Vita vya Kagera: Nini chanzo? Kulikuwa na ulazima?

Jasusi, nafikiri wengi wenu mmesahau kitu kimoja...Je unakumbuka taarifa tuliyowahi kupewa na Field Marshall ES humu JF kuhusu nia ya kuandika upya historia ya Tanzania? Hiki kitabu kinatakiwa kiende sambamba na kile cha Mohamed Said cha kukosoa historia ya harakati za uhuru wa Tanganyika. Hawa watu wanaamini kuwa kama wataweza kumcut down to size Mwalimu, basi watafanikiwa kuwainua watu wengine wamkaribie na ikiwezekana wamfikie na kumpita. Wakati Mohamed Said analilia wazee wake wa Gerezani, William anamlilia mzee wake wa Dodoma na kuna tetesi hiki kitabu kinaweza kutoka muda wowote kama kitakuwa hakijatoka tayari. Hizi mada anazoleta William ni katika kupima tu kina cha maji kabla ya kujitosa...na bado tutashuhudia mengi!
Mag3,
Kama usemayo ni kweli basi afadhali hicho kitabu kitoke mapema tujue ukweli na pumba. Mohamed Said amejitahidi sana kutuaminisha kuwa bila watu wa Gerezani Tanzania isingekuwa huru na Nyerere, aliyefadhiliwa nao, aliwatupa mkono. Sasa kama kweli Mzee Malecela ameandika kitabu kinachopotosha historia, na mimi ninamheshimu sana huyu mzee, basi ataonekana in his true colours, na sisi tuliokuwa tunamheshimu huyu mzee tutamwona mtu wa ovyo kama ilivyobainika kwa Iddi Simba.
 
JokaKuu, mwalimu hakuwa mpumbavu na mjinga. Ni rais mpumbavu tu ndie angechukua uamuzi wa kumsimika Obote moja kwa moja. Bado Mwalimu alitaka kuushawishi umma kwamba aliingia Uganda kwa ajili ya kuitetea Tanzania kwahiyo endapo Obote angesimikwa moja kwa moja basi tuhuma dhidi yake kwamba alijiingiza Uganda kwa ajili ya kumtetea Obote zisingekuwa na ubishi kama ilivyo sasa. Pamoja na Yusuf Lule kupachikwa urais wa Uganda(kwa msaada wa Tanzania); Nyerere alifahamu kwamba itabidi uchaguzi ufanyike Uganda na alikuwa na uhakika kwamba swahibu wake Obote atashinda tu!!

By the way, nini kitakachonifanya nitaharuki baada ya kuambiwa kwamba baada ya Amin kuondolewa ni Lule ndie alipachikwa Urais?! Yaani ulitarajia hiyo kwangu iwe ni habari ngeni? Usinichekeshe wakati sijisikii kucheka hivi sasa! Also, kwanini mnakwepa kujibu hoja ya msingi.....kwamba, je wakati Obote allies wanavuka mpaka wa Tanzania na kuingia Uganda na kufanya jaribio la mapinduzi; serikali ya Tanzania ilifahamu au haikufahamu?! Ingewezekana vipi Waganda wafanye maandalizi ya mapinduzi ndani ya Tanzania na Tanzania isifahamu! Na kwanini hata baada ya Tanzanaia kufahamu kwamba Obote na watu wake walikiuka miiko ya ukimbizi bado watu hao waliendelea kubaki Tanzania?! Acheni mawazo mgando, binafsi simchukii Nyerere lakini sioni taabu hata kidogo kuyaelezea mafyongo aliyoyafanya! Hata kama mtaona ni chuki dhidi ya Mwalimu, hayo ni yenu lakini ukweli bado utabaki pale pale.....katu siwezi kuisoma historia sawa na ninavyosoma maandiko ya dini!!
NazDaz,
Truth be told, Mwalimu hakutaka kumrudisha Obote mamlakani. Baada ya Waganda kualikwa kwenye ule mkutano wa Moshi, akina Museveni walituma ujumbe kuwa Obote will be a destabilizing force kwenye mkutano huo na wakamwomba Mwalimu amwombe Obote asihudhirie. Kama una kumbukumbu, Obote hakuhudhuria kwenye ule mkutano lakini aliwakilishwa na Paul Muwanga. Sasa kitu ambacho kilimuudhi Mwalimu, alimwomba Lule, wakati huo akiwa rais, amrudishie Obote nyumba yake kule kwao ambayo serikali ya Amin ilikuwa imeichukua, Lule akakataa kuwa hawezi kumruhusu Obote arudi Uganda. Mwalimu alitaka Obote arejee Uganda as a former president, wampe retirement package yake na nyumba ili aondoke Tanzania kwa sababu isingeeleweka kwamba Waganda wamerudi kwao lakini Obote amebaki Tanzania. Lakini Waganda wangejipanga vizuri, Obote angerudi kama former President na mambo kwisha.
 
Mag3,
Kama usemayo ni kweli basi afadhali hicho kitabu kitoke mapema tujue ukweli na pumba. Mohamed Said amejitahidi sana kutuaminisha kuwa bila watu wa Gerezani Tanzania isingekuwa huru na Nyerere, aliyefadhiliwa nao, aliwatupa mkono. Sasa kama kweli Mzee Malecela ameandika kitabu kinachopotosha historia, na mimi ninamheshimu sana huyu mzee, basi ataonekana in his true colours, na sisi tuliokuwa tunamheshimu huyu mzee tutamwona mtu wa ovyo kama ilivyobainika kwa Iddi Simba.

Kuna kila dalili ya agenda kubwa kujificha ndani ya haya maandishi tunayoyaona. Kwa upande mwingine si vibaya pia tukasikia nini waathirika wa maamuzi ya Nyerere na utawala wake wanachosema. Maana tutakuwa waongo kama kila siku ni kusikiliza upande mmoja tu wa hadithi. Hoja zitakuwa na uzito relative to the general progress of the country after Mwalimu. Maana kuna wakati ukitolewa mtihani, aliyepata 100 anakuwa amefaulu kuliko aliyepata 40. Ila kuna mitihani mingine aliyepata 40 ndiyo kipanga wao kama wengine wanagalagala kwenye 20 na kumi kumi.
 
