Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii ya kwako imekaa kidini zaidi.Echolima,
Nimependa umeandika vizuri mno na unajitahidi kujibu kwa ufasaha na uungwana mwema.
Kuna pahala umemtaja Lt. Col. Mazola,je ndie yeye yule baadae alikua full Colonel na kuna wakti alipata matata makubwa kwa kuwekwa ndani na Nyerere bila ya sababu zozote za maana!?
Colonel Mazola alikua Uk maskini,ghafula ati Nyerere akaamuru arejee nchini mara moja na kufikia kizuizini moja kwa moja bila ya kufunguliwa mashtaka ya aina yoyote yale!?
Kuna wakti alipotoka ndani alichoka mno kimaisha,lakini akawa mcha Mungu mzuri mno,alikua habanduki misikitini. Kuna wakti alirejea kwao Morogoro na kugombea ubunge wa Morogoro mjini na kufanikiwa nafikiri. Nijulishe ukipata wasaa tafadhali ndugu yangu.
Je yule Colonel Kibira wa pale Regent,nae mlikua nae huko vita ya Uganda!? Ukishanipa hayo majibu kuna vitu nataka kuunganisha dots!....kuna masuala yalompata Col. Mazola nataka kuhakikisha kutoka na kwako pia!
Kwa mtazamo wako ndugu yangu,nini ulikua mchango wa Brigade ya Nyuki kutoka Zanzibar. Je wale Paratroopers kutoka kambi ya Mwanyanya Zanzibar walifanya vizuri mno nasikia,je hizi khabari ni kweli!?
Je ni nani aliekua msimamizi wa ujenzi wa daraja la muda la Kagera kwenye upande wa JWTZ na alikua na cheo gani wakti huo!?
Ile khabari ya Nyerere ulotaja ya kuchelewa mno kumpandisha cheo Muhidin Kimario,imenihuzunisha mno,khasa ukichukulia kama ulivyotujuza yakuwa yeye alichukuliwa baada ya mwingine kushindwa ile shughuli...na alifanza kazi nzito na nzuri mno! Lakini matokeo yake baada ya vita kwisha takriban wakubwa woote walipandishwa vyeo,ikiwemo na yule Lupogo ambae ndo aloshindwa ile kazi. Nyerere akamwacha Muhidin Kimario na butwaa kubwa!? Hii khabari kuna wakti ilikua ni mojawapo ya minong'ono ya vikao vingi vya mjini wakti huo!
Kwa kifupi Nyerere alikua mtu matata na mapungufu mengi takriban penye kila jambo!!
Vipi Brigadier Simba Wazir,nae mlikua nae huko vitani,vipi mchango wake!?
Tafadhali tunasubiria kwa hamu hiyo sehemu ya pili.
Niwie radhi kama kuna lolote nimenena na hukupendezwa nalo ndugu yangu.
Ahsanta.
Cc;Shariff Ritz,Boko Haram,Prof.Ngongo,JokaKuu
handsome wa watu alijificha hukoooooooAsante kwa history nzuri na ya kusisimua kuhusu mashujaa wa Vita vya Kagera isipokuwa tu amesahaulika mtu mmoja nyeti sana Nchini naye ni Mh Rais Kikwete na ningependa kufahamu namna alivyoshiriki katika hivyo vita na alikuwa katika Battalion ipi.Asante.
Karma mkuu, Kombe anahusishwa na mipango ya Kumuondoa mmasai kipenzi cha watu, ila pia hakufika cheo cha general, akahamia TISS kama DG, Kombe kapambana sana hii aka yake ya General Ngono si mchezoHii stori imeelezea uhalisia wa vita kuliko stori za vita vya kagera nilizowahi kusoma.
Nimefadhaishwa sana na jinsi Polisi walivyomuua kihuni Gen Kombe mtu ambaye kwa stori hii alijitoa sana kupigania heshima ya nchi.
hiyo shule itakua ya kwako na bashiteWakuu vp mbona mnapotosha watu wengine humu coz kila mtu anaongea yake kwani historia ya vita hivi vya 78--79 c ipo kwenye vitabu vya historia kuanzia shule za msingi!!!!!
Mna laana nyie vijana wa hotpot na blue band! Mgambo wenyewe wakiwa tight mnajinyea! Maandamano yanatangazwa kila siku hamuendi kisa mnaogopa mabomu ya machozi na virungu. HALAFU MNABWABWAJA TU HUMU JUKWAANI BAADA YA KULA NA KUSHIBA WALI NA MAHARAGE NYUMBANI KWA SHEMEJI YAKO UNAKOISHI!ni kweli ile haikuwa vita ni fujo tu za wanajeshi wa idd amin dhidi ya dikteta uchwara nyerere