Vita vya Kagera: Historia yangu - Sehemu ya kwanza

Vita vya Kagera: Historia yangu - Sehemu ya kwanza

Kamanda yan kwa maelezo haya tukirekodi movie itauza hata kuliko ile tuliyoizoea. Kamilisha kitabu chako mapema na uwatafute wafadhili kutoka nje ya nchi wanaweza kudhamini utengenezaji wa Movie ya kagera part II.
 
Bw Echolima! Ni vyema ukaandika kitabu kuhusu vita ya Kagera kwa manufaa yetu sisi na vizazi vijavyo. Una kipaji kizuri cha usimulizi. Asante.
 
Poleni sana aisee; naomba hizi historia ziandikwe vizuri na tuijue nchi yetu vizuri, tupate picha halisi ya mchango wa nchi yetu huko uganda, zimbabwe, namibia, DRC, msumbiji na S.A. Im proud of my country.
 
Kuna jamaa wa Uganda namfahamu naye alikuwa uwanja wa mapambano, anasema kikosi chake kilikua chini ya Kanali Moyo. Inavyoonekana kulikua na makundi tofauti ya wanajeshi wa Uganda waliokuwa begakwabega
na majeshi yetu. Kuna walikuwa chini ya Yoweri K Museveni na wale wa Milton Obote ambao nadhani walikuwa chini
ya Ojok. Tafadhali tupe maelezo kuhusu hawa wapiganaji.

Naongezea hapa alikuwepo pia Tito OKELO.
 
Naongezea hapa alikuwepo pia Tito OKELO.
Gen.Tito Okello Lutwa alizaliwa katikakijiji cha Nam Okora wilaya ya Kitgum wakati wa vita vya kwanza vya Dunia mwaka 1914,Kuhusu elimu yake mengi hayajulikani hata hivyo alijiunga na Kings African Rifles(KAR)May 16,1940 kama ilivyokuwa kwa Idd-Amin naye alipigana vita vya Mau-Mau huko Kenya wakiwa upande wa waingereza mwaka 1957.
Gen.Tito Okello Lutwa alijiunga na Jeshi la Uganda na alipanda cheo kufikia Lieutenant mwaka 1962 na alifikia kuwa Colonel mwaka 1968.Wakati Amin anampindua Obote mwaka 1971 Gen.Tito Okello Lutwa alikimbilia Tanzania na alikaa sana Dar-es-salaam lakini pia alishawahi kukaa Nachingwea,Morogoro na Masange Tabora.
Mwaka 1978 wakati wa vita vya kumng`oa Idd Amin Gen Tito Okello Lutwa aliongoza kikosi maalumu(Special-Force)kikosi ambacho mimi mwenyewe nilikuwemo tulipigana bega kwa bega na waganda hao mpaka kung`oa Idd Amin madarakani mwaka 1979.
Mwaka huo huo 1979 baada ya Amin kuondolewa alikuwa sehemu ya Tume ya kijeshi,na baadaye 1980 alikuwa mkuu wa Majeshi wakati huo huo akiwa kwenye Tume ya kijeshi.Mwaka 1984 Alipandishwa cheo na kuwa Lieutenant General.
Gen.Tito Okello Lutwa alipitia magumu sana kipindi hicho maana kulikuwa na mambo mabaya sana jeshini Ukabila ulikuwa umetawala sana kulikuwa na vita kati ya makabila ya Acholi na Langi ilimuwia ngumu sana hata katika uteuzi wa maafisa wa jeshi mfano alimteua Bri.Smith Opon Acak toka kabila la Langi kuziba pengo la Maj.Gen.David Oyite-Ojok uteuzi huo ulipingwa sana na wanajeshi toka kabila la Acholi ambao wao walitaka mtu kutoka kabila lao Brig.Olara Okello ambaye alikuwa na uzoefu katika nafasi hiyo
Mwaka 1984 vita na waasi wa NRA alikuwa ameongeza mashambulizi yao kwa serikali hii pia iliezesha jeshi la taifa kugawanyika vipande viwili uapande mwingine ukiunga mkono Acholi na mwingine Langi kabila la Obote na Oyite Ojok.
Baada ya migogoro isiyokwisha ndani ya Jeshi la taifa UNLA na mapigano makali yaliyokuwa yakiongozwa na NRA chini ya Mseven Gen.Tito Okello aliamua kumpindua Rais Milton Obote July 25-27,1985 na Obote kukimbilia Kenya ka nia ya Barabara na kaenda uhamishoni Zambia ambako alifariki October 2005.
Baada ya mapinduzi hayo Gen.Tito Okello Lutwa alitangaza kuwa Uganda itatawaliwa na Baraza la kijeshi nay eye akiwemo kwa miezi 12 kabla ya Uchaguzi kufanyika.hata Gen.Okello alijaribu kuliunganisha jeshi ambalo tayari lilikua vipande vipande alijaribu kuunda serikali ya Mseto iliyojumlisha vyama vya Federal Democratic movement,Uganda National Rescue Front,Uganda Freedom Movement na NRA iliyokuwa inaongozwa na Yoweri Kaguta Mseven,Hata hivyo aligundua janja ya nyani aliyokuwa anataka kucheza Gen.Tito Okello na akakataa serikali hiyo na kuendelea na mapambano dhidi ya majeshi ya serikali UNLA
Yoweri Kaguta Mseven aliweka masharti magumu ili kukwamisha mazungumzo ya Amani yaliyokuwa yanaendelea huko Nairobi chini ya Rais Daniel Arap Moi wakati huo vikosi vyake vya NRA vilizidi kusonga mbele katika miji ya karibu na Kampala Barabara ya Masaka,Mubende,Mbarara na Katonga zote zilifungwa na kusababisha usalama katika maeneo yote kuwa hatarini Askari alianza uporaji na utekaji wa magari na vituo vya Mafuta,Maskini Gen.Okello hata hakumaliza kipindi alichoweka ili uchaguzi ufanyika na akapinduliwa January 26,1986 na alikimbilia uhamishoni hatimaye June 3,1996 alifariki akiwa na umri wa miaka 82,na mabaki ya mwili wake yalirudishwa Uganda na kuzikwa nyumbani huko wilaya ya Kitgum katika mazishi yake Rais Yoweri Kaguta Mseven alimtaja kuwa alikuwa mtu mkuu aliyelitumikia taifa lake na atakumbukwa kwa juhudi zake za kuleta Amani Uganda.
January 2010 wakati wa kumbukumbu ya vita vya Kagera alitunukiwa nishani ya Kagera National Medal Kwa heshima yake kwa kupigana vita kwenye miaka ya 1970-1979 dhidi ya Nduli Idd Amin.

