Vita vya Kagera: Nini chanzo? Kulikuwa na ulazima?

Vita vya Kagera: Nini chanzo? Kulikuwa na ulazima?

William;

US and EU countries are spending billion of dollars monthly to finance war and other projects in Afghanistan, do you want to tell me they don`t have problems in their countries? Sovereignty comes up with costs; he was ready to defend us at any cost! He worked hard to make sure every Tanzanian has a better life, the man died like an ordinary Tanzanian; the good thing about him he did not used the office of president to enrich himself or his family; instead of using him as a scapegoat let face the reality Mwl. Nyerere is past in Tanzania politics;may be we need to question our leaders why Tanzanians are facing the same problems? Mwl. had lots of challenges, all western countries and their institutions were worked against him; can`t you see the difference between then and now? You can argue on the issue but he was policy maker and not a follower; we have live long enough to know the truth. Who decides our foreign policy now?

Chama
Gongo la Mboto DSM
A really great thinker has said it all yooo
 
I see,like father,like son,kwa hiyo bado unakumbuka alipomtoa Cigweyemisi kwenye mkutano????hahaha shem on you,inabidi ukubali tu ukweli,kuna watu wengi tu wa kuongoza hii nchi,si ukoo mmoja ndo uongoze bro,so unamuandama nyerere kwa sababu hakuiva na cigweyemisi???alipomwambia ''agwe,out????acha siasa za visasi bhana
 
udini aliokuwa nao nyerere ndio ulisababisha kuingia vitani, alifanikiwa znz akataka na uganda amuondoshe idd amin.
 
Naona umekuja na nyingine, hivi Nyerere alikukosea nini?..

ndiye aliitia nchi katika janga la umasikini na madeni ambayo mpaka ulimwengu huu utakwisha hatuwezi kulipa

tutaendelea kulipa riba za deni,

sababu ni kumrudisha mkatoliki mlevi mwenzake madarakani
 
lege usiwe legelege kwenye kutafuta ukweli; soma majarida mbalimbali utapata sababu halisi za vita na uganda nimekwambia nenda bukoba ukaseme upuuzi huo uone watakachokufanya; vita si kitu kizuri na nyerere hakuwa na jinsi hatukuwa na muda wa kufanya mazungumzo ya kutafuta amani; isingekuwa rahisi hata kufanya maongezi yenyewe idd amin na majeshi tayari walikuwa ndani ya ardhi ya tanzania, unaposema kovu la bukoba sio ishu bali ishu ni tanzania labda nikuulize bukoba ilikuwa sehemu ya kenya? Hizi hadithi za kusikiliza kwenye vilinge vya kahawa vitafutie ukweli kabla ya kuvisema hadharani. Ukimkuta mtu chumbani kwako anamchapa makofi mkeo utapigana au utamuomba samahani?

Chama
gongo la mboto dsm

aliona raha kumweka yule mkatoliki mlevi pale dar-es salaam akamsaidia kupata askari wa kwenda kufanya hujuma kule kampala , unafikiri amin atafurahia yale .

Angaliwacha waganda wakasolve matatizo yao kwani imngalikuwa nini ??? Si angaliwanasuru kule bukoba na uvamizi??

KAMA ANAVYOSEMA MWENYEWE, "ukianza kula nyama ya mtu huwezi kuiwacha tena "

baada ya kula nyama za watu kule zanzibar akakimbilia uganda

na alipomaliza huko alishaanza vurugu na kenya kumbuka mambo ya unyang`au

pia alijaribu huko nyuma na malawi lakini kulikuwa kugumu

huyo ndiye mkatoliki nyerere
 
- Nimeuliza swali tu, unaweza kujibu kama unalo na kama huna kama unavyoonyesha waachie wengine wajibu, maana wapo humu wenye majibu!! William.
TENA WILLIAM KAZIDISHA CHUKI ZAIDI KUHUSU NYERERE BAADA YA KUSHINDWA BUNGE LA AFRICA MASHARIKI HUKU MAKOKNGORO AKIPETA HATA MTOTO ATAONA CHUKI HIZO, SASA hivi kuna mambo mengi ya msingi UFISADI REPORT YA CAG WILLIAM HATAKI KUZIJADILI ama kweli waliosema thinking yako imeshuka 100% katika topic nyingine hawakukosea BUT ndi mmefutika hivyo katika sisa comes 2015!
 
