Kwani Wale Mateka Wa Kiarabu Mliwapeleka Wapi? Wako Wapi Sasa? Na Vp Kuhusu Majina Ya Utani Ya Makamanda Yalikuwa Na Maana Gani?
Wale mateka wa kutoka Libya na Palestina wote walikabidhiwa nchi zao baada tu ya sherehe Kaboya kuwakaribisha wapiganaji wetu waliokuwa wakipigana huko Uganda.Kuhusu kazi na majina ya Makamanda soma sehemu yangu ya kwanza na ya pili nilielezea labda nielezee wachace tu.
1.Mhidini Kimario(Kamanda Mbogo)yeye aliitwa hivyo sababu alikuwa mkali sana hasa adui alipokuwa anatushambulia na wakati tunajibu mapigo alisimamia hasa kuhakikisha unapiga target yako vizuri.
2.Imran Kombe(Kamanda Ngono)Aliitwa hivyo baada ya kikosi chake kuvuka Mto NGONO walikokuwa wamezingirwa askari wetu na majeshi ya Idd-Amin
3.Kitete(Supersonic)Aliitwa hivyo sababu mipango yake ya kivita alitaka iende haraka na kufuata wakati
4.Msuguri(Mtukula)aliitwa hivyo sababu yeye ndiye aliyeanzisha vita vya kumtoa Nduli Idd-Amin Mtukula
5.Mayunga(Mti mkavu)aliitwa hivyo baada ya majeshi ya Amin kujaribu kuvirudisha nyuma vikosi vya Mayunga kushinda basi wakamwita yeye ni Mtu mkavu ambao hauchimbwi Dawa.
6.Moses Nnauye(Kamanda wa Hamasa)aliitwa hivyo sababu yeye alikuwa kitengo cha Propaganda kuhamasisha anajeshi vitani.Kama unataka kujua majumu yao vitani nitaanza na-
Luteni kanali R.R.Rajab alipewa jukumu la kusimamia ujenzi wa Daraja la mto KAGERA maana yeye alikuwa kamanda wa Uhandisi.Kitu cha kwanza ilikuwa kujenga Daraja la mda ambalo lilijengwa usiku na mchana na lilipokamilika lilianza kutumika mara moja lilikuwa na uwezo wa kupitisha magari ya kijeshi na zana zingine za kivita.
Meja Jenerali T.N.Kiwelu kamanda wa kwanza aliyepewa jukumu la kuyaongoza mapambano ya kuyasukuma nyuma Majeshi ya Amin toka Kagera Kiwelu ndiye aliyekusanya nguvu kubwa za awali ambazo ndizo zilizomng`oa Idd Amin katika eneo aliloliteka kazi hii ilikuwa ngumu sana lakini aliifanya kwa utulivu hatimaye akapanga mipango madhubuti iliyowezesha Majeshi ya Amini kuondolewa kabisa katika ardhi ya TANZANIA.
Meja Jenerali Mwita Marwa(Jenerali Kambale) alikuwa mkuu wa Brigedi iliyopewa jukumu la kuelekea uelekeo wa Mtukula na kuelekea Igayanza.Marwa alikuwa Mkuu wa brigedi ya 208,alishirikiana na Brigedi za 201 na 207 katika kuuteka mji wa Kampala Jinja Mbale na Moroto.
Meja Jenerali Silas Mayunga(Mti Mkavu)Ndiye aliyeyaongoza Majeshi ya TASK-FORCE yaliyokuwa uelekeo wa Kakunyu,Kasumba,Gayanza,Mbarara Bushenyi,Kasese,Fort-portal,Hoima,Masindi,Pakwachi,Arua,Koboko alikozaliwa Idd Amin mpaka Oraba mpakani na Sudan
Brigedia Walden(Black Mamba)Ndiye aliyeongoza Brigadi ya 207 yeye alichukua uelekeo wa Minziro mpaka Katera baada ya kuweza kumshinda adui maeneo hayo alijiunga tena na uelekeo wa Mtukula kuanza safari ndefu ya kuyachapa majeshi ya Amin hadi kukamata Kampala baadaye alipewa jukumu la kulinda mji mkuu Kampala na vitongoji vyake
Brigedia Helman Lupogo alikuwa anaongoza na kuamrisha Brigedi ya 205 kutoka mpaka wa Tanzania na Uganda hadi eneo la Sembabule baadaye alipewa kazi nyingine maalum na badala yake alipewa Brigedia Kimario.