.
 
Kuna jamaa wa Uganda namfahamu naye alikuwa uwanja wa mapambano, anasema kikosi chake kilikua chini ya Kanali Moyo. Inavyoonekana kulikua na makundi tofauti ya wanajeshi wa Uganda waliokuwa begakwabega
na majeshi yetu. Kuna walikuwa chini ya Yoweri K Museveni na wale wa Milton Obote ambao nadhani walikuwa chini
ya Ojok. Tafadhali tupe maelezo kuhusu hawa wapiganaji.
Historia ya Major-General David Oyite-Ojok
Major-General David Oyite-Ojok alizaliwa April 15,1940 huko Loro wilaya ya Lango,alimaliza shule ya msingi katika shule ya Loro aliendelea na masomo katika shule ya Nabumali high school huko wilaya ya Mbale kuanzia 1958 mpaka 1962 baadaye alijiunga na Jeshi wakati huo lilijulikana kama Uganda Rifles na mwaka 1963 alipelekwa kusoma Uingereza kwenye chuo cha kijeshi cha Mons officer cadet.na aliporudi alipandishwa na kuwa Luteni usu(Second lieutenant)na alipelekwa huko jinja kuongoza kikosi cha askari wa miguu ambako alitumika kama platoon commander.
Major-General David Oyite-Ojok baadaye 1966 alihamishiwa Fourth Infantry Battalion,Mbarara hatimaye alihamishiwa tena Kampala kuwa mkuu katika ofisi ya mkuu wa utawala Jeshini,baadaye tena alipandishwa cheo na kuwa Army`s Quartermaster General na alienda kusoma huko Uingereza katika chuo cha kijeshi cha Cumberley Staff College na alirudi Uganda 1967.kwa wakati ule kwa cheo alichokuwa nacho na kwa kuwa alikuwa Mpwa wa Rais Obote alikuwa mtu mhimu sana katika Uganda.
Major-General David Oyite-Ojok alimuoa Rebecca Ojok na alikuwa na ndugu waliokuwa jeshini mmoja wapo ni Lt Col Martin Okech aliyekuwa katika jeshi la anga la Uganda kipindi hicho Idd-Amin na David Oyite-Ojok walikuwa marafiki sana na waliheshimiana ingawaje kila mmoja alimuona mwenzie kuwa kama anaheshimiwa sana jeshini kuliko mwingine,lakini wote walikua maarufu sana Jeshini kuliko mtu yeyote.Kwa upande wa David Oyite-Ojok alijiona yeye kuwa ni Kamanda mkuu mtarajiwa katika jeshi la Uganda na alijiona hana mpinzani isipokuwa Idd-Amin pekee, Hivyo kwa kutumia ukaribu aliokuwa nao na Rais Obote aliweza kuingiza mambo ambayo yangemharibia sifa Idd-Amin kwa Rais Obote hata hivyo Rais Obote hakuona tatizo lolote kwa Idd-Amin
Katika tukio moja lililotokea katikati ya 1960 Oyite-Ojok wakati huo akiwa Lieutenant-Colonel aliwakilisha repoti ya uchunguzi ikimtuhumu Idd-Amin kwa kupanga njama za kumpindua Rais Obote,Ripoti hiyo ilimfanya Rais Obote aamuke toka usingizi dhidi ya Idd-Amin na akataka ushauri toka kwa Oyite-Ojok ni njinsi gani atamdhibiti Idd-Amin hapo ndipo Oyite-Ojok alipata fursa ya kummaliza Idd-Amin kwa kumwambia Rais Obote amwachie kazi hiyo yeye.Oyite-Ojok alipanga mpango wa Kumkamata Idd-Amin lakini mpango huo ulivuja na Idd-Amin alipata habari na hapo hapo alivaa mavazi rasmi ya Kijeshi na akabeba Pistol mbili na kuelekea kwenye majengo ya Bunge iliko ofisi ya Rais Obote akiwa amevalia Kijeshi(Full battle fatigues)na aliweza kuongea na Rais lakini haikujulikana ni nini aliongea na Rais Obote.
Baada ya tukio hilo 1969 Oyite-Ojok alibuni mpango mwingine wa kumuua Brig.Okoya na kusukuma lawama zote kwa Idd-Amin,Oyite-Ojok alimchukua Capt Okoth wa kikosi cha polisi wa Jeshi pamoja na Capt.Fredrick Guweddeko na Lt.Kasule Lutalo ambaye alikuwa anafanya kazi katika kituo cha anga cha Guru wanajeshi hawa waliteswa sana ili waweze kukiri kuwa Idd Amin alihusika katika mauaji ya Bri.Okoya lakini wanajeshi hao walikana kabisa kumhusisha Idd-Amin na mauaji hayo hivyo kulipelekea wao kutupwa Gerezani huko Luzira.
Baadaye ililipotiwa kuwa Oyite-Ojok aliwatembelea huko gerezani na kuwacheka kwa kuacha kuitumia hiyo nafasi kumkandamiza Idd-Amin hivyo walipoteza nafasi ya kupandishwa vyeo pamoja na kupata kitita kikubwa cha pesa walichoahidiwa kupewa ikiwa tu wangeliweza kumuunganisha Idd-Amin na mauaji ya Brig.Okoya na aliwaambia wakae waozee humo gerezani.
