Watanzania hakika tu watu wa ajabu sana. Kuna baadhi yetu ambao kwa bahati mbaya sana hawataki kabisa kusikia vipenzi wao wakisemwa kwa mabaya hata kama kweli mabaya hayo waliyafanya. Kama walivyo mashabiki wa CHADEMA ambao hawataki kabisa kusikia mtu kama Dr. Slaa akisemwa kwa mabaya, kuna wengine ambao hawataki hata kidogo kusikia baya likisemwa dhidi ya Nyerere. Hawa wote, ukisema baya kuhusu vipenzi vyao basi watakuja juu na kukupa majibu ya kifedhuli na kihayawani
.lakini wote hawa bado wanajiita ni Greatest Thinkers!!
Sasa nirudi kwenye mada.
Ukweli bado utabaki pale pale kwamba kwa pale ilipofikia, Tanzania haikuwa na budi bali kuingia vitani dhidi ya Amin. Hata hivyo, bado ukweli unabaki paleplae kwamba point ambayo ilikuwa lazima tuingie vitani ilisababishwa na Nyerere mwenyewe.
Baada ya Amin kumpindua Obotte, Milton Obotte alipewa hifadhi na Nyerere. Kimsingi, hapakuwa na ubaya wowote kwa Nyerere kumpa Obote hifadhi hapa Tanzania. Hadi Nyerere anampa hifadhi Obote pamoja na maelfu ya wakimbizi bado Amin alikuwa hajaonesha uchokozi wa wazi dhidi ya Tanzania. Tatizo kuu lilianza pale Wakimbizi wa Uganda waliopo Tanzania walipovuka mpaka wa Tanzania na kuingia Uganga na kufanya jaribio la kumpindua Amin. Hata hivyo, jaribio hilo lilishindwa na kasha kikosi hicho kikarudi tena Tanzania.
Haya sasa, wale wanaotaka kujitia upofu kwa makusudi; watuambie ni kiongozi gani duniani angevumilia kitendo ambacho kilifanywa na Tanzania kwa kuacha Waganda waliopo nchini wavuke mpaka na kuingia Uganda kwenda kufanya jaribio la mapinduzi kasha kurudi tena nchini. Je, hapo Tanzania ilikuwa ni hifadhi ya wakimbizi au kituo cha kijeshi kwa wale waliokuwa na nia ya kumtoa Amin madarakani?! Kimsingi, hakuna jaribio la mapinduzi ambalo linaweza kufanyika pasipo na maandalizi ya kijeshi. Hata mapinduzi madogo kama yale ya Zanzibar 1964 palikuwa na mafunzo pamoja na maandalizi ya kijeshi kabla ya mapinduzi hayo kufanyika. Je, hawa wakimbizi wa Uganda ambao walitoka Tanzania na kuingia Uganda kwenda kumpindua Amin walichukulia wapi maandalizi na mafunzo ya mapinduzi amabayo walienda kuyafanya?! Je, mnataka kusema kwamba serikali ya Tanzania hawakufahamu dhamira ya Waganda ambao walikuwepo nchini?! Hivi kweli Intelligence system ya Nyerere ambahyo ilikuwa very competent haikufahamu kwamba wakimabizi wa Uganda walikuwa na nia ya kuvuka mpaka na kuingia Uganda kufanya mapinduzi?! Kwa intelligence system ya sasa inawezekana lakini sio ile ya Nyerere!!
Hivyo basi, ingawaje Amin alivamia Tanzania na kuikalia sehemu ya Mkoa wa Kagera na kudai ni ya Uganda lakini source ya chokochoko ni Nyerere mwenyewe ambae hakufurahishwa kitendo cha Amin kumpindua Obote; swahiba wa Nyerere! Aidha, ikumbukwe kwamba, hata OAU haikuiunga mkono Tanzania kwa kile kilichoonekana Tanzania kuingilia masuala ya ndani ya Uganda!! Na kwa kunoesha kwamba hawakupendezwa na suala la Tanzania kuingilia masuala ya ndani Uganda, OAU ilikataa ombi la Nyerere alilotaka kwamba OAU imlaani Amin!! Na kwa kumuumbua zaidi, Mkutano wa OAU ulifanyika Uganda ambao Nyerere alisusa kwenda kwavile tu OAU haikukubaliana na takwa lake la kuitaka jumuiya hiyo imlaani Amin.
Swali lingine linafuata hapo! Hivi kweli OAU ilikuwa na mapenzi zaidi kwa Amin kuliko Nyerere ambae alijitolea kwa ari na mali katika ukombozi wa Afrika; Kusini mwa Jangwa la Sahara?! Bila shaka, jibu ni HAPANA
.sina shaka yoyote kwamba OAU ilikuwa inampenda zaidi NYerere(Tanzania) kuliko Amini lakini bila shaka walisukumwa na methali ya kiswahili isemayo Mnyonge Mnyongeni, Haki Yake Mpeni! Kwamba, hata kama ni kwali Amin alikuwa ni mshenzi dhidi ya Tanzania na watu wake lakini ushenz wake dhidi ya Tanzania ulisababishwa na sisi wenyewe.
Kitu kimoja ambacho alifudhu Nyerere kwenye vita hivyo ni PROPAGANDA! Alipiga propaganda za kutosha hadi akafanikiwa na kuonesha kwamba tatizo ni Amin
.! Propaganda hizi zilienezwa kwa nji mbaliambali ikwemo nyimbo, machapicho na kwa njia ya muziki. Watanzania wote wakaamini kwamba Amin ni tatizo ingawaje kiini cha tatizo ulikuwa ni Nyerere mwenyewe!!
Kwa kumalizia; kama alivyosema William; kwavile Amin aliivamia Tanzania kulikuwa na ulazima gani wa kuhakikisha tunamfutilia mbali?! Jibu ni kwamba, hatukuwa na sababu hiyo! Ilitosha kabisa kumwondoa kwenye mipaka ya Tanzania na kasha kuimarisha mipaka yaetu!! Lakini kwavile lengo la Nyerere alikuwa tu kuilinda mipaka ya Tanzania, basi alihakikisha anaingia ndani kabisa ya Uganda na kumwondoa Amin madarakani!!