Ndahani,
Ndiyo maana nilikipenda kitabu cha Mzee Mtei, "From Goathead to Governor." Mzee amejitahidi kuwa mkweli, factual, bila kuweka hisia zozote za kupotosha historia. Lakini kwa Malecela, kama ameandika kitabu, hadidurejea itakuwa ni "Our leadership and the destiny of Tanzania." Hiyo ndiyo mizani atakayopimwa nayo.
 
mkuu unajua kati ya uganda na tanzania ni nani alikuwa mchokozi??

Je? Wajua ni kwanin? Uganda waliitandika tanzania na mpaka kuvuka mipaka??

In short.Nyerere alikuwa swaiba ake sana obote na pind idd amin alipo mpindua abote nyerere hakufurahia kabisa.Hivyo tanzania ilimuhifanyi obote na mkakati kabambe wa kumng'oa idd amin madarakan uliundwa kuna vijana waganda na watanzania walipewa mafunzo na kuanza kumletea choko choko idd amin kwa kuingia uganda na kufanya fujo walivyo fukuzwa walikimbilia tanzania choko choko zikazid wakaenda tena kufanya fujo na wakafanya uharibifu mkubwa sana uganda idd amin akakasirika akawatandika na kuwafukuza mpaka tanzania na kuingia kilomita kazaa tanzania.
Hapo ndipo nyerere alipokuwa anapataka haraka haraka akautangazia umma kwamba idd amin anataka kuitwa baadhi ya ardhi ya tz na kutangaza vita.
Je? Hapo mwenye kosa nani?? Na je? Ni nani hapo ni mchokozi wa mwenzake?

Ndio mana hata kamanda gadafi alimuunga mkono idd amin na kumsaidia kwa sababu uhuni wote alikuwa anaufahamu.

duh.! Kumbe Nyerere kichwa balaa. Mungu amurehem maana tanzania tumebaki na vichwa vinavyogombe uraisi lakini havijui sera za nchi zaidi ya sera ccm.
 
NasDaz. Unaposema Idi Amin "hakuonesha uchokozi wa wazi" unamaanisha nini? Ultaka afanye nini kujua kweli katuchokoza? Kwa mfano angeshambulia kwa mabomu baadhi ya miji au kunyanyasa wananchi wetu na kuwaua ndio tujue katuchokoza? Au angeshambukia Dar na kuua wakazi wa Magomeni na Gerezani ndio tungejua kachokoza?
 
Ndahani,
Ndiyo maana nilikipenda kitabu cha Mzee Mtei, "From Goathead to Governor." Mzee amejitahidi kuwa mkweli, factual, bila kuweka hisia zozote za kupotosha historia. Lakini kwa Malecela, kama ameandika kitabu, hadidurejea itakuwa ni "Our leadership and the destiny of Tanzania." Hiyo ndiyo mizani atakayopimwa nayo.
Najitahidi kuelewa ila naona kama pia there is a drive to make a point that Mwalimu's stand, especially kwenye namna ya kumpata Rais baada ya awamu ya pili kukamilika was wrong. Well, nalo pia nalipa muda...pengine msimamo ule ulikuwa sahihi au sio sahihi. Nalipa muda kwa sababu, baada ya namna tulivyompata Rais wa awamu ya nne na utendaji wake, nimegundua watu wengi hatuwafahamu vema hawa wana siasa. Mitizamo yetu ya nje, haionyeshi uhalisia wao wa ndani na tunalipia kosa hilo kwa gharama kubwa sana. Mwalimu hakuwa mtu mpumbavu...alijua anachokifanya hata kama dunia nzima haikukipenda na alikisimamia kwa nguvu zake zote. Tena sio tu kwa kusema, bali hata kwa kuandika ili historia isijepindisha ukweli.
 
Kuna kitu kinakosekana ambacho kingejibu sehemu kubwa tu ya swali. Sijui kimesahaulika au kimeachwa makusudi.
Mwaka 1973 Amin alishambulia Tanzania. Watu wa Bukoba na Mwanza ni mashahidi.
Pamoja na madhila hayo Nyerere alikubali usuluhishi Adis Ababa chini ya Haile Selassi.

Swali lilikosa 'background' na kulenga mwaka 1978 kuvuka mpaka tu. Halikugusia Amin kuvuka mpaka na kuharibu maisha ya watu wa Kagera ambayo yamebadilisha historia.
Tukiangalia sheria za kimataifa tusisahau chanzo cha mgogoro na kujiuliza, je kulikuwa na mantiki ya kumfukuza hadi mtukula vita iishe? Kulikuwa na umuhimu wa kurudia kosa la mwaka 1973!

Kwa mara nyingine tunachagua sehemu moja ili ku-discredit Nyerere. Kama kumhifadhi Obote ilikuwa kosa, kwanini haikuwa kosa kumhifadhi Samora, Mbeki, Mugabe ,Kabila, Odinga n.k.

Tukiendelea tunaona historia inakatishwa ili kupata hukumu iliyotarajiwa. Amin alipoondoka aliyeongoza nchi alikuwa Yusuf Kironde Lule, then G.L.Binaisa n.k. Hkukuwa na kitu Amin to Obote.

Na mwisho tujiulize nani au nchi gani iliyowahi kuheshimu mkataba wa kimataifa kuhusu vita?
Tujiulize je uamuzi wa kumfukuza na kumuondoa Amin umeleta tija kwa taifa hasa watu wa Kagera au ulikuwa upotevu wa rasilimali? Tujiulize njia mbadala baada ya kipande cha nchi kumwegwa, mali kuibiwa na watu kuuawa ilikuwa ni ipi.
 