Baadaye katikati ya Dec.1970 Oyite-Ojok alijaribu mpango mwingine wa kumtia hatiani Idd-Amin,Siku moja usiku Oyite-Ojok aliendesha gari lake aina ya Mercedes Benz kuelekea kwenye kambi ya kijeshi ya Malire na alichagua askari wa ngazi za chini 12 na wote walipangwa karibu na lango kuu la chuo kikuu cha Makelele na wengine walipangwa Balintuna road huko Namirembe lwenye vilima vinavyotazama jiji la Kampala,Askari wote hao walikuwa wanatoka katika kambi ya kijeshi ya Malire,Oyite- Ojok aliwapa maagizo waangalie gari aina ya Peugeot 403 iliyokuwa na Antena mbili maalum za kijeshi aliwaagiza kipindi watakapoiona walimiminie risasi bila kusita.
Wakati askari hao wanasubiri hiyo wale askari waliokuwa wamewekwa kwenye lango kuu la chuo kikuu cha Makelele walianza kuulizana kuhusiana na lile gari walilopewa amri kuliangalia na baadaye kulimiminia risasi walijua ni lile gari la mkuu wa Majeshi Major General Idd-Amini maana hakuna gari aina hiyo yenye Antena mbili maalum za kijeshi nchini Uganda isipokuwa ni ile ya Idd-Amin,Askari hao walijiuliza kwa nini Oyite-Ojok anataka kumuua Idd-Amin na kwa nini anataka kushirikisha wanajeshi katika kitendo hicho?Askari hao walipeana habari na wakaamua kutotekeleza amri hiyo ya Oyite Ojok wakikumbuka kwa yale yaliyowatokea wenzao waliokuwa wamefungwa kenye gereza la Luzira.
Wakati wanajadiri hayo ghafla gari tajwa likaonekana likiwa na antenna maalum mbili za kijeshi likitokea Barabara ya Makelele kuelekea Nakulabye ilikuwa saa 8 usiku na Idd-Amin alikuwa akiendesha peke yake bila Bodyguard,Amin aliwaona askari wawili barabarani akasimama akawauliza kwa nini wanafanya ulinzi eneo la chuo kikuu cha Makelele??Mmoja wao alimjibu Kuwa hata wao walikuwa wakijiuliza usiku wote na Idd-Amin aliwapakiza kwenye gari yake na kuwaondoa katika lindo hilo wakati wakiwa ndani ya gari ya Idd-Amin waliendelea kumsimulia njinsi Oyite-Ojok alivyowapa maagizo ya kumuua,Idd-Amin aliapa mapumziko ya siku 14 askari wote waliokuwa kwenye mpango wa kumuua.
Asubuhi yake Oyite-Ojok alijuwa wazi kuwa mpango wake wa kumuua Idd-Amin umeshindwa na yeye kwa cheo chake hana mamlaka ya kuwaadibisha askari hao,hivyo kulimweka katika hali mbaya kwa jamii na kwa hasimu yake Idd-Amin
Hatimaye Rais Obote alikwenda kwenye mkutano wa Commonwealth huko Singapore Idd-Amin alipata wasaa mzuri na aliweza kutekeleza mapinduzi ya kijeshi January,25,1971 wakati huo Oyite-Ojok alikuwa kwenye majengo ya Bunge na aliponea chupu-chupu kukamatwa na askari waliokuwa eneo hilo hivyo alitimkia kusikojulikana.
Kesho yake Mwambata wa kijeshi wa Israel nchini Israel Col.Baruch Bar-Lev aliwauliza askari watiifu kwa Amin kama Oyite-Ojok amekamatwa au ameuwawa,lakini walipomjibu kuwa hajulikani wapi alipo Bar-Lev alisema mapinduzi hayo hayakufanikiwa,Mwambata huyo alisema hivyo kutokana na umaarufu aliokuwa nao na mafunzo aliyokuwa nayo Oyite-Ojok alikua na Imani ya kuwa na uwezo wa kutengua mapinduzi hayo.
Baada ya mapinduzi hayo ya January 25,1971 Oyite-Ojok alikimbilia Sudani kusini kupitia Adjumani na alienda kwenye sehemu iliyojulikana Owiny Kibul,hakuweza kusafiri mara moja kwenda Tanzania.Akiwa kwenye mji wa Owiny Kibul alianza kuwakusanya askari ili baadaye waanze mapambano ya kumtoa Idd-Amin madarakani.
Wengi wa askari aliowapa mafunzo ya kupigana vita kumuondoa Idd-Amin madarakani walikufa wakio bado kwenye kambi za mafunzo huko Sudan kusini,lakini baadaye walihamishiwa Masange Tabora na wengine Morogoro na wengine Nachingwea Tanzania,kwa msaada wa serikali ya Tanzania walipewa sehemu nzuri na silaha.
Katika mwaka huo 1971 akiwa askari wa msituni Oyite-Ojok aliweza kusafiri na kwenda Kampala na Sudan kusini kwa kutumia passport ya Sudani alikuwa kila mara anafikia kwenye hotel ya Soweto,vilevile alikuwa na kikosi maalum kilichokuwa kinamiliki mashua inayokwenda kwa kasi katika ziwa Victoria ambayo ilikuwa na uwezo wa kufika katika maeneo yote ya Uganda kupitia ziwa Victoria. waliweza kuteka silaha toka majeshi ya Amin ambazo walizificha huko Mayunge,mbarara Uganda ambazo baadaye walizitumia katika mapambano ya kumtoa Idd-Amin.Alishiriki kikamilifu katika vita vya kagera akiwa katika Kikosi Maalum(Special Force) akiwa na Tito Okello Lutwa na Kaguta Mseveni

