Vita vya Kagera: Historia yangu - Sehemu ya kwanza

Kwenye sehemu ya pili nitajikita zaidi kwenye medani za kivita vituko na mikasa kwenye uwanja wa vita vya KAGERA.

Asante MKuu kwa rejea hii ya vita vya Kagera.

Nakuomba sana fanya jinsi uandike kitabu kabisa ili kutunza kumbukumbu nzuri kuhusu vita hii. Hii itahamasisha uzalendo katika kizazi hiki cha ufisadi na sembe
 
Wiki iliyopita ningelitoa sehemu ya pili lakini baada ya kutoka safari nilishauriwa na jamaa wengi sana kuwa niongee na MAKAMANDA na WAPIGANAJI wengine waliokuwa mstari wa mbele na kutoka vikosi mbali-mbali vilivyoshiriki vita hiyo,maana sehemu ya kwanza nilikuwa nazungumzia tu hasa nilikopita mimi na kikosi changu cha MMJ,Lakini kwa sasa nita-cover karibu uwanja wote wa vita na hii itakuwa nzuri kuliko kusikia toka katika kikosi kimoja tu na kazi hiyo nimeshaianza ya kuongea na MAKAMANDA mbali-mbali walioshiriki ingawaje wengi wao Hatuko nao Duniani,lakini nitaowapata watatosha kutuletea habari nzuri na za UHAKIKA.Kuhusu kitabu kuna watu toka hapa GT nitawashirikisha kutengeneza kitabu hicho.
 
Echolima,

..kuna kitabu nilikisoma inaonekana kama Brig.Kitete na Maj.Gen.Kiwelu ndiyo walikuwa watu wa mipango ya kivita.

..hapo juu naona unaelekeza kwamba mtu wa mipango alikuwa ni Col.Lupogo, na Maj.Gen.Kiwelu na vijana walikuwa mstari wa mbele ndiyo waliorusha risasi za kwanza kumkabili adui.

..pia kuna taarifa za Col.Lupogo kwenda mstari wa mbele, na wakati fulani kubadilishana nafasi na Brig.Kimario.

..ushauri wangu ni kwamba utafute vitabu vyote vinavyohusiana na vita vya Kagera, halafu mkae na hao makamanda, maofisa, na wapiganaji, ili muweke mambo sawa.
 
Last edited by a moderator:
Ndiyo ni Ushauri mzuri sana JOKAKUU ninachotaka sana ni kupata coverage nzima vilevile vitabu hivyo ni mhimu kuwepo na kuvihakiki maana tunao watu waliopigana vita hiyo na itakuwa tumeweka HISTORIA vizuri hilo ndugu nalifanyia kazi kwa karibu sana.
 
haaaahaa teh teh! Wenyewe wanajihita waindi koko sijui wanagamahanisha nn

Hawa ndio yale matokeo ya boss wa kihindi kucheza faulo na mjakazi wa ndani!(mama juma)!!

Halafu anatoka mtoto mweusi lkn nywele laini kama ana utapia mlo!

Teh teh teh teh!

We wapi umeskia mtanzania safi anaitwa Somji Juma !!!

teh teh teh teh!!
 
Last edited by a moderator:
Echolima,

..kuna kitabu nilikisoma inaonekana kama Brig.Kitete na Maj.Gen.Kiwelu ndiyo walikuwa watu wa mipango ya kivita.

..hapo juu naona unaelekeza kwamba mtu wa mipango alikuwa ni Col.Lupogo, na Maj.Gen.Kiwelu na vijana walikuwa mstari wa mbele ndiyo waliorusha risasi za kwanza kumkabili adui.

..pia kuna taarifa za Col.Lupogo kwenda mstari wa mbele, na wakati fulani kubadilishana nafasi na Brig.Kimario.

..ushauri wangu ni kwamba utafute vitabu vyote vinavyohusiana na vita vya Kagera, halafu mkae na hao makamanda, maofisa, na wapiganaji, ili muweke mambo sawa.

