NasDaz;
Nimekusoma vizuri sana na nimekuelewa kama nitakuwa nimekosea nisahihishe; kwa ufupi zilikuwepo rabsha za maneno kati ya Uganda na Tanzania; Mwl. Nyerere hakuunga mapinduzi yaliyomuondoa Obote madarakani;
Chama, bado tatizo letu la msingi kati yangu na wewe lipo pale.....ROOT, SOURCE, MZIZI, CHANZO!! Labda nishawishike kwamba kuna tatuzo la matumizi ya lugha!! Hapo kweneye RED unamaanisha nini?! Kama ni suala la mapinduzi yaliyomwondoa Amin madarakani basi nazani hakuna mjadala kwamba ni majeshi ya Tanzania ndiyo yalimwondoa Amin Madarakani. Au tuseme unamaanisha si kweli kwamba Nyerere aliunga mkono harakati za Obote kumwondoa madarakani kwenye jaribio lililoshindwa la 1972!! Kama ndicho unachomaanisha, jibu ni kwamba NYERERE HAKUMUUNGA OBOTE KWA MANENO KWENYE JARIBIO LILE BALI ALIMUUNGA KWA VITENDO!! Umesema vizuri kwamba kwa kuhofia chokochoko za Amin, wakimbizi wa Uganda hawakuwekwa mpakani kama ilivyo kwa wale watokao Rwanda au Burundi. Bila shala unachomaanisha ni kwamba walikuwa ndani kabisa ya Tanzania. Sasa niambie wewe...wafuasi(wanajeshi) walioenda kufanya jaribio lililoshindwa Uganda waliweza vipi kusafiri kilometa kadhaa ndani ya Tanzania hadi wanaingia Uganda bila serikali kufahamu?! Hawa hawakuwa askari wa siafu wenye uwezo wa kuchimba na kupita chini kwa chini; bali ni askari wanadamu!!! Na ni kutokana na ukweli huo ndio maana nasema wazi kwamba Nyerere hakumuunga mkono kwa maneo bali kwa vitendo!! Na ukumbuke kwamba, kulikuwa na military training field wilayani Handeni ambayo ilikuja kufungwa baada ya kusainiwa Mogadishu Accord. Kama unakumbuka sawa sawa, Mogadishu Accord ilisainiwa October 7,1972....hii maana yake ni kwamba kumbe kabla ya October 1972 Tanzania ilikuwa inafadhili harakati za kijeshi za wanachama wa UPC waliokuwa chini ya Obote! Kitendo hicho hakikubaliki, hakivumiliki, na wala hakiwezi kukaribishwa na mtawala yeyote yule duniani labda mtawala sawa na kiongozi wa sasa wa Somalia ambae hana serikali yenye uwezo wa kujilinda!
pamoja na kuwa tulikaribisha wakimbizi kutoka Uganda; Amin alichopaswa ni kulinda mipaka yake na si vinginevyo; Tanzania haikutishia usalama wa Amin;
Hiyo hapo kwenye RED tunaita DOUBLE STANDARD! Kama unaamini alichotakiwa kufanya Amin ni kulinda tu mipaka yake ni kwanini majeshi yetu hayakuishia tu kuwatimua majeshi wa Amin ndani ya mipaka ya Tanzania na kuanza kulinda mipaka yetu na badala yake tukaingizamajeshi ndani kabisa ya Uganda na kumng'oa Amin madarakani?! Mkuu wangu Chama vipi?!