Najitahidi kuelewa ila naona kama pia there is a drive to make a point that Mwalimu's stand, especially kwenye namna ya kumpata Rais baada ya awamu ya pili kukamilika was wrong. Well, nalo pia nalipa muda...pengine msimamo ule ulikuwa sahihi au sio sahihi. Nalipa muda kwa sababu, baada ya namna tulivyompata Rais wa awamu ya nne na utendaji wake, nimegundua watu wengi hatuwafahamu vema hawa wana siasa. Mitizamo yetu ya nje, haionyeshi uhalisia wao wa ndani na tunalipia kosa hilo kwa gharama kubwa sana. Mwalimu hakuwa mtu mpumbavu...alijua anachokifanya hata kama dunia nzima haikukipenda na alikisimamia kwa nguvu zake zote. Tena sio tu kwa kusema, bali hata kwa kuandika ili historia isijepindisha ukweli.

MJUE NINI NYERERE ALITUFANYIA BAADA YA KUIVAMIA ZANZIBAR NA KUWAFUNGA VIONGOZI WAKE TANGANYIKA KABLA YA HUU MUUNGANO UITWAO TANZANIA APRIL 1964

MAISHA KATIKA JELA ZA NYERERE

Katika mwaka 1968 Hakimu Seaton, Hakimu wa Mahakama Kuu; alitembelea gereza la Mwanza.
Nilimuuliza kama kuna uhalali wowote juu ya kuwekwa kwetu kizuizini.

Mkuu wa gereza akamwambia Hakimu kuwa hakuna karatasi zozote zilizoletwa pamoja na mawaziri wa zamani wa Zanzibar.

Hakimu akaahidi kulifuatilia suala hili. Baada ya miaka minne tangu wakati huo, nikiwa katika gereza la Bukoba, Katibu wa Mkuu wa Mkoa alitoa shauri kuwa nimuombe Raisi anitoe kizuizini.

Nalimwambia kuwa kwa vile sijui nini kosa langu la kuwekewa kizuizini naona sina hoja za kimsingi juu ya ombi langu.

Alinijibu, "Hapana shaka ulipotiwa kizuizini ulisomewa amri ya kutiliwa kizuizini."

Nilimwambia kuwa, vile ninavyo kumbuka mimi hapakuwepo amri ya mimi kutiwa kizuizini.
Suprintendent wa magereza akanambia kuwa ilikuwepo amri, hapo akanisomea hio amri ambayo ikionesha kuwa inatokana na Raisi na ambayo imeandikwa kwa lugha ya kisharia.

Amri hio inasema kuwa Raisi baada ya kutoshelezeka kuwa, fulani na fulani; akiwataja mawaziri wote wa Serikali ya Muhammad Shamte, kuwa walikhusika na vitendo vya uchochezi wa kukhatarisha salama ya nchi, alitoa amri tutiwe kizuizini.

Nalipomuuliza amri hio ilitiwa sahihi lini, ilidhihiri ilikuwa ni mwaka wa 1968, baada ya muda mchache tangu pale nionane na yule Jaji Mkuu, Seaton kwenye gereza la Mwanza!

Sisi tulivamiwa nchi yetu na kutiwa vizuizini katika mwaka wa 1964. Najuwa kulikuwa na mapinduzi (mavamizi) huko Zanzibar, na hicho kitendo cha kiharamia iwe kimetokea huko.

Lakini tangu kati ya mwaka wa 1964 pale tulipotiwa vizuizini mpaka hii 1968 ambapo hii amri ya kutiwa kizuizini kutolewa na kutiwa sahihi; wakati huo wote - miaka minne - kuwekwa kwetu kizuizini na yeye Raisi Nyerere ambae ndie aliekuwa na hukumu yote huko Tanzania bara basi hakukuwa kisharia hata katika hio sharia ya kidhalimu ya Tanzania.

Kwa muda wa miaka minne kabla ya kutiwa sahihi hii amri ya kuwekwa vizuizini sisi tulikuwa basi ni wafungwa wake yeye Nyerere.

Je, ndio inayumkinika katika muda huo iwe yeyote miongoni mwetu sisi tuweze kufanya vitendo vya uchochezi wa kukhatarisha salama ya taifa?

Tujaalie kuwa inakusudiwa ule muda kabla ya kukamatwa na kutiwa kizuizini.

Wakati huo sisi tulikuwa ni mawaziri wenye mas-ulia kwa vile tulichaguliwa kulingana na sharia ya kikatiba iliokuwepo nchini - Zanzibar - wakati huo.

Je, sisi wakati huo tutaweza kuwa tutende kama vile ilivyoelezwa katika hio amri iliotiwa sahihi na Julius Nyerere?

Kama itakavyokuwa, hilo taifa linalo elezwa kuwa ni Tanzania; halikuwepo kabla ya sisi kukamatwa na kutiwa vizuizini.

Huyo ndio mkuu wa nchi, anaejigamba kuwa yeye ni mwenye kuweka haqi, anafika kuzuwa na kupanga uwongo kama huo; ni jambo la kushangaza sana; lakini kwa watu kama yeye sio ajabu kulitenda.

Baada ya kupata hoja hizi ndipo nilipomwandikia Raisi, bila shaka maandishi yangu yalikuwa ni ya upole na kweli za hakika.

Sikupata majibu. Kwa hakika sikupata hata mara moja jawabu au hata kuarifiwa kuwa zimefika, baruwa zangu kadhaa wa kadhaa nilizompelekea Nyerere, tangu niko kizuizini na hata baada ya kutoka. Utaritibu wa hishima kama hio Tanzania inaonekana ni mpango wa kikoloni uliokwisha pitwa na wakati.

