Vita vya Kagera: Historia yangu - Sehemu ya kwanza

Vita vya Kagera: Historia yangu - Sehemu ya kwanza

Hebu wacha kufira maneno wewe!unajua nini kuhusu vietnam? au kwa sababu umeona movie za vita vya vietnam basi akili yako ndipo ilipo ishia sio? nadhani hata vita vya majimaji jipole wewe utaita ghasia eh?subiri tukianza kuwachapa wanyarwanda nakukamata nakurushia upande wa rwanda halafu nakupa madochi ya maana tu!

Matusi hayafai mwezi mtukufu!

Jina zuri!
Tabia sasa!
Lahaula!
 
Kwa kweli Story za hii vita Vya Kagera huwa zinanisisimua sana tu, Nimesoma kile kitabu cha War In Uganda cha Martha Honey na Tony Avirgan yaani utapenda km unaangalia movie vile. Kuna picha mle za akina Ben Msuya, Mti Mkavu, Oyite Ojok huyu alikuwa kamanda ktk jeshi la ukombozi wa Uganda waliopigana bega kwa bega na majeshi yetu. Nakumbuka vita hivi vinapiganwa mie nilikuwa km na 4yrs tulikuwa Songea, kule kuna kambi kubwa za jeshi basi ikasemekana ndege za Nduli zaweza fika na kupiga kule, mji mzima kila family tukachimba mahandaki ya kujificha, mbaya zaidi mzee wangu alikuwa Polisi upande wa upelelezi, dah nilikuwa naomba mungu tusiambiwe mzee kapelekwa mstari wa mbele! ndege zikipita angani watu wanakimbia kujificha. nakumbuka baada ya vita kwisha askari wengi walirudi Songea mjini basi walikuwa km wamechanganyiiwa hivi na watu waliaswa kutowachokoza. siku moja niko na bro wangu tunakwenda town si nikagongana na soldier akasimama akaniambi mtoto Kaa chonjo kule saa mbaya i nearly did in my pant! hahahaha. Mkuu simulizi zako ziendelee huwa napensa sana jinsi mashujaa wetu walivyomtosa Nduli na kumchakaza vibaya!
 
Aksante sana RUVUMAN umeongea maneno mazuri sana na ushauri mzuri kwangu nilikuwa najibu tu swali aliloniuliza kuwa ni kitu gani nakikumbuka sana katika Vta hiyo,Najua sana vitani kuna mambo mengine yanatendeka huko si mazuri kwa jamii lakini nitajitahidi sana na staadhiri USALAMA WA TAIFA nitakuwa naongelea tu hali halisi iliyotokea nashukuru kwa maoni yako.
"Kitu ambacho nakikumbuka sana ni pale nilipoingia kwenye uwanja wa vita na kupokelewa na Maiti za askari wetu watatu waliouwawa na Bomu la kutupwa kwa Mkono najua umesoma habari hiyo nimeiandika kwenye sehemu yangu ya kwanza,hiyo ilinifanya mimi nijisikie vibaya na kuwa hiyo ilikuwa kama Balaa fulani kwangu,lakini kibaya zaidi tukio hilo lilinisababishia mimi kuacha kula zile nyama za makopo na nyama zingine hasa nikifikiria miili ya askari wetu wale waliolipuliwa na Bomu la kutupwa kwa Mkono,Nilishindwa kabisa kula chakula kwa siku nzima lakini Rafiki yangu mmoja Jmanne Mwandamba yeye alipigana pia vita huko Msumbiji alinishauri nivute Bangi ili niondoe hiyo hali nami nilikubali na alinisimamamia ili nivute na akaniambia nimeze ule moshi mpaka aone umetokea puani nami kwa kuwa nilikuwa na tatizo nilifanya hivyo mara mbili"
-----------------------------------------------------------------------------------------
Komredi Echolima. Hongera sana. Viva ! Ila mengine ni siri za vitani. Si vizuri kuyaanika yote yanayotendeka uwanjani hadharani. Vita mara nyingi ni kipimo cha ustahimilivu na ukatili wa mwanadamu. Unajikuta ukifanya, kutenda au kushuhudia mambo ambayo huwezi kuthubutu katika hali ya kawaida. Hi ndiyo sababu mtu anapojitolea kujiunga na jeshi -hususan jeshi la ulinzi au kwenda vitani kuipigania nchi yake: huwa hiyo ndiyo biggest sacrifice ambayo mzalendo yoyote anaweza kufanya kwa ajili ya nchi yake. Somo kutokana na vita nyingi duniani ni kwamba "Msukumo wa kwanza wa kujiunga na jeshi la taifa unatakiwa kuwa uzalendo, na kwenda vitani ndicho kipimo cha uzalendo huo".
 
