Vita vya Kagera: Historia yangu - Sehemu ya kwanza

Vita vya Kagera: Historia yangu - Sehemu ya kwanza

uploadfromtaptalk1375110337290.jpg
 
Mkuu Echolima

mbali na majeshi ya miguu mlitumia pia majeshi ya majini katika vita hii??

Vipi kuhusu majeshi ya anga nayo yalitumika sana au hatukua wazuri sana upande wa anga??
MFUMO DUME yote hayo nimeelezea katika sehemu ya pili labda tu subiri tu sehemu ya pili nimeelezea kila kitu pamoja na mengine mengi tu.
 
Last edited by a moderator:
@Echolima
Kitu kinachinishangaza ni kuwa sasa hivi ni karibu 33 tangu vita imalizike, kwa maana kuwa habari za jeshi ni declassified kwamba zinaweza kuwekwa hadharani au kuongelewa bila kuathiri usalama.
Sijui kwanini watu kama akina Kiwelu, Msuya ,Maneno na wengine hawajitokezi kueleza experience zao kama documentary au vita.
Pasco hamuoni opportunity ya habari hapo?
Mkuu Nguruvi3, sisi Watanzania tuna problem na serious writers!. Tangu miaka ya 60 UDSM ilipoanzishwa, tumekuwa tukitoa wahitimu wa fasihi, lakini mpaka leo miaka 50 baadae hatuna fasihi yoyote ya maana!. Hadi kesho, kiada na rejea za literature bado kina Chinua Achebe, Ngungi wa Thing'o, Okot P'Bitek etc, where are the Tanzanians?!.

Hivi unajua mpaka leo hata historia ya Uhuru wametuandikia wazungu?!. Waandishi wetu wako wapi ili hali wapigania Uhuru wapo?!. Ndio maana nilimpongeza Maalim Mohamed Said na ile historia ya wazee wake wa Gerezani, japo mauongo mengi!, but he did something!.
Biographies za viongozi wetu tunangoja tuandikiwe na wazungu!.

Hivi unaweza kuamini mpaka sasa leo hapa ninapoandika, hakuna historia rasmi ya TANU iliyoko documented?!. Tenda alipewa Kanyama Chiume (Malawi), alipofariki kabla ya kukamilisha kazi, kazi hiyo imeishia hapo!.

Interview Public and Private Nyerere, ilifanywa once na jarida la African Now, hadi ameondoka nothing more!.
Jumbe is bed ridden, Mwinyi is growing old, Ben anawadharau Watanzania, hutuna simulizi zao zozote!, na wataondoka!.

Licha kukosa wenye uwezo to that job right, sisi wenye interest tupo, but with what resources?.
Niliwahi kuripoti humu kuhusu kuanzishwa kwa kituo cha kuhifadhi kumbukumbu za waasisi wetu.
Pasco
 
Hio usiite vita!
Hio ilikuwa ni fujo tu!
Na ghasia za watu wenye magobole!

Sasa hii ukiita vita na vietnam uite nini!?
Mkuu, hapa umenifanya nicheke sanaaaa. Sikujua kuwa kuwa yale mapigano na Idd Amin yalikuwa ni fujo na ghasia zilizosababishwa na watu wenye magobore! Hebu nipe darsa kiundani niweze kuelewa. Manake mimi na watanzania tulio wengi ile ilikuwa ni vita
 
Hapo Mkuu umepiga mkuki moyoni WE MUST WAKE-UP AND ACT NOW yote uliyoyasema mimi yameniingia sana ni lazima nasi tutende..
Mkuu Nguruvi3, sisi Watanzania tuna problem na serious writers!. Tangu miaka ya 60 UDSM ilipoanzishwa, tumekuwa tukitoa wahitimu wa fasihi, lakini mpaka leo miaka 50 baadae hatuna fasihi yoyote ya maana!. Hadi kesho, kiada na rejea za literature bado kina Chinua Achebe, Ngungi wa Thing'o, Okot P'Bitek etc, where are the Tanzanians?!.

Hivi unajua mpaka leo hata historia ya Uhuru wametuandikia wazungu?!. Waandishi wetu wako wapi ili hali wapigania Uhuru wapo?!. Ndio maana nilimpongeza Maalim Mohamed Said na ile historia ya wazee wake wa Gerezani, japo mauongo mengi!, but he did something!.
Biographies za viongozi wetu tunangoja tuandikiwe na wazungu!.

Hivi unaweza kuamini mpaka sasa leo hapa ninapoandika, hakuna historia rasmi ya TANU iliyoko documented?!. Tenda alipewa Kanyama Chiume (Malawi), alipofariki kabla ya kukamilisha kazi, kazi hiyo imeishia hapo!.

