Vita vya Kagera: Nini chanzo? Kulikuwa na ulazima?

Vita vya Kagera: Nini chanzo? Kulikuwa na ulazima?

Muulize baba yako kwani yeye alikuwa kwenye saddle.Great thinkers tunazungumzia ya magamba wanavyo tumaliza.tatizo nimegundua huna mawasiliano na baba yako; hayo ndio yakuongea mkinywa kahawa. Nilitegemea utuambie meli ina nanga ngapi n.k usituvuruge

Mkuu inaonekana familia nzima ilimchukia babu baada ya yeye kuivurugia familia hiyo ndoto ya Magogoni.
 
Nyerere screwed Jumanne's plan to be a president, and if that plan would materialize... his son wouldnt be jobless and struggling to be a politician (in a jackass way)

Umenisaidia sana, mtaalam Janjaweed nakushukuru! Nilikua sijapata sababu ya kuridhisha dhidi ya upinzani wa huyu dogo kwa Nyerere. Mambo yaliyopo na yajayo yeye hayaoni kazi ni kukosoa historia tu! Ananiboa sana
 
[1] Mwl kumpatia hifadhi Obote ilikuwa kosa ?.

Haikuwa kosa hata kidogo huku nikiamini alifanya hivyo kwa dhamira ya kibinadamu, kinyume chake ni kosa!

[2] Mwl kuwapatia hifadhi wakimbizi toka Uganda ilikuwa kosa ?.

Haikuwa kosa hata kidogo huku nikiamini alifanya hivyo kwa dhamira ya kibinadamu, kinyume chake ni kosa!

[3] Wakimbizi toka Uganda walikuwa wakwanza kuivamia Uganda au majeshi ya Uganda walianzisha vita na Tanzania ?.

Wakimbizi wa Uganda ndio walikuwa wa kwanza kuivamia Uganda!

[4] Idd Amin kuitangazia dunia kwamba Kagera ni sehemu ya Uganda alikuwa sahihi ?.

Hakukuwa Sahihi kwakuwa Kagera ilikuwa ni sehemu ya Tanzania.

[5] Mwl[Tanzania] kuipiga Uganda hadi kumwondoa Idd Amini madarakani alifanya vema ?.

Hakufanya vema.Busara ya Vita ya vita ya aina ile ni sawa Gulf War ambapo UN ilipitisha Azimio la kuishambulia Iraq ambayo ilikuwa imeikalia Kuwait. Kilichofanyika ni kumwondoa Sadaam toka ardhi ya Kuwait tu na si zaidi ya pale. Kinyume chake, ni uhuni ambao ulifanywa na Geroge Bush JR ambae kwa kutumia kisingizo cha uwepo wa silaha za maangamizi, alihakikisha hadi Sadam anaondoka kabisa madarakani....!! Hivyo basi, ilitosha tu kumwondoa Amin ndani ya mipaka ya Tanzania na sisi kuimarisha mipaka yetu huku tukihakikisha Waganda waliomo ukimbizini hawaitumii ardhi yetu kufanya chokochoko.

Nikipewa majibu ya maswali yangu machache bila kuingiza ushabiki tunaweza kujua kwa uhakika zaidi nani alikuwa mkosaji.

Mkuu kwny jibu la mwisho hapo, je, Uganda ilikuwa haiwajibiki kulinda mipaka yake dhidi ya waleta chokochoko kutoka tanzania?
Haya naomba kuelimishwa,mosi, kwa wakati ule, msimamo wa OAU na UN ulikuwa unasemaje kuhusu kukabidhiana madaraka na demokrasia kwa ujumla?(maana post yako 1 pale juu umesema wali mtambua, wakati alipindua kuingia madarakani) pili, Obote aliingia madarakani kwa kupigiwa kura au naye alimpinduwa mtangulizi wake?
 
