Echolima
Hii ni kazi nzuri sana kwetu sote. Hatupaswi kuisahau historia yetu.
Ili kufanikisha uandikwaji na uchapaji wa kitabu najitolea kuifanya kazi ya Professional Typesetting and Graphic Design.
Watunzi na wachapishaji wengi wa vitabu siku hizi wamekuwa hawazingatii muonekano bora zaidi wa vitabu vyao, hivyo huishia kupata mapato duni yanayowakatisha tamaa.
Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi katika kubaini, kutambua, kukuza na kuimarisha soko la wasomaji. Kwa kuwa mbinu za kukabiliana na changamoto hizi zote ninazijua, niko tayari kufanya kazi na wewe pia katika hili, kwa manufaa yetu na taifa pia. Tukifanya kazi nzuri ninaamini kwamba Serikali inaweza kutuunga mkono na kukifanya kitabu hiki kuwa sehemu ya vitabu ambavyo vinaweza kuchukuliwa kama mojawapo ya vitabu vya somo la historia kwa shule za sekondari.
Licha ya kuwa mwanaharakati mwanamapinduzi, mimi pia ni mjasiriamali kwenye sekta ya ubunifu.
Trust me. I know what I am saying. You are looking at the goose that is about to lay its famous golden eggs.