Kwangu mimi fahari sana kushiriki vita katika maisha yangu hii ni nadra sana kwa watu,nimepata uzoefu mwingi sana katika uwanja wa vita nimepata Marafiki wengi huko Uganda na si hivyo tu bali nilijua kabisa kuwa VITA si LELEMAMA vita ni kujitoa AMA ZAKO AMA ZAO na ukipoteza nafasi hiyo Umekwisha hutaacha chochote cha kukumbukwa.Kitu ambacho nakikumbuka sana ni pale nilipoingia kwenye uwanja wa vita na kupokelewa na Maiti za askari wetu watatu waliouwawa na Bomu la kutupwa kwa Mkono najua umesoma habari hiyo nimeiandika kwenye sehemu yangu ya kwanza,hiyo ilinifanya mimi nijisikie vibaya na kuwa hiyo ilikuwa kama Balaa fulani kwangu,lakini kibaya zaidi tukio hilo lilinisababishia mimi kuacha kula zile nyama za makopo na nyama zingine hasa nikifikiria miili ya askari wetu wale waliolipuliwa na Bomu la kutupwa kwa Mkono,Nilishindwa kabisa kula chakula kwa siku nzima lakini Rafiki yangu mmoja Jmanne Mwandamba yeye alipigana pia vita huko Msumbiji alinishauri nivute Bangi ili niondoe hiyo hali nami nilikubali na alinisimamamia ili nivute na akaniambia nimeze ule moshi mpaka aone umetokea puani nami kwa kuwa nilikuwa na tatizo nilifanya hivyo mara mbili moshi ukatokea puani cha ajabu nilisikia mlio mkali sana Masikioni mwangu ambao haukukoma nikasikia usingizi mzito nikaenda kulala kwenye Handaki langu lilokuwa la watu wanne cha ajabu nilipoingia ndani kulala niliona najibana sana maana kwangu limekuwa dogo sana nilitoka ndani ya handaki na kwenda kulala vihakani sikujua nimelala saa ngapi lakini nimekuja kuamka saa mbili asubuhi watu wamenitafuta kwenye ngome yetu sionekani na nilipoamka niliweza kula chakula vizuri sana niliweza kufuta kopo nne za nyama na chupa mbili za maji ya machungwa baada ya hapo niliendelea kula bila shida lakini tatizo share yangu nilikuwa sishibi mpaka nile mbili ndiyo najisikia toka siku hiyo sikujaribu tena kuvuta bangi maana ilinifanya ni-risk maisha yangu kwa kulala nje ya handaki nafikiria kama ningeamuka usiku huo na kuja kwenye ngome yangu wasingejua ni mimi wangenipiga Risasi na kufa bure kabisa,Hivyo tukio hili nalo nalikumbuka sana katika maisha yangu ya VITANI.Kuhusu kupoteza askari hiyo ni kwaida kabisa si rahisi mnabadirishana risasi wewe lisikupate hata moja lakini kikubwa ni Ushindi katika MEDANI.
Mkuu Echolima,

Nashukuru kwa majibu yako murua, nadhani imefika wakati kuandika kitabu, nadhani kitafanya vizuri.
 
Last edited by a moderator:
Wakati naleta uzi huu nilikuwa naelezea tu kumbukumbu zangu baada ya kuangalia TBC Wakati wanaonyesha siku ya mashujaa lakini kwa kuwa hapa ni kwa GT Mmenipandikizia wazo hili zuri la kutunga kitabu nawashukuru sana wote walionitia moyo katika sehemu hii ya kwanza,Naongea na jamaa ili lengo hilo litimie la kutengeneza kitabu Nimeona kweli kitapendeza sana lakini shukrani nyingi zitakuwa kwenu GT.
Mkuu Echolima,

Nashukuru kwa majibu yako murua, nadhani imefika wakati kuandika kitabu, nadhani kitafanya vizuri.
 
Last edited by a moderator:
Echolima,

..umesema ulikwenda vitani ukitokea chuo cha maafisa wa kijeshi monduli.unaweza kutupa historia fupi ya chuo hiki? kilianzishwa mwaka gani? wakuu waliopata kukiongoza etc etc. je, ni kweli kilianzishwa kwa msaada wa wachina??
 