Unaona sasa....kumbe wewe ndo umedhirisha kwamba unaongelea kuamini kilichopangwa kutokea!!! Kwahiyoo unakiri wazi kwamba Nyerere ndie kiini cha matatizo na alilazimika kumwondoa Amin kwavile tu Amin alikuwa na Close tie na Ghadaff?! Kama ndivyo, basi hilo pia halikubaliki kwakuwa hakuna ushahidi kwamba Amin angeisumbua Tanzania kwavile tu alikuwa na close tie na Ghadaff!!

Mkuu kuwa makini.
Unachokiquote kwenye post yangu ya pili ni maoni yangu, ninasimamia maoni hayo katika namna ya kutaka kumaliza hoja hii ambayo kama nilivyoonyesha wasi wasi kwenye thread hii hii, kwamba sielewi ni kwa nini tunajadiri hii issue.

Kilinichofanya nikuulize wewe ni kitendo cha kutaka kuonyesha kwamba mwenzako anapotosha kwa makusudi wakati alikuwa anaelezea kilichotokea, alafu unareplace na ukweli ambao ni dhahiri kwamba umejikita kwenye kile unachokiamini au kukifiria, kama ulivyothibisha sasa, kwamba unachukulia maoni yangu yanafanya yakwako yawe fact. Point of correction dear Sir.
 
JokaKuu,
Sina tatizo na wewe hata kidogo kuhusu uwezo wako wa kuchambua mambo....u're great! hata hivyo, tatizo lako JokaKuu ni kwamba upo very biased!! Wewe huoni taabu kupotosha ukweli kwa ajili tu ya kulinda kile unachokiamini au kukitetea!! Ni kweli, baada ya Amin kuondolewa madarakani ni Yusuf Lule ndie alishika hatamu za uongozi!! Hivi unazani Nyerere could be stupid enough amweke Obote soon after kumwondoa Amin madarakani wakati tayari tuhuma zilishaanza kutolewa kwamba kilichomfanya Nyerere kuingia vitani ni kumtetea Obote?! Only the most Foolish President could do otherwise!! Ingawaje ni Yusuf Lule ndie alishika hatamu, Nyerere alishajua sooner or later Obote angerudi tu kwenye kiti chake kwavile tayari paliwekwa nia ya kuitisha uchaguzi ambao kila mtu, including Nyerere alifahamu fika kwamba lazima Obote angeshinda tu!!
It amazes me when one who is truly biased calls another biased! NazDaz, umeshasema kwa kauli yako mwenyewe kwamba wewe ni anti-Nyerere. Kwa hiyo hata kama jokaKuu anaweka facts, alimradi zinamwonyesha Nyerere in a good light hutokubaliana nazo.
 
William natamani uje bukoba uone makaburi ya babu zangu na ndugu zangu waliouwawa na majeshi ya Amini. Wewe uko huko mbali na mzee wako wala hukufiwa unakuja na hoja ya kibazaziiiiii............. siku ukifiwa undo utajua uchungu wa kufiwa.

Ta Muganyizi, nilitaka kukuongezea thanks juu ya ile like.
 
William, inaonekana una ajenda zako binafsi dhidi ya Baba wa taifa nazo ni kwa nini alimdhibiti vilivyo baba yako na pili ni ajenda ya kidini. Hivyo basi naomba nikuambie tu kwamba propaganda zote chafu dhidi ya Baba wa taifa kamwe hazina nafasi na hazitafanikiwa. Kwa ushauri tu nakusihi ujikite katika mambo ambayo ni relevant na yenye maslahi kwa jamii yote ya kitanzania.[ Mnyisanzu 02.06.2012].

Kasikia JK alivo na chuki/hasira, asivompenda Mwl Nyerere so anajaribu kujipambanua humu kuwa naye hampendi Nyerere ili labda mkulu amwangalie,,kingine inaweza kuwa ile hali ya Nyerere kumdhibiti sana Baba yake,,lkn mbona still amenufaika sana na hicho alichopata mzee Malecela i.e kusomeshwa bure kwa kodi za watz nk?
 
