Echolima
JF-Expert Member
- Oct 28, 2007
- 3,824
- 2,079
- Thread starter
- #61
Haaa!!!!!1Umenifanya nikumbuke hata Recordplayer yangu ambayo nilikuwa nikiweka santuri 12 harafu yenyewe inadondosha moja baada ya nyingine.Ndugu penye wengi pana mengi ni kweli baada ya kuteka KAMPALA mwezi APRIL 1979 Kweli kabisa kulikuwa na watu ambao hawakuwa waaminifu na hii ni kawaida kwa majeshi mengi askari wengi huwa wanashindwa kuuzuia Munkari hivyo kupelekea kufanya vitu ambavyo vinasababisha Uvunjifu wa Amani kama vile kupora vitu na hata kuwafanya vibaya Wanawake hii ni kwa majeshi yote Duniani Hasa vitendo kwa wanawake inabidi tu maana chukulia tu watu wamekaa Mstuni miezi sita siku askari wakiingia mjini lazima kunakuwa na patashika tu.Lakini vitendo hivi haviruhusiwi kabisa ila mara nyingi vinafanywa na Askari.Echolima,
Umetaja basi la Lupondije umenikumbusha mbali sana mimi binafsi nimeishalipanda sana.
Zamani tulikuwa tunatoka Dar es Salaam kwenda Mwanza na basi Kauma au Tanganyika basi, ukifika Mwanza kwenda Magu au Nyanguge, unapanda Lupondije basi, teh teh teh.
Naomba nikuulize kitu kama kilikuwa cha kweli, wakati mnatoka vitani, mlikuja na vifaa vingi sana radio/tv/friji/magari/vyombo/ ni kweli mliwapora raia wa Uganda.
Nakumbuka mlivyokuwa mnagawa biskuti kwa raia barabarani.
CC; Jasusi, gombesugu, Prof. Ngongo,
Last edited by a moderator: