Vita vya Kagera: Nini chanzo? Kulikuwa na ulazima?

Vita vya Kagera: Nini chanzo? Kulikuwa na ulazima?

Kuna watu hata hawajui kuwa Idi Amin wakati Uganda inapata uhuru alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya waganda 14 ambayo Obote aliyamezea kitu kilichokuwa kosa kubwa sana kwa Obote baadaye. Sasa watu wanaotaka kumtukuza Idi Amin kwa sababu ya dini yake basi wafanye hivyo tu lakini wasipoteshe historia. Hivi Abdallah Twalipo (aliyeongoza majeshi yetu) leo hii sijui angetushangaa vipi kwamba ilikuwa ni vita ya kidini.

Kama Nanren ulivyosema, kama mtu unamchukua mtu basi umchukie japo kwa sababu za ukweli. Lakini unamchukia kiasi kwamba unapotosha ukweli sidhani kama ni vyema.
 
  • Thanks
Reactions: ffn
Ni kweli, Mzee Mwanakijiji.
Watu wengi wanakosa objectivity matokeo yake ndio haya ya kupindisha history.
 
Swali la kujiuliza ni je
(1) kulikuwa na motive yoyote ya kumpiga Amini kabla hajavamia nchi yetu?
(2)Je kulikuwa na Covert actions zozote dhidi ya Amini zilizofanywa na Serikali yetu kabla ya Amini kuvamia nchi yetu?
(3)Ni nani alivunja daraja la mto Kagera, Amini au Majeshi ya Tanzania?
(4)Ni matukio gani yalitake place kuanzia mwaka 1971 Iddi Amini alipompindua Obote hadi mwaka 1978 vita vilipolipuka, je mapigano ya mwaka 1972 ambapo vikosi vya waasi vilishambulia Uganda kutokea Tanzania, ni nini role ya Serikali ya Tanzania dhidi ya Uvamizi huo?

haya mambo nadhani yanahitaji uchunguzi huru
 
Hakuna cha uchunguzi wala nini; historia si ipo. Jaribu kuyajibu kwa kuonesha kuwa daraja la Kagera lilivunjwa na Tanzania, au utuoneshe kuwa Idi Amin hakusherehekea majeshi yake kuvamia Tanzania na kurudi kwa ushindi; au mtuoneshe kuwa utawala wa Idi Amin haukuwa na mauaji ya wananchi wake.
 
Sijui kama umepata nafasi ya kusoma hotuba ile ya kutangaza vita. Watu wengi wanakumbuka maneno ya "nia tunayo" lakini hawakumbuki sababu zilizotolewa.
Ndugu, na huo ndio ulikuwa msingi wa mada hii, kabla haujachukua sura nyingine, nikasema hivi:
"... hoja ya vita anayoijenga ni nzito zaidi ya makaririsho ya "Sababu Tunayo, Uwezo Tunao."

Ila sijabahatika kusoma au kusikia hotuba nzima, na kama mwanafunzi wa historia ya marais wa Tanzania, sitaki kujinyima tunu ya historia ya hoja ya vita ya J. Kambarage Nyerere. Kuna mtu anayo tafadhali?

Basi, kama unayo hiyo hotuba, naiomba tafadhali.
 
Waberoya said:
Got u, so tunaweza kusema Nyerere alikuwwa mkorofi kwanza na Idd Amin alikuwa mkorofi baadae!

what Nyerere did? alichukua hatua gani kuzuia hili swala ? maana OAU walikuwa against naye! any info please. I mean, je bunge lilihusika kusema JWTZ waende Kagera?

Waberoya,

..naweza kusema kwamba kitendo cha Mwalimu kumkaribisha Obote, na kujaribu kumrudisha madarakani 72/73 kiliifanya Tanzania na Nyerere kuwa target ya vituko vya Idi Amini.

..kuna tukio ambalo halijawahi kutangazwa ambapo waasi wa Uganda "waliteka" ndege ya East African Airways ndani ya Tanzania na kujaribu kwenda kutua Entebe. inasemekana jaribio hilo lilifeli, baada ndege kupata matatizo na kushindwa kuruka toka KIA. waasi wengine waliokuwa wametangulia nchi kavu kuingia Uganda waligundulika na majeshi ya Amini na wengi wao waliuwawa.