Kasikia JK alivo na chuki/hasira, asivompenda Mwl Nyerere so anajaribu kujipambanua humu kuwa naye hampendi Nyerere ili labda mkulu amwangalie,,kingine inaweza kuwa ile hali ya Nyerere kumdhibiti sana Baba yake,,lkn mbona still amenufaika sana na hicho alichopata mzee Malecela i.e kusomeshwa bure kwa kodi za watz nk?
Like I said, he is on the outside looking in. The question is: will "they" let him in?
 
It amazes me when one who is truly biased calls another biased! NazDaz, umeshasema kwa kauli yako mwenyewe kwamba wewe ni anti-Nyerere. Kwa hiyo hata kama jokaKuu anaweka facts, alimradi zinamwonyesha Nyerere in a good light hutokubaliana nazo.
Jasusi, nafikiri wengi wenu mmesahau kitu kimoja...Je unakumbuka taarifa tuliyowahi kupewa na Field Marshall ES humu JF kuhusu nia ya kuandika upya historia ya Tanzania? Hiki kitabu kinatakiwa kiende sambamba na kile cha Mohamed Said cha kukosoa historia ya harakati za uhuru wa Tanganyika. Hawa watu wanaamini kuwa kama wataweza kumcut down to size Mwalimu, basi watafanikiwa kuwainua watu wengine wamkaribie na ikiwezekana wamfikie na kumpita. Wakati Mohamed Said analilia wazee wake wa Gerezani, William anamlilia mzee wake wa Dodoma na kuna tetesi hiki kitabu kinaweza kutoka muda wowote kama kitakuwa hakijatoka tayari. Hizi mada anazoleta William ni katika kupima tu kina cha maji kabla ya kujitosa...na bado tutashuhudia mengi!
 
Sheria za vita haziruhusu tu kumuondoa adui kwenye ardhi yako bali kuweza pia kuondoa tishio la adui huyo na kumlazimisha kusalimu amri. Tanzania isingeweza kumuondoa Amin hadi mpakani na kuendelea kumuacha awe tishio. Katika vita - na hapa watu lazima watambue ni vita - anayeshinda ndiye anaamua terms of surrender. Tanzania haimkurudisha Obote; Obote alikuwa ni Rais wa Wauganda aliyepinduliwa na Idi Amin (kama watu wamesahau) na Obote alirudishwa kwenye nafasi yake (status quo). Sasa kama alipinduliwa tena hilo ni jingine lakini kama aliyempindua angekuwa tishio kwa Tanzania tungewajibika pia kumkung'uta.
 
William natamani uje bukoba uone makaburi ya babu zangu na ndugu zangu waliouwawa na majeshi ya Amini. Wewe uko huko mbali na mzee wako wala hukufiwa unakuja na hoja ya kibazaziiiiii............. siku ukifiwa undo utajua uchungu wa kufiwa.
Ta Muganyizi, huyu William hakuwahi kuusikia huu wimbo uliotungwa na Mayunga Ngata, naomba mwenye kuijua hii lugha atupe maana yake.

Kambarage, ng’eshimiwa
Nyerere watukombola​
Wayimala ivita ya bana Buganda​
Mnanzika wanatula ilihindi​
Aligalagala,​
Agulalaga majigulu​
Wabile wigwa chagachaga, obanda​
Ogahagai Tanzania​
Aho akatuvamia​
Twalitulembelile​
Tuli ng’wa walwa​
Tulisoma na kusoma​
Nikumbaga yabuyaga​
Tuhimbulwa jinga (2x)​
Aho nigwa guli giki ya binwa​
iBugando​
Ing’holo yukolwa​
‘Yulya malumba na malumba’​
Bugando baliko,​
Baliko balema bingi​
Na bakubyalaga na balinda​
Baliko bingi​
Nang’ho bulihaya​
Kupiga njinga!​
iTanzania bulihage​
Wabiyona indege nyuklia​
Ya kunya lyochi ukunuma?​
Ukubutongi balishila​
Bakwanaga buyaga​
‘Baganda, toshila’​
 
Last edited by a moderator:
It amazes me when one who is truly biased calls another biased! NazDaz, umeshasema kwa kauli yako mwenyewe kwamba wewe ni anti-Nyerere. Kwa hiyo hata kama jokaKuu anaweka facts, alimradi zinamwonyesha Nyerere in a good light hutokubaliana nazo.