Uko correct kabisa kuhusu umahiri wa Col Kitete katika battlefield tactics.

Il niinajua kuwa battlefiled tactics za vita ile zilipangwa na Col Lupogo, ingawa Col Kitete pia alikuwa ni mmoja wa wataalamu wakubwa sana wa vita wakati huo. Sikumbuki kuwa yeye alishiriki vipi, ila mwaka ule 1978 mara tu baada ya Rais Nyerere kutangaza vita, taarifa za kijeshi tulizokuwa tunapata kwenye institutions za kijeshi wakati huo zilikuwa zinaonyesha kuwa ni Col Lupogo ndiye aliyekuwa amebebeshwa jukumu la kupanga mipango ya vita ile. Inawezekana kuwa Kitete na Lupogo walifanya pamoja au alianza Lupogo akamalizia Kitete, ila jina la kwanza kabisa lilikuwa ni la Lupogo.
 
Wiki iliyopita ningelitoa sehemu ya pili lakini baada ya kutoka safari nilishauriwa na jamaa wengi sana kuwa niongee na MAKAMANDA na WAPIGANAJI wengine waliokuwa mstari wa mbele na kutoka vikosi mbali-mbali vilivyoshiriki vita hiyo,maana sehemu ya kwanza nilikuwa nazungumzia tu hasa nilikopita mimi na kikosi changu cha MMJ,Lakini kwa sasa nita-cover karibu uwanja wote wa vita na hii itakuwa nzuri kuliko kusikia toka katika kikosi kimoja tu na kazi hiyo nimeshaianza ya kuongea na MAKAMANDA mbali-mbali walioshiriki ingawaje wengi wao Hatuko nao Duniani,lakini nitaowapata watatosha kutuletea habari nzuri na za UHAKIKA.Kuhusu kitabu kuna watu toka hapa GT nitawashirikisha kutengeneza kitabu hicho.

Niletee drafts nitawasaidia kufanyia editing na typesetting. Nilikuwa shabiki sana wa vita ile wakati nikiwa faru brigade miaka hiyo ingawa binafsi sikupelekwa frontline.
 
Mkuu hebu hii history andika kitabu,najua kweli sio mwandishi omba msaada kwa waandishi wakusaidie,nadhani watu kama nyinyi ni watu muhimu katika history ya nchi yetu,
Watoto wetu leo hata mashuleni sidhani kama wanafundishwa habari za vita ya kagera wala kujua tu majina ya mashujaa wetu,
Khofu yangu miaka 20 ijayo nchi itakuwa imepoteza history yake yote,

Hata kwenye syllabus haipo mkuu,nimeipenda sana hapa nasubiri atoe matoleo yote matatu niyaunganishe kwa kumbukumbu bora kabisa kwa familia yangu na vizazi kijacho.
Ila kama wanajamvi walivyo shauri yafaa atoe kitabu,kwanini iwe wazungu tu?
 
Uko correct kabisa kuhusu umahiri wa Col Kitete katika battlefield tactics.

Il niinajua kuwa battlefiled tactics za vita ile zilipangwa na Col Lupogo, ingawa Col Kitete pia alikuwa ni mmoja wa wataalamu wakubwa sana wa vita wakati huo. Sikumbuki kuwa yeye alishiriki vipi, ila mwaka ule 1978 mara tu baada ya Rais Nyerere kutangaza vita, taarifa za kijeshi tulizokuwa tunapata kwenye institutions za kijeshi wakati huo zilikuwa zinaonyesha kuwa ni Col Lupogo ndiye aliyekuwa amebebeshwa jukumu la kupanga mipango ya vita ile. Inawezekana kuwa Kitete na Lupogo walifanya pamoja au alianza Lupogo akamalizia Kitete, ila jina la kwanza kabisa lilikuwa ni la Lupogo.
Kichuguu,

..ushauri wangu ni kwamba iandikwe historia ya ujumla ya vita vya Kagera.

..vilevile iandikwe historia ya specific battles ambazo zilikuwa muhimu ktk mwenendo mzima wa vita ya Kagera/Uganda. Kwa mfano, the battle of Lukaya, kuanzia planning mpaka mwisho wake inaweza pia kufanywa ni kitabu au documentary film.

NB:

..kwenye kitabu cha Vita vya Kagera kilichoandikwa na Joseph Ngatuni, Albert Kigadye, na Muhammad Ghahae, wanamuelezea Colonel.Kitete a.k.a "kamanda supersonic" kama mkuu wa shughuli za utendaji kivita, mara nyingine kama mkuu wa mipango ya uamrishaji kivita.

..Pia kwenye kitabu hicho wametajwa makamanda wengine ambao hawavumi sana kama Colonel.Tumbi a.k.a "kamanda radi" ambaye alikuwa ni kamanda wa mizinga ya masafa marefu. Yupo Brigadier.Rowland Makunda a.k.a "kamanda torpedo." Lt.Colonel.Rajabu ambaye alipewa jukuma la kujenga daraja la muda la mto Kagera. Halafu yupo Brigadier.Martin Mwakalindile ambaye anatajwa kuwa kamanda mkuu wa mafunzo wakati wa vita ya Kagera.

cc Echolima, gobore, Nyenyere
 
Mkuu umenena jambo la msingi kabisa. Kuna wakati nilikuwa UK nikataka kufanya research juu ya vita vya Kagera. Nilishindwa kabisa kwa sababu hakukuwa na kumbukumbu zozote za vita hivyo, licha ya waingereza kuwa na kumbukumbu za vita mbalimbali duniani. Kwa scale ya vita ile si sahihi kabisa kutokuwamo katika kumbukumbu za vita duniani.

Niliporudi bongo nikaamua kufuatilia sababu hasa ya kutokuwa na maandiko ya kutosha. Jibu nililopata lilinikatisha tamaa kabisa. Eti tactics zilizotumika hazielezeki kwa vile makamanda wengi walitumia uchawi. Sijui ukweli hasa kuhusu hili.

All in all ni muhimu kuandika kumbukumbu hizi muhimu.
 
Wewe mwenyewe ulikuwa kwenye battlefield kwa hiyo usikatishwe tamaa na hayo maoni (japo na mimi niliambiwa habari za uchawi wakati ule wa vita na baadhi ya watu).

Nasubiria part two kwa hamu. Siye wa dotcom tuna mengi ya kujifunza toka kwenu.
 
Mkuu umenena jambo la msingi kabisa. Kuna wakati nilikuwa UK nikataka kufanya research juu ya vita vya Kagera. Nilishindwa kabisa kwa sababu hakukuwa na kumbukumbu zozote za vita hivyo, licha ya waingereza kuwa na kumbukumbu za vita mbalimbali duniani. Kwa scale ya vita ile si sahihi kabisa kutokuwamo katika kumbukumbu za vita duniani.

Niliporudi bongo nikaamua kufuatilia sababu hasa ya kutokuwa na maandiko ya kutosha. Jibu nililopata lilinikatisha tamaa kabisa. Eti tactics zilizotumika hazielezeki kwa vile makamanda wengi walitumia uchawi. Sijui ukweli hasa kuhusu hili.

All in all ni muhimu kuandika kumbukumbu hizi muhimu.
Ama kweli penye wengi hapakosi jambo si kweli kuwa Makamanda wengi walikuwa wanatumia UCHAWI mimi binafsi siamini mambo hayo,Mfano mmoja ni kuwa mimi na kikosi chetu cha Makao Makuu watu wengi walikuwa wanaamini sisi tunatumia UCHAWI hasa kwa sababu sisi Hatujawahi kurudishwa nyuma,Hatujawahi kuingia kwenye AMBUSH(Mtego wa kuvizia)wa adui na hatujawahi kushambuliwa kwenye Ngome yetu toka tunaanza Vita mpaka kumaliza hii iliwafanya watu wengi toka vikosi vingine waamini kuwa sisi tulikuwa tunatumia UCHAWI kitu ambacho si kweli kabisa bali tu ilikuwa Bahati yetu vilevile INTELIJENSIA yetu ilikuwa nzuri sana watu waliokuwa wanapangwa kwenda tafuta habari za wapi alipo adui walikuwa wanafanya kwa Usahihi kabisa na wanarudisha habari hivyo habari hizo zilikuwa zinatusaidia sana kufanya Maamuzi ya namna gani tufanye,Mfano tunaambiwa Adui yuko kilomita moja toka ngome yetu hivyo tunajua kabisa kuwa wakati wowote adui anaweza kutushambulia hivyo tunaweza kufanya Option yoyote aidha kuhama tulipo au kufanya counter-attack Shambulio la kustukiza kwa adui na hii ndiyo ilikuwa salama yetu.
Mfano wa pili nilikuwa na kijana mmoja yeye alikuwa hataki kabisa kulala au kuingia kwenye HANDAKI yeye alikuwa tayari kuchimba lakini kulitumia alikuwa hataki unaweza kumwambia aingie lakini ukitoka tu naye anatoka analala nje kitu ambacho ilikuwa ni kuhatarisha maisha yake pindi kama tungelengwa na mashambulizi ya adui lakini tulimaliza Vita naye salama bila shida huyu naye watu walikuwa wanasema anatumia UCHAWI eti tu kwa sababu aliweza kumaliza vita nzima bila kutumia HANDAKI,
Kitu kingine askari wengine walikuwa wanavitumia vipaji vyao vizuri kwenye eneo lao hivyo walikuwa wanaonekana kama wanatumia UCHAWI wakati sivyo kabisa kuna wengine waliweza kutumia hisia kali za kijeshi na kugundua kuwa leo usiku tunaweza kuvamiwa hapa na kweli wakati mwingine inatokea kwa watu wengine wanaweza fikiria ni UCHAWI wakati sivyo kabisa.Mimi siwezi wasemea wengine labda wengine walikuwa wanatumia UCHAWI lakini kwa ujumla UCHAWI kwenye vita Haupo kabisa kama ungekuwepo basi tusingepoteza watu namna hiyo tungetuma tu wachawi wachache wakamaliza kazi tukarudi salama,Kwa utafiti wangu Kukosa-Elimu kunasababisha watu wengi wakiona tu kitu kimefanywa vizuri na kwa Ujuzi wa hali ya juu Mtu anaamini ni UCHAWI hata kama utalenga shabaha yako vizuri na kupiga target yako sawa sawa wengine watakuambia unatumia Uchawi,Mimi siamini UCHAWI na sitakuja niamini UCHAWI.
 
umenifunza meng mzaz, nangojea sehemu ya pili kwa hamu. itatoka lini?

Inabidi sasa mumlipe afande japo kidogo!
Duhh wabongo kwa kupenda dezo!?!

We mtu kasota uganda kule! Sasa hivi kawaonjesha tu kidogo! Mnataka na part 2 bure! Lkn vitabu vya udaku mnanunua ma alfu!
Nimeona sapoti nyingi sana humu watu wanazompa afande! Lkn hakuna hata mbongo mmoja akatoa hata ushauri wa kumkatia chochote afande kama asante kwa kupigania nchi yenu!

Oovyoo!
Mtabaki tu!

Safi sana afande!
We ndio mwenyewe afande! Umenipa raha sana afande!
Lkn kitu kidogo!? Mnapeleka uwanja wa fisi!! Usiku!

Mhhhh! Acheni ubakhili nyie!
 
Back
Top Bottom