Last edited by a moderator:
Jana wkati naangalia TBC Kwenye sherehe za Mashujaa zilizoongozwa na Rais nilipatwa na masikitiko makubwa sana hasa nilipouona ule Mnara wa MASHUJAA wa vita vya kagera Niliwakumbuka sana wapiganaji wenzangu waliopoteza maisha yao wakiwa mstari wa mbele wa mapambano ya kuuondoa Utawala wa Nduli Idd-Amin wa Uganda.
Niliwakumbuka askari 25 waliokufa wakiwa kwenye platoon yangu niliwakumbka mmoja baada ya mwingine na nilisema MASHUJAA TULIORUDI TUMERUDI KISHUJAA NA MASHUJAA WALIOKUFA WAMEKUFA KISHUJAA LENGO NA NIA YETU ILIKUWA NI MOJA TU KUILINDA HADHI YETU YAANI NCHI YETU.
Tarehe 28-10-1978 nilikuwa kambini LUGARO kikosi cha MMJ nilikuwa nimejipumzisha ghafla likapigwa Baragumu na tulipoenda kusikiliza tuliambiwa kuwa kuwa Idd-Amin kavamia huko Kagera tukaamliwa kuchukua vitu vyetu na kuvipeleka kwa STORE-KEEP vikiwa na majina mimi nilichukua bage langu na kuliandika jina langu na kulikabidhi kwa STORE-KEEPER.Na hapo hapo tulianza kuchukua vifaa vya kivita kama vile Combat mpya Bunduki SMG ya kwangu ilikuwa NHN 66482612.
Jioni hiyo ya 28-10-1978 Tulichukuliwa na magari ya Jeshi kwenda station ya Railway huko Dar-es-salaam na tuliondoka usiku huo huo kuelekea station ya ISAKA-Kahama.
Tulifika Station ya Railway ya Isaka 01-01-11-1978 Mchana tulikuta mabasi mengi sana ya kiraia yametusubiri kwenda Vitani mimi na wenzangu tulipanda Basi moja lilikuwa limeandikwa LUPONDIJE lilikuwa na namba MZA 234 Tuliondoka hapo isaka saa 9 mchana kuelekea Kahama mjini bahati mbaya sana Basi letu lilipofika tu pale stand ya Kahama Msafara wa magari yote ndo ulipoanza kuondoka na sisi ilibidi tupitilize tu bila kupata chakula hapo na kwa kufupisha habari nilifika kwenye uwanja wa Mapambano 03-11-1978 Mchana
Nilipofika wakati nateremka Kwenye Basi mimi niliitwa naMajor mmoja kuwa nichukue askari wanne niende kwenye Landrover ya Jeshi ilikuwa imefunikwa na turubai na nilifanya hivyo nilipofungua nilikutana na Maiti za askari wetu watatu waliolipuliwa na Bomu la kutupwa ilibidi tuzishushe Maiti hizo na mimi ilikuwa mara yangu ya kwanza kubeba Maiti katika Maisha yangu Kwangu mimi niliona kama ni Uchuro kwangu kufika tu Mstari wa mbele na kukutana na Maiti kwangu mimi ilinipa taabu sana.
VITA VILIPOANZA
Baada ya plani ya vita kukamilika ndipo majeshi yalipojipanga katika Brigade nne zikiongozwa na Brigadier Kiwelu, Brigadier Mayunga, Brigadier Marwa, na Brigadier Walden.
Msimamo wa vita ulikuwa umepangwa vizuri sana na ulikuwa na MAKAMANDA wafuatao-
1. Brigadier Marwa waliingia Uganda kwa kupitia mpaka na Rwanda na Zaire.
2. Brigadier Kiwelu alielekea Mbarara,
3. Brigadier Marwa alielekea Masaka
4. Brigadier Walden aliingia Uganda pia kwa kupitia Rwanda na kuelekea Kasese
5. Brigadier Mayunga yeye alibaki upande wa Tanzania ambapo brigade yake iligawanya katika makundi mawili, kundi moja liingia maeneo ya Mtukula kutokea Rwanda, , wakati kundi jingine lilibaki pale pale mto Kagera lakini likiwa na mizinga mizito (BM-40) kiasi cha kuweza kurushia makombora hayo moja kwa moja hadi askari wa Amini waliokuwa pale Mutukula. Ilichukua muda wa karibu wiki tatu kwa plani ya vita kukamilika na majeshi yetu kujipanga vile.