Jasusi,

..LOL!!

..jamaa ametaharuki baada kumwambia kwamba Nyerere alimtoa Iddi Amini "akampachika" Yussuf Lule.

..hiyo inavunja hoja ilee ambayo Mwalimu hasakamwa nayo.

..nimebahatika kusoma kitabu " The War in Uganda ", wanaelezea vizuri sana jinsi process nzima ya kupatikana kwa post-Amini government. Sikumbuki mahali popote pale ambapo Mwalimu alitia mkono wake.

..zaidi, kwa nguvu za kijeshi alizokuwa nazo Mwalimu, na jinsi Waganda walivyokuwa wakimtegemea, Mwalimu asingeshindwa kumuweka Obote madarakani. Ukweli ni kwamba Mwalimu hakuwa na nia hiyo.
 
jmushi1,
kitu cha kwanza ni Nyerere kumpokea Obote....lakini nasisitiza, hakuna mtu mwenye akili timamu ambae anaweza kumlaumu Nyerere kwa kumpokea Obote; hata mimi base yangu haipo katika Nyerere kumpokea Obote bali Waganda kuitumia Tanzania kama uwanja wao wa mafunzo huku serikali ikifahamu. Naamini serikali ilifahamu hilo kwavile isingewezekana Waganda waingie nchini mwao na kufanya jaribio la mapinduzi na waliposhindwa wakarudi tena Tanzania bila serikali kufahamu. Kama walifanya njama za mapinduzi kimya kimya, siri ilishafichuka baada ya wao kufurumushwa na wanajeshi watiifu wa Amin. Baada ya hayo kutokea, Nyerere angemfukuza Obote na watu wake kwavile tayari walishauka sheria za ukimbizi.

NasDaz,

..baada ya Tanzania na Uganda kusaini mkataba wa amani wa Mogadishu hakukuwa na kikundi chochote kile cha Waganda kilichokuwa kikipata msaada wa kijeshi toka Tanzania.

..Yoweri Museveni anaeleza ktk kitabu chake kwamba walikuwa wamekata tamaa ya kumuondoa Iddi Amini madarakani mpaka pale Mwalimu alipotoa hotuba ya "uwezo tunao,..."
 
ndiye aliitia nchi katika janga la umasikini na madeni ambayo mpaka ulimwengu huu utakwisha hatuwezi kulipa

tutaendelea kulipa riba za deni,


sababu ni kumrudisha mkatoliki mlevi mwenzake madarakani

Mmh! Kweli udini utatumaliza, yaani udini unaweza ukamfanya mtu asifikiri kabisa. Pamoja na JK kukubali kupewa suti in exchange with our land, kamwe si haki kusema ni dini yake imemfanya ashindwe kufikiri. Madhaifu ya kiongozi hayatokani na dini au kabila lake jamani. Tukianza kufikiri hivi; kweli kwenye huu umaskini hatuwezi kuondoka.
 
Kama kuna kitu kitatusumbu sana ni hii historia mpya; tumeona hili kwa M. Said na simulizi lake ambalo sasa nina uhakika limepata mhusika mpya Vedastus Kyaruzi!
 
Watanzania hakika tu watu wa ajabu sana. Kuna baadhi yetu ambao kwa bahati mbaya sana hawataki kabisa kusikia vipenzi wao wakisemwa kwa mabaya hata kama kweli mabaya hayo waliyafanya. Kama walivyo mashabiki wa CHADEMA ambao hawataki kabisa kusikia mtu kama Dr. Slaa akisemwa kwa mabaya, kuna wengine ambao hawataki hata kidogo kusikia baya likisemwa dhidi ya Nyerere. Hawa wote, ukisema baya kuhusu vipenzi vyao basi watakuja juu na kukupa majibu ya kifedhuli na kihayawani….lakini wote hawa bado wanajiita ni Greatest Thinkers!!

Sasa nirudi kwenye mada.

Ukweli bado utabaki pale pale kwamba kwa pale ilipofikia, Tanzania haikuwa na budi bali kuingia vitani dhidi ya Amin. Hata hivyo, bado ukweli unabaki paleplae kwamba point ambayo ilikuwa lazima tuingie vitani ilisababishwa na Nyerere mwenyewe.

Baada ya Amin kumpindua Obotte, Milton Obotte alipewa hifadhi na Nyerere. Kimsingi, hapakuwa na ubaya wowote kwa Nyerere kumpa Obote hifadhi hapa Tanzania. Hadi Nyerere anampa hifadhi Obote pamoja na maelfu ya wakimbizi bado Amin alikuwa hajaonesha uchokozi wa wazi dhidi ya Tanzania. Tatizo kuu lilianza pale Wakimbizi wa Uganda waliopo Tanzania walipovuka mpaka wa Tanzania na kuingia Uganga na kufanya jaribio la kumpindua Amin. Hata hivyo, jaribio hilo lilishindwa na kasha kikosi hicho kikarudi tena Tanzania.

Haya sasa, wale wanaotaka kujitia upofu kwa makusudi; watuambie ni kiongozi gani duniani angevumilia kitendo ambacho kilifanywa na Tanzania kwa kuacha Waganda waliopo nchini wavuke mpaka na kuingia Uganda kwenda kufanya jaribio la mapinduzi kasha kurudi tena nchini. Je, hapo Tanzania ilikuwa ni hifadhi ya wakimbizi au kituo cha kijeshi kwa wale waliokuwa na nia ya kumtoa Amin madarakani?! Kimsingi, hakuna jaribio la mapinduzi ambalo linaweza kufanyika pasipo na maandalizi ya kijeshi. Hata mapinduzi madogo kama yale ya Zanzibar 1964 palikuwa na mafunzo pamoja na maandalizi ya kijeshi kabla ya mapinduzi hayo kufanyika. Je, hawa wakimbizi wa Uganda ambao walitoka Tanzania na kuingia Uganda kwenda kumpindua Amin walichukulia wapi maandalizi na mafunzo ya mapinduzi amabayo walienda kuyafanya?! Je, mnataka kusema kwamba serikali ya Tanzania hawakufahamu dhamira ya Waganda ambao walikuwepo nchini?! Hivi kweli Intelligence system ya Nyerere ambahyo ilikuwa very competent haikufahamu kwamba wakimabizi wa Uganda walikuwa na nia ya kuvuka mpaka na kuingia Uganda kufanya mapinduzi?! Kwa intelligence system ya sasa inawezekana lakini sio ile ya Nyerere!!

Hivyo basi, ingawaje Amin alivamia Tanzania na kuikalia sehemu ya Mkoa wa Kagera na kudai ni ya Uganda lakini source ya chokochoko ni Nyerere mwenyewe ambae hakufurahishwa kitendo cha Amin kumpindua Obote; swahiba wa Nyerere! Aidha, ikumbukwe kwamba, hata OAU haikuiunga mkono Tanzania kwa kile kilichoonekana Tanzania kuingilia masuala ya ndani ya Uganda!! Na kwa kunoesha kwamba hawakupendezwa na suala la Tanzania kuingilia masuala ya ndani Uganda, OAU ilikataa ombi la Nyerere alilotaka kwamba OAU imlaani Amin!! Na kwa kumuumbua zaidi, Mkutano wa OAU ulifanyika Uganda ambao Nyerere alisusa kwenda kwavile tu OAU haikukubaliana na takwa lake la kuitaka jumuiya hiyo imlaani Amin.