Interview Public and Private Nyerere, ilifanywa once na jarida la African Now, hadi ameondoka nothing more!.
Jumbe is bed ridden, Mwinyi is growing old, Ben anawadharau Watanzania, hutuna simulizi zao zozote!, na wataondoka!.

Licha kukosa wenye uwezo to that job right, sisi wenye interest tupo, but with what resources?.
Niliwahi kuripoti humu kuhusu kuanzishwa kwa kituo cha kuhifadhi kumbukumbu za waasisi wetu.
Pasco
 
Mkuu, hapa umenifanya nicheke sanaaaa. Sikujua kuwa kuwa yale mapigano na Idd Amin yalikuwa ni fujo na ghasia zilizosababishwa na watu wenye magobore! Hebu nipe darsa kiundani niweze kuelewa. Manake mimi na watanzania tulio wengi ile ilikuwa ni vita

We kama umecheka basi inatosha!
manake ukichokoa sana hapa, utasababisha afande anitafute na lile gobole lake!!
na mimi kukimbia siwezi!

We kubali tu kuwa hio ya tz na uganda na ile ya Hitler zote zinaitwa vita! Hata sisi zile biscuti ngumuu za jeshi tulikula pia!
Na amin tulimfuata kwake tukamchapa vlvl!

kwa hiyo sina la kuongezea hapo!
 
Ni wanajeshi wangapi wa Tz waliopoteza maisha kwenye vita ya kagera.
Maana nikiangalia kama ulivyoeleza ni kama wachache
 
Mkuu Nguruvi3, sisi Watanzania tuna problem na serious writers!. Tangu miaka ya 60 UDSM ilipoanzishwa, tumekuwa tukitoa wahitimu wa fasihi, lakini mpaka leo miaka 50 baadae hatuna fasihi yoyote ya maana!. Hadi kesho, kiada na rejea za literature bado kina Chinua Achebe, Ngungi wa Thing'o, Okot P'Bitek etc, where are the Tanzanians?!.

Hivi unajua mpaka leo hata historia ya Uhuru wametuandikia wazungu?!. Waandishi wetu wako wapi ili hali wapigania Uhuru wapo?!. Ndio maana nilimpongeza Maalim Mohamed Said na ile historia ya wazee wake wa Gerezani, japo mauongo mengi!, but he did something!.
Biographies za viongozi wetu tunangoja tuandikiwe na wazungu!.

Hivi unaweza kuamini mpaka sasa leo hapa ninapoandika, hakuna historia rasmi ya TANU iliyoko documented?!. Tenda alipewa Kanyama Chiume (Malawi), alipofariki kabla ya kukamilisha kazi, kazi hiyo imeishia hapo!.

Interview Public and Private Nyerere, ilifanywa once na jarida la African Now, hadi ameondoka nothing more!.
Jumbe is bed ridden, Mwinyi is growing old, Ben anawadharau Watanzania, hutuna simulizi zao zozote!, na wataondoka!.

Licha kukosa wenye uwezo to that job right, sisi wenye interest tupo, but with what resources?.
Niliwahi kuripoti humu kuhusu kuanzishwa kwa kituo cha kuhifadhi kumbukumbu za waasisi wetu.
Pasco

Taaluma ya uandishi wa vitabu Tanzania ilikufa siku nyingi sana baada ya vita wakati uchumi ulipoanza kuharibika, na watu wakaanza kuwa wanatafuta namna ya kusurvive kwa njia yoyote ile. Kwa hiyo manunuzi ya vitabu yakatoweka kabisa. Ndiyo maana kwa muda mrefu Tanzania imekuwa haina maduka binafsi ya vitabu ispokuwa vile vya kiada tu. Vitabu karibu vyote vya fasihi na riwaya viliandikwa kabla ya mwaka 1980: Musiba (ingawa walikuwa akikopi baadhi kutoka Nick Carter), Kezilahabi, Shaffi, Ben Mtobwa, Katalambula, na wengineo waanidhsi mashuhuri waliandika kabla ya mwaka huo wa 1980. Baada ya hapo kukatokea waandishi uchwara sana hasa pale UDSM waliokuwa wakiandika bila kutumia akili, na vitabu vyao vikawa pia havinunuliwi. Uandishi wa vitabu huchochewa na market, watu huandika vitabu ili vinunuliwe.
 