..nadhani baada ya tukio hilo ndipo kukafanyika mazungumzo ya amani yaliyosimamiwa na SOMALIA, na kupelekea kusainiwa kwa mkataba wa amani uliojulikana kama MOGADISHU ACCORD.

..baada ya mkataba wa Mogadishu, Tanzania iliacha kuwasaidia kijeshi wakimbizi wa Uganda waliokuwa nchini kwetu.

..so fast forward to 1978, unaweza ukajiuliza kwanini Amini alikiuka makubaliano ya amani ya Mogadishu na kuvamia ardhi ya Tanzania, kuharibu mali, kuua wananchi wasiokuwa na hatia, na kuzusha madai kwamba Kagera ni eneo la Uganda?

..pia unaweza ukang'ang'ania matukio ya 1972/73, na kujiuliza busara za Mwalimu ktk kumpa hifadhi Obote na kuwasaidia kijeshi waasi wa Uganda.

NB:

..inawezekana Bunge la Tanzania, au CCM [miaka ile chama kilikuwa kimeshika hatamu] walibariki vita vya kumngoa Amini. sina uhakika na hili. lakini kuna maeneo mengine ambayo JWTZ walipelekwa na si bunge wala chama vilishirikishwa. Raisi wetu ana madaraka makubwa kupindukia.

..
 
Kuna watu hata hawajui kuwa Idi Amin wakati Uganda inapata uhuru alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya waganda 14 ambayo Obote aliyamezea kitu kilichokuwa kosa kubwa sana kwa Obote baadaye. Sasa watu wanaotaka kumtukuza Idi Amin kwa sababu ya dini yake basi wafanye hivyo tu lakini wasipoteshe historia. Hivi Abdallah Twalipo (aliyeongoza majeshi yetu) leo hii sijui angetushangaa vipi kwamba ilikuwa ni vita ya kidini.

Kama Nanren ulivyosema, kama mtu unamchukua mtu basi umchukie japo kwa sababu za ukweli. Lakini unamchukia kiasi kwamba unapotosha ukweli sidhani kama ni vyema.

Na siyo Abdallah Twalipo tu. Wangemuulizia Brigadia General Himid Hemed ambaye alikuwa Bukoba nini kiliendelea Amini alipovamia Bukoba yeye akiwa na wanajeshi wachache sana kuweza kuwamudu hao waganda.
Dini ya kweli inasimamia ukweli no matter what! Sasa hali ya sasa hivi ukweli unakuja baada ya dini ya mtu kwanza. Kama mtu ni mwizi au muuaji au hawajabiki hatakiwi kuulizwa ati kwasababu ni dini yako!
Huo ndio umaskini wa mawazo ambao tukiuendekeza tuandae majozi ya kujililia wenyewe. Haki na ukweli hauwezi kusimama pamoja na uongo hata siku moja.
 
Nitakuja kutua kumbukumbu zangu hapa kuhusu swala hili nikipata muda mwafaka. Kuna historia ndefu kidogo inayounganisha vita hii kuanzia madai ya uhuru wa Rhodesia ambayo leo ni Zimbabwe, makubaliano ya Mulungushi Club, Mkutano wa Commonwealth wa 1971 huko Singapore ambapo Obote alipinduliwa na Amini akiwa njiani, msimamo wa serikali ya Uingereza kuhusiana na mapinduzi yale na uteuzi wa Bob Astles, Vita ya Kagera mwaka huo huo wa 1971 iliyosababisha mkuu wa mkoa wa Kagera awe Mwanajeshi (Luteni Kanali Abdallah Twalipo), Mabomu ya Amini pale Mwanza, makubaliano ya Mogadishu kuhusu amani mpakani mwa Tanzania na Kagera, kuanguka kwa EAC mwaka 1977, na vita kamili hiyo ya Kagera ya mwaka 1978 iliyomwondoa madarakani Amin na kuharibu uchumi wa Tanzania.
 