Dr. Kleru alikuwa ni Mkuu wa Mkoa aliepigwa risasi na mkulima, Abdulla Saidi Mwamindi; siku ya krismasi mwaka 1971. Mkulima huyu, Abdulla Saidi, alikuwa ni miongoni mwa watu kadhaa wa kadhaa walionyang'anywa mashamba yao kwa kuwanzishia vile vijiji vya ujamaa. Jeuri ya Mkuu wa Mkoa huyu ilifurutu ada.

Waliokuwa wakiteswa na kudhulumiwa na Mkuu wa Mkoa huyu walishitaki kwa wakuu wa chama.
Kila wakishitaki huambiwa wakashitaki polisi; na wakifanya hivyo.

Kamanda wa Polisi, Abubakar aliwaonya wakuu huko Dar es Salaam juu ya vitendo viovu na vya kuudhi vya Mkuu wa Mkoa huyu na juu ya ile tabia yake ya ulevi kufika kuanguka na kuingiliwa na wahuni.

Baada ya kupigwa marisasi na kuuliwa, wale jamaa wote waliokuwa wakipeleka mashtaka yao Polisi walikamatwa na kuwekwa kizuizini mpaka Abdulla Saidi Mwamindi ahukumiwe na kunyongwa. Hata kabla ya kesi kumalizika, magazeti na vyombo vyote vya khabari vya Serikali na vya Chama, vyote vilianza shutuma zao, sio tu dhidi ya Mwamindi, bali dhidi ya wakulima wote, huku wakisemwa, "mabepari", "wanyonyaji", "wakoloni" na makhaini".

Mudhahara uliopangwa na Sirikali ukaingia njiani kupita kuwashutumu na kuwalaani watu hawa. Kwa hali hii ikawa Mwamindi kesha hukumiwa na vibaraka vya Sirikali hata kabla ya kufikishwa mahakamani.

Mashahidi wote wale ambao wangeliweza kutowa ushahidi japo kuthibitisha juu ya vitendo vya uchokozi vya yule Mkuu wa Mkoa walizuiliwa mpaka pale kesi kumalizika.

Khatuwa hii ilikusudiwa kumtia khofu yeyote yule aliekuwa na fikra ya kutaka kutowa ushahidi upande wa mshitakiwa.

Hivi ndivyo sharia inavyo firigiswa katika nchi kama hivi Tanzania wakati ambapo sharia ya kumtia mtu kizuizini bila ya kupelekwa mahakama inatumika.

Watu kumi na mbili wa Iringa pamoja na yeye Mwamindi mwenyewe walikuwa pamoja na mimi gerezani Dodoma.
Kamanda wa Polisi Abubakar, na yeye vilevile aliwekwa na sisi siku mbili gerezani akiwa yumo katika pirika za kuhamishwa kutoka gereza hii na kupelekwa gereza jengine.

Ilani nyingi zilitolewa na kutangazwa ulimwenguni juu ya maafa na mateso katika magereza ya Zanzibar na Pemba.

Lakini hapana lililosemwa na kuelezwa walimwengu kukhusu mateso yanayowapata wazuiwa katika magereza ya Tanzania bara.

Sio kuwa uwovu na mateso wanayotendewa wazuiwa magerezani huko Tanzania bara hayajuulikani; mengi yake hayafiki ulimwenguni basi kwa sababu ya kukosekana demokrasia na heshima ya haki za binadamu juu ya haki ya kueleza na kujieleza.

Kutokana na hali hii, mateso na vitendo vya kikhabithi havielezwi nje kwa walimwengu kukhofia hao watakaoeleza kuadhibiwa na utawala wa kidikteta. Niliona kwa macho yangu nilipokuwa gereza la Mwanza, wakati ambapo Superintendent Odenyo ndie aliekuwa mkuu wa gereza wakati huo; niliona wafungwa walipozuiliwa chakula na maji kwa muda wa siku nne, kisha wakapelekwa hospitali (nusu maiti) na ripoti kuwa (ati) walikuwa wamegoma kula.

Nilipokuwa Dodoma nilikuwa nikisikia kadhia kama hizo.
Nikisikia, kwani baina yetu ilikuwa ni kuta, baina ya chumba niliokuwemo na vile vyumba vya mateso.

Katika gereza la Dodoma aliekuwa katili hivyo ni Ofisa Mkuu, aliepangwa jina "Iron Face" (Uso wa Chuma), kwa vile akijuulika kuwa hajapata kuwa na huruma.

Mkuu wa magereza hapa, alifika kuwa hajishughulishi tena na kazi yake; hivi ni kwa sababu kwa hichi cheo chake cha juu na daima kuwemo katika vikao na sherehe za kisiyasa, takribani alimuachilia uendeshaji wote wa gereza mikononi mwa msaidizi wake - huyu Ofisa Mkuu. Mabwana wawili hawa waliyafanya maisha ya gerezani hapa hayastahamiliki hata kidogo.

Ile mikutano ya kawaida ya kila Jumamosi ambapo ofisa mas-uli hutarajiwa asikilize malalamiko ya wafungwa ikawa haifanywi tena.

Ziara za kila mwezi gerezani za Mahakimu mbalimbali nazo pia zikasita. Wafungwa hutiwa gerezani na kufika kutolewa bila ya kujuwa kuwa wanahaki ya kuwasiliana na watu wao.

Inafaa ifahamike kuwa hivi kuharibika hali kiwango hichi, sio tu katika gereza la Dodoma. Niliiona hali kama hiyo katika gereza la Mwanza.

Gereza la Bukoba ilikuwa haijambo pale nilipoondoka.
Lakini, wakuu wa kisiasa; kama vile Mkuu wa Mkoa na Mawaziri dhahiri shaahir walikuwa wakijiepusha kuyazuru magereza na kujuwa hali za wafungwa na wazuiwa waliomo humo magerezani.

Ama Raisi na Makamu wa Raisi, si dhani kama iko siku wamewahi kuzuru gereza lolote lile katika Tanzania bara, licha kuzungumza na mabwana au mabibi waliowatia humo magerezani.