Watanzania hakika tu watu wa ajabu sana. Kuna baadhi yetu ambao kwa bahati mbaya sana hawataki kabisa kusikia vipenzi wao wakisemwa kwa mabaya hata kama kweli mabaya hayo waliyafanya. Kama walivyo mashabiki wa CHADEMA ambao hawataki kabisa kusikia mtu kama Dr. Slaa akisemwa kwa mabaya, kuna wengine ambao hawataki hata kidogo kusikia baya likisemwa dhidi ya Nyerere. Hawa wote, ukisema baya kuhusu vipenzi vyao basi watakuja juu na kukupa majibu ya kifedhuli na kihayawani….lakini wote hawa bado wanajiita ni Greatest Thinkers!!

Sasa nirudi kwenye mada.

Ukweli bado utabaki pale pale kwamba kwa pale ilipofikia, Tanzania haikuwa na budi bali kuingia vitani dhidi ya Amin. Hata hivyo, bado ukweli unabaki paleplae kwamba point ambayo ilikuwa lazima tuingie vitani ilisababishwa na Nyerere mwenyewe.

Baada ya Amin kumpindua Obotte, Milton Obotte alipewa hifadhi na Nyerere. Kimsingi, hapakuwa na ubaya wowote kwa Nyerere kumpa Obote hifadhi hapa Tanzania. Hadi Nyerere anampa hifadhi Obote pamoja na maelfu ya wakimbizi bado Amin alikuwa hajaonesha uchokozi wa wazi dhidi ya Tanzania. Tatizo kuu lilianza pale Wakimbizi wa Uganda waliopo Tanzania walipovuka mpaka wa Tanzania na kuingia Uganga na kufanya jaribio la kumpindua Amin. Hata hivyo, jaribio hilo lilishindwa na kasha kikosi hicho kikarudi tena Tanzania.

Haya sasa, wale wanaotaka kujitia upofu kwa makusudi; watuambie ni kiongozi gani duniani angevumilia kitendo ambacho kilifanywa na Tanzania kwa kuacha Waganda waliopo nchini wavuke mpaka na kuingia Uganda kwenda kufanya jaribio la mapinduzi kasha kurudi tena nchini. Je, hapo Tanzania ilikuwa ni hifadhi ya wakimbizi au kituo cha kijeshi kwa wale waliokuwa na nia ya kumtoa Amin madarakani?! Kimsingi, hakuna jaribio la mapinduzi ambalo linaweza kufanyika pasipo na maandalizi ya kijeshi. Hata mapinduzi madogo kama yale ya Zanzibar 1964 palikuwa na mafunzo pamoja na maandalizi ya kijeshi kabla ya mapinduzi hayo kufanyika. Je, hawa wakimbizi wa Uganda ambao walitoka Tanzania na kuingia Uganda kwenda kumpindua Amin walichukulia wapi maandalizi na mafunzo ya mapinduzi amabayo walienda kuyafanya?! Je, mnataka kusema kwamba serikali ya Tanzania hawakufahamu dhamira ya Waganda ambao walikuwepo nchini?! Hivi kweli Intelligence system ya Nyerere ambahyo ilikuwa very competent haikufahamu kwamba wakimabizi wa Uganda walikuwa na nia ya kuvuka mpaka na kuingia Uganda kufanya mapinduzi?! Kwa intelligence system ya sasa inawezekana lakini sio ile ya Nyerere!!

Hivyo basi, ingawaje Amin alivamia Tanzania na kuikalia sehemu ya Mkoa wa Kagera na kudai ni ya Uganda lakini source ya chokochoko ni Nyerere mwenyewe ambae hakufurahishwa kitendo cha Amin kumpindua Obote; swahiba wa Nyerere! Aidha, ikumbukwe kwamba, hata OAU haikuiunga mkono Tanzania kwa kile kilichoonekana Tanzania kuingilia masuala ya ndani ya Uganda!! Na kwa kunoesha kwamba hawakupendezwa na suala la Tanzania kuingilia masuala ya ndani Uganda, OAU ilikataa ombi la Nyerere alilotaka kwamba OAU imlaani Amin!! Na kwa kumuumbua zaidi, Mkutano wa OAU ulifanyika Uganda ambao Nyerere alisusa kwenda kwavile tu OAU haikukubaliana na takwa lake la kuitaka jumuiya hiyo imlaani Amin.

Swali lingine linafuata hapo! Hivi kweli OAU ilikuwa na mapenzi zaidi kwa Amin kuliko Nyerere ambae alijitolea kwa ari na mali katika ukombozi wa Afrika; Kusini mwa Jangwa la Sahara?! Bila shaka, jibu ni HAPANA….sina shaka yoyote kwamba OAU ilikuwa inampenda zaidi NYerere(Tanzania) kuliko Amini lakini bila shaka walisukumwa na methali ya kiswahili isemayo "Mnyonge Mnyongeni, Haki Yake Mpeni!" Kwamba, hata kama ni kwali Amin alikuwa ni mshenzi dhidi ya Tanzania na watu wake lakini ushenz wake dhidi ya Tanzania ulisababishwa na sisi wenyewe.
Kitu kimoja ambacho alifudhu Nyerere kwenye vita hivyo ni PROPAGANDA! Alipiga propaganda za kutosha hadi akafanikiwa na kuonesha kwamba tatizo ni Amin….! Propaganda hizi zilienezwa kwa nji mbaliambali ikwemo nyimbo, machapicho na kwa njia ya muziki. Watanzania wote wakaamini kwamba Amin ni tatizo ingawaje kiini cha tatizo ulikuwa ni Nyerere mwenyewe!!

Kwa kumalizia; kama alivyosema William; kwavile Amin aliivamia Tanzania kulikuwa na ulazima gani wa kuhakikisha tunamfutilia mbali?! Jibu ni kwamba, hatukuwa na sababu hiyo! Ilitosha kabisa kumwondoa kwenye mipaka ya Tanzania na kasha kuimarisha mipaka yaetu!! Lakini kwavile lengo la Nyerere alikuwa tu kuilinda mipaka ya Tanzania, basi alihakikisha anaingia ndani kabisa ya Uganda na kumwondoa Amin madarakani!!


 
nafurahi na kufarijika kwamba hukupata nafasi ya ubunge wa EAC......jana sijui juzi umekuja na thread ya biafra..tumekusaidia majibu tukidhani pengine ulikuwa mdogo sana kujua kilichotokea na ulikuwa unaimbishwa nyimbo bila kujua OJUKWU alikuwa ni nani na ilikuwaje hadi biafra ikataka kujitenga..

leo unapokuja na hili la kuhusu vita ya uganda basi naona kna shida kubwa sana katika akili yako na ufahamu wako....uwezo wako wa kpambanua mambo ni mdogo kiasi kwamba huwezi kujua nini kilitokea na leo unauliza swali la kipuuzi..... Jasusi ndugu yangu amekujibu vizuri sana na sijui kama umemwelewa!!! anyway polse sana willie pole sana kijana wa mzee jumanne..pole sana
 
Last edited by a moderator:
Naona umekuja na nyingine, hivi Nyerere alikukosea nini?..
Huyu Jamaa hivi sasa ndio anapata muda wa kukaa na mzee, nadhani mzee anamuelezea namna mwalimu alivyoingia mission zake. kumbuka ilifikia hatua ya mzee kusilimu ili kufikia malengo yake lakini bado mwalimu alikomaa nae. Kwa msingi huu jamaa ana haki na wajibu wa kumchimba mwalimu.
 
Lege usiwe legelege kwenye kutafuta ukweli; soma majarida mbalimbali utapata sababu halisi za vita na Uganda nimekwambia nenda Bukoba ukaseme upuuzi huo uone watakachokufanya; vita si kitu kizuri na Nyerere hakuwa na jinsi hatukuwa na muda wa kufanya mazungumzo ya kutafuta amani; isingekuwa rahisi hata kufanya maongezi yenyewe Idd Amin na majeshi tayari walikuwa ndani ya ardhi ya Tanzania, unaposema kovu la Bukoba sio ishu bali ishu ni Tanzania labda nikuulize Bukoba ilikuwa sehemu ya Kenya? Hizi hadithi za kusikiliza kwenye vilinge vya kahawa vitafutie ukweli kabla ya kuvisema hadharani. Ukimkuta mtu chumbani kwako anamchapa makofi mkeo utapigana au utamuomba samahani?