Jana wkati naangalia TBC Kwenye sherehe za Mashujaa zilizoongozwa na Rais nilipatwa na masikitiko makubwa sana hasa nilipouona ule Mnara wa MASHUJAA wa vita vya kagera Niliwakumbuka sana wapiganaji wenzangu waliopoteza maisha yao wakiwa mstari wa mbele wa mapambano ya kuuondoa Utawala wa Nduli Idd-Amin wa Uganda.
Niliwakumbuka askari 25 waliokufa wakiwa kwenye platoon yangu niliwakumbka mmoja baada ya mwingine na nilisema MASHUJAA TULIORUDI TUMERUDI KISHUJAA NA MASHUJAA WALIOKUFA WAMEKUFA KISHUJAA LENGO NA NIA YETU ILIKUWA NI MOJA TU KUILINDA HADHI YETU YAANI NCHI YETU.
Tarehe 28-10-1978 nilikuwa kambini LUGARO kikosi cha MMJ nilikuwa nimejipumzisha ghafla likapigwa Baragumu na tulipoenda kusikiliza tuliambiwa kuwa kuwa Idd-Amin kavamia huko Kagera tukaamliwa kuchukua vitu vyetu na kuvipeleka kwa STORE-KEEP vikiwa na majina mimi nilichukua bage langu na kuliandika jina langu na kulikabidhi kwa STORE-KEEPER.Na hapo hapo tulianza kuchukua vifaa vya kivita kama vile Combat mpya Bunduki SMG ya kwangu ilikuwa NHN 66482612.
Jioni hiyo ya 28-10-1978 Tulichukuliwa na magari ya Jeshi kwenda station ya Railway huko Dar-es-salaam na tuliondoka usiku huo huo kuelekea station ya ISAKA-Kahama.
Tulifika Station ya Railway ya Isaka 01-01-11-1978 Mchana tulikuta mabasi mengi sana ya kiraia yametusubiri kwenda Vitani mimi na wenzangu tulipanda Basi moja lilikuwa limeandikwa LUPONDIJE lilikuwa na namba MZA 234 Tuliondoka hapo isaka saa 9 mchana kuelekea Kahama mjini bahati mbaya sana Basi letu lilipofika tu pale stand ya Kahama Msafara wa magari yote ndo ulipoanza kuondoka na sisi ilibidi tupitilize tu bila kupata chakula hapo na kwa kufupisha habari nilifika kwenye uwanja wa Mapambano 03-11-1978 Mchana
Nilipofika wakati nateremka Kwenye Basi mimi niliitwa naMajor mmoja kuwa nichukue askari wanne niende kwenye Landrover ya Jeshi ilikuwa imefunikwa na turubai na nilifanya hivyo nilipofungua nilikutana na Maiti za askari wetu watatu waliolipuliwa na Bomu la kutupwa ilibidi tuzishushe Maiti hizo na mimi ilikuwa mara yangu ya kwanza kubeba Maiti katika Maisha yangu Kwangu mimi niliona kama ni Uchuro kwangu kufika tu Mstari wa mbele na kukutana na Maiti kwangu mimi ilinipa taabu sana.
VITA VILIPOANZA
Baada ya plani ya vita kukamilika ndipo majeshi yalipojipanga katika Brigade nne zikiongozwa na Brigadier Kiwelu, Brigadier Mayunga, Brigadier Marwa, na Brigadier Walden.
Msimamo wa vita ulikuwa umepangwa vizuri sana na ulikuwa na MAKAMANDA wafuatao-
1.Brigadier Marwa waliingia Uganda kwa kupitia mpaka na Rwanda na Zaire.
2.Brigadier Kiwelu alielekea Mbarara,
3.Brigadier Marwa alielekea Masaka
4.Brigadier Walden aliingia Uganda pia kwa kupitia Rwanda na kuelekea Kasese
5. Brigadier Mayunga yeye alibaki upande wa Tanzania ambapo brigade yake iligawanya katika makundi mawili, kundi moja liingia maeneo ya Mtukula kutokea Rwanda, , wakati kundi jingine lilibaki pale pale mto Kagera lakini likiwa na mizinga mizito (BM-40) kiasi cha kuweza kurushia makombora hayo moja kwa moja hadi askari wa Amini waliokuwa pale Mutukula. Ilichukua muda wa karibu wiki tatu kwa plani ya vita kukamilika na majeshi yetu kujipanga vile.