Swali lingine linafuata hapo! Hivi kweli OAU ilikuwa na mapenzi zaidi kwa Amin kuliko Nyerere ambae alijitolea kwa ari na mali katika ukombozi wa Afrika; Kusini mwa Jangwa la Sahara?! Bila shaka, jibu ni HAPANA….sina shaka yoyote kwamba OAU ilikuwa inampenda zaidi NYerere(Tanzania) kuliko Amini lakini bila shaka walisukumwa na methali ya kiswahili isemayo “Mnyonge Mnyongeni, Haki Yake Mpeni!” Kwamba, hata kama ni kwali Amin alikuwa ni mshenzi dhidi ya Tanzania na watu wake lakini ushenz wake dhidi ya Tanzania ulisababishwa na sisi wenyewe.
Kitu kimoja ambacho alifudhu Nyerere kwenye vita hivyo ni PROPAGANDA! Alipiga propaganda za kutosha hadi akafanikiwa na kuonesha kwamba tatizo ni Amin….! Propaganda hizi zilienezwa kwa nji mbaliambali ikwemo nyimbo, machapicho na kwa njia ya muziki. Watanzania wote wakaamini kwamba Amin ni tatizo ingawaje kiini cha tatizo ulikuwa ni Nyerere mwenyewe!!

Kwa kumalizia; kama alivyosema William; kwavile Amin aliivamia Tanzania kulikuwa na ulazima gani wa kuhakikisha tunamfutilia mbali?! Jibu ni kwamba, hatukuwa na sababu hiyo! Ilitosha kabisa kumwondoa kwenye mipaka ya Tanzania na kasha kuimarisha mipaka yaetu!! Lakini kwavile lengo la Nyerere alikuwa tu kuilinda mipaka ya Tanzania, basi alihakikisha anaingia ndani kabisa ya Uganda na kumwondoa Amin madarakani!!



Umeongea vyema sana ila kuna sababu nyengine umeificha ambayo ni moja ya sababu kuu ya nyerere kumuondoa AMIN
 
It amazes me when one who is truly biased calls another biased! NazDaz, umeshasema kwa kauli yako mwenyewe kwamba wewe ni anti-Nyerere. Kwa hiyo hata kama jokaKuu anaweka facts, alimradi zinamwonyesha Nyerere in a good light hutokubaliana nazo.

Jasusi,
Sina shaka yoyote kwamba miongoni mwa watu makini humu jamvini wewe ni mmoja wao. Mtu aliye makini hawezi kukurupuka na kusema kitu kisicho na ushahidi hata kidogo.....kwahiyo je, unaweza kunionesha post yangu angalau moja ambayo nimesema kwamba mimi ni anti-Nyerere?! Niwekee hiyo post, iwe ya leo au siku za nyuma ambayo nimetamka kwamba mimi ni anti-Nyerere!! Am very confidence kwamba hamna hiyo post na kama nimepitiwa basi ibandike hapa!! Nakiri wazi kwamba mara nyingi nimekuwa nikikosoa na baadhi ya mambo yaliyofanywa na Nyerere, mathalani hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/199759-nyerere-hakuwa-na-mapungufu-alikuwa-kiongozi-mbovu.html . Na sio Nyerere tu, hata Kikwete nimewahi kukosoa baadhi ya yale ninayoona amekosea, mathalani hapa: https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/223514-happy-valentine-h-e-jakaya-mrisho-kikwete.html .

Haya nielimishe mkuu wangu, je kumkosoa mtu ni kuwa anti-him/her?! Ina maana unataka tuwe tunakubali na kushangilia kila tunaloambiwa kama inavyotokea tunavyoambiwa na vitabu vyetu vya kidini kwa kuhofu kwamba kupinga ni kukufuru?!

Niwekee hiyo post niliyotamka kwa maneno yangu kwamba mimi ni anti-Nyerere!!!!!
 
William,
Jibu rahisi ni kwamba hatukuwa na sababu ya kumhifadhi Obote. Hatukuwa na sababu ya kuwa na uhusiano hasimu na Iddi Amin. Iddi Amin was the best thing that ever happened to Africa and Uganda. We should have loved him and not make war on him. Simply Nyerere was mad to fight with Amin. Tulifanya makosa makubwa sana. Nadhani hapo utaridhika. Anzisha sasa topic nyingine tumkosoe na kumdadavua Nyerere. Ngoja nikusaidie; Nyerere and African liberation. Big mistake. Nyerere and Pan Africanism: ndoto ya mchana. Nyerere and the Development of Man: it will never happen. Niendelee?

