Echolima,
Nimependa umeandika vizuri mno na unajitahidi kujibu kwa ufasaha na uungwana mwema.
Kuna pahala umemtaja Lt. Col. Mazola,je ndie yeye yule baadae alikua full Colonel na kuna wakti alipata matata makubwa kwa kuwekwa ndani na Nyerere bila ya sababu zozote za maana!?
Colonel Mazola alikua Uk maskini,ghafula ati Nyerere akaamuru arejee nchini mara moja na kufikia kizuizini moja kwa moja bila ya kufunguliwa mashtaka ya aina yoyote yale!?
Kuna wakti alipotoka ndani alichoka mno kimaisha,lakini akawa mcha Mungu mzuri mno,alikua habanduki misikitini. Kuna wakti alirejea kwao Morogoro na kugombea ubunge wa Morogoro mjini na kufanikiwa nafikiri. Nijulishe ukipata wasaa tafadhali ndugu yangu.
Je yule Colonel Kibira wa pale Regent,nae mlikua nae huko vita ya Uganda!? Ukishanipa hayo majibu kuna vitu nataka kuunganisha dots!....kuna masuala yalompata Col. Mazola nataka kuhakikisha kutoka na kwako pia!
Kwa mtazamo wako ndugu yangu,nini ulikua mchango wa Brigade ya Nyuki kutoka Zanzibar. Je wale Paratroopers kutoka kambi ya Mwanyanya Zanzibar walifanya vizuri mno nasikia,je hizi khabari ni kweli!?
Je ni nani aliekua msimamizi wa ujenzi wa daraja la muda la Kagera kwenye upande wa JWTZ na alikua na cheo gani wakti huo!?
Ile khabari ya Nyerere ulotaja ya kuchelewa mno kumpandisha cheo Muhidin Kimario,imenihuzunisha mno,khasa ukichukulia kama ulivyotujuza yakuwa yeye alichukuliwa baada ya mwingine kushindwa ile shughuli...na alifanza kazi nzito na nzuri mno! Lakini matokeo yake baada ya vita kwisha takriban wakubwa woote walipandishwa vyeo,ikiwemo na yule Lupogo ambae ndo aloshindwa ile kazi. Nyerere akamwacha Muhidin Kimario na butwaa kubwa!? Hii khabari kuna wakti ilikua ni mojawapo ya minong'ono ya vikao vingi vya mjini wakti huo!
Kwa kifupi Nyerere alikua mtu matata na mapungufu mengi takriban penye kila jambo!!
Vipi Brigadier Simba Wazir,nae mlikua nae huko vitani,vipi mchango wake!?
Tafadhali tunasubiria kwa hamu hiyo sehemu ya pili.
Niwie radhi kama kuna lolote nimenena na hukupendezwa nalo ndugu yangu.
Ahsanta.
Cc;Shariff Ritz,Boko Haram,Prof.Ngongo,JokaKuu