KIPIGO TOKA MAJESHI YA AMIN Baada ya majeshi ya Amin kuchukua eneo la Mutukula, walipandisha bendera ya Uganda na kubomoa lile daraja la mto Kagera. Brigadier Yusuf Himid ambaye alikuwa Brigade Commander wa Kanda ya Magharibi wakati huo alituma Battalion moja kujaribu kuvuka mto ule kwa kutumia mitumbwi wakati wa usiku kusudi wakapambane na wavamizi wale. Hata hivyo wakati platoon za kwanza kwanza zinaanza kutekeleza amri hiyo, wakaonekana na majeshi ya Amin ambayo yalikuwa yamejikita kilimani; Askari wetu wale walimiminiwa mizinga ambayo ilisababisha hasara kubwa kwa askari. ..bahati mbaya sana tulipigwa sana na majeshi ya amin na kupelekea Majeshi yetu kurudi nyuma kujijenga upya na kupelekea lile daraja kuvunjwa conteravertially Bahati nzuri mimi na wenzangu tulikuwa tumewahi kuvuka kwenye hilo Daraja na Tulipojijenga upya kazi ilianza na ilikuwa ngumu sana maana ilikuwa ni masika Mvua zilikuwa zinanyesha sana sana kwa sababu mimi na wenzangu tulikuwa askari wa Miguu Infrantry haikutupa taabu tuliendelea kusonga mbele kitendo hicho cha kurudishwa nyuma kilisababisha Brigedier Yusuph Hamid kuondolewa mstari wa mbele hivyo Brigade ya magharibi ikawekwa mikononi mwa Colonel (wakati huo) Kotta ambaye legacy yake kama kamanda shupavu pamoja na vijana aliopigana nao bega kwa bega na wote wakiwemo makamanda ,maafisa na askari waliokomboa afrika ..kama mnavyojua role ya jeshi letu kivita angola,msumbiji,namibia,comoro ets...kwa waliopo na waliotangulia mbele za haki.....

baada ya kile kipigo bregedia Yusuph Hamid aliondolewa from front line kama ilivyokawaida ya war plans...maana kamanda aliyepigwa hulazimika kupumzishwa kwanza ili atafakari wapi wapi alikosea.

Pale Ngome, kamanda aliyepanga vita ile yote alikuwa ni Colonel Lupogo Baada ya plani ya vita kukamilika ndipo majeshi yalipojipanga katika Brigade nne zikiongozwa na Brigadier Kiwelu, Brigadier Mayunga, Brigadier Marwa, na Brigadier Walden.

Kipindi hicho mimi nilikuwa na ki-radio kidogo cha mfukoni niliweza kusikiliza Radio Ujeruman na Radio nyingi tu kila zilipokuwa zinatangaza kutadhimini uwezo wetu wa kivita na uwezo wa Majeshi ya Amini ilionekana wazi kuwa Maeshi ya Amini yalikuwa Bora na zana Bora kuliko zetu kwa upande wa vifaru sisi tulikuwa na T 34 vya kizamani sana na Uganda vifaru walikuwa navyo T 55 Kwa wakati huo walikuwa navyo Bora sana kuliko sisi.Pia Amini alisikika kwenye vyombo vya habari akishangilia kuwa jeshi lake limeweka rekodi kwa kuteka Mtukula kwa muda wa dakika 25 tu.

VITA VYAANZA RASMI FRONTLINE Baada ya mejeshi yetu kujipanga ndipo filimbi ilipopigwa na Brigadier Kiwelu akarusha risasi ya kwanza dhidi ya Barracks moja ya Amin iliyokuwa pale Mbarara. Brigadier Marwa naye akawarushia risasi (ya kuwambia kuwa kazi imeanza) wale askari wa Amini walikuwa pale Mutukula. Brigadier Mayunga naye akadonoa kidogo kutokea Magharibi, harafu akatumia ujumbe mwingine wa BM-40 kutokea Kagera. Askari hao wa Amin waliokuwa pale Mutukula (Simba Battalion) walipoona wanapata kipigo kutoka pande zote wakaomba msaada kutoka Mbarara, hata hivyo wakaambiwa kuwa ile Battalion ya Mbarara nayo ilikuwa imeelemewa na kipigo cha Kiwelu, ndipo wakaomba msaada utokee Entebbe. Ile Battalion iliyoletwa kutokea Entebbe ikakutana na kizingiti pale Masaka ambapo Brigadier Marwa alikuwa kajichimbia. Wakati Amin bado anafikiria afanyeje kuhusu vipigo hivi vya Masaka, Mbarara na Mtukula, akapewa taarifa nyingine kuwa kulikuwa na kipigo kingine kimeanza kutokea Kasese kuelekea Kampala; hiki kilikuwa ni kipigo cha Brigadier Walden. Basi kuanzia hapo ndipo vita ile ilipoanza kupendeza kweli kweli kwa majeshi yetu,. Walianza kuwabomoa majeshi ya Amini yaliyokuwa miji hiyo huku yakiayaacha yale ya Mtukula pale pale na bendera yao ili wajifie wenyewe kwa kukosa supplies kwa vile walikuwa hawapati chakula wala msaada wowote kutoka ndani ya Uganda tena.