Katika mwezi huu wa December ulimwengu ulikuwa ukiomboleza kifo cha aliyekuwa Rais wa Afrika kusini ambaye alikuwa alama ya mapambano ya kupinga ubaguzi wa Rangi,Na miaka 30 iliyopita mwezi huu wa December Uganda walipoteza mmoja wa mashujaa waliokuwa wanaongoza, kiongozi huyo alijulikana kwa jina la Major-General David Oyite-Ojok aliyekuwa mkuu wa utawala jeshini aliyekuwa taa ya kuongoza katika mapambano ya kumng`oa Idd-Amin.
Ilikuwa jumapili December 2,1983 helicopter iliyokuwa imembeba Major-General David Oyite-Ojok ilianguka katika kijiji cha Kashozi Wilaya ya Nakasongola alikoenda kukagua mapambano na waasi wakati huo waasi walikuwa wakiongozwa na Yoweri Kaguta Mseveni.
Kifo chake kilileta mshituko mkubwa kwa Taifa, Major-General David Oyite-Ojok alikuwa ni mtu wa mwisho kwa Waganda kumtegemea kufa kwa wakati huo na kwa ajali kama hiyo.maana toka vita vya kumng`oa Idd-Amin Major-General David Oyite-Ojok alionekana kuwa shujaa na watu wengi wakiwemo askari wa Tanzania waliopigana vita vya kumtoa Idd-Amin katika ardhi ya Tanzania na hatimaye kumng`oa katika madaraka,alionekana kuwa kiongozi wa kijeshi mwenye nguvu pia kulikuwa na uvumi kuwa alikuwa na nguvu kama Rais Obote na kumzidi aliyekuwa makamu wa Rais wakati ule Paulo Muwanga.
Baada ya kifo cha Major-General David Oyite-Ojok nchi iliingia kwenye maombolezo ya kitaifa,Radio Uganda na Television viliendelea kutoa salamu za rambi-rambi kwa Rais na Makamu wake na waziri mkuu wakati huo Otema Alimadi na kwa serikali nzima ya Uganda kulikuwa na makundi makubwa ya watu huko Kampala,Lira na miji mingine walionekana wakiomboleza kifo cha shujaa huyu.
 