Hali katika gereza la Dodoma ilizidi kufanywa kuwa mbaya kwa ukhabithi wa huyu "Uso wa Chuma" na kulemaa kwa ulevi wa marungi Msaidizi wa Superintendent.

Mpango ulifanywa kumuuwa "Uso wa Chuma". Mmoja wa wafungwa aliweza kupata kisu na akataka kumpiga nacho huyo "Uso wa Chuma", kwa bahati akaanguka kifudifudi, kichwa chake mbali na yule mfungwa ambae alikuwa na pingu za chuma miguuni mwake na yeye vilevile akaanguka upande wake.

Wakati huo mfungwa aliweza basi kuipata miguu ya "Uso wa Chuma" na kuanza kumpiga visu vya miguuni mpaka pale ilipowezekana kuzidiwa nguvu akanyang'anywa hicho kisu.

Hapo tena akaingiliwa mfungwa huyo kupigwa marungu mpaka akawahijiwezi ndipo alipotiwa pingu za mikono. Askari wa gereza akaamrishwa kumpiga marisasi ya miguu.

Hivyo ikawa kafungwa kila upande na marisasi miguuni mwake, hapo tena akasukumizwa katika chumba cha adhabu.
Baadae kidogo msaidizi wa superintendent akaja na yeye akaanza kumpiga vile alivyopenda.

Vilio vyake tukivisikia kutokea katika hicho chumba cha adhabu alimokuwemo na tukamuona askari aliekuwa zamu kwenye kidungu akigeuza uso na kupiga ukelele: "Wanamuuwa huyu mtu!" Binadamu huyu akavurumishwa tena humo chumbani kisha bomu la kutowa machozi likatupwa katika hicho chumba ambacho sehemu yake ya kupitia upepo ni ndogo kabisa. Usiku uleule akajifia.

Asubuhi yake wafungwa wote wakasimamishwa kwenye uwanja na maiti ikaletwa mbele yao uchi kama alivyozaliwa. Hapo tena msaidizi wa superintendent akawa anamchocha maiti kwa gongo huku akimwambia yule maiti: "Inuka uwaambie wenzio vipi ulivyokuwa hodari, na nini mwisho wa uhodari wako?"

Baada ya hivyo tena akawahutubia wafungwa kwa kuwaambia kuwa hivihivi ndivyo tutakavyomfanya yeyote yule miongoni mwenu asiposhika adabu yake.
Hapo tena wafungwa wote wakafungiwa vyumbani mwao kisha mabomu ya kutowa machozi yakatupwa humo vyumbani mwao.

Haya yalifanywa kwa makusudio ya kuwataka watajane wale waliokhusika na mpango huu. Haukupita muda isipokuwa wengi wakatajana na kukiri makosa yao.

Lakini adhabu na mateso yaliendelea kwa wiki kadhaa wa kadhaa. Chakula kikapunguzwa, hata kwetu sisi wazuiwa. Kila mtu alitaraji mauwaji haya yatafanyiwa uchunguzi na hukumu ya haki kupitishwa. Askari wa gereza ikawa wanasema hadharani kuwa ukifanywa uchunguzi watawaambia askari Polisi hakika ya mambo ilivyo. Lakini hapana lilokuwa.

Tulisikia katika redio, kama maneno ya kupita tu yaliosemwa Bungeni - kwa woga - na mmoja wa Wabunge kuwa kulikuwa na askari makhabithi walio waadhibisha wafungwa mpaka kufika kuwauwa.

Kubwa lililotokea ni uhamisho wa kawaida wa maofisa wa magereza wa vyeo vya juu kutoka magereza mbali mbali nchini. Khabari ikamalizikia hapo.

Katika nchi yenye sheria ya kutiwa watu vizuizini bila ya kupelekwa mahakamani, kelele zozote zile ni sawa na mbwa mwenye kubweka hazina athari yoyote ile, na sharia basi ni kwa kumtumikia bwana mtawala aendelee katika utawala wake na atende vile anavyopenda.

Anda what is this???
 
Umenisaidia sana, mtaalam Janjaweed nakushukuru! Nilikua sijapata sababu ya kuridhisha dhidi ya upinzani wa huyu dogo kwa Nyerere. Mambo yaliyopo na yajayo yeye hayaoni kazi ni kukosoa historia tu! Ananiboa sana

kama sikosei, jumanne na mkewe wana issue kama tatu na juliasi, pia kama sikosei tena, jumanne na mkewe wana kashfa ya kupokea pesa toka kwa yule mhindi ambaye kama wahindi wengi walimchukia nyerere

na kwasbabu hiyohiyo, kama sintakosea tena, mtoto wa nyoka aweza kuwa na ahadi au kuendeleza chuki na juliasi kwani siajabu pesa za kampeni atapata kutoka kwa wafadhili wa jumanne

clues zinaanzia pale alipokua tayari kulamba butts za wengi tu including chadema wakati anataka EALA representation na alipokosa akarudi kumwagia mbaya walewale waliomuunga mkono

nasikitika sana kuwaza kwa sauti kwamba kama jumanne, lusinde na huyu mzee wa waste management wanatoka sehemu moja halafu almost wana tabia zinafanana, je tatizo ni ule udongo wa pale ?? genes?? au heredit
 
NasDaz,

..baada ya Tanzania na Uganda kusaini mkataba wa amani wa Mogadishu hakukuwa na kikundi chochote kile cha Waganda kilichokuwa kikipata msaada wa kijeshi toka Tanzania.

..Yoweri Museveni anaeleza ktk kitabu chake kwamba walikuwa wamekata tamaa ya kumuondoa Iddi Amini madarakani mpaka pale Mwalimu alipotoa hotuba ya "uwezo tunao,..."