Baada ya kugundua kuwa kuwa alikuwa amezungukwa sana kwa vile majeshi yake mazito yalikuwa ndiyo yameshathibitiwa, Amini akaitangazia dunia kuwa amevamiwa na majeshi ya Tanzania (na kweli safari hii alikuwa amevamiwa kikwelikweli). Hata hivyo Nyerere naye akajibu kuwa jamaa huyu alituvamia akachukua sehemu ya Kagera, na kuitangazaia dunia. Ili kuionyesha dunia kuwa anasema kweli, Nyerere na Sokoine walikaribisha ujumbe wa OAU pale Kagera na kuwaomnyesha kuwa lie eneo la Mutukula bado lilikuwa linakaliwa na majeshi ya Amin na bendera yake bado inapepea. Kufanya hivyo kulifanya jumuia ya kimataifa isimwamini Amin katika kipindi ambacho alikuwa akipewa kipigo safi sana.
HISTORIA FUPI YA MAKAMANDA Mwaka 1978 jeshi letu likuwa na Major General wawili tu, Major General Twalipo (aliyekuwa mkuu wa majeshi wakati huo) na Major General Sarakiya ambaye alikuwa balozi wetu huko Nigeria. Baadaya ya Major General kulikuwa na Mabrigadier sita au saba tu: Brigadier Marwa, Brigadier Musuguri, Brigadier Mayunga, Brigadier Walden, Brigadier Kiwelu, Brigadier Yusuf Himid nadhani na Brigadier Mkisi. Chini ya Mabrigadier kulikuwa na makanali kadhaa ikiwa ni pamoja na akina Moses Nnauye, Abdallah Natepe na wengineo.

Jeshi letu lilikuwa limegawanyika katika Brigade kama nne hivi: Kusini, Magharibi, Mashariki, na Zanzibar. Baada ya vita ile, ndipo Twalipo alipopandiswa cheo na kuwa Luteni General wakati Mabrigadier wale walipandishwa kuwa ma-major general;Muundo wa jeshi letu ukabadilishwa kidogo kuwa na division tatu. Miaka wiliwili baadaye Luteni General Twalipo alipandishwa cheo tena na kuwa General ambapo chief of staff wa Jeshi akawa na cheo cha Luteni General. Baadaye sana cheo cha Brigadier kikabadilishwa na kuwa Brigadier General.

Kuhusu majina kama 'Black mamba" hayo yalikuwa maalumu au tunaweza kuita "usernames" ili kuficha utambulisho wao halisi hasa kwenye mawasiliano ya kijeshi vitani. Kila kamanda alikuwa na username yake.of course mengine yalitokana na jinsi kamanda alivyokabiliana na changamoto za kivita. Mfano Maj.Gen. Mwita Marwa (Kambale)aliitwa hivyo kwa sababu yeye binafsi na brigade yake walipigana wakiwa ndani ya maji kwa muda wa wiki mbili maji yanayofika kiunoni.Na bado walijitoa kimasomaso kukabiliana na adui. Brigade hiyo ilipata shida sana ya kuharibikiwa vifaa kama vile vya mawasiliano n.k.

KIPIGO CHA LUKAYA Hapo mimi mwenyewe nilishiriki na nilijua kabisa kuwa sasa ushindii ni wetu baada ya kufanyia AMBUSH ambayo askari wengi wa Libya walipoteza maisha yao na wengine wengi kutekwa ilikuwa AMBUSH tamu sana yenye mshiko ambayo baada ya saa moja magari mengi sana yalionekana yakiwaka moto na Vilio vilikuwa vimetawala eneo hilo walisikika wakisema ALLAH-AKBAR enzi hizo mimi sikujua wana maana gani
Kilichonihakikishia ushindi ni Amin kuleta askari ambao wana uwezo kupigana Jangwani leo kawaleta kupigana kwenye misitu minene kama ya Uganda nilijua fika kuwa wata-Prove failer tu.Mateka waliletwa mpaka Dar-es-salaam Cha kilichowashangaza wengi ni kuwa walirudishwa makwao Bure kabisa Mwalimu alikataa Msaada wa mafuta kwa mwaka mzima ambayo Libya iliahidi kulipa kukomboa askari wao waliotekwa katika vita hiyo.Hapo Mwalimu alisema sisi hatufanyi Biashara ya kuuza watu. lakini kuna historia nzuri kuhusu kutekwa kwa mji wa kampala, ambapo Brig. Kiwelu (wakati huo) aliongoza mapambano kutokea lukaya, kuanzia usiku wa manane mfululizo kwa karibu masaa nane, BM 24 zikiunguruma na Kampala ikawa mikononi mwa jeshi la ukombozi.

