Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwenye sehemu ya pili nitajikita zaidi kwenye medani za kivita vituko na mikasa kwenye uwanja wa vita vya KAGERA.
Kweli kwenye msafara wa Mamba kenge nao wamo
haaaahaa teh teh! Wenyewe wanajihita waindi koko sijui wanagamahanisha nn
Kweli kwenye msafara wa Mamba kenge nao wamo
Echolima,
..kuna kitabu nilikisoma inaonekana kama Brig.Kitete na Maj.Gen.Kiwelu ndiyo walikuwa watu wa mipango ya kivita.
..hapo juu naona unaelekeza kwamba mtu wa mipango alikuwa ni Col.Lupogo, na Maj.Gen.Kiwelu na vijana walikuwa mstari wa mbele ndiyo waliorusha risasi za kwanza kumkabili adui.
..pia kuna taarifa za Col.Lupogo kwenda mstari wa mbele, na wakati fulani kubadilishana nafasi na Brig.Kimario.
..ushauri wangu ni kwamba utafute vitabu vyote vinavyohusiana na vita vya Kagera, halafu mkae na hao makamanda, maofisa, na wapiganaji, ili muweke mambo sawa.
Wiki iliyopita ningelitoa sehemu ya pili lakini baada ya kutoka safari nilishauriwa na jamaa wengi sana kuwa niongee na MAKAMANDA na WAPIGANAJI wengine waliokuwa mstari wa mbele na kutoka vikosi mbali-mbali vilivyoshiriki vita hiyo,maana sehemu ya kwanza nilikuwa nazungumzia tu hasa nilikopita mimi na kikosi changu cha MMJ,Lakini kwa sasa nita-cover karibu uwanja wote wa vita na hii itakuwa nzuri kuliko kusikia toka katika kikosi kimoja tu na kazi hiyo nimeshaianza ya kuongea na MAKAMANDA mbali-mbali walioshiriki ingawaje wengi wao Hatuko nao Duniani,lakini nitaowapata watatosha kutuletea habari nzuri na za UHAKIKA.Kuhusu kitabu kuna watu toka hapa GT nitawashirikisha kutengeneza kitabu hicho.
Mkuu hebu hii history andika kitabu,najua kweli sio mwandishi omba msaada kwa waandishi wakusaidie,nadhani watu kama nyinyi ni watu muhimu katika history ya nchi yetu,
Watoto wetu leo hata mashuleni sidhani kama wanafundishwa habari za vita ya kagera wala kujua tu majina ya mashujaa wetu,
Khofu yangu miaka 20 ijayo nchi itakuwa imepoteza history yake yote,
Kichuguu,Uko correct kabisa kuhusu umahiri wa Col Kitete katika battlefield tactics.
Il niinajua kuwa battlefiled tactics za vita ile zilipangwa na Col Lupogo, ingawa Col Kitete pia alikuwa ni mmoja wa wataalamu wakubwa sana wa vita wakati huo. Sikumbuki kuwa yeye alishiriki vipi, ila mwaka ule 1978 mara tu baada ya Rais Nyerere kutangaza vita, taarifa za kijeshi tulizokuwa tunapata kwenye institutions za kijeshi wakati huo zilikuwa zinaonyesha kuwa ni Col Lupogo ndiye aliyekuwa amebebeshwa jukumu la kupanga mipango ya vita ile. Inawezekana kuwa Kitete na Lupogo walifanya pamoja au alianza Lupogo akamalizia Kitete, ila jina la kwanza kabisa lilikuwa ni la Lupogo.
Kichuguu,
..ushauri wangu ni kwamba iandikwe historia ya ujumla ya vita vya Kagera.
..vilevile iandikwe historia ya specific battles ambazo zilikuwa muhimu ktk mwenendo mzima wa vita ya Kagera/Uganda. Kwa mfano, the battle of Lukaya, kuanzia planning mpaka mwisho wake inaweza pia kufanywa ni kitabu au documentary film.