Brigadia Muhidini Kimario(Kamanda Mbogo)yeye alichukua uongozi wa Brigedi ya 205 katika eneo la Sembabule kutoka kwa Brigedia Lupogo ambaye alipewa shughuli nyingine mhimu,Brigedia Kimario aliongoza Brigedi hii kuanzia Sembabule hadi Masindi na kuelekea Guru,alipambana vikali sana na Adui katika eneo la Sembabule,Hoima na Masindi.
Brigedia Imran Kombe(Brigedia Ngono) yeye alikuwa kamanda wa Brigedi ya 201 ambaye alishirikiana na Brigedi ya 207 na 208 waliweza kuuteka mji mkuu wa Uganda ikumbukwe kuwa Brigedi ya 201 ndiyo iliyopambana vikali sana na majeshi ya Amin katika mji wa Lira na kuua askari wa Amin zaidi ya 200 na kuteka silaha nyingi sana za Adui,Baada ya hapo Brigedi hiyo ya 201 ilijikusanya katika mto Ngono na kusonga mbele mpaka Adjumani kama maili hamsini kutoka mpaka na Sudan
Brigedia Yusuph Himid naye alikuwa wa kwanza kwanza kupambana na majeshi ya Amin mwezi October 1978.
Brigedia Haji aliongoza Brigedi ya Kagera katika mapambano jukumu lake kubwa lilikuwa kulinda maeneo yote ya nyuma yaliyotekwa na majeshi yetu,pia Brigedi yake ilipewa jukumu la kuyafundisha majeshi ya Uganda Huru.
Kanali Kitete(Supersonic) yeye alikuwa Mkuu wa shughuli za Utendaji Kivita yaani Mkuu wa mipango Uamrishaji Kivita katika Division ya 20 baadaye aliteuliwa kuwa Brigedia wa muda na aliongoza Brigedi ya minziro iliyomchakaza nduli sehemu za Bushenyi,Kasese,Fort-portal,Hoima,Masindi,Karuma Falls,Pakwachi,Bondo,Arua,Yumbe hadi Moyo mpakani na Sudan.
Kanali Tumbi(Kamanda Radi) yeye alikuwa Mkuu wa kikosi cha Mizinga ya masafa marefu BM
Brigedia Makunda(Kamanda Torpedo)alichukua uongozi wa Brigedi ya 206 na kuiongoza kuanzia miji ya Mbarara,Fort-portal,Hoima,Masindi,Karuma Falls,Pakwachi Bondo,Arua,Koboko,Oraba mpakani na Sudan.
Brigedia Mboma-Kamanda mkuu wa ndege za kivita-Tanzania uongozi wake mzuri na kazi yake kubwa aliyoifanya katika Vita haina budi kupongezwa daima.
Kanali Bayeke alikuwa anaongoza na kuamrisha kikosi cha askari wa miguu Mstari wa mbele eneo la Minziro.
Meja Jenerali David Msuguri (Jenerali Mtukula)Kamanda aliyeamrisha Mapambano ndani ya Uganda alikabiliwa na kazi nzito ya kuyaongoza na kuyaamrisha Majeshi ya Tanzania na yale ya Umoja wa kuikomboa Uganda yapatayo zaidi ya wapiganaji 40,000 pamoja na zana za kivita
Brigedia M.N.Mwakalindile wakati wote wa vita alikuwa Kamanda mkuu wa mafunzo ya vita COT katika Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania alifanya kazi kubwa mno ya kuyahusisha majeshi ya nyuma nay ale yaliyoko mstari wa mbele pia ndiye mwenye kuweza kuyaendeleza mafunzo yote ya mbele na nyuma katka vita.bidii yake katika kuipenda kazi ilianza tangu zamani akingali katika uongozi wa kati aliweza kukutana na makamanda wa vikosi imara na kuwapa mawazo na mbinu kamambe kuhusu matumizi ya silaha kubwa,