KIPIGO TOKA MAJESHI YA AMIN Baada ya majeshi ya Amin kuchukua eneo la Mutukula, walipandisha bendera ya Uganda na kubomoa lile daraja la mto Kagera. Brigadier Yusuf Himid ambaye alikuwa Brigade Commander wa Kanda ya Magharibi wakati huo alituma Battalion moja kujaribu kuvuka mto ule kwa kutumia mitumbwi wakati wa usiku kusudi wakapambane na wavamizi wale. Hata hivyo wakati platoon za kwanza kwanza zinaanza kutekeleza amri hiyo, wakaonekana na majeshi ya Amin ambayo yalikuwa yamejikita kilimani; Askari wetu wale walimiminiwa mizinga ambayo ilisababisha hasara kubwa kwa askari. ..bahati mbaya sana tulipigwa sana na majeshi ya amin na kupelekea Majeshi yetu kurudi nyuma kujijenga upya na kupelekea lile daraja kuvunjwa conteravertially Bahati nzuri mimi na wenzangu tulikuwa tumewahi kuvuka kwenye hilo Daraja na Tulipojijenga upya kazi ilianza na ilikuwa ngumu sana maana ilikuwa ni masika Mvua zilikuwa zinanyesha sana sana kwa sababu mimi na wenzangu tulikuwa askari wa Miguu Infrantry haikutupa taabu tuliendelea kusonga mbele kitendo hicho cha kurudishwa nyuma kilisababisha Brigedier Yusuph Hamid kuondolewa mstari wa mbele hivyo Brigade ya magharibi ikawekwa mikononi mwa Colonel (wakati huo) Kotta ambaye legacy yake kama kamanda shupavu pamoja na vijana aliopigana nao bega kwa bega na wote wakiwemo makamanda ,maafisa na askari waliokomboa afrika ..kama mnavyojua role ya jeshi letu kivita angola,msumbiji,namibia,comoro ets...kwa waliopo na waliotangulia mbele za haki.....

baada ya kile kipigo bregedia Yusuph Hamid aliondolewa from front line kama ilivyokawaida ya war plans...maana kamanda aliyepigwa hulazimika kupumzishwa kwanza ili atafakari wapi wapi alikosea.

Pale Ngome, kamanda aliyepanga vita ile yote alikuwa ni Colonel Lupogo Baada ya plani ya vita kukamilika ndipo majeshi yalipojipanga katika Brigade nne zikiongozwa na Brigadier Kiwelu, Brigadier Mayunga, Brigadier Marwa, na Brigadier Walden.

Kipindi hicho mimi nilikuwa na ki-radio kidogo cha mfukoni niliweza kusikiliza Radio Ujeruman na Radio nyingi tu kila zilipokuwa zinatangaza kutadhimini uwezo wetu wa kivita na uwezo wa Majeshi ya Amini ilionekana wazi kuwa Maeshi ya Amini yalikuwa Bora na zana Bora kuliko zetu kwa upande wa vifaru sisi tulikuwa na T 34 vya kizamani sana na Uganda vifaru walikuwa navyo T 55 Kwa wakati huo walikuwa navyo Bora sana kuliko sisi.Pia Amini alisikika kwenye vyombo vya habari akishangilia kuwa jeshi lake limeweka rekodi kwa kuteka Mtukula kwa muda wa dakika 25 tu.

VITA VYAANZA RASMI FRONTLINE Baada ya mejeshi yetu kujipanga ndipo filimbi ilipopigwa na Brigadier Kiwelu akarusha risasi ya kwanza dhidi ya Barracks moja ya Amin iliyokuwa pale Mbarara. Brigadier Marwa naye akawarushia risasi (ya kuwambia kuwa kazi imeanza) wale askari wa Amini walikuwa pale Mutukula. Brigadier Mayunga naye akadonoa kidogo kutokea Magharibi, harafu akatumia ujumbe mwingine wa BM-40 kutokea Kagera. Askari hao wa Amin waliokuwa pale Mutukula (Simba Battalion) walipoona wanapata kipigo kutoka pande zote wakaomba msaada kutoka Mbarara, hata hivyo wakaambiwa kuwa ile Battalion ya Mbarara nayo ilikuwa imeelemewa na kipigo cha Kiwelu, ndipo wakaomba msaada utokee Entebbe. Ile Battalion iliyoletwa kutokea Entebbe ikakutana na kizingiti pale Masaka ambapo Brigadier Marwa alikuwa kajichimbia. Wakati Amin bado anafikiria afanyeje kuhusu vipigo hivi vya Masaka, Mbarara na Mtukula, akapewa taarifa nyingine kuwa kulikuwa na kipigo kingine kimeanza kutokea Kasese kuelekea Kampala; hiki kilikuwa ni kipigo cha Brigadier Walden. Basi kuanzia hapo ndipo vita ile ilipoanza kupendeza kweli kweli kwa majeshi yetu,. Walianza kuwabomoa majeshi ya Amini yaliyokuwa miji hiyo huku yakiayaacha yale ya Mtukula pale pale na bendera yao ili wajifie wenyewe kwa kukosa supplies kwa vile walikuwa hawapati chakula wala msaada wowote kutoka ndani ya Uganda tena.