Kwani Wale Mateka Wa Kiarabu Mliwapeleka Wapi? Wako Wapi Sasa? Na Vp Kuhusu Majina Ya Utani Ya Makamanda Yalikuwa Na Maana Gani?
Wale mateka wa kutoka Libya na Palestina wote walikabidhiwa nchi zao baada tu ya sherehe Kaboya kuwakaribisha wapiganaji wetu waliokuwa wakipigana huko Uganda.Kuhusu kazi na majina ya Makamanda soma sehemu yangu ya kwanza na ya pili nilielezea labda nielezee wachace tu.
1.Mhidini Kimario(Kamanda Mbogo)yeye aliitwa hivyo sababu alikuwa mkali sana hasa adui alipokuwa anatushambulia na wakati tunajibu mapigo alisimamia hasa kuhakikisha unapiga target yako vizuri.
2.Imran Kombe(Kamanda Ngono)Aliitwa hivyo baada ya kikosi chake kuvuka Mto NGONO walikokuwa wamezingirwa askari wetu na majeshi ya Idd-Amin
3.Kitete(Supersonic)Aliitwa hivyo sababu mipango yake ya kivita alitaka iende haraka na kufuata wakati
4.Msuguri(Mtukula)aliitwa hivyo sababu yeye ndiye aliyeanzisha vita vya kumtoa Nduli Idd-Amin Mtukula
5.Mayunga(Mti mkavu)aliitwa hivyo baada ya majeshi ya Amin kujaribu kuvirudisha nyuma vikosi vya Mayunga kushinda basi wakamwita yeye ni Mtu mkavu ambao hauchimbwi Dawa.
6.Moses Nnauye(Kamanda wa Hamasa)aliitwa hivyo sababu yeye alikuwa kitengo cha Propaganda kuhamasisha anajeshi vitani.Kama unataka kujua majumu yao vitani nitaanza na-
Luteni kanali R.R.Rajab alipewa jukumu la kusimamia ujenzi wa Daraja la mto KAGERA maana yeye alikuwa kamanda wa Uhandisi.Kitu cha kwanza ilikuwa kujenga Daraja la mda ambalo lilijengwa usiku na mchana na lilipokamilika lilianza kutumika mara moja lilikuwa na uwezo wa kupitisha magari ya kijeshi na zana zingine za kivita.
Meja Jenerali T.N.Kiwelu kamanda wa kwanza aliyepewa jukumu la kuyaongoza mapambano ya kuyasukuma nyuma Majeshi ya Amin toka Kagera Kiwelu ndiye aliyekusanya nguvu kubwa za awali ambazo ndizo zilizomng`oa Idd Amin katika eneo aliloliteka kazi hii ilikuwa ngumu sana lakini aliifanya kwa utulivu hatimaye akapanga mipango madhubuti iliyowezesha Majeshi ya Amini kuondolewa kabisa katika ardhi ya TANZANIA.
Meja Jenerali Mwita Marwa(Jenerali Kambale) alikuwa mkuu wa Brigedi iliyopewa jukumu la kuelekea uelekeo wa Mtukula na kuelekea Igayanza.Marwa alikuwa Mkuu wa brigedi ya 208,alishirikiana na Brigedi za 201 na 207 katika kuuteka mji wa Kampala Jinja Mbale na Moroto.
Meja Jenerali Silas Mayunga(Mti Mkavu)Ndiye aliyeyaongoza Majeshi ya TASK-FORCE yaliyokuwa uelekeo wa Kakunyu,Kasumba,Gayanza,Mbarara Bushenyi,Kasese,Fort-portal,Hoima,Masindi,Pakwachi,Arua,Koboko alikozaliwa Idd Amin mpaka Oraba mpakani na Sudan
Brigedia Walden(Black Mamba)Ndiye aliyeongoza Brigadi ya 207 yeye alichukua uelekeo wa Minziro mpaka Katera baada ya kuweza kumshinda adui maeneo hayo alijiunga tena na uelekeo wa Mtukula kuanza safari ndefu ya kuyachapa majeshi ya Amin hadi kukamata Kampala baadaye alipewa jukumu la kulinda mji mkuu Kampala na vitongoji vyake
