..at least Kamuzu Banda madai yake kuhusu Ziwa Nyasa yalikuwa yanabebwa na Heligoland treaty.
..sasa madai ya Iddi Amini kuwa eneo la Kagera ni mali ya Uganda yanahalalishwa na kitu gani?
..hivi ndugu yangu, hudhani kwamba Amini alifanya makosa kutuvamia, kuuwa ndugu zetu, kuharibu mali, na kulikalia kwa mabavu eneo la Kagera?
..wewe kwa mtizamo wako unafikiri Mwalimu Nyerere na wa-Tanzania walipaswa kufanya nini katika mazingira yale?
cc
Jasusi,
chama
JokaKuu,
Tunapozungumzia suala la mgogoro wa Uganda na Tanzania enzi za Mwalimu na Amin wengi huwa tunaangalia reactions za Iddi Amin lakini hatutaki kuangalia chanzo kilichopelekea ufedhuli wa Amin. Katika hili mimi siumi meno... na sisi wenyewe, chini ya uongozi wa Mwalimu tulichangia sana uhasama kati yetu na Amin.
Kaa unakumbuka, angalia kwa kusoma historia zisizopotoshwa, Rais Obotte aliwahi kufanya jaribio la kumfukuza kazi Idd Amin ambae alikuwa Mkuu wake wa Majeshi. Jaribio la Obotte likashindwa. Kwa bahati mbaya sana, wiki chache baada ya jaribio hilo, Obotte akawa amepata safari kwenda Singapore, kama sikosei kuhudhuria mkutano wa Jumuiya Madola. Iddi Amin akatumia nafasi hiyo kuingia Ikulu na kumpiga marufuku Obotte kurudi Uganda.
Kuona hivyo, Obotte hakurudi Uganda na badala yake akaenda Lusaka. Alikaa huko kwa muda, akaja Dar es salaam na kupewa hifadhi na Mwalimu. Mwalimu hakufanya kosa lolote kumpa hifadhi Obotte.
Wafuasi wa Obotte walipoona Rais wao yupo Tanzania, ambao hata hivyo walikuwa wanapata joto ya jiwe la Amin, nao wakaamua kwa wingi sana kuvuka mpaka na kuingia Tanzania. Hadi hapo hakuna kosa lolote kwa kuwakaribisha wafuasi hao wa Obotte.
Kosa ambalo alifanya Mwalimu ni kuwageuza Wakimbizi wale wa Uganda kuwa kikosi cha Uasi. Hawa wakapewa kambi kule Handeni ambako wakawa wanapatiwa mafunzo ya kijeshi kwa lengo moja tu; wakiiva, warudi Uganda kumpindua Iddi Amin. Tusisahau, Obotte na Mwalimu walikuwa maswahibu wakubwa sana na ndio maana pakawa na hii covert operation iliyokuwa na lengo la kumrejesha Obotte madarakani. Na kwa hakika hili likafanyika... kama kumbukumbu zangu zipo sawa, kikosi cha kwanza cha waasi hawa kikavuka mpaka 1971 kwenda Uganda na kufanya jaribio la mapinduzi ambalo hata hivyo lilishindwa... wngi wao walifyekwa na Amin na waliosalia wakatoka nduki kurudi tena Tanzania.
Hivyo basi, kimsingi hicho ndicho chanzo cha ugomvi wetu na Idd Amin... sasa unapomchokoza Mwendawazimu kama Idd Amin, hatachagua pa kuku-hit! Aidha, tujikumbushe tu kwamba, wafuasi hawa wa Obotte walifanya majaribio mengine mawili na yote yalishindwa.
Sasa Mkuu wangu nisaidie. Ni kiongozi gani Afrika hii, na in fact duniani ambae anaweza kukaa kimya hata baada ya kuona Rais mwenzake wa nchi jirani anafadhili military covert operation dhidi ya utawala wake?
Sasa basi, tukija kwenye concern yako ya mwisho kwamba Tanzania ingefanya nini ni kwamba tayari tulishalikoroga hivyo tulipaswa kulinywa. Kwavile tuliingia na gia ndogo lakini Iddi Amin akaingia na gia kubwa, hatukuwa na budi kukabiliana na hali hiyo. Hivyo basi, kwavile Amin aliamua kujibu mapigo kwa kuivamia Tanzania, hapo nasi hatukuwa na namna isipokuwa ku-fight back bila kujali kwamba ni wenyewe ndio tulianza chokochoko.