huyajui kwa uchambuzi wa intelijensia ya kijeshi kwa wakati huo.

Kwanza kabisa unapaswa kuijua hulka ya adui wetu wa kipindi hicho(Amini), ndio maana Amin aliamua kukimbia baada ya majeshi yetu kuamua kumsaka huko Uganda.

Kwa kifupi ili kudumisha amani kwenye mipaka ya Tz na Uganda ilikuwa ni lazima kumuondoa Amin kwenye kiti na ikiwezekana kumweka mtu wetu

Tungebweteka mpakani ilikuwa na maana KUMPA AMIN MUDA WA KUJIANDAA UPYA NA KUPANGA MIKAKATI YA KUISHAMBULIA TENA. (Kumbuka malengo yake ya kutwaa kagera yaliambatana na interests za washirika wake ili kupata eneo la Minziro kwa kilimo cha umwagiliaji) maana yake kulikuwa na uwezekano wa kuendelea na vita kwa muda mrefu zaidi.

Kumbuka kabla ya vita hii hakuna kitu chochote Tanzania tulikuwa tunahitaji kutoka Uganda ila ni huyu nduli ndiye aliyekuwa mkorofi.

VIJANA KITU AMBACHO HAMJUI AMIN alikuwa na kiu ya kuishambulia Tz kwa muda mrefu kabla ya 1978 (jambo hili wengi hawalijui) nadhani mwaka 1972/74/76(sikumbuki vizuri) Amini aliishambulia Bukoba kwa mabomu ya angani, ila Mzee Nyerere alitumia busara kumaliza huo mgogoro.
 
Kazi kumuelimisha RAIA daraja la tatu
 
Mkuu, sisi vijana tuna mengi sana ya kujifunza kupitia wazalendo kama ninyi.

Ninapenda sana fafanuzi zako katika mada hii.
 
Upo nje ya mada mkuu.

Anzisha uzi wako wa mambo ya Zanzibar kisha uandike haya alafu sisi tutakuja kuchangia huko.
 
Sorry sisemi mimi ni Mapadri wa kanisa lake ndio walioandika vitabu na wakayasema hayo au na wewe huelewi nimeandika kitu gani ??? Rejea post nilizojibu
Chizi hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…