Brigedia Helman Lupogo alikuwa anaongoza na kuamrisha Brigedi ya 205 kutoka mpaka wa Tanzania na Uganda hadi eneo la Sembabule baadaye alipewa kazi nyingine maalum na badala yake alipewa Brigedia Kimario.
Brigadia Muhidini Kimario(Kamanda Mbogo)yeye alichukua uongozi wa Brigedi ya 205 katika eneo la Sembabule kutoka kwa Brigedia Lupogo ambaye alipewa shughuli nyingine mhimu,Brigedia Kimario aliongoza Brigedi hii kuanzia Sembabule hadi Masindi na kuelekea Guru,alipambana vikali sana na Adui katika eneo la Sembabule,Hoima na Masindi.
Brigedia Imran Kombe(Brigedia Ngono) yeye alikuwa kamanda wa Brigedi ya 201 ambaye alishirikiana na Brigedi ya 207 na 208 waliweza kuuteka mji mkuu wa Uganda ikumbukwe kuwa Brigedi ya 201 ndiyo iliyopambana vikali sana na majeshi ya Amin katika mji wa Lira na kuua askari wa Amin zaidi ya 200 na kuteka silaha nyingi sana za Adui,Baada ya hapo Brigedi hiyo ya 201 ilijikusanya katika mto Ngono na kusonga mbele mpaka Adjumani kama maili hamsini kutoka mpaka na Sudan
Brigedia Yusuph Himid naye alikuwa wa kwanza kwanza kupambana na majeshi ya Amin mwezi October 1978.
Brigedia Haji aliongoza Brigedi ya Kagera katika mapambano jukumu lake kubwa lilikuwa kulinda maeneo yote ya nyuma yaliyotekwa na majeshi yetu,pia Brigedi yake ilipewa jukumu la kuyafundisha majeshi ya Uganda Huru.
Kanali Kitete(Supersonic) yeye alikuwa Mkuu wa shughuli za Utendaji Kivita yaani Mkuu wa mipango Uamrishaji Kivita katika Division ya 20 baadaye aliteuliwa kuwa Brigedia wa muda na aliongoza Brigedi ya minziro iliyomchakaza nduli sehemu za Bushenyi,Kasese,Fort-portal,Hoima,Masindi,Karuma Falls,Pakwachi,Bondo,Arua,Yumbe hadi Moyo mpakani na Sudan.
Kanali Tumbi(Kamanda Radi) yeye alikuwa Mkuu wa kikosi cha Mizinga ya masafa marefu BM
Brigedia Makunda(Kamanda Torpedo)alichukua uongozi wa Brigedi ya 206 na kuiongoza kuanzia miji ya Mbarara,Fort-portal,Hoima,Masindi,Karuma Falls,Pakwachi Bondo,Arua,Koboko,Oraba mpakani na Sudan.
Brigedia Mboma-Kamanda mkuu wa ndege za kivita-Tanzania uongozi wake mzuri na kazi yake kubwa aliyoifanya katika Vita haina budi kupongezwa daima.
Kanali Bayeke alikuwa anaongoza na kuamrisha kikosi cha askari wa miguu Mstari wa mbele eneo la Minziro.
Meja Jenerali David Msuguri (Jenerali Mtukula)Kamanda aliyeamrisha Mapambano ndani ya Uganda alikabiliwa na kazi nzito ya kuyaongoza na kuyaamrisha Majeshi ya Tanzania na yale ya Umoja wa kuikomboa Uganda yapatayo zaidi ya wapiganaji 40,000 pamoja na zana za kivita
Brigedia M.N.Mwakalindile wakati wote wa vita alikuwa Kamanda mkuu wa mafunzo ya vita COT katika Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania alifanya kazi kubwa mno ya kuyahusisha majeshi ya nyuma nay ale yaliyoko mstari wa mbele pia ndiye mwenye kuweza kuyaendeleza mafunzo yote ya mbele na nyuma katka vita.bidii yake katika kuipenda kazi ilianza tangu zamani akingali katika uongozi wa kati aliweza kukutana na makamanda wa vikosi imara na kuwapa mawazo na mbinu kamambe kuhusu matumizi ya silaha kubwa,
 