NB:
..kwenye kitabu cha Vita vya Kagera kilichoandikwa na Joseph Ngatuni, Albert Kigadye, na Muhammad Ghahae, wanamuelezea Colonel.Kitete a.k.a "kamanda supersonic" kama mkuu wa shughuli za utendaji kivita, mara nyingine kama mkuu wa mipango ya uamrishaji kivita.
..Pia kwenye kitabu hicho wametajwa makamanda wengine ambao hawavumi sana kama Colonel.Tumbi a.k.a "kamanda radi" ambaye alikuwa ni kamanda wa mizinga ya masafa marefu. Yupo Brigadier.Rowland Makunda a.k.a "kamanda torpedo." Lt.Colonel.Rajabu ambaye alipewa jukuma la kujenga daraja la muda la mto Kagera. Halafu yupo Brigadier.Martin Mwakalindile ambaye anatajwa kuwa kamanda mkuu wa mafunzo wakati wa vita ya Kagera.
cc Echolima, gobore, Nyenyere
Mkuu umenena jambo la msingi kabisa. Kuna wakati nilikuwa UK nikataka kufanya research juu ya vita vya Kagera. Nilishindwa kabisa kwa sababu hakukuwa na kumbukumbu zozote za vita hivyo, licha ya waingereza kuwa na kumbukumbu za vita mbalimbali duniani. Kwa scale ya vita ile si sahihi kabisa kutokuwamo katika kumbukumbu za vita duniani.
Niliporudi bongo nikaamua kufuatilia sababu hasa ya kutokuwa na maandiko ya kutosha. Jibu nililopata lilinikatisha tamaa kabisa. Eti tactics zilizotumika hazielezeki kwa vile makamanda wengi walitumia uchawi. Sijui ukweli hasa kuhusu hili.
All in all ni muhimu kuandika kumbukumbu hizi muhimu.
Ama kweli penye wengi hapakosi jambo si kweli kuwa Makamanda wengi walikuwa wanatumia UCHAWI mimi binafsi siamini mambo hayo,Mfano mmoja ni kuwa mimi na kikosi chetu cha Makao Makuu watu wengi walikuwa wanaamini sisi tunatumia UCHAWI hasa kwa sababu sisi Hatujawahi kurudishwa nyuma,Hatujawahi kuingia kwenye AMBUSH(Mtego wa kuvizia)wa adui na hatujawahi kushambuliwa kwenye Ngome yetu toka tunaanza Vita mpaka kumaliza hii iliwafanya watu wengi toka vikosi vingine waamini kuwa sisi tulikuwa tunatumia UCHAWI kitu ambacho si kweli kabisa bali tu ilikuwa Bahati yetu vilevile INTELIJENSIA yetu ilikuwa nzuri sana watu waliokuwa wanapangwa kwenda tafuta habari za wapi alipo adui walikuwa wanafanya kwa Usahihi kabisa na wanarudisha habari hivyo habari hizo zilikuwa zinatusaidia sana kufanya Maamuzi ya namna gani tufanye,Mfano tunaambiwa Adui yuko kilomita moja toka ngome yetu hivyo tunajua kabisa kuwa wakati wowote adui anaweza kutushambulia hivyo tunaweza kufanya Option yoyote aidha kuhama tulipo au kufanya counter-attack Shambulio la kustukiza kwa adui na hii ndiyo ilikuwa salama yetu.Mkuu umenena jambo la msingi kabisa. Kuna wakati nilikuwa UK nikataka kufanya research juu ya vita vya Kagera. Nilishindwa kabisa kwa sababu hakukuwa na kumbukumbu zozote za vita hivyo, licha ya waingereza kuwa na kumbukumbu za vita mbalimbali duniani. Kwa scale ya vita ile si sahihi kabisa kutokuwamo katika kumbukumbu za vita duniani.
Niliporudi bongo nikaamua kufuatilia sababu hasa ya kutokuwa na maandiko ya kutosha. Jibu nililopata lilinikatisha tamaa kabisa. Eti tactics zilizotumika hazielezeki kwa vile makamanda wengi walitumia uchawi. Sijui ukweli hasa kuhusu hili.
All in all ni muhimu kuandika kumbukumbu hizi muhimu.
umenifunza meng mzaz, nangojea sehemu ya pili kwa hamu. itatoka lini?