Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Swali la kujiuliza ni je
(1) kulikuwa na motive yoyote ya kumpiga Amini kabla hajavamia nchi yetu?
(2)Je kulikuwa na Covert actions zozote dhidi ya Amini zilizofanywa na Serikali yetu kabla ya Amini kuvamia nchi yetu?
(3)Ni nani alivunja daraja la mto Kagera, Amini au Majeshi ya Tanzania?
(4)Ni matukio gani yalitake place kuanzia mwaka 1971 Iddi Amini alipompindua Obote hadi mwaka 1978 vita vilipolipuka, je mapigano ya mwaka 1972 ambapo vikosi vya waasi vilishambulia Uganda kutokea Tanzania, ni nini role ya Serikali ya Tanzania dhidi ya Uvamizi huo?
haya mambo nadhani yanahitaji uchunguzi huru
Ndugu, na huo ndio ulikuwa msingi wa mada hii, kabla haujachukua sura nyingine, nikasema hivi:Sijui kama umepata nafasi ya kusoma hotuba ile ya kutangaza vita. Watu wengi wanakumbuka maneno ya "nia tunayo" lakini hawakumbuki sababu zilizotolewa.
"... hoja ya vita anayoijenga ni nzito zaidi ya makaririsho ya "Sababu Tunayo, Uwezo Tunao."
Ila sijabahatika kusoma au kusikia hotuba nzima, na kama mwanafunzi wa historia ya marais wa Tanzania, sitaki kujinyima tunu ya historia ya hoja ya vita ya J. Kambarage Nyerere. Kuna mtu anayo tafadhali?
Waberoya said:Got u, so tunaweza kusema Nyerere alikuwwa mkorofi kwanza na Idd Amin alikuwa mkorofi baadae!
what Nyerere did? alichukua hatua gani kuzuia hili swala ? maana OAU walikuwa against naye! any info please. I mean, je bunge lilihusika kusema JWTZ waende Kagera?
Kuna watu hata hawajui kuwa Idi Amin wakati Uganda inapata uhuru alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya waganda 14 ambayo Obote aliyamezea kitu kilichokuwa kosa kubwa sana kwa Obote baadaye. Sasa watu wanaotaka kumtukuza Idi Amin kwa sababu ya dini yake basi wafanye hivyo tu lakini wasipoteshe historia. Hivi Abdallah Twalipo (aliyeongoza majeshi yetu) leo hii sijui angetushangaa vipi kwamba ilikuwa ni vita ya kidini.
Kama Nanren ulivyosema, kama mtu unamchukua mtu basi umchukie japo kwa sababu za ukweli. Lakini unamchukia kiasi kwamba unapotosha ukweli sidhani kama ni vyema.
Nitakuja kutuo kumbukumbu yangu kuhusu swala hili nikipata muda mwafaka. Kuna historia ndefu kidogo inayounganisha vita hii kuanzaia madai ya uhuru wa Rhodesia ambayo leo ni Zimbabwe, makubaliano ya Mulungushi Club, Mkutano wa Commonwealth wa 1971 huko Singapore amabpo Obote alipinduliwa na Amini akiwa njiani, msimamo wa serikali ya Uingereza kuhusiana na mapinduzi yale na uteuzi wa Bob Astles, Vita ya Kagera mwaka huo huo wa 1971 iliyosababisha mkuu wa mkoa wa Kagera awe Mwanajeshi (Luteni Kanali Abdallah Twalipo), Mabomu ya Amini pale Mwanza, Makubaliano ya Mogadishu kuhusus amani mpakani mwa Tanzania na Kagera, Kuanguka kwa EAC mwaka 1977, na vita kamili hiyo ya Kagera ya mwaka 1978.
Ndugu, na huo ndio ulikuwa msingi wa mada hii, kabla haujachukua sura nyingine, nikasema hivi:
Basi, kama unayo hiyo hotuba, naiomba tafadhali.
Mwanakijiji, vita vya Kagera vimetokea wengine wetu tukiwa tu ni watu wazima lakini kuna mambo yanaongelewa humu hata sijui wanaoyasema wana lengo gani. Baada ya Idi Amin kuvamia ardhi yetu hatukukurupuka tu tukaanza kupambana naye. Kuna kipindi Mwalimu aliyaomba siyo tu mataifa ya nje, umoja wa mataifa hadi umoja wa nchi za kiafrika kulaani uvamizi huo lakini ni kama vile kuna mataifa yalifurahia kitendo cha Amin. Tukumbuke kuwa wakati huo Mwalimu alikuwa kama adui wa mataifa ya magharibi kwani alikuwa kikwazo sana kwa maslahi yao sehemu hii ya Afrika.
Pia wanaojaribu kuingiza Udini ni lazima wafahamu kuwa katika kipindi hicho Mwalimu alikuwa mstari wa mbele kuwatetea Wapalestina katika harakati zao dhidi ya Israel. Ni sababu hiyo iliyopelekea Tanzania kuvunja mahusiano ya kibalozi na Israel na Mwalimu alikuwa rafiki mkubwa wa Gadafi wa Libya. Tendo la Gadafi na Wapalestina kutuma majeshi kuja kumsaidia Idi Amin dhidi ya Tanzania lilimshtua sana na kumhuzunisha Mwalimu.
Mwalimu hakupenda mapinduzi ya kijeshi na ndiyo sababu kubwa sana ya kukataa kumtambua Idi Amin toka mwanzo kabisa na hili hakulificha hata siku moja. Nawashauri wenye nia ya kweli ya kutaka kujua historia ya vita vya Kagera waachane na malimbukeni wanaojitokeza kujaribu kupindisha historia kwa sababu za wivu na ujinga. Bahati mbaya kumejitokeza watu ambao hukesha wakipanga kumkebehi Hayati Mwalimu asiyeweza kujitetea.
Ilichukuwa kipindi cha miezi kadhaa kuwahamasisha Watanzania kuwa tayari kupambana na adui aliyevamia ardhi yetu - kumtoa nyoka pangoni na tulifanikiwa.
Labda tunasahau, Idi Amin aliweza vipi kuwa rais mara ya kwanza, tusije kuwa tunaruka ssehemu ya historia. Maana watu wanazungumzia Nyerere alitaka kumrudisha Obote lakini hawatuambii kwa misingi gani au Obote alikuwa na haki gani ya kurudishwa madarakani.
Sijui kama umepata nafasi ya kusoma hotuba ile ya kutangaza vita. Watu wengi wanakumbuka maneno ya "nia tunayo" lakini hawakumbuki sababu zilizotolewa.
Waberoya,
..naweza kusema kwamba kitendo cha Mwalimu kumkaribisha Obote, na kujaribu kumrudisha madarakani 72/73 kiliifanya Tanzania na Nyerere kuwa target ya vituko vya Idi Amini.
..NB:
..inawezekana Bunge la Tanzania, au CCM [miaka ile chama kilikuwa kimeshika hatamu] walibariki vita vya kumngoa Amini. sina uhakika na hili. lakini kuna maeneo mengine ambayo JWTZ walipelekwa na si bunge wala chama vilishirikishwa. Raisi wetu ana madaraka makubwa kupindukia.
..
Ile ni vita ya kidini nilivyosikia mimi kwa wakongwe!mambo yale yalikuwa ya kivatcan against muslim ndo mambo mengine tukadanganywa oooh anakula nyama za watu yote ile ni kujastify tu ili wamvamie. Ila angekuwepo mpaka sasa hivi uganda ingekuwa nchi ya kiislam. baba wa taifa alikuwa mroman karibu sana na papa!
Na ule urafiki na Gadaffi uliwatishia amani sana.
haya na mimi niliyasikia tu
Asante kuwa unakubali lengo ni Obote, whatever Amin did that time prime source was Obote was in our land, this made Amin unrest! the question here is how far Nyerere went to prevent this war, is there any written report/hostory. documents that Nyerere did this and that to prevent this war?? will appreciate for that!
Kilimasera ukiona mdogo wakoa anampiga ngumi mwezio na mwenzi akarudishia mkorofi ni yule aliyeanza kurusha ngumi??
Tafuta Literatures, uliza waganda, nenda kulia nenda kushoto......
Uganda mpaka leo wanamkumbuka Amin! ambaye wewe unamwona dictator
Amin aliua makumi
Obote kaua maelfu
Museven kaua makumi elfu.......
Kwa kufupi mkuu, Nyerere alikuwa na mtu ambaye anatakwa sana na Amin..Mr.Obote,
kwa kifupi ulikuwa mpango wa Nyerere kumuweka Obote madarakani!!! yale ya kagera n.k ni hasira za Amin, ukweli NYERERE NDIYE ALIKUWA MKOROFI!!!!!
Sikutaka kusema kitu kwenye mjadala huu kwa sababu nilishasema mengi hapo awali huu mjadala ulipojitokeza mara ya kwanza.Asante kuwa unakubali lengo ni Obote, whatever Amin did that time prime source was Obote was in our land, this made Amin unrest! the question here is how far Nyerere went to prevent this war, is there any written report/hostory. documents that Nyerere did this and that to prevent this war?? will appreciate for that!
Joka kuu ala kumbe kifupi cha jina lako ni JK!!
Thanks for this piece of information, we are looking back so that we canb predict and evaluate how are we doing now. Briefly you have decribed that Nyerere was confident and trouble shooter this is a quality of any good leader.
However, in your information it seems you have relied on 'mwalimu did this' or mwalimu did that...this is where my problems arises
Je ni nani aliamua Obote akaribishwe ilikuwa Nyerere kama Nyererere au Nyerere kama rais wa nchi! I mean decision za maamuzi mengi inaonyesha ilikuwa personal zaidi na hatuonyeshwi kwenye historia ( au mimi sijaona) kuwa kulikuwa na organ ya kufanya maamuzi!!!
Mathalan vita ya ghuba, iraq ambavyo USA aljiingiza, inaonekana kuna organ zinafanya maamuzi au kupitisha maamuzi ya rais! I bet you, kuna wengi leo hii hawakufurahishwa na yale maamuzi ya vita!!! they were blinded by good speech 'nia tunayo' baada ya vita kila mtu akaanza kulia na hata leo hii tuna suffer!! my question is HAKUKUWA NA ARGUMENT ZOZOTE ZA twende au tusiende??
Leo hii Kikwete anafanya very same thing, mara kwenda kuokoa comoro sijui wapi, wanajiamulia amulia tu, zikifika athari tunalia sote!!
je japo Obote alikuwa nchini, intelijinsia hazikuonyesha kuwa anything like that might happen?? mpakani hakukuwa na ukilinzi?
Nani alisimamia usuluhishi wa Mogadishu? je huyu mpatanishi hakuwa consulted baada ya vita...I BELIEVE OAU WANGEONA KABISA IDD AMIN AMEVUNJA MKATABA WA AMANI, BASI OAU INGEKUWA UPANDE WA NYERERE!! what happened there..... AU OAU ilichakachuliwa?? kama OAU ilichakachuliwa Nyerere alichukua hatua gani baada ya vita?? kuendela kuwa mwanachama?? what for??? kuna mwenye info?? sijapata jibu la kuridhisha nafsi yangu, japo maswali haya yanazua hisia labda Nyerere hapendwi la! lets discuss FACTS!!!
nawachukia watu kama nyie msiojua historia yetu kagera ila mnataka kuleta upuuzi hapa. Hata wazazi wetu wametuonesha mpaka sehemu alipokuwa anawamwaga watu,vikongwe na walemavu ktk mto kagera kwa ukatili wake Amini. Mi sikuipenda vita ile kwa kuwa iliirudisha Kagera Tanzania ila ikawaache wananchi wale wafe maskini. Ni bora ingetuacha tukaelea Uganda kuliko tanzania ya mkoloni mweusi ila siwezi kuileta vita ile katika udini,hapana. Msiwe wavivu wa kufikiri,hadi leo wazazi wetu tunao na wanatueleza kilichojiri,hamna udini. Hata ukiangalia pale Muhutwe na Kemondo ambako Obote alijificha palikuwa na waislam wengi waliomsaidia na baadae amin kapinduliwa!udini haukuwepo na usiingizwe kamwe.
Kama ungesoma mwanzo nimesema na mimi nilisikia hilo, na aliyekuwa anasimulia nae ni mzee na nimewasilisha hapa kama comment tu na sio fact!
historia inajulikana kama tulivyosoma, hata watoto wetu nao wakija sikia mambo ya dowans watasema mengi, wengine wataamini serikali ya sasa kwamba ilikuwa lazima dowans ilipwe na wengine watakuwa against. Mimi nasimamia kwamba ukweli wanajua waliokuwa madarakani wakati huo. inaweza kuwa mipaka, inaweza kuwa udini au lolote. usicheze na intelijensia ikiamua vitu vyake.