Echolima Nafurahi sana kuona namna unavyo ichambua historia vzur na jinsi ulivyo na upeo mzur wa kiuvumilivu probably ni result ya mafunzo ya jeshi nikusifu pia kwa pamoja memory nzur.. naomba kuuliza je wewe ni mmoja wa askar wa kwanza walioenda nje kupata mafunzo ya ukomandoo.. ?? Nafaham katika vita hii kaz kubwa ya Reconaissance ilifanywa na kikosi hiki maalum. Na mafunzo haya mliyapata wapi.?? shukran sana Echolima.
 
Echolima maelezo yako yanaifanya niongeze imani kwa Jwtz.Vipi mchango wa makomando wetu ulikuwaje?Tunaweza tembea kufua mbele hata kipindi hiki dhidi ya majirani zetu yaani ke,ug,rwanda na malawi?
 
Echolima maelezo yako yanaifanya niongeze imani kwa Jwtz.Vipi mchango wa makomando wetu ulikuwaje?Tunaweza tembea kufua mbele hata kipindi hiki dhidi ya majirani zetu yaani ke,ug,rwanda na malawi?
Kijeshi si vizuri ku-Under-estimate adui yako maana huwezi jua ana uwezo gani kwenye silaha,mafunzo yao,mbinu zao na nidham za askari wao. hasa majibu yote hutokea kwenye uwanja wa MEDANI mara nyingi sana ingawaje si mara zote watu hutumia udhaifu wa upande wa adui hapo ndipo unaweza kupiga Bao kirahisi sana,Kumbuka pia vita si lelemama au mchezo wa kuigiza once you make any mistake you did great-mistake to you,your family and your country.Mimi binafsi nisingependa sisi kuwa POLISI au VIRANJA dhidi ya majirani zetu.
 
Ndo maana huwa nikisikia majina ya makamanda walioliongoza jeshi letu kule uganda najawa na furaha na uzalendo wa hali ya juu kuhusu jeshi letu.
 
nimebahatika kufika maeneo ambayo tunapakana na uganda maeneo ya kyaka kwenye kumbukumbu ya kanisa na daraja vilivyopigwa mabomu kipindi cha vita hii na mutukula kwenye mabaki ya magari ya kivita na vifaru vya uganda vilivyotekwa na majeshi yetu. kwa kweli maeneo haya japo vita hii ilipiganwa zaidi ya miaka thelathini iliyopita ukipita leo hii unapata feeling uko "war zone". kweli vita ni kitu kibaya sana si cha kuomba kitokee nchini mwako. hongera sana mashujaa wetu.
 
Mkuu Echolima malizia hiko kitabu mimi ni miongoni mwa wanaongoja kwa hamu sana kupata nakala zako mwanzo kabisa. Km ilivyoelezwa waone TBC, uongozi wa jeshi, makumbusho ya taifa kuboresha chapisho.
 
Kuna tetesi niliwakusikia kutoka kwa mmoja ya askari aliyewahishiriki vita ya kagera kuwa Jwtz commando unit waliwahifanya rescue operation kwa raia wa Tz waliokuawametekwa na waasi wa Sudan miaka ya 1980's.Inadaiwa wtz hao waliwatoroka waasi wa sudan na kujificha kwenye misitu ya upande wa Uganda ndipo wakajaokolewa na Jwtz. Mwenyekulifahamu hili anaweza kutujuza
 
HISTORIA FUPI YA MAKAMANDA

Mwaka 1978 jeshi letu likuwa na Major General wawili tu, Major General Twalipo (aliyekuwa mkuu wa majeshi wakati huo) na Major General Sarakiya ambaye alikuwa balozi wetu huko Nigeria. Baadaya ya Major General kulikuwa na Mabrigadier sita au saba tu: Brigadier Marwa, Brigadier Musuguri, Brigadier Mayunga, Brigadier Walden, Brigadier Kiwelu, Brigadier Yusuf Himid nadhani na Brigadier Mkisi. Chini ya Mabrigadier kulikuwa na makanali kadhaa ikiwa ni pamoja na akina Moses Nnauye, Abdallah Natepe na wengineo.

Nitaendelea...

Mkuu,

Kwanza nashindwa nikusamilie kwa heshima ipi kutuletea thread tamu ya kishujaa hivi. Maana naona hata LIKE haustahili bali ninastahili kukpa SHIKAMOOOOOO.

Mkuu,

Mimi naongezea kitu kidogo sana ili wenzetu wakumbuke. Umetaja kwamba wakati huo mabrigedia walikuwa sita au saba hivi na ukawataja sita hapo kwenye RED.