Jambo jingine, Generali Mboma wakati huo alikuwa Pilot na ndiye aliyeongoza kipigo kilichoziacha ndege yingi za amini kwenye uwanja wa Entebe taabani. Kama mnakumbuka ndege yetu iliyotunguliwa na majeshi yetu wenyewe kwa bahati mbaya,Rubani wa kijeshi aliyetunguliwa kwa makosa na JWTZ alikuwa ni Capt. Alexander Kaleya Mshana. Basi hawa akina mbona waliondoka Ngerere bila kutoa taarifa kwa makamanda wa vikosi vya nchi kavu (Hili lilifanyika makusudi) na wakaruka hadi Uganda. This wa the most precise target JWTZ did hadi Amin akalalamika kwamba JWTZ ina mamluki wa kukodiwa. Kwa sababu ndege za amini zilikuwa zinajianda kuja kushambulia TZ, lakini ghafla, wakajikuta Ndege zatu zinaruka chini sana usawa wa ziwa hivyo kusababisha taharuki kubwa sana, na kwa kuwa ziliruka chini sana na kwa mwendo wa SUPERSONIC yaani mwendo unaozidi sauti zilisababisha hofu kubwa na majengo mengi ya vioo vilivunjika-vunjika na wetu wengi walitibiwa kwa Presha,wakati huo Benki kuu ya Uganda nayo ikapigwa.

Battelfield tactics zilipangwa na Col. Lupogo.

Makamnada walioongoza vita walikuwa ni Brig. Marwa, Brig. Mayunga, Brig. Kiwelu, na Brigadier Walden. Hawa ndio waliongia msituni na wapiganaji. Makamanda hawa alipata vyeo vyao hivyo kutokana na umahiri wao wa katika uongozi wa kijeshi, na wote walihudhuria mafunzo ya uongozi wa kijeshi ndani na nje ya nchi mara kadhaa. Baada ya Uhuru hatukuwa na wasomi wengi katika majeshi yetu. In fact ni hawa hawa makamanda walioweka mkakati wa kuhimiza elimu jeshini na kuanzisha Elimu ya sekondari compulsory kwa wanajeshi wote na kuhimiza ajira za kijeshi kwa wasomi.

BRIG GEN MOSES NNAUYE huyu alishiriki kama muhamasishaji ..ni muhimu sana..akiwa ni vikosi vya bendi na burudani...[ie mwenge jazz,na kwaya ya luteni komba...]hawa walikuwa na wajibu wa kuhakikisha askari wanaburudishwa na kuliwazwa baada ya kazi ngumu...na kuwatia hamasa...na propaganda za ushindi...
Ma-CDF wetu kwa kadri niwezavyo.
WAKUU WA MAJESHI CDF

1.1964-1974: Sarakikya
2.1974-1980: Twalipo
3.1980-1988: Musuguri
4.1988-1994: Kiaro
5.1994-2001: Mboma
6.2001-2007: Waitara
7.2007- Mwamunyange

CHANGAMOTO ZA VITANI
Kuna askari wengi waliokuwa mstari wa mble wanasema Lupogo alishindwa KABISA kuendesha vita na kurudishwa makao makuu. Kikosi chake cha 205 kuchukuliwa na Kimario. Kimario aliendesha mapigano makali na kikosi chake cha 205 kiliweza kukata katikati ya Uganda mpaka Nimule kwenye mpaka wa Uganda na Sudan. 205 ndiyo kikosi kilichopoteza kifaru kimoja baada ya mapigano makali ya masaa 8 ili kuteka daraja muhimu la Maporomoko ya KarumaKwa maajabu, Nyerere alimpandisha cheo Lupogo kuwa Meja Jenerali na kumuacha yule aliyepiganisha vita na kushinda Kimario. Wewe jiulize inakuaje aliyeshindwa vita kupandishwa cheo na yule liyeshinda kuachwa mpaka alipopandishwa cheo na Rais A.H Mwinyi.Hizo ndizo changamoto za Mstari wa mbele walizokuwa wanazipata wapiganishaji wetu. ikimzunguzia Marehemu Gen. Imran Kombe. Katika makamanda waliopiganisha vita kitaalamu na kwa ufundi wa hali ya juu mmoja wao alikuwa ni Gen Kombe
2.Gen Msuguri alikuwa siyo msomi sana lakini mabrigedia wake walikuwa wanaelimu ya kutosha na ndiyo maana waliweza kupanga mashambulizi ya kiufundi, ungeweza kuona jinsi hivi vikosi vilikuwa vinasonga mbele basi ungeona haikuwa kazi ya kubahatisha.Kutokusoma kwa Gen Msuguri siyo hoja kwani alikuwa na uwezo wa kujua mapungufu yake na ndio maana alizungukwa na makamanda wazuri, na hiyo ni sifa kubwa kwa kiongozi.
3.Askari wa Lupogo walipata matatizo kwasababu walikuwa wanapigana na kikosi cha Amini kilichokuwa mlimani.Hivyo wao walikosa OP Obsevartion Post wakajikuta wanashambuliwa kirahisi.

..kuna uwezekano kabisa kwamba Lupogo alipandishwa cheo kwa kuzingatia rekodi yake ktk vita nzima na siyo wiki tatu za mapambano ambayo alifanya vibaya. labda tatizo lilitokana na intelligence na military planning.

Lt.Col.Ben Msuya. Huyu ndiyo aliongoza utekaji wa jiji la kampala, na baadaye ku-act kama mayor wa kampala, mkuu wa itifaki, na mwisho kuandaa shughuli ya kuapishwa Yussuf Lule.

..Lt.Col.Hassani Boma na Lt.Col.Mazora wametajwa kwa umahiri wao ktk medani ya vita.

Maj.Gen.Silas Mayunga "mti mkavu" ndiyo aliingia kijiji cha koboko ambako alizaliwa Iddi Amini.
luteni col ben msuya ..alistaafu jeshi akiwa MEJA JENERALI..na jukumu lake la mwisho alikuwa mkuu wa kamandi ya tabora...yenye jukumu la kuangalia hadi kigoma ,Rukwa
..Masaka na Mbarara zilikuwa smoothered na mizinga kabla ya kutekwa. Hapo hatukupoteza askari wengi.

..Amini na askari wake waliingia uoga tangu wapigwe na kutolewa Kagera. walianza kudai kuna Wacuba,Wachina,...ati wanasaidia Tanzania.

..baada ya Mbarara kutekwa Mayunga alipandishwa cheo kuwa Major General na kupewa Brigade mbili kuziongoza. Chini yake walikuwepo Brig.Hemedi Kitete[rip] na Brig.Roland Makunda.

..Namkumbuka Brig.Gen.Ramadhani Haji Faki kama mmoja wa makamanda toka Zenj waliotunukiwa nishani na Mwalimu Nyerere uwanja wa taifa.

..Mchango wa Mwita Marwa ktk vita vya Kagera ulikuwa mkubwa.
Every nation and every country has been blessed by great individuals. They have left footprints. Their lives and actions tells us the purpose of life and living. Maj. Gen Mwita Chacha Marwa a.k.a Kambale was never a scholar neither a good politicians but he is worth a role model to many of us. we can learn from him and make our lives beuatiful and worth living. God has decided to call him at the time when Tanzania may have wanted him more, we are in a critical time of struggle, struggle that can not be compared to theirs at that time. But it a struggle that pose danger to survival of this nation
Ndugu zangu vita huwa havipiganiwi ardhini, angani au kwenye maji peke yake..., vita hupiganwa pia kwenye Media, na kuongeza chumvi hufanya watu wasife moyo na kuwapa motisha..., "Ingekuwa ajabu sana kama vyombo vya habari vya nchi yetu vingesema jana tulipigwa sana lakini leo afadhali tunajaribu kuwapiga........." Think about it.. Mimi Binafsi siwezi kumsahau Baba Nape kweli alikuwa Mwanasiasa safi aliweza kuwahamasisha watu mpaka wengine tulisahau kama kuna kufa vitani alikuwa na uwezo mzuri sana wa kujieleza na kumwelezea Adui alivyo dhaifu mpaka ninyi askari mnamkubali na mnaamini kuwa kweli Adui huyu si chochote tutamfumua tu,vilevile John komba alikuwa anauwezo wa kutuburudisha kiasi cha kujisikia kuwa tuko nyumbani na aliyekuwa tunamzimia sana ni wale vijana wa Johns corner ile Bendi ya JKT na tuliporudi kweli walituimbia wimbo ambao wengi uliwatoa macchozi ambao unasema hivi-MASHUJAA TULIORUDI TUMERUDI KISHUJAA NA MASHUJAA WALIOKUFA WAMEKUFA KISHUJAA……………….Mwenge Jazz nao hawakuwa nyuma kutumbuiza wapiganaji tunawashukuru sana.