Mkuu Pan Africanism ni jambo jema sana, only shortsighted atapinga! Mtu yeyote mwenye hisia za Umoja hapendwi na Wazungu, watafanya chochote aonekane mbaya! Mifano: Gadaffi, Mugabe, Nyerere, nk! Only Waafrika hatujui kuwa mchawi wetu ni sisi wenyewe.
Back to topic kuhusu Vita ya Uganda, Idi Amin alianza chokochoko tangu mwaka 1972, mwaka mmoja baada ya kuchukua madaraka! Hizi chokochoko ziliendelea hadi alipivamia nchi yetu na kuimega mwaka 1978! Mimi nionavyo ilikuwa ni sahihi kumtoa huyu nduli kwa kuwa alikuwa ni threat kwa amani ya nchi yetu!
 
Jasusi,

..LOL!!

..jamaa ametaharuki baada kumwambia kwamba Nyerere alimtoa Iddi Amini "akampachika" Yussuf Lule.

..hiyo inavunja hoja ilee ambayo Mwalimu hasakamwa nayo.

..nimebahatika kusoma kitabu " The War in Uganda ", wanaelezea vizuri sana jinsi process nzima ya kupatikana kwa post-Amini government. Sikumbuki mahali popote pale ambapo Mwalimu alitia mkono wake.

..zaidi, kwa nguvu za kijeshi alizokuwa nazo Mwalimu, na jinsi Waganda walivyokuwa wakimtegemea, Mwalimu asingeshindwa kumuweka Obote madarakani. Ukweli ni kwamba Mwalimu hakuwa na nia hiyo.

JokaKuu, mwalimu hakuwa mpumbavu na mjinga. Ni rais mpumbavu tu ndie angechukua uamuzi wa kumsimika Obote moja kwa moja. Bado Mwalimu alitaka kuushawishi umma kwamba aliingia Uganda kwa ajili ya kuitetea Tanzania kwahiyo endapo Obote angesimikwa moja kwa moja basi tuhuma dhidi yake kwamba alijiingiza Uganda kwa ajili ya kumtetea Obote zisingekuwa na ubishi kama ilivyo sasa. Pamoja na Yusuf Lule kupachikwa urais wa Uganda(kwa msaada wa Tanzania); Nyerere alifahamu kwamba itabidi uchaguzi ufanyike Uganda na alikuwa na uhakika kwamba swahibu wake Obote atashinda tu!!

By the way, nini kitakachonifanya nitaharuki baada ya kuambiwa kwamba baada ya Amin kuondolewa ni Lule ndie alipachikwa Urais?! Yaani ulitarajia hiyo kwangu iwe ni habari ngeni? Usinichekeshe wakati sijisikii kucheka hivi sasa! Also, kwanini mnakwepa kujibu hoja ya msingi.....kwamba, je wakati Obote allies wanavuka mpaka wa Tanzania na kuingia Uganda na kufanya jaribio la mapinduzi; serikali ya Tanzania ilifahamu au haikufahamu?! Ingewezekana vipi Waganda wafanye maandalizi ya mapinduzi ndani ya Tanzania na Tanzania isifahamu! Na kwanini hata baada ya Tanzanaia kufahamu kwamba Obote na watu wake walikiuka miiko ya ukimbizi bado watu hao waliendelea kubaki Tanzania?! Acheni mawazo mgando, binafsi simchukii Nyerere lakini sioni taabu hata kidogo kuyaelezea mafyongo aliyoyafanya! Hata kama mtaona ni chuki dhidi ya Mwalimu, hayo ni yenu lakini ukweli bado utabaki pale pale.....katu siwezi kuisoma historia sawa na ninavyosoma maandiko ya dini!!
 
Back
Top Bottom