Sasa hapo kwenye BLUE inaonesha kwamba hata vyanzo ambavyo wewe mwenyewe umevileta hapa huvitaki kuviamini!!! Ulitaka Tanzania itishie vipi usalama wa Amin zaidi ya kitendo chake cha kuwa na military training ya wafuasi wa UPC waliokuwa na lengo la kwenda kumpindua Amin?! Ulitaka Tanzania itishie vipi usalama wa Amin zaidi ya kuruhusu Waganda wapinzani wa Amin watumie ardhi ya Tanzania kufanya maandalizi ya mapinduzi?!
kumbuka Amin mara kadhaa alituma vikosi vyake kuvuka mpaka hayo yote Mwl. aliyavumilia;
Hayo yote ni matokeo ya uchokozi ambao ulikuwa engineered na sisi wenyewe, ikiwa nitataka kuiga tabia ya kinafiki basi naweza sema kwamba the one to be blamed is ourselves na endapo nitataka kuwa partial hypocrite, basi naweza sema kwamba the one to be blamed is Nyerere and his government lakini endapo nita-opt kujiweka mbali kabisa na unafiki basi sitakuwa na budi kusema wazi kwamba the one to be blamed is The Late Nyerere ambae alikuwa ndie Jemedari Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Tanzania.
kumbuka wakimbizi wa Uganda hawakuwekwa mpakani kama walivyowakimbizi wa Rwanda na Burundi; yote hiyo ilikuwa ni kuepusha shari; ili Amin asilete visingizio;
Hapo ndipo panapojenga concern ya sisi wengine.....hawa jamaa hawakuwekwa mpakani; sasa sijui iliwezekana vipi kutembea maili kadhaa ndani ya ardhi ya Tanzania hadi wanafika mpakani na kuvuka na bado serikali ya Tanzania isifahamu!!
tatizo la Amin alikuwa NAIVE AND STUPID;
I'll be even MORE STUPID if i disagree with you on this!
kumtupia lawama Mwl. Nyerere alianzisha vita ni kumuonea;
Kutompa pongezi kwamba he was not an ASSOCIATE ENGINEER in engineering the conflict between Amin and Tanzania itakuwa ndo kumuonea zaidi...!!
kama angetaka vita angeweka brigedi nzima Ziwa Magharibi;
Nyerere was a very smart person...and only stupid leader ambae angefanya kinyume na alivyokuwa amefanya Nyerere!!
Amin ndiye aliyevunja makubaliano ya Mogadishu;
Kama mimi na wewe tumepatanishwa halafu nakupa mkono na hautaki kuupokea hapo maana yake ni kwamba mapatano hayo ni ya kinafiki. Kama kweli umeukabali upatanisho wetu then huna sababu ya kukataa mkono wangu. Usisahau kwamba, Mogadishu Accord ilisainiwa Otober 07,1972 na October 21,1972 kulikuwa na sherehe za kusherehekea mapinduzi ya Somalia. Nyerere alisusa kuhudhuria sherehe hizo kwavile tu Amin alihudhuria!!!! Na alifanya hivyo wakati alishathibitisha hapo kabla kwamba angehudhuria!!! Hivyo basi, ikiwa Nyerere alisusia sherehe kwavile tu Amin alihudhuaria, je unataka kuniambia alikuwa na nia ya dhati ya makubaliano hayo?! Kama utaniuliza maoni yangu, nitakueleza wazi kwamba Nyerere hakuwa na nia ya dhati ya makubaliano hayo lakini alilazimika tu kusaini. Na kwavile Nyerere ni mtu smart, alijitahidi kuonesha anayaheshimu makubaliano hayo ingawaje kwa siri aliendelea kufadhili harakati za kijeshi za Obote.
hata utafiti umeonyesha Tanzania haikuvunja mkataba ule. NasDaz naamini wapo watu hamuelewani hivi ikitokea mimi na wewe hatuelewani nikikupiga ngumi kwa dhana ya kutokuelewana kwetu utaniacha? Na nani atakaepaswa kulaumiwa?
Chama
Gongo la Mboto DSM
Safi sana!! Kama mimi ni goi goi, nitakuacha lakini kama nafahamu haki na hutu wangu sikuachi....lazima tuzichape!! Nyerere kampiga ngumi Amin, kwa bahati mbaya, Amin si goi goi hivyo akakata shauri la kurudisha mashambulizi. Kwa bahati mbaya, watu wanamuangalia huyu ambae ame-respond to attach!
Am afraid, bado unaamua kuvuka matukio yote tangu Obote kuingia Tanzania na unarukia matukio yaliyotokea baada ya Obote kuanza uchokozi!