Nimesoma bila kuchoka!!
 
Ni wanajeshi wangapi wa Tz waliopoteza maisha kwenye vita ya kagera.
Maana nikiangalia kama ulivyoeleza ni kama wachache

Ndugu si rahisi kupata takwimu exactly kwa Vita kama hii ambayo imechua mezi ni ngumu sana labda uongozi wa juu wao wanaweza kutoa ilikuwa rahisi kidogo kama vita ingechukua wiki au siku chache.
 
Ndugu si rahisi kupata takwimu exactly kwa Vita kama hii ambayo imechua mezi ni ngumu sana labda uongozi wa juu wao wanaweza kutoa ilikuwa rahisi kidogo kama vita ingechukua wiki au siku chache.

Kwann takwimu zisipatikane??kwani serikali haijui ilipeleka askari wangapi??na wangapi walirudi waki hai,majeruhi au waliofariki??
 
Kwann takwimu zisipatikane??kwani serikali haijui ilipeleka askari wangapi??na wangapi walirudi waki hai,majeruhi au waliofariki??
Takwimu za vita inategemea unataka kupata kwa wakati gani.
Ni lazima uwe specific kwasababu madhara ya vita yanaendelea hata baada ya vita kwisha.

Kwa mfano, Nyerere alisema katika hotuba yake ya kurudisha askari 'tumepoteza vijana wetu 400'.
Leo makaburi ya Bunazi yana masuijaa 630 kama sijasoksea kwa kauli za JK juzi.

Hata baada ya vita vifo viliendelea kutokana na post war traumatic disorder syndrome (PTSD).
Kwa nchi masikini kama yetu na isiyokuwa na utaratibu ni ngumu kujua wangapi wali commit sucide, wangapi walifariki kutokana na majeraha ambayo hayakupata matibabu sahihi, wangapi walipatwa na matatizo kwa chanzo chake kikiwa ni vita n.k. katika wakati huo wa vita na hata miezi michache baadaye.

Na pengine chombo ambacho kingeweza kutoa japo takwimu zinazokaribiana na ukweli ni JWT.
Sidhani Echolima au askari mwingine anaweza kuongea kwa usahihi, nadhani ni swali gumu sana let us be fair
 
Kwann takwimu zisipatikane??kwani serikali haijui ilipeleka askari wangapi??na wangapi walirudi waki hai,majeruhi au waliofariki??
Takwimu zenyewe zipo na serikali ndiyo walizozitoa mimi nilikuwa nasema kama mimi siwezi kupata takwimu hizo labda Uongozi wa juu ndio unaweza kutoa lakini kama nilivyosema inakuwa ngumu sana kuzitoa kwa mtu binafsi.
 
WELL-DONE Nguruvi3 ni kweli kabisa uliyoyasema kwenye sehemu yangu ya tatu nimeongelea sana kuhusiana na PTSD ambayo naweza kusema imeua askari wengi sana waliotoka Vitani askari aliyekuwa akikumbwa na PTSD wanakufa sana na ikumbukwe kwa nchi kama yetu haikuweza kukundua hili.
Takwimu za vita inategemea unataka kupata kwa wakati gani.
Ni lazima uwe specific kwasababu madhara ya vita yanaendelea hata baada ya vita kwisha.

Kwa mfano, Nyerere alisema katika hotuba yake ya kurudisha askari 'tumepoteza vijana wetu 400'.
Leo makaburi ya Bunazi yana masuijaa 630 kama sijasoksea kwa kauli za JK juzi.

Hata baada ya vita vifo viliendelea kutokana na post war traumatic disorder syndrome (PTSD).
Kwa nchi masikini kama yetu na isiyokuwa na utaratibu ni ngumu kujua wangapi wali commit sucide, wangapi walifariki kutokana na majeraha ambayo hayakupata matibabu sahihi, wangapi walipatwa na matatizo kwa chanzo chake kikiwa ni vita n.k. katika wakati huo wa vita na hata miezi michache baadaye.

Na pengine chombo ambacho kingeweza kutoa japo takwimu zinazokaribiana na ukweli ni JWT.
Sidhani Echolima au askari mwingine anaweza kuongea kwa usahihi, nadhani ni swali gumu sana let us be fair
 
Kuna huyu afande mstaafu wa JKT alikuwa anaitwa Brigedia Gen Stanslaus Msilu yeye hakupigana vita hii Echolima.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom