NasDas
Kumwita Mwl. Nyerere ni Principle architect wa vita vya Kager si sahihi lakini kwa vile una uhuru wa kutoa mawazo ni haki yako; tumeshakueleza haionyeshi mahala popote pale kuwa Tanzania ilivunja makubaliano ya amani tuliyosaini Somalia; utafiti unakueleza wazi kuwa baada ya Idd Amin kukabiliwa na uasi wa wanajeshi wake aliamua kuivamia Tanzania ili wanajeshi wake wapate shughuli ya kufanya; hata yeye hakuwa nasababu hata moja ya kuivamia Tanzania; kwasababu uvamizi wake hauonyeshi kwamba alikuwa anavitafuta vikosi vya waasi wa Uganda vilivyopo Tanzania; nashindwa kuelewa kwanini umechagua kukubali baadhi ya vipengele na kufumbia macho vingine; upinzani dhidi ya Amin ulikuwa mkubwa ndani ya Uganda na ndio sababu alikuwa akiiuwa raia zake hadharani; kama Amin asiingeivamia Tanzania ni vita ile isingetokea, Nyerere hakuwa na sababu ya kupeleka askari wetu Uganda; For Tanzania Kagera war was not just war; we had legitimate reasons to fight that war.
Chama
Gongo la Mboto DSM
Chama,
Nitangulie tu kusema kwamba hata mimi nilipata taabu sana na kujisikia ukakasi kutumia hiyo brand ya Principal War Architect!!Kwanini nilijisikia taabu sana....naamini wengi wanaweza wasiamini, lakini amini usiamini, Nyerere nilikuwa nam-feel sana yule mzee!! Na hata kama leo hii angekuwa hai, halafu mtu akiniuliza ungependa nikukutanishe na nani....wala nisingesita kumtaja Nyerere!! Lakini vilevile nina uhakika, endapo baada ya kukutana huko tungeanza kubadilishana mawazo hususani ya wakati wa uongozi wake, naamini hapo hapo ningeanza kumkosoa!! Na hii imeshawahi kunikuta....kuna siku nilienda nyumbani kwa mheshimiwa mmoja aliye ndani ya serikali ya JK....Hii ilikuwa ni baada ya kusaga sana lami kutafuta kibarua lakini nisipate. Ikatokea zali, kuna uncle wangu mmoja akanituma kwake nami nikakata shauri kwamba lazima mheshimiwa yule nikamwambie anisaidie kupata kazi!!! Basi bana, ile tumeanza kuongea tu mara nikajikuta naanza kuipiga madongo CCM mbele yake!!Lakini bila aibu, mwisho wa maongezi, nikampa shida yangu!!! Hivyo ndivyo nilivyo...am firm to what i believe is right!
Sasa tuje na hilo la kumuita Nyerere kwamba ni Principal War Architect! Sincerly, bado sijutii and i stil believe in that! WHY? Nimejaribu kwanza kuangalia ROLE ya Architect!! Kwamba, majengo yote tuyaonayo hata kama ni mazuri au mabaya kiasi gani, source ya muonekano huo ni ARCHITECT kwavile yeye ndie ambae ali-design jengo husika!! So, Nyerere naamini ni Principal War Architect ni kwavile bado naamini kwamba baada ya kumpa hifadhi Obote, yeye akaanza kumsadia Obote operations dhidi ya serikali ya Amin...na hapo ndipo lilipoanza tatizo. Na katika masuala ya kiusalama, nchi ina haki ya kuishambulia nchi nyingine hata kama yenyewe haijashambuliwa provided ina ushahidi kwamba isipofanya hivyo inaweza ikashambiluliwa yenyewe! Sina hakika kama nimeeleweka!
Let's assume kwamba kuna taarifa za kiitelejensia ambazo zime-prove beyond reasonable doubt kwamba Rwanda ina mpango wa kuivamia Tanzania! Katika mazingira kama hayo, Tanzania ina HAKI na WAJIBU wa kushambulia/kuvamia kabla Rwanda haijafanya hivyo!! Ni bahati mbaya sana, katika mazingira kama hayo watu wanaweza kuilaumu Tanzania kwa kuishambulia Rwanda kwavile hawafahamu nini kilikuwa kinaendelea! Hivyo, kwavile tayari kulishakuwa na uthibitisho kwamba Obote alikuwa anafanya mipango ya kuivamia Uganda, basi serikali ya Amin ilikuwa na HAKI na WAJIBU wa kutuwahi kabla sisi hatujafanya hivyo....hiyo, ndiyo rule of the game!! Na kama intelligency ya Nyerere ingekuwa inafanya kazi vizuri ni kufahamu in advance kwamba Amin alikuwa anataka kuishambulia Tanzania (ile ya 1978) basi JWTZ walitakiwa wao waanze kabla Amin hajavuka mipaka na kuja kuua watu Tanzania! Hiyo, ndiyo rule of the game! Kama ambavyo tunaamini kwamba salama ya Tanzania ilikuwa ni kumwondoa Amin, basi salama ya Amin nayo ilikuwa ni kuitia adabu Tanzania inayomuhifadhi mtu anayetishia madaraka yake! Ni kama Bush ambayo ilikata shauri la kwenda kuivamia Afghanistan kwavile tu wanamuhifadhi Osama....hiyo ndiyo rule of the game!!
Chama, amimi usiamini....NYerere na Obote walikuwa wanausubiria kwa hamu uvamizi ule ambao ulifanywa na Amin! Ni kama walimtegea kitanzi, na yeye akaingia! Lazima ukumbuke kwamba Nyerere was very intelligent, kwahiyo mipango yake nayo ilihitaji mtu aliyeenda shule na sio mtu kama Amin!! Kama Amin nae angekuwa mwerevu sawa na Nyerere, basi si ajabu hivi sasa wala pasingekuwa na ubishani ni nani hasa mgomvi kwenye vita ile!! Ingekuwa ni sawa na Vita ya Bush Jr na Iraq, alitafuta sana sababu za kumwondoa Saadam madarakani lakini akazikosa na alipoona hatazipata akaamua tu kuvamia Iraq hivyo hivyo!
Lakini pamoja na yote hayo....unasema mkuu wangu kutokana na nukuu ambazo zimewekwa na Zakumi kwamba ni maelezo ya Obote wakati wa interview! Nukuu zile unazikubali au unazikataa?!