Chama
Gongo la Mboto DSM

Chama
Labda tu tuseme wazi kwamba ama huifahamu historia ya Vita Vya Kagera au nawe ni miongoni mwa watu ambao hawapo tayari kusema ukweli ikiwa wanahisi ukweli huo unauma au unaingilia maslahi yao. Hilo la pili si jambo jema hata kidogo kwa mustakabali wa Taifa linalohitaji ukombozi wa kweli! Kama tatizo ni hilo la kwanza (kwamba huifahamu historia ya vita ile) basi ningekushauri tafuta ukweli!

Kwa kuzingatia hapo kwenye RED, ni kweli Tanzania hapo ilikuwa katika POINT OF NO RETURN! Hata hivyo, hiyo Point of No Return tuliisababisha sisi wenyewe!! Ni bahati mzuri kwa Nyerere kwamba Amin hakuwa mzungumzaji mzuri kiasi cha kumfanya awe mwana-propaganda mahiri vinginevyo uchokochoko wa Nyerera ungedhihirika wazi! Madai kwamba mtu aende Bukoba akaseme huo unaouita upuuzi ni madai yasiyo na msingi na katu hayawezi kuondoa ukweli kwamba chokochoko tuliifanya wenyewe! Wana-Bukoba wana kila sababu ya kuwa hivyo kwavile hakuujua upande wa pili wa shilingi. Walichojuzwa wao ni ujeuri wa Amin na kwavile wameshuhudia majeshi yake yakiingia Bukoba kabla ya kwetu hayajaenda huko basi wana kila sababu ya kuamini kwamba Amin ndo chanzo cha yote! Kitu ambacho kilitokea kwa Nyerere na Ami ni sawa na yale yanayotokea kwenye dimba la kandanda! Unakuta mchezaji anampiga Dole makusudi mchezaji wa timu pinzani huku akiamini kwamba ni lazima mchezaji huyo atachukia na kurusha makonde na hatimae kuvuna kadi nyekundu!! Nyerere alimpiga Amin kidole cha kwenye makalio na kwa bahati mbaya Amin hakukubali kufanywa fa.ra na hivyo karudisha makonde!!

Kwa tunaopenda haki, ingawaje wengine mnatuita tuna chuki na Nyerere hapo tunafahamu kwamba tatizo ni huyo aliyempiga finger mwenzake....ni nani aliye rijali atakubali apigwe finger?!
 
- Ina maana somo limeeleweka, that is all I could ask from Great Thnkers!!

William.

Bado acha kukimbiza Mwenge.
Kilichofanyika dhidi ya Iddi Amini ni kitu cha kujivunia sana watanzania, kumuondoa kwenye ardhi ya Tanzania pekee ilikuwa haitoshi, sababu angerudi kujipanga na angeweza kurudi tena kutusumbua sababu iliishathibitika kwamba alikuwa na akili za kishenzi, kitu ambacho kingetufanya kama Taifa wakati wote kywa na hofu ya kuingia vitani tena, kwa hiyo kilichofanyika ni kuondoa mzizi wa fitina, uproot him.

Mpaka sasa nyie mnao vaa mashati yakijani mmeendelea kuimba nyimbo za nchi ya amani na utulivu japo mnaonyesha kuanza kusahau, lakini msingi wa amani na utulivu katika nchi yetu ulipatikana baada ya

1. Kuiunganisha Tanganyika na Zanzibar
2. Kumuondoa Idd Amini Kampala

Huu ni ukweli mchungu kukubarika kwenu, vibaraka na makuhadi wa mataifa ya magharibi na matajiri uchwara wasiojari maslahi ya mtanzania maskini.