Baada ya kugundua kuwa kuwa alikuwa amezungukwa sana kwa vile majeshi yake mazito yalikuwa ndiyo yameshathibitiwa, Amini akaitangazia dunia kuwa amevamiwa na majeshi ya Tanzania (na kweli safari hii alikuwa amevamiwa kikwelikweli). Hata hivyo Nyerere naye akajibu kuwa jamaa huyu alituvamia akachukua sehemu ya Kagera, na kuitangazaia dunia. Ili kuionyesha dunia kuwa anasema kweli, Nyerere na Sokoine walikaribisha ujumbe wa OAU pale Kagera na kuwaomnyesha kuwa lie eneo la Mutukula bado lilikuwa linakaliwa na majeshi ya Amin na bendera yake bado inapepea. Kufanya hivyo kulifanya jumuia ya kimataifa isimwamini Amin katika kipindi ambacho alikuwa akipewa kipigo safi sana.
HISTORIA FUPI YA MAKAMANDA Mwaka 1978 jeshi letu likuwa na Major General wawili tu, Major General Twalipo (aliyekuwa mkuu wa majeshi wakati huo) na Major General Sarakiya ambaye alikuwa balozi wetu huko Nigeria. Baadaya ya Major General kulikuwa na Mabrigadier sita au saba tu: Brigadier Marwa, Brigadier Musuguri, Brigadier Mayunga, Brigadier Walden, Brigadier Kiwelu, Brigadier Yusuf Himid nadhani na Brigadier Mkisi. Chini ya Mabrigadier kulikuwa na makanali kadhaa ikiwa ni pamoja na akina Moses Nnauye, Abdallah Natepe na wengineo.

Jeshi letu lilikuwa limegawanyika katika Brigade kama nne hivi: Kusini, Magharibi, Mashariki, na Zanzibar. Baada ya vita ile, ndipo Twalipo alipopandiswa cheo na kuwa Luteni General wakati Mabrigadier wale walipandishwa kuwa ma-major general;Muundo wa jeshi letu ukabadilishwa kidogo kuwa na division tatu. Miaka wiliwili baadaye Luteni General Twalipo alipandishwa cheo tena na kuwa General ambapo chief of staff wa Jeshi akawa na cheo cha Luteni General. Baadaye sana cheo cha Brigadier kikabadilishwa na kuwa Brigadier General.

Kuhusu majina kama 'Black mamba" hayo yalikuwa maalumu au tunaweza kuita "usernames" ili kuficha utambulisho wao halisi hasa kwenye mawasiliano ya kijeshi vitani. Kila kamanda alikuwa na username yake.of course mengine yalitokana na jinsi kamanda alivyokabiliana na changamoto za kivita. Mfano Maj.Gen. Mwita Marwa (Kambale)aliitwa hivyo kwa sababu yeye binafsi na brigade yake walipigana wakiwa ndani ya maji kwa muda wa wiki mbili maji yanayofika kiunoni.Na bado walijitoa kimasomaso kukabiliana na adui. Brigade hiyo ilipata shida sana ya kuharibikiwa vifaa kama vile vya mawasiliano n.k.

KIPIGO CHA LUKAYA Hapo mimi mwenyewe nilishiriki na nilijua kabisa kuwa sasa ushindii ni wetu baada ya kufanyia AMBUSH ambayo askari wengi wa Libya walipoteza maisha yao na wengine wengi kutekwa ilikuwa AMBUSH tamu sana yenye mshiko ambayo baada ya saa moja magari mengi sana yalionekana yakiwaka moto na Vilio vilikuwa vimetawala eneo hilo walisikika wakisema ALLAH-AKBAR enzi hizo mimi sikujua wana maana gani
Kilichonihakikishia ushindi ni Amin kuleta askari ambao wana uwezo kupigana Jangwani leo kawaleta kupigana kwenye misitu minene kama ya Uganda nilijua fika kuwa wata-Prove failer tu.Mateka waliletwa mpaka Dar-es-salaam Cha kilichowashangaza wengi ni kuwa walirudishwa makwao Bure kabisa Mwalimu alikataa Msaada wa mafuta kwa mwaka mzima ambayo Libya iliahidi kulipa kukomboa askari wao waliotekwa katika vita hiyo.Hapo Mwalimu alisema sisi hatufanyi Biashara ya kuuza watu. lakini kuna historia nzuri kuhusu kutekwa kwa mji wa kampala, ambapo Brig. Kiwelu (wakati huo) aliongoza mapambano kutokea lukaya, kuanzia usiku wa manane mfululizo kwa karibu masaa nane, BM 24 zikiunguruma na Kampala ikawa mikononi mwa jeshi la ukombozi.

Jambo jingine, Generali Mboma wakati huo alikuwa Pilot na ndiye aliyeongoza kipigo kilichoziacha ndege yingi za amini kwenye uwanja wa Entebe taabani. Kama mnakumbuka ndege yetu iliyotunguliwa na majeshi yetu wenyewe kwa bahati mbaya,Rubani wa kijeshi aliyetunguliwa kwa makosa na JWTZ alikuwa ni Capt. Alexander Kaleya Mshana. Basi hawa akina mbona waliondoka Ngerere bila kutoa taarifa kwa makamanda wa vikosi vya nchi kavu (Hili lilifanyika makusudi) na wakaruka hadi Uganda. This wa the most precise target JWTZ did hadi Amin akalalamika kwamba JWTZ ina mamluki wa kukodiwa. Kwa sababu ndege za amini zilikuwa zinajianda kuja kushambulia TZ, lakini ghafla, wakajikuta Ndege zatu zinaruka chini sana usawa wa ziwa hivyo kusababisha taharuki kubwa sana, na kwa kuwa ziliruka chini sana na kwa mwendo wa SUPERSONIC yaani mwendo unaozidi sauti zilisababisha hofu kubwa na majengo mengi ya vioo vilivunjika-vunjika na wetu wengi walitibiwa kwa Presha,wakati huo Benki kuu ya Uganda nayo ikapigwa.

Battelfield tactics zilipangwa na Col. Lupogo.

Makamnada walioongoza vita walikuwa ni Brig. Marwa, Brig. Mayunga, Brig. Kiwelu, na Brigadier Walden. Hawa ndio waliongia msituni na wapiganaji. Makamanda hawa alipata vyeo vyao hivyo kutokana na umahiri wao wa katika uongozi wa kijeshi, na wote walihudhuria mafunzo ya uongozi wa kijeshi ndani na nje ya nchi mara kadhaa. Baada ya Uhuru hatukuwa na wasomi wengi katika majeshi yetu. In fact ni hawa hawa makamanda walioweka mkakati wa kuhimiza elimu jeshini na kuanzisha Elimu ya sekondari compulsory kwa wanajeshi wote na kuhimiza ajira za kijeshi kwa wasomi.




BRIG GEN MOSES NNAUYE huyu alishiriki kama muhamasishaji ..ni muhimu sana..akiwa ni vikosi vya bendi na burudani...[ie mwenge jazz,na kwaya ya luteni komba...]hawa walikuwa na wajibu wa kuhakikisha askari wanaburudishwa na kuliwazwa baada ya kazi ngumu...na kuwatia hamasa...na propaganda za ushindi...
Ma-CDF wetu kwa kadri niwezavyo.
WAKUU WA MAJESHI CDF

1.1964-1974: Sarakikya
2.1974-1980: Twalipo
3.1980-1988: Musuguri
4.1988-1994: Kiaro
5.1994-2001: Mboma
6.2001-2007: Waitara
7.2007- Mwamunyange

CHANGAMOTO ZA VITANI
Kuna askari wengi waliokuwa mstari wa mble wanasema Lupogo alishindwa KABISA kuendesha vita na kurudishwa makao makuu. Kikosi chake cha 205 kuchukuliwa na Kimario. Kimario aliendesha mapigano makali na kikosi chake cha 205 kiliweza kukata katikati ya Uganda mpaka Nimule kwenye mpaka wa Uganda na Sudan. 205 ndiyo kikosi kilichopoteza kifaru kimoja baada ya mapigano makali ya masaa 8 ili kuteka daraja muhimu la Maporomoko ya KarumaKwa maajabu, Nyerere alimpandisha cheo Lupogo kuwa Meja Jenerali na kumuacha yule aliyepiganisha vita na kushinda Kimario. Wewe jiulize inakuaje aliyeshindwa vita kupandishwa cheo na yule liyeshinda kuachwa mpaka alipopandishwa cheo na Rais A.H Mwinyi.Hizo ndizo changamoto za Mstari wa mbele walizokuwa wanazipata wapiganishaji wetu. ikimzunguzia Marehemu Gen. Imran Kombe. Katika makamanda waliopiganisha vita kitaalamu na kwa ufundi wa hali ya juu mmoja wao alikuwa ni Gen Kombe
2.Gen Msuguri alikuwa siyo msomi sana lakini mabrigedia wake walikuwa wanaelimu ya kutosha na ndiyo maana waliweza kupanga mashambulizi ya kiufundi, ungeweza kuona jinsi hivi vikosi vilikuwa vinasonga mbele basi ungeona haikuwa kazi ya kubahatisha.Kutokusoma kwa Gen Msuguri siyo hoja kwani alikuwa na uwezo wa kujua mapungufu yake na ndio maana alizungukwa na makamanda wazuri, na hiyo ni sifa kubwa kwa kiongozi.
3.Askari wa Lupogo walipata matatizo kwasababu walikuwa wanapigana na kikosi cha Amini kilichokuwa mlimani.Hivyo wao walikosa OP Obsevartion Post wakajikuta wanashambuliwa kirahisi.

..kuna uwezekano kabisa kwamba Lupogo alipandishwa cheo kwa kuzingatia rekodi yake ktk vita nzima na siyo wiki tatu za mapambano ambayo alifanya vibaya. labda tatizo lilitokana na intelligence na military planning.

Lt.Col.Ben Msuya. Huyu ndiyo aliongoza utekaji wa jiji la kampala, na baadaye ku-act kama mayor wa kampala, mkuu wa itifaki, na mwisho kuandaa shughuli ya kuapishwa Yussuf Lule.



..Lt.Col.Hassani Boma na Lt.Col.Mazora wametajwa kwa umahiri wao ktk medani ya vita.

Maj.Gen.Silas Mayunga "mti mkavu" ndiyo aliingia kijiji cha koboko ambako alizaliwa Iddi Amini.
luteni col ben msuya ..alistaafu jeshi akiwa MEJA JENERALI..na jukumu lake la mwisho alikuwa mkuu wa kamandi ya tabora...yenye jukumu la kuangalia hadi kigoma ,Rukwa
..Masaka na Mbarara zilikuwa smoothered na mizinga kabla ya kutekwa. Hapo hatukupoteza askari wengi.

..Amini na askari wake waliingia uoga tangu wapigwe na kutolewa Kagera. walianza kudai kuna Wacuba,Wachina,...ati wanasaidia Tanzania.


..baada ya Mbarara kutekwa Mayunga alipandishwa cheo kuwa Major General na kupewa Brigade mbili kuziongoza. Chini yake walikuwepo Brig.Hemedi Kitete[rip] na Brig.Roland Makunda.

..Namkumbuka Brig.Gen.Ramadhani Haji Faki kama mmoja wa makamanda toka Zenj waliotunukiwa nishani na Mwalimu Nyerere uwanja wa taifa.

..Mchango wa Mwita Marwa ktk vita vya Kagera ulikuwa mkubwa.
Every nation and every country has been blessed by great individuals. They have left footprints. Their lives and actions tells us the purpose of life and living. Maj. Gen Mwita Chacha Marwa a.k.a Kambale was never a scholar neither a good politicians but he is worth a role model to many of us. we can learn from him and make our lives beuatiful and worth living. God has decided to call him at the time when Tanzania may have wanted him more, we are in a critical time of struggle, struggle that can not be compared to theirs at that time. But it a struggle that pose danger to survival of this nation
Ndugu zangu vita huwa havipiganiwi ardhini, angani au kwenye maji peke yake..., vita hupiganwa pia kwenye Media, na kuongeza chumvi hufanya watu wasife moyo na kuwapa motisha..., "Ingekuwa ajabu sana kama vyombo vya habari vya nchi yetu vingesema jana tulipigwa sana lakini leo afadhali tunajaribu kuwapiga........." Think about it.. Mimi Binafsi siwezi kumsahau Baba Nape kweli alikuwa Mwanasiasa safi aliweza kuwahamasisha watu mpaka wengine tulisahau kama kuna kufa vitani alikuwa na uwezo mzuri sana wa kujieleza na kumwelezea Adui alivyo dhaifu mpaka ninyi askari mnamkubali na mnaamini kuwa kweli Adui huyu si chochote tutamfumua tu,vilevile John komba alikuwa anauwezo wa kutuburudisha kiasi cha kujisikia kuwa tuko nyumbani na aliyekuwa tunamzimia sana ni wale vijana wa Johns corner ile Bendi ya JKT na tuliporudi kweli walituimbia wimbo ambao wengi uliwatoa macchozi ambao unasema hivi-MASHUJAA TULIORUDI TUMERUDI KISHUJAA NA MASHUJAA WALIOKUFA WAMEKUFA KISHUJAA……………….Mwenge Jazz nao hawakuwaw nyuma kutumbuiza wapiganaji tunawashukuru sana.[/QUOTE
Eti Mbowe naye kamanda
 
Wakati naleta uzi huu nilikuwa naelezea tu kumbukumbu zangu baada ya kuangalia TBC Wakati wanaonyesha siku ya mashujaa lakini kwa kuwa hapa ni kwa GT Mmenipandikizia wazo hili zuri la kutunga kitabu nawashukuru sana wote walionitia moyo katika sehemu hii ya kwanza,Naongea na jamaa ili lengo hilo litimie la kutengeneza kitabu Nimeona kweli kitapendeza sana lakini shukrani nyingi zitakuwa kwenu GT.
Mkuu Echolima,

Ni kweli unachosema hujue Tanzania hakuna vitabu vya kumbukumbuku vya historia yetu, mfano ukitaka kusoma historia ya Tanganyika mpaka utafute vitabu vya wazungu kina Judith Listowel, John Iliffe na wengine.