Nitakuja kutuo kumbukumbu yangu kuhusu swala hili nikipata muda mwafaka. Kuna historia ndefu kidogo inayounganisha vita hii kuanzaia madai ya uhuru wa Rhodesia ambayo leo ni Zimbabwe, makubaliano ya Mulungushi Club, Mkutano wa Commonwealth wa 1971 huko Singapore amabpo Obote alipinduliwa na Amini akiwa njiani, msimamo wa serikali ya Uingereza kuhusiana na mapinduzi yale na uteuzi wa Bob Astles, Vita ya Kagera mwaka huo huo wa 1971 iliyosababisha mkuu wa mkoa wa Kagera awe Mwanajeshi (Luteni Kanali Abdallah Twalipo), Mabomu ya Amini pale Mwanza, Makubaliano ya Mogadishu kuhusus amani mpakani mwa Tanzania na Kagera, Kuanguka kwa EAC mwaka 1977, na vita kamili hiyo ya Kagera ya mwaka 1978.

Hope that day will come soon ili tuweze kujua kwa undani mambo yanayohusu historia ya nchi yetu,
 
Ndugu, na huo ndio ulikuwa msingi wa mada hii, kabla haujachukua sura nyingine, nikasema hivi:

Basi, kama unayo hiyo hotuba, naiomba tafadhali.

hivi hata mnaangalia? Mzee Mbegu kakuweka video za youtube wakati Nyerere anatoa sehemu ya hotuba hiyo... ungesikiliza kidogo ingekusaidia au kuona ile documentary. Au unataka nikusimulie kilichomo kwenye video hiyo?
 
Ile ni vita ya kidini nilivyosikia mimi kwa wakongwe!mambo yale yalikuwa ya kivatcan against muslim ndo mambo mengine tukadanganywa oooh anakula nyama za watu yote ile ni kujastify tu ili wamvamie. Ila angekuwepo mpaka sasa hivi uganda ingekuwa nchi ya kiislam. baba wa taifa alikuwa mroman karibu sana na papa!
Na ule urafiki na Gadaffi uliwatishia amani sana.
haya na mimi niliyasikia tu
 
Mwanakijiji, vita vya Kagera vimetokea wengine wetu tukiwa tu ni watu wazima lakini kuna mambo yanaongelewa humu hata sijui wanaoyasema wana lengo gani. Baada ya Idi Amin kuvamia ardhi yetu hatukukurupuka tu tukaanza kupambana naye. Kuna kipindi Mwalimu aliyaomba siyo tu mataifa ya nje, umoja wa mataifa hadi umoja wa nchi za kiafrika kulaani uvamizi huo lakini ni kama vile kuna mataifa yalifurahia kitendo cha Amin. Tukumbuke kuwa wakati huo Mwalimu alikuwa kama adui wa mataifa ya magharibi kwani alikuwa kikwazo sana kwa maslahi yao sehemu hii ya Afrika.

Pia wanaojaribu kuingiza Udini ni lazima wafahamu kuwa katika kipindi hicho Mwalimu alikuwa mstari wa mbele kuwatetea Wapalestina katika harakati zao dhidi ya Israel. Ni sababu hiyo iliyopelekea Tanzania kuvunja mahusiano ya kibalozi na Israel na Mwalimu alikuwa rafiki mkubwa wa Gadafi wa Libya. Tendo la Gadafi na Wapalestina kutuma majeshi kuja kumsaidia Idi Amin dhidi ya Tanzania lilimshtua sana na kumhuzunisha Mwalimu.

Mwalimu hakupenda mapinduzi ya kijeshi na ndiyo sababu kubwa sana ya kukataa kumtambua Idi Amin toka mwanzo kabisa na hili hakulificha hata siku moja. Nawashauri wenye nia ya kweli ya kutaka kujua historia ya vita vya Kagera waachane na malimbukeni wanaojitokeza kujaribu kupindisha historia kwa sababu za wivu na ujinga. Bahati mbaya kumejitokeza watu ambao hukesha wakipanga kumkebehi Hayati Mwalimu asiyeweza kujitetea.

Ilichukuwa kipindi cha miezi kadhaa kuwahamasisha Watanzania kuwa tayari kupambana na adui aliyevamia ardhi yetu - kumtoa nyoka pangoni na tulifanikiwa.

Bahati mbaya sana ndugu yangu kila anaposemwa Nyerere unapata nguvu ya ziada ya kusema na kupinga kwa kutumia maneno yoyote yale!