Well said JokaKuu,
Naona umejitahidi kuuficha ukweli na hatimae umejikuta kuuweka hadharani! In what is so called The Mogadishu Accord, "hakukuwa na kikundi chochote kile cha Waganda kilichokuwa kikipata msaada wa kijeshi toka Tanzania.....!" Good job! Kwahiyo unakubali kwamba Nyerere alikuwa anatoa msaada wa kijeshi kwa Waganda waliokuwa wanampinga Amin?! Mogadishu Accord ilifanyika october 7, 1972; na Waganda ambao walifanya jaribio la mapinduzi dhidi ya Amin walifanya hivyo mwaka 1972....!! So, tukisema kwamba jaribio hilo lilifadhiliwa na Tanzania tutakuwa tumekosea?! Kama ndivyo, hadi wakati huo, Amin alikuwa amefanya baya gani la kutisha hata Tanzania iamue kufadhili wana mapinduzi hao ili kwenda kumpindua Amin?! Litajeni hapa halafu tulipime uzito wake!

Tukirudi kwenye Mkataba wa Amani uliokuwa umesainiwa Mogadishu chini ya Siad Barre, si kweli hata kidogo kwamba Mogadishu Accord ilimaliza tatizo kati ya Tanzania na Uganda. Ikumbukwe kwamba, Wakati inasainiwa Mogadishu Accord hapo October 7, 1972; October 21, 1972 ilikuwa ni siku ya Sherehe za Mapinduzi ya wa Somalia. Nyerere alisusia sherehe hizo wakati hapo kabla alishathibitisha kwamba angehudhuria. Sababu inayosemwa sana ni kwamba, Balozi Augustine Mahiga ambae alikuwa ni Mshauri wa John Malecela, alimwamabia Mwalimu kwamba pamoja na kusainiwa kwa mkataba huo, Somalia(Siad Barre) ilikuwa inampendelea zaidi Amin kwavile wote ni waislamu!! Na huenda pamoja na mambo mengine, hii inawezekana ilichangiwa zaidi na jinsi ambavyo uhusiano kati ya Somalia na Uganda ya Amin ulivyoimarika ghafla mara baada ya kusainiwa kwa mpango huo wa amani. Na tokea hapo, hata uhusiano kati ya Somalia na Tanzania ukayumba!
 
NasDaz. Unaposema Idi Amin "hakuonesha uchokozi wa wazi" unamaanisha nini? Ultaka afanye nini kujua kweli katuchokoza? Kwa mfano angeshambulia kwa mabomu baadhi ya miji au kunyanyasa wananchi wetu na kuwaua ndio tujue katuchokoza? Au angeshambukia Dar na kuua wakazi wa Magomeni na Gerezani ndio tungejua kachokoza?

Mwanakijiji, siku hizi hatuna haya tena kuishi double standard life. Kwanini tulienda kupigana Comoro? Kwani Comoro walituvamia? Kabla ya kuanguka kwa ukomunist 1989, hivi kulikuwa na threat kubwa kwenye nchi za ulimwengu huu kama security? Maana kambi zile mbili zilikuwa busy kutafuta wanachama na walitumia mbinu zozote zile kufanikisha hilo.
Kumpinga Nyerer kunakofanywa leo ni sababu ya kushindwa kwetu kuonyesha uongozi imara na thabiti wenye uwezo wa kutolea majibu changamoto mbali mbali zinazotuzunguka. Badala ya kuhangaika ku raise our standard, poor thinkers have decided to wage a war against Nyerere's name...kam ni kweli basi huu ni wakati muafaka. Ila kama ni kwa hila historia inayanukuu yote na katika muda muafaka tutayapima yote kwenye mizani ili kuona nani ni nani na amefanya nini.
 
aliona raha kumweka yule mkatoliki mlevi pale dar-es salaam akamsaidia kupata askari wa kwenda kufanya hujuma kule kampala , unafikiri amin atafurahia yale .

Angaliwacha waganda wakasolve matatizo yao kwani imngalikuwa nini ??? Si angaliwanasuru kule bukoba na uvamizi??

KAMA ANAVYOSEMA MWENYEWE, "ukianza kula nyama ya mtu huwezi kuiwacha tena "

baada ya kula nyama za watu kule zanzibar akakimbilia uganda

na alipomaliza huko alishaanza vurugu na kenya kumbuka mambo ya unyang`au

pia alijaribu huko nyuma na malawi lakini kulikuwa kugumu

huyo ndiye mkatoliki nyerere

Huwezi hata kuficha udini na umbumbumbu ulionao ndugu yangu? Unashindwa kudhibiti hata hisia zako ndugu yangu? Kwani ni lazima kuchangia? Aibu kwako na William anaelipiza visasi kwa niaba ya mzazi wake hata haya haoni. Shame on you and William.
 
Kuna kitu kinakosekana ambacho kingejibu sehemu kubwa tu ya swali. Sijui kimesahaulika au kimeachwa makusudi. Mwaka 1973 Amin alishambulia Tanzania. Watu wa Bukoba na Mwanza ni mashahidi.
Pamoja na madhila hayo Nyerere alikubali usuluhishi Adis Ababa chini ya Haile Selass
Hayo ya mwaka 1973 unayoyasema wewe yalitokea wakati 1972 Obote allies walivuka mpaka wa Tanzania na kuingia Uganda na kufanya jaribio la mapinduzi ambalo lilishindwa. Baada ya kushindwa, walirudi tena Tanzania. Swali langu lile lile; Je, serikali ya Tanzania haikufahamu haya yaliyokuwa yanafanywa na Wakimbizi wa Uganda ambao there's no way kwamba waliingia Uganda kufanya mapinduzi bila ya kufanya maandalizi ya mapinduzi hayo walipokuwa ardhi ya Tanzania! Hivyo basi , kwa kuangalia ukweli huo utaona wazi kwamba chokochoko wa kwanza alikuwa ni Tanzania aliyeruhusu Wakimbizi wa Uganda kuruhusu ardhi ya Tanzania kama kituo cha mafunzo. Acheni kutetea maovu, hilo halikubaliki hata kidogo. Hakuna asiyefahamu(including wewe mwenyewe, JokaKuu, Jasusi, Mzee Mwanakijiji) kwamba Nyerere alifanya hivyo kutokana na uswahibu aliokuwa nao na Obote!

Kwa mara nyingine tunachagua sehemu moja ili ku-discredit Nyerere. Kama kumhifadhi Obote ilikuwa kosa, kwanini haikuwa kosa kumhifadhi Samora, Mbeki, Mugabe ,Kabila, Odinga n.k.
Binafsi nilishatamka kabla na sasa narudia. Nyerere hakufanya kosa kumpa hifadhi Obote na watu wake. Kosa alilofanya ni kumruhusu Obote na watu wake kuitumia ardhi ya Tanzania kuandaa mapinduzi dhidi ya Amin. Hakuna kiongozi yeyote duniani ambae angekaa kimya hata baada ya kuona jirani yake anawahifadhi na kuwafadhili watu waliokuwa na lengo la kumng'oa madarakani. Hata kama haikuwa sahihi kwa Amin kumpindua Obote, lakini hilo liikuwa ni suala la Waganda wenyewe na Tanzania haikutakiwa kuingilia kwa namna aliyoitumia Nyerere....hiyo si sawa hata kidogo!

Tukiendelea tunaona historia inakatishwa ili kupata hukumu iliyotarajiwa. Amin alipoondoka aliyeongoza nchi alikuwa Yusuf Kironde Lule, then G.L.Binaisa n.k. Hkukuwa na kitu Amin to Obote.
Hoja kwamba baada ya Amin kuondolewa madarakani ni Yusuf Lule ndie aliyetawazwa kuwa rais na sio Obote sio hoja itakayoweza kuondoa tuhuma kwamba chokochoko za Nyerere zilikuwa ni kwa ajili ya kutaka kumrudisha swahibu wake Obote madarakani! Nyerere was a smart man hivyo asingefanya stupid mistake ya kumweka Obote moja kwa moja na kisha ahitimishe hoja kwamba aliyafanya yote hayo si kwa maslahi ya Tanzania bali ni kwa ajili ya masklahi ya swahibu wake! Hata hivyo, Nyerere alifahamu wazi pindi uchaguzi utakapoitishwa, basi bila shaka Obote angerudi tu madarakani na hivyo ndivyo ilitokea! waswahili wana msemo; Kuku wa kwako ya nini kumshikia manati wakati unafahamu hata akitimua mbio vipi, lazima usiku atarejea tu!

Na mwisho tujiulize nani au nchi gani iliyowahi kuheshimu mkataba wa kimataifa kuhusu vita?
Tujiulize je uamuzi wa kumfukuza na kumuondoa Amin umeleta tija kwa taifa hasa watu wa Kagera au ulikuwa upotevu wa rasilimali? Tujiulize njia mbadala baada ya kipande cha nchi kumwegwa, mali kuibiwa na watu kuuawa ilikuwa ni ipi.

Njia mbadala ilikuwa ni kumpa masharti Obote na watu wake kwamba ni lazima wazingatie sheria za ukimbizi na katu wasiitumie Tanzania kama daraja la kurudi madarakani Uganda. Njia mbadala ilikuwa ni kutoruhusu ardhi yetu kutumika katika harakati za kijeshi dhidi ya Amin. Njia mbadala ilikuwa ni kutotoa misaada ya kijeshi kwa wale waliokuwa wanampinga Amin. To make story short, nji mbadala ilikuwa ni kutotumia unfair practices dhidi ya Amin na badala yake ilikuwa ni kutumia Diplomasia kutatua mgogoro kati ya Amin na Obote. Kwa bahati mbaya, Nyerere aliamini Amin ni mtu mkorofi asiyefaa kwa A wala Be na hivyo njia pekee ni kumwondoa tu madarakani!
 
Kuna kitu kinakosekana ambacho kingejibu sehemu kubwa tu ya swali. Sijui kimesahaulika au kimeachwa makusudi.
Mwaka 1973 Amin alishambulia Tanzania. Watu wa Bukoba na Mwanza ni mashahidi.
Pamoja na madhila hayo Nyerere alikubali usuluhishi Adis Ababa chini ya Haile Selassi
Njia mbadala ilikuwa ni kumpa masharti Obote na watu wake kwamba ni lazima wazingatie sheria za ukimbizi na katu wasiitumie Tanzania kama daraja la kurudi madarakani Uganda. Njia mbadala ilikuwa ni kutoruhusu ardhi yetu kutumika katika harakati za kijeshi dhidi ya Amin. Njia mbadala ilikuwa ni kutotoa misaada ya kijeshi kwa wale waliokuwa wanampinga Amin. To make story short, nji mbadala ilikuwa ni kutotumia unfair practices dhidi ya Amin na badala yake ilikuwa ni kutumia Diplomasia kutatua mgogoro kati ya Amin na Obote. Kwa bahati mbaya, Nyerere aliamini Amin ni mtu mkorofi asiyefaa kwa A wala Be na hivyo njia pekee ni kumwondoa tu madarakani!
NazDaz,
Let me be a bit provocative here. Siwezi kuingia kwenye fikra za Julius Nyerere lakini naamini kuwa hakumwona Obote na Waganda waliokimbilia Tanzania kama wakimbizi (refugees) ila freedom fighters. Nyerere detested Amin, that is no secret and if he could, he would have got rid of him. Nyerere dested military coups in all its forms, kwa hiyo asingeweza kutumia diplomatic means to deal with Amin kwa sababu hiyo ingekuwa na maana kwamba amemkubali Amin. Museveni was able to go to Mozambique to get military training and back to Tanzania. Of course maafisa wetu wa usalama walijua. Ilifika wakati Amin alimkamata Kambona Uganda na kutaka wabadilishane na Obote. Nyerere would not have any of that. Ilifika wakati Amin alipanga njama ku "hijack" ndege alimokuwa anasafiri Nyerere kutoka mkutano wa Commonwealth. Vijana wetu got wind of it, wakaenda London, na siku ndege inaondoka (ilikuwa ni ya EAA) wakatangaza kuwa ndege haitatua Entebbe na wasafiri wote wa Uganda washuke. Walipofika Dar-es-salaam, Nyerere akamuuliza kijana mmoja wa usalama "mbona hatukutua Entebbe?" Na kabla hajamjibu akamwambia huyo afisa, "mmefanya kazi nzuri vijana," which means he already new. That was the atmosphere between us and Uganda, kusingeweza kufanyika maridhiano ya kidiplomasia.
 
NazDaz,
Truth be told, Mwalimu hakutaka kumrudisha Obote mamlakani. Baada ya Waganda kualikwa kwenye ule mkutano wa Moshi, akina Museveni walituma ujumbe kuwa Obote will be a destabilizing force kwenye mkutano huo na wakamwomba Mwalimu amwombe Obote asihudhirie. Kama una kumbukumbu, Obote hakuhudhuria kwenye ule mkutano lakini aliwakilishwa na Paul Muwanga. Sasa kitu ambacho kilimuudhi Mwalimu, alimwomba Lule, wakati huo akiwa rais, amrudishie Obote nyumba yake kule kwao ambayo serikali ya Amin ilikuwa imeichukua, Lule akakataa kuwa hawezi kumruhusu Obote arudi Uganda. Mwalimu alitaka Obote arejee Uganda as a former president, wampe retirement package yake na nyumba ili aondoke Tanzania kwa sababu isingeeleweka kwamba Waganda wamerudi kwao lakini Obote amebaki Tanzania. Lakini Waganda wangejipanga vizuri, Obote angerudi kama former President na mambo kwisha.

My major concern si kama Nyerere alitaka kumrudisha Obote madarakani au hapana ingawaje nalo ni jambo ambalo katu siwezi kulipuuza. My concern ni kwanini Waganda na Obote Supportes walitumia ardhi ya Tanzania katika harakati zao za kumpindua Amin tena very soon baada ya Amin kupoka madaraka toka kwa Obote! Vile vile usisahau kwamba wakati Amin anaondoshwa madarakani tayari palishakuwa na tuhuma toka sehemu mbalimbali kwamba uadui wa Nyerere na Amin ulitokana zaidi na uswahibu uliokuwepo kati ya Nyerere na Obote. Hivyo, sitashangaa hata kidogo nikiambiwa kwamba baada ya kuondolewa kwa Amin, Nyerere hakupendezewa tena na suala la Obote kurudi madarakani kwani ingetoa jibu la moja kwa moja la nia ya Nyerere. Lazima tukumbuke kwamba, kwa kariba ambayo Nyerere alikuwa nayo asingependa hata kidogo kuudhihirishia umma wa kimataifa kwamba ni kweli alichokuwa anataka yeye ni kumrejesha swahibu wake madarakani!
 
William hawezi mpenda Nyerere kwa kuwa alimdiscipline babaake baada ya babaake kuleta uhuni wa kisiasa
Si hivyo tu bali hata yeye wamemdiscipline kule Dodoma wakati anataka kwenda A-town kunako mjengo wa EAC assembly. Hapa naona hasira zimempanda akikumbuka na ya baba yake.
 
My major concern si kama Nyerere alitaka kumrudisha Obote madarakani au hapana ingawaje nalo ni jambo ambalo katu siwezi kulipuuza. My concern ni kwanini Waganda na Obote Supportes walitumia ardhi ya Tanzania katika harakati zao za kumpindua Amin tena very soon baada ya Amin kupoka madaraka toka kwa Obote! Vile vile usisahau kwamba wakati Amin anaondoshwa madarakani tayari palishakuwa na tuhuma toka sehemu mbalimbali kwamba uadui wa Nyerere na Amin ulitokana zaidi na uswahibu uliokuwepo kati ya Nyerere na Obote. Hivyo, sitashangaa hata kidogo nikiambiwa kwamba baada ya kuondolewa kwa Amin, Nyerere hakupendezewa tena na suala la Obote kurudi madarakani kwani ingetoa jibu la moja kwa moja la nia ya Nyerere. Lazima tukumbuke kwamba, kwa kariba ambayo Nyerere alikuwa nayo asingependa hata kidogo kuudhihirishia umma wa kimataifa kwamba ni kweli alichokuwa anataka yeye ni kumrejesha swahibu wake madarakani!
Mbona swali lako lina jibu rahisi? Obote alikuwa kafara wa Nyerere na ukombozi wa Afrika katika mkutano wa Commonwealth uliofanyika Singapore. Nyerere alitaka na alihimiza Uingereza, kama nchi ya Commonwealth, isitishe kuiuzia silaha Afrika kusini. Na waliokuwa vocal supporters wa Nyerere katika mkutano huo walikuwa ni Obote na Kaunda. Ikafikia mahali waziri mkuu wa Uingereza akasema wazi "wengine hapa mnasema maneno maneno lakini hamtaweza kurudi nyumbani." Of course alikuwa anamsema Obote. Na kweli wakati Obote anajiandaa kurudi Amin akatangaza kupindua serikali. Obote kwanza alikimbilia Kenya, Waingereza wakamwambia Kenyatta asimpe makao. Ndipo alipokimbilia Tanzania.
Sasa NazDaz, katika hali kama hii, ungekuwa wewe Nyerere ungefanya nini? Kuhusu kusita kwa Nyerere kumrudisha Obote ni baada ya kugundua kuwa miongoni mwa Waganda waliokusanyika Moshi, Obote was not wanted. Mwalimu alitaka zoezi la kupatikana serikali mpya Uganda liwe zoezi litakaloungwa na Waganda wote hasa wale waliowakilishwa Moshi. Lakini alitaka Obote arudi kwao kama former head of state. Kwangu nafikiri that would have been the best option.
 
Back
Top Bottom