Angalia watu kama kina Shigongo leo matajiri kwa kuandika vitabu vya udaku tu.

Kwa nini wewe usipate utajiri kupitia kitabu chako ambacho kina facts tupu, takupa mfano mmoja.

Wanajeshi wa Marekani wale wote waliopigana vita vya Vietnam wote waliandika vitabu mpaka wale wapishi, achilia mbali hawa waliopigana vita Iraq, Libya.

Kuna vitabu maarufu vya vita vya Vietnam, kama Things The Carried, The Bettle That Changed, A Rumor of War, The Quiet American, vipo vingi sana na vinaendelea kusomwa duniani kote.

Kuna vizazi vipya havijuhi chochote kuhusu vita vya Kagera, hata hao waliokuwepo wakati wa vita bado walikuwa wanaitaji kujua mengi.

Anzisha Project hii mapema kama una kumbukumbu za wanajenshi wenzako jipange kaka, kitabu chako kikiwa na matoleo mawili moja la Kiingereza lingine la Kiswahili mbona utapumzika vizuri.

51-xywZN09L.jpg
a-rumor-of-war-book-review1.jpg


CC; JokaKuu,
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hebu hii history andika kitabu,najua kweli sio mwandishi omba msaada kwa waandishi wakusaidie,nadhani watu kama nyinyi ni watu muhimu katika history ya nchi yetu,
Watoto wetu leo hata mashuleni sidhani kama wanafundishwa habari za vita ya kagera wala kujua tu majina ya mashujaa wetu,
Khofu yangu miaka 20 ijayo nchi itakuwa imepoteza history yake yote,
 
Kuna mtu ameni-PM na kuniuliza vyeo alivyokuwa anaitwa AMIN kipindi hicho kwa faida ya wengine alikuwa anaitwa LIFE PRESDENT,FIELD MARSHAL,DR.IDD AMIN DADA VC,MC,DSO and CBE.Vyombo vyote vya habari nchini Uganda walipokuwa wanatangaza habari za Amin Lazima wataje vyeo hivyo vyote.labda tu nielezee kirefu cha vifupisha vya vyeo vyake hivyo.VC-Victoria Cross,MC-Military cross.DSO-Distinguished Service Order.CBE-Coqueror Of the British Empire.
 
Kuna mtu ameni-PM na kuniuliza vyeo alivyokuwa anaitwa AMIN kipindi hicho kwa faida ya wengine alikuwa anaitwa LIFE PRESDENT,FIELD MARSHAL,DR.IDD AMIN DADA VC,MC,DSO and CBE.Vyombo vyote vya habari nchini Uganda walipokuwa wanatangaza habari za Amin Lazima wataje vyeo hivyo vyote.labda tu nielezee kirefu cha vifupisha vya vyeo vyake hivyo.VC-Victoria Cross,MC-Military cross.DSO-Distinguished Service Order.CBE-Coqueror Of the British Empire.

sembuse dogo kagame mdeki barabara na kujiona kashakuwa superpower!
 
Mkuu wa Kaya alikuwa amemaliza UDSM miaka minne kabla ya vita, na katika viongozi maarufu wanaoonekana karibu na high table wakati mwalimu Nyerere akihutubia wananchi kuhusu nia, sababu na uwezo wa kumpiga Amin, ni JK na Mkapa tu. Psychologically walionyesha special type ya concentration, excitement na labda ukaribu na Mwalimu. Wote wanaotangaza nia ya kugombea sasa hivi wenye umri unaofanana na akina JK au Mkapa hawaonekani. Tafakari...........
 
Mkuu Echolima

mbali na majeshi ya miguu mlitumia pia majeshi ya majini katika vita hii??

Vipi kuhusu majeshi ya anga nayo yalitumika sana au hatukua wazuri sana upande wa anga??
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wa Kaya alikuwa amemaliza UDSM miaka minne kabla ya vita, na katika viongozi maarufu wanaoonekana karibu na high table wakati mwalimu Nyerere akihutubia wananchi kuhusu nia, sababu na uwezo wa kumpiga Amin, ni JK na Mkapa tu. Psychologically walionyesha special type ya concentration, excitement na labda ukaribu na Mwalimu. Wote wanaotangaza nia ya kugombea sasa hivi wenye umri unaofanana na akina JK au Mkapa hawaonekani. Tafakari...........

Kwa hiyo unataka kusema nini??

Ili iweje??
 
Back
Top Bottom