Nitakuwa si mkweli kukubali na kusema kila kilichoandikwa kwenye historia zetu ni sahihi kabisa na watu hawana uwezo wala hawatakiwi kujiuliza na katika kujiuliza huku ndioko kunakuja maneno ya kejeli kana kwamba historia hii wewe niye uliyeandika!

Ni wangapi leo hii TZ wanajua kuwa chokochoko ya vita hii sababu hasa ni Nyerere mwenyewe? kwa nini mnasema mataifa ya magaharibi yalikwua upande wa Amin, na hamsemi hata OAU ilikuwa gainsta Nyerere? na Kwa nini Nyerere baada ya kujua hapendwi aliendela na harakati za ukombozi wa barala Afrika? je ni kwa namna gani uhusiano wa Tz na mataifa ya magharibi ulisuasua?

Hili swala Mag3 hata kama utalizimisha humu kwamaneno yoyote yale still people will question and they deserve to be answered, kusema ulikuwa mtu mzima ni wakati mzuri wa wewe kufunguka na kuona ukweli! SI dhambi kuuliza!!! kama kuna watu wanachuki na Nyerere si dhambi wakazionyesha! ebo! kama yeye alionyesha hampendi Idd Amin, wengine nao wanasababu zao za kunyesha kutompenda Nyerere?? hii si dhambi Mag3!! kwako wewe Nyerere ni mtume, nabii, saint to be, hana doa, personally namchukulia Nyerere kama kiongozi aliyefanikiwa sehemu fulani na aliyeshindwa sehemu fulani!! this is reality! wangapi wanamsifia Nyerere usiku na mchana, akinyooshewa kidole amekosea hapa Mag3 uko tayari wakati wote kumtetea!!

Kazi na uzuri wa Nyerere utasimama tu that is a fact, na tukitaka kuangalia mbele na udhaifu wakke. failure zake zitasemwa tu! sio kuwa HAJITETEI hata kama leo hii angekuwa mzima asingeweza kujitetea! kwani angekuwa Jamii Forums?? mtu yuko kwenye noti kila siku unataka asisemwe kweli??

Umejibu vizuri sana hoja ya udini, which for me I knew very well is not true, lakini ndio story za mitaani Mag3!! people say that, so many rumours conerning this war! we are luck that ulikuwa mtu mzima, then wajibu kwa facts! unapowazima eti siku hizi kimeibuka KIZAZI au watu wanaompinga Nyerere!!!, unaweza kuwazimisha?? maana wengine hawako JF eti!!
 
Labda tunasahau, Idi Amin aliweza vipi kuwa rais mara ya kwanza, tusije kuwa tunaruka ssehemu ya historia. Maana watu wanazungumzia Nyerere alitaka kumrudisha Obote lakini hawatuambii kwa misingi gani au Obote alikuwa na haki gani ya kurudishwa madarakani.

Sijui kama umepata nafasi ya kusoma hotuba ile ya kutangaza vita. Watu wengi wanakumbuka maneno ya "nia tunayo" lakini hawakumbuki sababu zilizotolewa.

Asante kuwa unakubali lengo ni Obote, whatever Amin did that time prime source was Obote was in our land, this made Amin unrest! the question here is how far Nyerere went to prevent this war, is there any written report/hostory. documents that Nyerere did this and that to prevent this war?? will appreciate for that!

Waberoya,

..naweza kusema kwamba kitendo cha Mwalimu kumkaribisha Obote, na kujaribu kumrudisha madarakani 72/73 kiliifanya Tanzania na Nyerere kuwa target ya vituko vya Idi Amini.

..NB:

..inawezekana Bunge la Tanzania, au CCM [miaka ile chama kilikuwa kimeshika hatamu] walibariki vita vya kumngoa Amini. sina uhakika na hili. lakini kuna maeneo mengine ambayo JWTZ walipelekwa na si bunge wala chama vilishirikishwa. Raisi wetu ana madaraka makubwa kupindukia.

..

Joka kuu ala kumbe kifupi cha jina lako ni JK!!

Thanks for this piece of information, we are looking back so that we canb predict and evaluate how are we doing now. Briefly you have decribed that Nyerere was confident and trouble shooter this is a quality of any good leader.

However, in your information it seems you have relied on 'mwalimu did this' or mwalimu did that...this is where my problems arises

Je ni nani aliamua Obote akaribishwe ilikuwa Nyerere kama Nyererere au Nyerere kama rais wa nchi! I mean decision za maamuzi mengi inaonyesha ilikuwa personal zaidi na hatuonyeshwi kwenye historia ( au mimi sijaona) kuwa kulikuwa na organ ya kufanya maamuzi!!!
Mathalan vita ya ghuba, iraq ambavyo USA aljiingiza, inaonekana kuna organ zinafanya maamuzi au kupitisha maamuzi ya rais! I bet you, kuna wengi leo hii hawakufurahishwa na yale maamuzi ya vita!!! they were blinded by good speech 'nia tunayo' baada ya vita kila mtu akaanza kulia na hata leo hii tuna suffer!! my question is HAKUKUWA NA ARGUMENT ZOZOTE ZA twende au tusiende??

Leo hii Kikwete anafanya very same thing, mara kwenda kuokoa comoro sijui wapi, wanajiamulia amulia tu, zikifika athari tunalia sote!!

je japo Obote alikuwa nchini, intelijinsia hazikuonyesha kuwa anything like that might happen?? mpakani hakukuwa na ukilinzi?

Nani alisimamia usuluhishi wa Mogadishu? je huyu mpatanishi hakuwa consulted baada ya vita...I BELIEVE OAU WANGEONA KABISA IDD AMIN AMEVUNJA MKATABA WA AMANI, BASI OAU INGEKUWA UPANDE WA NYERERE!! what happened there..... AU OAU ilichakachuliwa?? kama OAU ilichakachuliwa Nyerere alichukua hatua gani baada ya vita?? kuendela kuwa mwanachama?? what for??? kuna mwenye info?? sijapata jibu la kuridhisha nafsi yangu, japo maswali haya yanazua hisia labda Nyerere hapendwi la! lets discuss FACTS!!!
 
Ile ni vita ya kidini nilivyosikia mimi kwa wakongwe!mambo yale yalikuwa ya kivatcan against muslim ndo mambo mengine tukadanganywa oooh anakula nyama za watu yote ile ni kujastify tu ili wamvamie. Ila angekuwepo mpaka sasa hivi uganda ingekuwa nchi ya kiislam. baba wa taifa alikuwa mroman karibu sana na papa!
Na ule urafiki na Gadaffi uliwatishia amani sana.
haya na mimi niliyasikia tu

nawachukia watu kama nyie msiojua historia yetu kagera ila mnataka kuleta upuuzi hapa. Hata wazazi wetu wametuonesha mpaka sehemu alipokuwa anawamwaga watu,vikongwe na walemavu ktk mto kagera kwa ukatili wake Amini. Mi sikuipenda vita ile kwa kuwa iliirudisha Kagera Tanzania ila ikawaache wananchi wale wafe maskini. Ni bora ingetuacha tukaelea Uganda kuliko tanzania ya mkoloni mweusi ila siwezi kuileta vita ile katika udini,hapana. Msiwe wavivu wa kufikiri,hadi leo wazazi wetu tunao na wanatueleza kilichojiri,hamna udini. Hata ukiangalia pale Muhutwe na Kemondo ambako Obote alijificha palikuwa na waislam wengi waliomsaidia na baadae amin kapinduliwa!udini haukuwepo na usiingizwe kamwe.
 
Asante kuwa unakubali lengo ni Obote, whatever Amin did that time prime source was Obote was in our land, this made Amin unrest! the question here is how far Nyerere went to prevent this war, is there any written report/hostory. documents that Nyerere did this and that to prevent this war?? will appreciate for that!

Kwanini Obote alikuwa Tanzania?
Kabla ya kuja Tanzania Obote alikuwa na cheo gani kabla huko Uganda na alikipotezaje hicho cheo?
 
Kilimasera ukiona mdogo wakoa anampiga ngumi mwezio na mwenzi akarudishia mkorofi ni yule aliyeanza kurusha ngumi??

Tafuta Literatures, uliza waganda, nenda kulia nenda kushoto......

Uganda mpaka leo wanamkumbuka Amin! ambaye wewe unamwona dictator

Amin aliua makumi
Obote kaua maelfu
Museven kaua makumi elfu.......

Kwa kufupi mkuu, Nyerere alikuwa na mtu ambaye anatakwa sana na Amin..Mr.Obote,

kwa kifupi ulikuwa mpango wa Nyerere kumuweka Obote madarakani!!! yale ya kagera n.k ni hasira za Amin, ukweli NYERERE NDIYE ALIKUWA MKOROFI!!!!!

Unajua Mutukula sio mbali sana kutoka Dar, tena wahenga wa mashambulizi ya Iddi Amin bado wapo, kwa nini usichukue basi mara moja ukaenda ukawaulize kwa nini walishiriki na kuitaka serikali ya Nyerere impige Amin! Hivi unataka kusema nini? Kweli wakati dunia nzima ilimwona Amin na Bokasa kama wauaji wakubwa wewe ni nani hata uone tofauti. Usituudhi ambao tulikuwepo, tulishudia vifo na mateso yaliyosababishwa na Amin. Usiombe yakufike hayo. Wewe unatakiwa upelekwe mbele ya mtutu uambiwe 'advance' yaani umkimbilie adui ambaye amejiandaa kukutungua! Naweza kufikiria kinachoweza kukutokea. Vita sio utani, na ukome kabisa kufikiria Nyerere alikuwa mchokozi. 1972 Amin alivamia Tanzania, tukavumilia, akajaribu tena 1974-75 na chokochoko nyingi, na 78 akiwa na msaada mkubwa wa Jamhuri ya Libya wakiwa na agenda ya ajabu wakavamia, tuliwakunguta. Waingereza na wamarekani walifikiri Nyerere angeshindwa lakini tuliwaweza. Ndio maana waganda wanatusifu sisis kama wakombozi, isipokuwa wale wa kaskazini kwa Iddi
 
Asante kuwa unakubali lengo ni Obote, whatever Amin did that time prime source was Obote was in our land, this made Amin unrest! the question here is how far Nyerere went to prevent this war, is there any written report/hostory. documents that Nyerere did this and that to prevent this war?? will appreciate for that!

Joka kuu ala kumbe kifupi cha jina lako ni JK!!

Thanks for this piece of information, we are looking back so that we canb predict and evaluate how are we doing now. Briefly you have decribed that Nyerere was confident and trouble shooter this is a quality of any good leader.

However, in your information it seems you have relied on 'mwalimu did this' or mwalimu did that...this is where my problems arises

Je ni nani aliamua Obote akaribishwe ilikuwa Nyerere kama Nyererere au Nyerere kama rais wa nchi! I mean decision za maamuzi mengi inaonyesha ilikuwa personal zaidi na hatuonyeshwi kwenye historia ( au mimi sijaona) kuwa kulikuwa na organ ya kufanya maamuzi!!!
Mathalan vita ya ghuba, iraq ambavyo USA aljiingiza, inaonekana kuna organ zinafanya maamuzi au kupitisha maamuzi ya rais! I bet you, kuna wengi leo hii hawakufurahishwa na yale maamuzi ya vita!!! they were blinded by good speech 'nia tunayo' baada ya vita kila mtu akaanza kulia na hata leo hii tuna suffer!! my question is HAKUKUWA NA ARGUMENT ZOZOTE ZA twende au tusiende??

Leo hii Kikwete anafanya very same thing, mara kwenda kuokoa comoro sijui wapi, wanajiamulia amulia tu, zikifika athari tunalia sote!!

je japo Obote alikuwa nchini, intelijinsia hazikuonyesha kuwa anything like that might happen?? mpakani hakukuwa na ukilinzi?

Nani alisimamia usuluhishi wa Mogadishu? je huyu mpatanishi hakuwa consulted baada ya vita...I BELIEVE OAU WANGEONA KABISA IDD AMIN AMEVUNJA MKATABA WA AMANI, BASI OAU INGEKUWA UPANDE WA NYERERE!! what happened there..... AU OAU ilichakachuliwa?? kama OAU ilichakachuliwa Nyerere alichukua hatua gani baada ya vita?? kuendela kuwa mwanachama?? what for??? kuna mwenye info?? sijapata jibu la kuridhisha nafsi yangu, japo maswali haya yanazua hisia labda Nyerere hapendwi la! lets discuss FACTS!!!
Sikutaka kusema kitu kwenye mjadala huu kwa sababu nilishasema mengi hapo awali huu mjadala ulipojitokeza mara ya kwanza.
Kwa Nyerere kumpa hifadhi Obote was a given. Kwenye mkutano wa Commonwealth wa Singapore lengo la Heath lilikuwa ni kum-isolate Nyerere aonekane kama ndiye yuko out of step kwa kuishinikiza Uingereza isitishe kuiuzia silaha Afrika kusini. Obote alisimama kidete na Nyerere katika suala hili ikafikia wakati Heath akamtishia kuwa wengine hapa hawatarudi nyumbani kwao. Kumbe Uingereza ilishajua mipango iliyosukwa na intelligence yao na Israel kumpindua Obote. Ungekuwa wewe Nyerere katika hali kama hii kweli ungemsaliti rafiki yako? Obote kwanza alikimbilia Kenya, Waingereza wakamwambia Kenyatta asimpe hifadhi. Ungekuwa wewe Nyerere ungefanya nini? Waberoya, kuna wakati nashindwa kukuelewa kabisa!
 
Kama ungesoma mwanzo nimesema na mimi nilisikia hilo, na aliyekuwa anasimulia nae ni mzee na nimewasilisha hapa kama comment tu na sio fact!
historia inajulikana kama tulivyosoma, hata watoto wetu nao wakija sikia mambo ya dowans watasema mengi, wengine wataamini serikali ya sasa kwamba ilikuwa lazima dowans ilipwe na wengine watakuwa against. Mimi nasimamia kwamba ukweli wanajua waliokuwa madarakani wakati huo. inaweza kuwa mipaka, inaweza kuwa udini au lolote. usicheze na intelijensia ikiamua vitu vyake.
nawachukia watu kama nyie msiojua historia yetu kagera ila mnataka kuleta upuuzi hapa. Hata wazazi wetu wametuonesha mpaka sehemu alipokuwa anawamwaga watu,vikongwe na walemavu ktk mto kagera kwa ukatili wake Amini. Mi sikuipenda vita ile kwa kuwa iliirudisha Kagera Tanzania ila ikawaache wananchi wale wafe maskini. Ni bora ingetuacha tukaelea Uganda kuliko tanzania ya mkoloni mweusi ila siwezi kuileta vita ile katika udini,hapana. Msiwe wavivu wa kufikiri,hadi leo wazazi wetu tunao na wanatueleza kilichojiri,hamna udini. Hata ukiangalia pale Muhutwe na Kemondo ambako Obote alijificha palikuwa na waislam wengi waliomsaidia na baadae amin kapinduliwa!udini haukuwepo na usiingizwe kamwe.
 
I'm so done.. hawa vijana wetu kama wanataka kujifunza kweli historia ya nchi yao wavue kwanza haya madudu wanayopandikizwa siku hizi kwanza.. vinginevyo ni vigumu kweli hata kukubali kuwa sasa "wanajua".. maana kukubali kujua wakati ulifikiri unajua ni ngumu kweli.
 
Kama ungesoma mwanzo nimesema na mimi nilisikia hilo, na aliyekuwa anasimulia nae ni mzee na nimewasilisha hapa kama comment tu na sio fact!
historia inajulikana kama tulivyosoma, hata watoto wetu nao wakija sikia mambo ya dowans watasema mengi, wengine wataamini serikali ya sasa kwamba ilikuwa lazima dowans ilipwe na wengine watakuwa against. Mimi nasimamia kwamba ukweli wanajua waliokuwa madarakani wakati huo. inaweza kuwa mipaka, inaweza kuwa udini au lolote. usicheze na intelijensia ikiamua vitu vyake.

narudia kusema kweli ata mi sikuipenda vita ya mkoa wangu lakini wazee wangu na shangazi zangu ambao hata walikuwa wanajeshi wanathibitisha kuwa Idi alikuwa jitu mbaya sana. Kwa kuwatelekeza mtoni wasio na hatia ilinikwaza sana. Nichoomba ni kuwa ile vita isingehusishwa na udini. Pia idi ndo aliyetungua daraja la kagera na ghafla wanajeshi wa Tz kwa kutumia vifaru na vyuma walijenga jipya ndani ya masaa na kuvuka mpaka,apa idi ndo aliposhtuka na kukimbilia kijijini Arua. Mambo yako wazi ila wachangiaji wanaedit history ili iendane na 'market' demand ya sasa ya wasikilizaji.
 
Back
Top Bottom