Vita vya Kagera: Nini chanzo? Kulikuwa na ulazima?

Mkuu ritz,
Upo serious au unatania?! Ina maana ni kweli watu walikuwa wanalazimishwa kuvaa t-shirt za UPC?! Tell me u're kidding!

Mkuu NasDaz

Watu walikuwa hawalazimishwi kwa nguvu lakini wataki unapewa unaambiawa uvaae bahati mbaya zaidi watu wengi walikuwa hawana nguo walikuwa wanaomba mbili mbili mpaka tatu mkuu wewe ukubahatika kuvaa?...swali langu je ililukuwa sawa raia wa Tanzania kuvalishwa t-shirts za Apolo Milton Obote.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ritz,
Upo serious au unatania?! Ina maana ni kweli watu walikuwa wanalazimishwa kuvaa t-shirt za UPC?! Tell me u're kidding!

Mkuu NasDaz

Watu walikuwa hawalazimishwi kwa nguvu lakini wataki unapewa unaambiawa uvaae bahati mbaya zaidi watu wengi walikuwa hawana nguo walikuwa wanaomba mbili mbili mpaka tatu mkuu wewe ukubahatika kuvaa?...swali langu je ililukuwa sawa raia wa Tanzania kuvalishwa t-shirts za Apolo Milton Obote.
 
Last edited by a moderator:
Ukipewa ukaambiwa uvae ni sawa na kulazimishwa uvae?Na kuvua ni the same way?We kweli "maharagwe ya mbeya maji mara moja"

Unasema hawakulazimishwa kwa nguvu, waliambiwa wavae, wakawa wanaziomba, hapo ndo kuvalishwa kivipi?

Ukiambiwa uvue nguo, usipolazimishwa, ukavua, utasema ulivuliwa nguo?
 
Hii ni duplicate, "mind the server"
 

- Chama saafi sana sasa unaongea hoja: HOWEVER tizama mimi ninakuja hapa kutoa maoni yangu bila kujali anybody, niaamini JF kazi yetu inatakiwa kuwa kukosoa, kukosoa kila kiongozi hakuna wa kumbakisha wala kumuogopa, maneno ya agenda na propaganda siyajui, mimi umeona ninaposhambuliwa personal, huwa ninatumia fursa hiyo kujiweka vizuri na public kwa sababu ninajaribu kumuonyesha aliyerusha matusi hana FACTS, wala haelewi anachosema, lakini sio kumjibu matusi na vitisho kama mnavyofanya!

- Lets say mimi nime-specialize na mapungufu ya policies za MWalimu, kwa nini na wewe usi-specialize na mapungufu ya policies za Rais wa sasa, badala yake unaleta maneno ya propaganda hakuna hapa hizo hapa, mimi ninakata ishus tu sina cha nani wala nani, kama kuna anyeijhisi kwamba nina personal problems naye then waombeni utawala wa JF kuwa na limiti ya uwezo wa mtu hapa kufikiria, asiruhusiwe kufikiria mapungufu ya policies za MWalimu!

- I mean mbona sasa hizi kurasa tatu za mwisho tunajadili ishus na kinaeleweka kabisa kinachozungumzwa, kwa nini haumkuanza hivi toka mwanzo, I mean bravo people naona sasa tunaanza kukata ishu kama JF style. Kwamba Mwalimu aliamaliza madeni ndio kwanza leo ninasikia kwa mara ya kwanza.

- Mimi sipo hapa JF kujadili mazuri kihivyo, nipo hapa kukosoa kwanza kama for that ninavunja sheria yoyote ya JF then nitaacha kuchangia, lakini otherwise mwendo ni ule ule mdundo, mnanishngaza sana kwamba ninaanzisha thread ambayo hamuipendi, lakini mnakuja kulalamika na kuigeuza another story huo sio ustaarabu, jamani tuwacheni tukate ishus hapa msitutishe na vitabu uchwara wala hoja uchwara, kama thread ni mbaya iwache au omba mods waifute, lakini wacheni vitisho na mikwara jamani!!