William kinachokusumbua ni maisha ya tamaa na anasa, umezunguka dunia nzima na kuona namna watoto wa watawala na wanavyofaudi maisha ya hanasa kwenye mataifa mbali mbali africa, na sasa umejawa na hasira dhidi ya mwalimu kwa sababu aliwadhibiti wote waliokuwa karibu naye wasiweze kufanya hujuma kwa watanzania ambao walikuwa bado hawajafunguka macho, imani yako inakuambia kwamba kama asingekuwa mwalimu kwa nafasi alizoshika mzee kwenye Taifa hili wewe haukustahili kwenda kufanya kazi za kipagazi kwenye meli za mizigo, inakuuma kwamba ulilazimika kutafuta maisha kwa ugumu sana kama vijana wengine wa kitanzania, na unalithibitisha hilo kwa kumuonea wivu ridhiwani ambaye mzee wake ameshika hatamu za uongozi wa taifa hili katika kipindi ambacho mwalimu anaozea ardhini na hivyo kuyaenjoy maisha kama watoto wa marais na viongozi wengine wakubwa wa mataifa ya africa, unamuonea wivu January sio, na wakina malima.

kweli ukubwa wa mwili sio wingi wa busara
 
Muulize baba yako kwani yeye alikuwa kwenye saddle.Great thinkers tunazungumzia ya magamba wanavyo tumaliza.tatizo nimegundua huna mawasiliano na baba yako; hayo ndio yakuongea mkinywa kahawa. Nilitegemea utuambie meli ina nanga ngapi n.k usituvuruge
WILLY GAMBA,una akili sana.
 
Last edited by a moderator:
Bado kidogo tu ataanza kumuandama MKAPA kwa kuondoa jina la Malecela 2005, kumbe waliokaa na huyo mzee inawezekana akili zake ni kama za mwanae ndio maana WALIMUTUPILIA MBALI KUKAMATA UONGOZI WA TAIFA HILI! AKIMALIZANA NA MKAPA ATAANZANA NA KIKWETE KWA KUMUNG'OA MALECELA KATIKA UMAKAMU MWENYEKITI NA KUMUWEKA MSEKWA!! kazi kweli bado ipo willy!!
 
Last edited by a moderator:
William,

..baada ya vita na mazungumzo ya vikundi vya waganda yaliyofanyika Moshi, Raisi aliyefuatia wa Uganda alikuwa Prof.Yussuf Kironde Lule.

..Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania aliyesimamia mazungumzo ya Moshi alikuwa Benjamin Mkapa.

..Prof.Yussuf Lule alikosana na wenzake ktk serikali, wakamtoa, na kumuweka, Godfrey Lukongwa Binaisi. Baadaye kukatokea mgogoro mwingine Uraisi ukakaimiwa na Paulo Muwanga.

..Apollo Milton Obote aliingia madarakani kupitia uchaguzi uliofanyika Uganda. Kwa msingi huo, kusema Mwalimu alimtoa Amini na kumpachika Obote, nadhani is a little stretching.

JokaKuu,
Sina tatizo na wewe hata kidogo kuhusu uwezo wako wa kuchambua mambo....u're great! hata hivyo, tatizo lako JokaKuu ni kwamba upo very biased!! Wewe huoni taabu kupotosha ukweli kwa ajili tu ya kulinda kile unachokiamini au kukitetea!! Ni kweli, baada ya Amin kuondolewa madarakani ni Yusuf Lule ndie alishika hatamu za uongozi!! Hivi unazani Nyerere could be stupid enough amweke Obote soon after kumwondoa Amin madarakani wakati tayari tuhuma zilishaanza kutolewa kwamba kilichomfanya Nyerere kuingia vitani ni kumtetea Obote?! Only the most Foolish President could do otherwise!! Ingawaje ni Yusuf Lule ndie alishika hatamu, Nyerere alishajua sooner or later Obote angerudi tu kwenye kiti chake kwavile tayari paliwekwa nia ya kuitisha uchaguzi ambao kila mtu, including Nyerere alifahamu fika kwamba lazima Obote angeshinda tu!!
 
Malecela,Idi Amini hakufanya uvamizi mara moja tu,na pia nia yake ilikuwa ni kui annex Kagera,kumwacha madarakani ni guarantee kuwa atarudi tena more forcefuly,so unaweza kuona ili watanzania waweze kuishi kwa amani bila wasi wasi wa lini watavamiwa,basi ni muhimu aliondolewa,pia sidhani kama aliwahi kukanusha kuwa Kagera ni ya UGANDA.btw mkuu umebadili dini nini?
 
JokaKuu,
Sina tatizo na wewe hata kidogo kuhusu uwezo wako wa kuchambua mambo....u're great! hata hivyo, tatizo lako JokaKuu ni kwamba upo very biased!! Wewe huoni taabu kupotosha ukweli kwa ajili tu ya kulinda kile unachokiamini au kukitetea!! Ni kweli, baada ya Amin kuondolewa madarakani ni Yusuf Lule ndie alishika hatamu za uongozi!! Hivi unazani Nyerere could be stupid enough amweke Obote soon after kumwondoa Amin madarakani wakati tayari tuhuma zilishaanza kutolewa kwamba kilichomfanya Nyerere kuingia vitani ni kumtetea Obote?! Only the most Foolish President could do otherwise!! Ingawaje ni Yusuf Lule ndie alishika hatamu, Nyerere alishajua sooner or later Obote angerudi tu kwenye kiti chake kwavile tayari paliwekwa nia ya kuitisha uchaguzi ambao kila mtu, including Nyerere alifahamu fika kwamba lazima Obote angeshinda tu!!

Sasa tuamini kilichotokea au kilichopangwa kutokea, mi naona hapa wewe ndio unayepotosha ukweli kwa ajili ya kulinda unachokiamini.samahani aisee, mimi huu nauita ni unafiki na uchonganishi.
 
Malecela,Idi Amini hakufanya uvamizi mara moja tu,na pia nia yake ilikuwa ni kui annex Kagera,kumwacha madarakani ni guarantee kuwa atarudi tena more forcefuly.btw mkuu umebadili dini nini?
Possible, anaweza kuwa ameamua kufuata njia ya mzee.
 
Possible, anaweza kuwa ameamua kufuata njia ya mzee.

Hizi issue zishajadiliwa sana humu,nilidhani labda mleta mada ana data mpya kuhusiana na hizi issue.Nadhani alikasirika ,Nyerere alipomwita baba yake "muhuni" Tena na hivi wamempa Makongoro ulaji wa EA,basi mutegemee vurugu sana za magamba.
 
Chama
Labda tu tuseme wazi kwamba ama huifahamu historia ya Vita Vya Kagera au nawe ni miongoni mwa watu ambao hawapo tayari kusema ukweli ikiwa wanahisi ukweli huo unauma au unaingilia maslahi yao. Hilo la pili si jambo jema hata kidogo kwa mustakabali wa Taifa linalohitaji ukombozi wa kweli! Kama tatizo ni hilo la kwanza (kwamba huifahamu historia ya vita ile) basi ningekushauri tafuta ukweli!

Kwa kuzingatia hapo kwenye RED, ni kweli Tanzania hapo ilikuwa katika POINT OF NO RETURN! Hata hivyo, hiyo Point of No Return tuliisababisha sisi wenyewe!! Ni bahati mzuri kwa Nyerere kwamba Amin hakuwa mzungumzaji mzuri kiasi cha kumfanya awe mwana-propaganda mahiri vinginevyo uchokochoko wa Nyerera ungedhihirika wazi! Madai kwamba mtu aende Bukoba akaseme huo unaouita upuuzi ni madai yasiyo na msingi na katu hayawezi kuondoa ukweli kwamba chokochoko tuliifanya wenyewe! Wana-Bukoba wana kila sababu ya kuwa hivyo kwavile hakuujua upande wa pili wa shilingi. Walichojuzwa wao ni ujeuri wa Amin na kwavile wameshuhudia majeshi yake yakiingia Bukoba kabla ya kwetu hayajaenda huko basi wana kila sababu ya kuamini kwamba Amin ndo chanzo cha yote! Kitu ambacho kilitokea kwa Nyerere na Ami ni sawa na yale yanayotokea kwenye dimba la kandanda! Unakuta mchezaji anampiga Dole makusudi mchezaji wa timu pinzani huku akiamini kwamba ni lazima mchezaji huyo atachukia na kurusha makonde na hatimae kuvuna kadi nyekundu!! Nyerere alimpiga Amin kidole cha kwenye makalio na kwa bahati mbaya Amin hakukubali kufanywa fa.ra na hivyo karudisha makonde!!

Kwa tunaopenda haki, ingawaje wengine mnatuita tuna chuki na Nyerere hapo tunafahamu kwamba tatizo ni huyo aliyempiga finger mwenzake....ni nani aliye rijali atakubali apigwe finger?!

Kwa vyovyote itakavyokuwa, Uwapo wa Idd Amini Madarakani Uganda kungeweka security interest za Tanzania Matatani, Kumuondoa ilikuwa maamuzi sahihi bila kujalisha kwamba alituchokoza au hakutuchokoza acheni kufikiria ndani ya box.

Idd Amini alikuwa na close relation na ghadafi, Mwalimu alikwisha kuona madhara ya kuwa close na Taifa lolote linalofungamana na utawala wa ghadafi, kuonyesha kwamba mwalimu alikuwa sahihi angalia madhara ambayo ghadafi ameyaacha africa sasa, Instability ya Mali na Algeria ni matokeo ya interest za ghadafi.

Katika kila taifa ambalo tunalizodoa leo kwamba halina amani na utulivu, matatizo kwenye mataifa hayo yanachangiwa kwa viwango vikubwa na mataifa jirani zao.
Angalia, Burundi, Rwanda, Uganga,Somalia,Sudani,Congo,Mali, kote uko, waasi wanajificha kwenye nchi jirani ama wanapata direct support kutoka nchi za jirani, angalia matatizo yanayoisumbua Nairobi sasa,source ni somalia.

Kama mmeamua kufikiri, ni lazima mfikiri kweli kweli, msisukumwe na hisia zenu ama kuchukua maelezo ya upande mmoja, na nikumbushe kwamba the great thinker as long as Tanzania is concerned is the one who think in the best interest of Tanzania, I do not settle for less than that.

Chuki dhidi ya Mwalimu zinajengwa juu ya dhana dhaifu sana, na yanapata support za watu wenye vichwa vidogo sana, Kwamba Mwalimu aliua watu, which president does not kill, Yes He killed so many people, hata sasa, for the best interest of responsible politics and economical stability of this country, so many people were supposed to have got silenced.

Just like they silenced Balali, Kolimba & CO. Kwa ajiri ya kulinda interest zenu.

Look at Kagame and his Burundi, unazijua siri za kutawalika kwa Burundi wewe. Poor Me. Only the stupid mind will blame the dead.
 
William,

Maoni ya ngu ni kuwa haikuwa ni lazima kumkaribisha Obote Tanzania mwaka wa 1971!.

Alipopinduliwa na Idi Amin alikuwa akirudi toka mkutano wa Commonwealth uliofanyika Singapore, akiwa katika ndege moja na rafiki yake Nyerere. Walipofika Nairobi, Obote hakuthubutu kuendelea mpaka Entebbe, na Nyerere akaamua kumkaribisha Dar es Salaam.

Idi Amin alitambuliwa kama mtawala halisi wa Uganda na nchi nyingi, hata Umoja wa Kimataifa na Kenya. Lakini Tanzania tulikataa kumtambua kama mtawala wa Uganda kutokana na Obote kuwa mgeni wa Nyerere. Wengi wetu tuliokuwa serikalini tulipendekeza Obote atafutiwe makazi katika neutral country kama Switzerland, lakini rafiki yake akang'ang'ania akae pale Msasani jirani naye.

Huu ndio mwanzo wa vituko vya Waganda walio-support Obote kuhamia Tanzania na mizozo iliyotugharimu sana, in terms of lives and wasted resources in unnecessary wars. Maendeleo yetu yakudumaa au kutokuenda mbele kwa kasi inayostahili kutokana na ung'ang'anizi huu wa Rais wetu.

Wote wawili ni marehemu sasa. Mungu alaze roho zao mahala pema peponi. AMEN!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom