William
Wewe ni msomi kila uandishi una agenda na kila agenda utumika kama propaganda machine; kama uliwahi kuongea na Binaisa na Lule hilo hatuwezi kulithibitisha wote ni marehemu (R.I.P) ukweli wa hilo unalijua wewe binafsi; labda nikuulize tu mbona umelitoa leo hii na si jana; "halafu mnakuja watu wazima hapa mnataka kutudanganya na kututisha na maneno mengi uongo uongo as if wote hapa ni watoto wadogo, kama mmezidiwa hoja ni kukaa pembeni tu"! Hapa hatutishani tunadebate kutafuta ukweli wa hoja; katika mada yako unadai vita vimetugharimu hadi leo ninachotaka kukwambia tu kabla Mwl. Nyerere hajaachia madaraka alifanya kazi kubwa ya kuhakikisha madeni yetu na Urusi na China yanasamehewa kitu ambacho alifamikiwa kwa kiasi kikubwa; nimegusia ufisadi ili ujue nini kinachotugharimu watanzania umejaribu kuhusisha gharama vita ndio inayotugharimu umejaribu kukwepa ukweli watanzania wanajua nini kinachowagharimu; Mkuu unapo debate ni wigo mkubwa yataingia yaliyomo na yasiyokuwamo umesoma hilo kwenye humanities; nimesema hizo ni propaganda za wazi najua unaelewa vyema siasa na propaganda vinamix bila matatizo. HIZI NI PROPAGANDA KWANI ULIANZA NA BIAFRA NA SASA VITA NA IDD AMIN HIVI WEWE KAMA MTANZANIA HUNA HATA MOJA ZURI LA KUMJADILI NYERERE? NAAMINI YAPO MENGI SANA ALIYOYAFANYA NYERERE AMBAYO YALIKUNUFAISHA NA YANAENDELEA KUKUNUFAISHA HADI LEO HII. Tuendelee na hoja
Chama
Gongo la Mboto DSM
- Chama saafi sana sasa unaongea hoja: HOWEVER tizama mimi ninakuja hapa kutoa maoni yangu bila kujali anybody, niaamini JF kazi yetu inatakiwa kuwa kukosoa, kukosoa kila kiongozi hakuna wa kumbakisha wala kumuogopa, maneno ya agenda na propaganda siyajui, mimi umeona ninaposhambuliwa personal, huwa ninatumia fursa hiyo kujiweka vizuri na public kwa sababu ninajaribu kumuonyesha aliyerusha matusi hana FACTS, wala haelewi anachosema, lakini sio kumjibu matusi na vitisho kama mnavyofanya!
- Lets say mimi nime-specialize na mapungufu ya policies za MWalimu, kwa nini na wewe usi-specialize na mapungufu ya policies za Rais wa sasa, badala yake unaleta maneno ya propaganda hakuna hapa hizo hapa, mimi ninakata ishus tu sina cha nani wala nani, kama kuna anyeijhisi kwamba nina personal problems naye then waombeni utawala wa JF kuwa na limiti ya uwezo wa mtu hapa kufikiria, asiruhusiwe kufikiria mapungufu ya policies za MWalimu!
- I mean mbona sasa hizi kurasa tatu za mwisho tunajadili ishus na kinaeleweka kabisa kinachozungumzwa, kwa nini haumkuanza hivi toka mwanzo, I mean bravo people naona sasa tunaanza kukata ishu kama JF style. Kwamba Mwalimu aliamaliza madeni ndio kwanza leo ninasikia kwa mara ya kwanza.
- Mimi sipo hapa JF kujadili mazuri kihivyo, nipo hapa kukosoa kwanza kama for that ninavunja sheria yoyote ya JF then nitaacha kuchangia, lakini otherwise mwendo ni ule ule mdundo, mnanishngaza sana kwamba ninaanzisha thread ambayo hamuipendi, lakini mnakuja kulalamika na kuigeuza another story huo sio ustaarabu, jamani tuwacheni tukate ishus hapa msitutishe na vitabu uchwara wala hoja uchwara, kama thread ni mbaya iwache au omba mods waifute, lakini wacheni vitisho na mikwara jamani!!
William.