Vita vya Kagera: Historia yangu - Sehemu ya kwanza

hata mie nimeliona hilo aisee....
sio udini hata kidogo, nasikia muhidin kimario alikuwa rafiki mkubwa wa idd amin kabla ya vita ya kagera na hii inatokana kwamba walishahudhuria mafunzo ya kijeshi pamoja.kutokana na sababu hiyo majeshi ya tz yalipoingia kampala alikuwa anawasiliana nae na akamshauri atoroke kwani alikuwa karibu kukamatwa! Hii aliifanya makusudi kwani kimario alikuwa ameshachoshwa na vita na kusababisha scandle kubwa kwa kimario kwani nia ya tanzania ilikuwa ni kumkamata akiwa hai au akiwa amekufa. Pia ikumbukwe amini aliendelea kujificha kampala wiki tatu baada ya majeshi ya tanzania kuiteka kampala.
 
Naona hapa Echolima atatuwekea Historia ya vuta sawasawa, maana wakati wa kupiganisha Mawasiliano yote yanasikika kwa walio upande mmoja na hasa kuanzia Platoon mpaka kwa Makamanda wa juu na ndio maana misaada km ndege na vifaru vinashambuliwa bila kugongana, sasa km Kamanda Mbogo aliweza wasiliana na Idd amini bila wenzake kujua ni AJABU.
Kuhusu kupandishwa vyeo, naweza kukubaliana na Ngongo kwani Vita vya Kagera vilipoisha tuwanajeshi walipewa vyeo Serikalini na sehemu nyingine, na licha ya kuupata Ubunge wa Moshi Mjini Kamanda Mbogo Waziri wa mambo ya ndani na ni yeye aliyebadilisha Vyeo vya KiPOLISI vilivyokuwa vikitambulika tangu enzi za mkoloni na kuweka hivi vya sasa vinavyowiana na vya Kijeshi na alijaribu kuondoa tofauti nyingi katika majeshi hayo na kuwa moja.
Amekuwa mkuu wa Mkoa wa Dar-Es-Salaam na akahamishiwa Dodoma kuwa Mkurugenzi wa CDA na enzi hizo ni wakati wa Awamu ya Pili ya Mzee ruksa na huenda hapo ndipo udhaifu wake au upendeleo ukaanza kujionyesha na akashtakiwa mahakamani kwa matumizi mabaya ya Madaraka hasa kiwanda cha vigae cha ZUZU na ugawaji viwanja.
Nakumbuka Jeshini walimwita na ndipo akatunukiwa Maja Generali na marupurupu yote
anaishi Dodoma Msalato ni Mkulima wa zabibu na Mjasiria mali wa ufyatuaji wa vigae na matofali hasa kwa ujenzi wa hizi barabara mpya. Echolima mwaga hiyo awamu ya pili maana tunaisubiri kuliko ilivyo
 
Last edited by a moderator:
​Asante sana mkuu kwa historia hiyo nzuri. Imetukumbusha sana mashujaa wa nchi yetu. We're soooo proud of you. God bless you.
 
Historia hii inapaswa kuandikwa sasa hivi kwa uhakika na kwa makini sana. baadhi ya mambo aliyoandika ndugu Echolima ni mambo niliyoandika hapa zamani sana mara tu baada ya kifo cha General Marwa. Kuna watu wana rekodi kamili za vita ile lakini hawataki kuitoa; sisi tunaojitahidi kutumia kumbukumbu zetu tu kulingana tulivyokuwa tunajulishwa wakati ule inawezekana tunakosea hapa na pale au kusahau baadhi ya facts za muhimu. Kama ningekuwa katika taaluma ya Historia nadhani hii ni topiki moja mbayo ningeifanyia kazi kwa nguvu sana ili vizazi vyetu vijavyo viwe na picha kamili ya vita ile. Leo hii mimi pamoja na kuwa kuanzia mwaka 1982 nilihamishia nguvu za ubongo wangu katika uwanja wa Science, hupenda sana kusoma historia; leo hii nina rekodi nyingi zana za kihistoria kuhusu nchi yetu wakati wa mkoloni. Ninaamini kuwa akipatikana mtu mzuzri wa kuandika historia ya vita hii, itsaidia sana katika training za askari wetu na kwenye uwanja wa diplomacy.
 
Mkuu Echolima wanaukumbi wanasubiri awamu ya pili.Suala la Kamanda Mbogo unaweza kulizungumzia kiduchu nimejitahidi kueleza yale ninayoyajua lakini bado kuna baadhi ya wanaukumbi wangependa kusikia kutoka kwako.
 
Last edited by a moderator:
Natarajia kurudi wiki ijayo maana nilikuwa safari,Mengi kweli umeyaelezea na wazo la kitabu nimelichukua kwa uzito wa hali ya juu nitashirikiana na GREAT-THINKERS ili tuweze kufanya kitu cha kuweka mambo kuwa sawa.Vuta tu subira nakuja na sehemu ya pili.
Mkuu Echolima wanaukumbi wanasubiri awamu ya pili.Suala la Kamanda Mbogo unaweza kulizungumzia kiduchu nimejitahidi kueleza yale ninayoyajua lakini bado kuna baadhi ya wanaukumbi wangependa kusikia kutoka kwako.
 
Last edited by a moderator:
waislam bhana,mnakera sana..
yani mnaleta udini kwenye kila kitu,.
punguzeni ujinga bhana..ptuuuuuuuu

Halafu mi sijaona muhindi anaitwa juma!
Hebu regebisha hilo jina kwanza!


Nakutahadharisha Unapoandika hoja zako usijumuisha 1.7 bilion muslims! Kwa sababu ya hoja ya mtu mmoja!

Mbona yule mgalatia aliyebaka mtoto mdogo juzi kanisani sisi hatukusema "nyie wagalatia wabakaji!"
Na kwanini siku zote akikosea Athumani inakuwa "WAISLAMU wamekosea" lkn akikosea JOHN inabaki John kakosea?

Unatoa kashfa kwa mabilion ya watu wasiohusika kwa Kosa la mtu mmoja?
 

mkuu hata ungekua wewe ndio sisi ungechoka kusubiri..
 

haaaahaa teh teh! Wenyewe wanajihita waindi koko sijui wanagamahanisha nn
 

Mkuu Kichuguu umeshaambiwa hii haikuwa vita. Sasa kuna sababu gani za kuandika historia?
 
Mkuu Kichuguu umeshaambiwa hii haikuwa vita. Sasa kuna sababu gani za kuandika historia?
Labda historia ina maana nyingine tena. Kimsingi historia ni rekodi kamili ya jambo lolote lililotokea zamani; je hakukuwa na mapigano ya kijeshi baina ya Tanzania na Uganda hata kama haikuwa vita?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…