Mkuu kumbukumbu yako ni nzuri maana katika uliowataja umesahau tu Brigedia Augustine Ramadhani kutoka Zanzibar. Huyu Brigedia Augustine Ramadhani ndiye aliyekuja kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania na hivi majuzi alikuwa Makamu wa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba tunayoiita ya Warioba.

Hivyo, ule upuuzi kwamba Tume ya Katiba ni wasaliti ni utoto wa baadhi ya wabunge wa Katiba kuwa mambumbumbu wa historia.

Kingine ninachokiona ni kwamba mgogoro wa kikatiba wa Zanzibar na Muungano yaani kati ya Aboud Jumbe na Nyerere ulianza hata kipndi hiki.

Umeeleza kiusahihi kwamba vita ilichukua miezi kadhaa kwisha na iliisha June 1979. Idadi ya mabrigedia ilikuwa chache kama ulivyoeleza.

Huwa najiuliza, ni kwa nini wakati huu wa vita Rais Aboud Jumbe akaamua kumteua Brigedia Augustine Ramadhani kuwa mwanasheria Mkuu wa Zanzibar: {SUNDAY NEWS: November 26, 1978, pg. 26}?

Pia ninamkumbuka Luteni Colonel Victor Felix Rusubi ambaye baadaye alipewa kazi ya kuhamasisha wanafunzi wa sekondari kuhusu vita na akawa anasimulia jinsi askari wa Libya walivyokuwa wanavamia kama kuku. Bahati nzuri na wewe umeeleza kipigo cha Lukaya ambako walibywa walilia ALAHHU AKBAR.

Zaidi ya hapo tunakusubiri mtiririko mkuu.

Cc: Jasusi,
 
Kwa kweli Story za hii vita Vya Kagera huwa zinanisisimua sana tu, Nimesoma kile kitabu cha War In Uganda cha Martha Honey na Tony Avirgan yaani utapenda km unaangalia movie vile. Kuna picha mle za akina Ben Msuya, Mti Mkavu, Oyite Ojok huyu alikuwa kamanda ktk jeshi la ukombozi wa Uganda waliopigana bega kwa bega na majeshi yetu. Nakumbuka vita hivi vinapiganwa mie nilikuwa km na 4yrs tulikuwa Songea, kule kuna kambi kubwa za jeshi basi ikasemekana ndege za Nduli zaweza fika na kupiga kule, mji mzima kila family tukachimba mahandaki ya kujificha, mbaya zaidi mzee wangu alikuwa Polisi upande wa upelelezi, dah nilikuwa naomba mungu tusiambiwe mzee kapelekwa mstari wa mbele! ndege zikipita angani watu wanakimbia kujificha. nakumbuka baada ya vita kwisha askari wengi walirudi Songea mjini basi walikuwa km wamechanganyiiwa hivi na watu waliaswa kutowachokoza. siku moja niko na bro wangu tunakwenda town si nikagongana na soldier akasimama akaniambi mtoto Kaa chonjo kule saa mbaya i nearly did in my pant! hahahaha. Mkuu simulizi zako ziendelee huwa napensa sana jinsi mashujaa wetu walivyomtosa Nduli na kumchakaza vibaya!

Mkuu,

Kitabu hiki ninacho na ninakitunza kama mboni ya jicho langu. Niliwahi kumuonyesha mkubwa mmoja hapa nchini mwaka jana, kumbe hakuwahi kukiona na alishangaa sana kuniona nacho.

Na humo utagundua kwamba kumbe Nyerere alikuwa mmoja wa marais wachache kumuweka detention rais wa nje.

Nyerere alimuweka detention Rais Yusuf Lule wa Uganda kwenye ikulu ya D'Salaam kuanzia June NN, 1979 hadi July 06, 1979 kama inavyoelezwa kwenye ukurasa wa 204 hadi 206.

Nyerere alikuwa kiboko.
 
Aksante sana RUVUMAN umeongea maneno mazuri sana na ushauri mzuri kwangu nilikuwa najibu tu swali aliloniuliza kuwa ni kitu gani nakikumbuka sana katika Vta hiyo,Najua sana vitani kuna mambo mengine yanatendeka huko si mazuri kwa jamii lakini nitajitahidi sana na staadhiri USALAMA WA TAIFA nitakuwa naongelea tu hali halisi iliyotokea nashukuru kwa maoni yako.

Mkuu usibabaike.

Mimi nina kitabu kiitwacho War In Uganda: 9789976100563. Kimeandikwa na waingereza ambao waliruhusiwa na Nyerere kwenda mstari wa mbele baada ya kipigo cha Masaka.

Wameandika mengi bila kuficha lolote. Hivyo, wasikutishe chochote eti usalama wa taifa au nini.
 
Back
Top Bottom