William.
 

Mzee Mwanakijiji,
Nimesoma reference yako uliyonipatia ambayo unaamini inamwahalalishia Nyerere kuivamia Uganda! Labda tu kwanza nitamke wazi jambo ambalo nilishalitamka kwenye post zangu za nyuma. Kwa faida yako napenda nirudie hapa kwamba kwa hali ile ambayo ilitokea 1978 baada ya majeshi ya Amin kuvuka mpaka na kushambulia Kagera/Tanzania; hapo hapakuwa na jinsi. Ilikuwa ni LAZIMA Tanzania nayo iingie vitani. Hapo hapakuwa na jinsi; na hili nimeshaliongelea kabla.

Kimsingi, hoja yangu ni mazingira yaliyopelekea kuwapo na intense conflict kati ya Tanzania/Nyerere na Amin. Vita ilikuwa ni matokeo tu. Hoja yangu ya msingi ni kwanini tulifika hapo hali ilipofikia! Hapo ndipo ninapomlaumu Nyerere. Ninacholaumu ni Nyerere kuruhusu ardhi ya Tanzania kama military training ground dhidi ya Amin. Hapo ndipo tatizo linapoanza. Reference yako inaelezea masuala ambayo yanahalalisha vita…..na kama nilivyosema, ukishambuliwa kama ambavyo Amin alifanya ni lazima nawe uingie vitani. Hilo halina ubishi. Lakini hiyo vita ni matokeo tu ya mambo mbalimbali ambayo yanatokea kabla ya vita rasmi. Labda, tuangalie moja ya nukuu kutoka kwenye reference uliyoitoa:
“ The main externally based position to Amin was Milton Obote’s Uganda People’s Congress based in Dar es salaam with offices in Nairobi, London and Lusaka. Nyerere provided Obote with the facilities necessary to wage a very small scale guerrilla style campaign against Amin’s regime. Somalia, also a “socialist” state joined Tanzania and Obote’s UPC in drawing up a plan in February 1972 whereby a joint force of several thousand troops would invade Uganda from the Kagera Salient and overthrow Idi Amin. The plan was called off because Chinese Premier Chou En-lai was against it, and because Tanzania feared the British and Israelis might intervene directly on Amin’s behalf. In succeedimng years, additional planned strikes into Uganda similar to the one in 1972 were cancelled due to Nyerere’s fear that Britain and Israel would intervene."

Mwandishi, ametoa nukuu hiyo toka kwenye kitabu War in Uganda kilichoandikwa na Tony Avirgan & Martha Honey na kuchapishwa na Tanzania Publishing House, 1983.

Hivyobasi, nukuu hiyo hapo juu inaonesha wazi kile ninachokisema. Kwamba, kumbe Obote na wafuasi wake walikuwa wanaitumia Tanzania kama military training ground. Hilo lisingeweza kuvumiliwa na kiongozi yeyote yule. Na hapo inaonesha wazi kwamba kama si Nyerere kuihofia Uingereza na Israel, kumbe Obote na wafuasi wake wangekuwa wameshaivamia Uganda kwa msaada kutoka kwa Nyerere. Hilo, halikubaliki. Na kama ulivyosema mwenyewe, Nyerere hakumchukulia Obote kama mkimbizi, bali ni kiongozi halali wa Uganda ambae ameondolewa madarakani isivyo halali. Lakini kwa jinsi inavyonesha, kumbe huyo Obote alikuwa hatakiwi na Waganda wenyewe na ndio maana hata baada ya kurudi tena madarakani kwa njia ya sanduku la kura, bado alipinduliwa kwa mara nyingine . Sasa Nyerere alipata wapi uhalali wa kutoa msaada wa kijeshi kwa Obote na wafuasi wake mkwa lengo la kutaka kumtoa Amin madarakani?! Kwanini alitaka kushirikiana na Somalia pamoja na UPC ya Obote kutaka kwenda kumng’oa Amin?! Bahati mzuri, baada ya Mogadishu Accord hapo October 1972, uhusiano kati ya Amin na Somalia ukaimarika. Kwahiyo, kwa kungalia reference yako, uimarikaji huo ulitokea chini ya mwaka mmoja tangu Somalia nayo ipange kuungana na Nyerere kumng’oa Amin!!! Kwenye sherehe za mapinduzi ya Somalia October 21, Amin na watu wake walihudhuria sherehe hizo lakini Nyerere alisusa baada ya kuona Amin angehudhuria wakati hapo kabla alithibitisha kuhudhuria kwenye sherehe hizo. Na studies kadha wa kadha, including reference yako uliyoitoa, zinaonesha kwamba Nyerere alikuwa hataki kabisa kufanya mazungumzo na Amin!!!! WHY?! KWANINI?! Hivyo basi, wakati tunamwangalia Amin anaivamia Tanzania, hatuna budi vile vile kungalia ROOT ya tatizo. Haitoshi tu kusema kwamba Amin alikuwa haaminiki.
 

Wewe kweli maharagwe ya Kibosho nadhani utakuwa umeshiba Kitawa au Sohoo.

Mie nimeuliza ni sawa raia wa Tanzania kuvalishwa t-shirt za Obote hakiamasisha mapambano ya chama chake kutokea Tanzania..badala ya kujibu unaleta vioja.
 

Mkuu vipi wewe...!!! Mtu hawezi kuamini kitu mbacho kipo real....unaamini jambo ambalo lipo kihisia zaidi. Itakuwa ni kichekesho mtu akisema anaamini PPF House ni Jengo wakati linaonekana na kuna evidence zote kwamba PPF house ni jengo. Tunaamini kwamba kuna mungu kwavile hamna scientific eveidence juu ya uwapo wake. Hivyo suala la nani mchokozi sio suala la KUAMINI kwavile ushahidi upo kwamba Nyerere ndie chokochoko kwa hatua yake ya kutoa msaada wa kijeshi kwa Obote kwa lengo la kutaka kwenda kumpindua Amin. Yote hayo uliyoeleza wewe ni matokeo tu ambayo kiini chake ndo hicho nilichokueleza!
 

Hii ililenga kupiga propaganda kwa kutaka Watanzania wamkubali Obote na hivyo kuhalalisha harakati zozote zitazofanywa na Obote ndani ya ardhi ya Tanzania kwa msaada wa Nyerere. Hili ndilo ninalosema halikubaliki hata kidogo...na ndio maana wapo wanaoamini kwamba Nyerere hakufurahi kuona Obote anapinduliwa kutokana na uswahibu wao. Siamini kama aliyepinduliwa angekuwa Kenyatta Nyerere angefanya ambayo alifanya hivyo kudhihirisha wazi si kwamba alichukia mapinduzi ya kijeshi bali alichukia kupinduliwa Obote.
 
Wewe kweli maharagwe ya Kibosho nadhani utakuwa umeshiba Kitawa au Sohoo.

Mie nimeuliza ni sawa raia wa Tanzania kuvalishwa t-shirt za Obote hakiamasisha mapambano ya chama chake kutokea Tanzania..badala ya kujibu unaleta vioja.
Avatar yako na ubongo wako havina tofauti.
Umeulizwa kama watu walilazimishwa, ukasema waliomba wakapewa (ukatoa sababu kuwa hawakuwa na nguo), sasa kuomba ndo kuvalishwa, hopeless kabisa wewe.
 
Kamanda ulisomea UGANDAAAANINI ndugu yangu; ukapata marafiki sana ukafahamu wawazayo wao.
 
your problem is that you don't read and understand things...ungesoma post yangu mpaka mwisho na kuelewa ungejua jibu langu......na pia ungejijibu...yaani ulivyo mediocre..umeacha ku quote jibu langu na ume quote pre-amble ya jibu(kwa makusudi unayoyajua)....jifunze kusoma na kuelewa vitu...it will help you...don't entertain mediocrity....
 
Zakumi, nchi ambayo ufisadi umekithiri to the extent umekuwa kama a way of life, yani kila kitu ni rushwa utajenga vipi human resources capabilities?Please tell me its a joke!
chama, a very good question...

JMUsh1,

Kwani ufisadi umeanza leo? Kilichobadilika ni matumizi ya maneno tu. Lakini matendo ya kifisadi yalikuwepo. Hivyo vita vya Uganda vyenyewe vilijaa ufisadi mtupu.

Viwanda na uzalishaji wa bidhaa nchini Tanzania, haukutosheleza mahitaji ya watanzania. Baada ya vita na kuwatuliza waganda, bidhaa za kuwalisha watanzania zilianza kupelekwa Uganda. Na makamanda wakubwa wa jeshi la Tanzania walitumia nafasi hiyo kujitajirisha.
 
Last edited by a moderator:

Mimi sina chuki yoyote na Nyerere. Topic at hand ni vita vya Uganda na Obote. Huwezi kujenga hoja katika mada hii kwa kwa kutumia ufisadi. Ufisadi and the topic at hand arealmost always mutually exclusive.
 
Saadam Hussein aliingia Kuwait, kisha Marekani wala sio Kuwait walopigana ila Marekani walikuja kumwondoa na kuingia hadi Iraq wala sii ugonvi wao. Je, Marekani walivunja sheria?
 
Saadam Hussein aliingia Kuwait, kisha Marekani wala sio Kuwait walopigana ila Marekani walikuja kumwondoa na kuingia hadi Iraq wala sii ugonvi wao. Je, Marekani walivunja sheria?

Karl Peter alivamia Dola ya wahehe, je alivunja sheria?
 
Hivi ilikuwa inahusu nini sisi raia wa Tanzania kulazimishwa kuvaa T-Shirts za Uganda People's Congress (UPC).

Mkuu Ritz sikuwahi kuvaa fulana ya Obote nadhani maana ya kulazimishwa huijui; kama watu walivaa walitaka wenyewe; labda ungehoji kwanini waligaiwa hili la kulazimishwa umeishiwa na hoja.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Saadam Hussein aliingia Kuwait, kisha Marekani wala sio Kuwait walopigana ila Marekani walikuja kumwondoa na kuingia hadi Iraq wala sii ugonvi wao. Je, Marekani walivunja sheria?

Bila shaka unazungumzia Gulf War (1991) ambayo ilipiganwa na Bush Sr. Marekani (NATO) hawakuvunja sheria kwavile vita ile ilikuwa na baraka za UN. Hata hivyo, NATO walichofanya ni kumuondoa tu Saadam toka Kuwait na hakwenda mbali zaidi ya hapo. Endapo wangefikia hatua ya kumng'oa Saadam madarakani kama ambavyo alifanya Bush Jr basi vita ile ingekuwa na tafsiri tofauti.
 
Je vipi kuhusu Hitler si aliondolewa na majeshi ya NATO au, Hao Taliban wameondolewa na nani?..Nuriega, kina Milosovic na kadhalika. Iweje kweli jambo limetutokea sisi wenyewe na tukachukua jukumu la kulimaliza sisi wenyewe leo hii liwe swala la sheria na kufikiri wakati Idd Amin alivamia nchi yetu na kuua watu kibao huko Bukoba. Kapiga mabomu Mwanza nikiwa nimelala nyumba tatu tu toka pale yalipoangukia au sisi hatukuwa Watanzania kihivyo?..Hivi lini Ubinafsi wenu utakwisha na mkaweza kuyatazama maswlaa haya kwa mabana zaidi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…