..mnaodai ile ilikuwa vita ya kidini mmepotoka.
..zipo nchi za Kiislamu ambazo zilikuwa zinaisaidia Tanzania.
..msikiti wa Kampala umejengwa kwa msaada wa Gaddafi, tena umefunguliwa miaka siyo mingi iliyopita wakati wa utawala wa Museveni.
..hakuna nchi za Magharibi zilizotusaidia ktk vita ile. kama tungesaidiwa basi tusingeporomoka kiuchumi na kufilisika kiasi kile.
..kosa kubwa tulilofanya ni kupigana vita kwa muda mrefu kwa kutumia fedha zetu wenyewe.
..miaka ya 1970, Tanzania[Nyerere] ilikuwa mwiba kwa interest za nchi za magharibi kuliko Uganda/Amini. kumbukeni kwamba mwaka 1975 Mreno alifukuzwa Msumbiji na Frelimo ambao walipata msaada mkubwa toka Tanzania. baada ya hapo tuliendelea kuwasumbua Waingereza tukipinga utawala wa walowezi wa Zimbabwe.
..kwa msingi wa hoja hiyo hapo juu utaona kwamba nchi za magharibi zilikuwa zinaomba dua Amini atupige ktk vita ile.
..siyo kweli kwamba Mwalimu alikuwa anataka Obote arudi madarakani. suala la nani atawale Uganda baada ya Amini liliamuliwa na Waganda wenyewe. hata habari za kuanguka kwa utawala wa Amini, baada ya Kampala kutekwa, zilitangazwa na Oyite O'jok. habari hizo zingeweza kabisa kutangazwa na Lt.Col.Ben Msuya aliyekuwa kamanda wa kwanza wa JWTZ kuingia Kampala, au hata na Maj.Gen.Musuguri aliyekuwa divisional commander.
..baada ya Amini kukimbia, Waganda walikusanyika Moshi kuchagua serikali ya mpito, kuandika katiba ya muda, na kupanga ni baada ya muda gani uchaguzi ungefanyika. Nyerere hakuwa na leverage yoyote ile katika maamuzi ya vikao vya Waganda vilivyokuwa vikifanyika Moshi.
..Obote aliweza kurudi madarakani kwasababu alikuwa na watu wake[Paulo Muwanga,..] ambao aliwatuma kwenda kwenye vikao vilivyofanyika Moshi. chama cha Obote, UPC, kiliweza kupenyeza makada wake ndani ya serikali ya mpito ya Uganda, bila ya Obote kushiriki ktk vikao vya Moshi. vilevile ni yeye pekee aliyekuwa na network ya kisiasa ndani ya Uganda. hawa wakina Museveni etc walikuwa ma-activists na wapiganaji wa msituni, not politicians.
NB:
..Amini alikuwa na haki ya kutushambulia mwaka 1972 au 73 ambapo Tanzania tulikuwa tunawapa silaha waasi wa Uganda.
..baada ya hapo Tanzania na Uganda zilisaini mkataba wa amani wa Mogadishu, na Tanzania ilikuwa inauheshimu mkataba huo.
..Amini hakuwa na justification yoyote ile ya kutuvamia, kuua raia wa Tanzania, kuharibu mali, na kudai kwamba ardhi ya Tanzania ni sehemu ya Uganda.