Vita vya Kagera: Nini chanzo? Kulikuwa na ulazima?

It's all about UHURU, HAKI na USAWA ukiweza kuviona hivyo na kuvianisha kwa nani, utaweza kupembua mchele toka ktk pumba.

That's my problem. I can't separate the rice from the chaff. Anyway, sometimes egos of those in power get the best of them. They use every execuses at their disposal to justify wars.
 
Je vipi kuhusu Hitler si aliondolewa na majeshi ya NATO au, Hao Taliban wameondolewa na nani?..Nuriega, kina Milosovic na kadhalika. Iweje kweli jambo limetutokea sisi wenyewe na tukachukua jukumu la kulimaliza sisi wenyewe leo hii liwe swala la sheria na kufikiri wakati Idd Amin alivamia nchi yetu na kuua watu kibao huko Bukoba. Kapiga mabomu Mwanza nikiwa nimelala nyumba tatu tu toka pale yalipoangukia au sisi hatukuwa Watanzania kihivyo?..Hivi lini Ubinafsi wenu utakwisha na mkaweza kuyatazama maswlaa haya kwa mabana zaidi?

Hitler aliondolewa na Allied Forces. NATO ilianza baada ya vita vya pili vya dunia.
 
Hivi ilikuwa inahusu nini sisi raia wa Tanzania kulazimishwa kuvaa T-Shirts za Uganda People's Congress (UPC).

Mkuu Ritz sikuwahi kuvaa fulana ya Obote nadhani maana ya kulazimishwa huijui; kama watu walivaa walitaka wenyewe; labda ungehoji kwanini waligaiwa hili la kulazimishwa umeishiwa na hoja.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
- Nimewahi kukaa chini na Binaisa na Lule, story zao ninaziamini sana maana zinakaribiana sana na za viongozi wetu ambazo huwa wanzitoa kwa siri sana, kwa kuogopa kuonekana wana tatizo na Mwalimu.

- Binaisa anasema aliambiwa wazi kwamba yeye ni RC tu wa Uganda sio rais, yaani Mkuu wa mkoa wa Tanzania wakati ule, Lule alipojaribu kuwa objective anasema aliwekwa under house arrest, halafu mnakuja watu wazima hapa mnataka kutudanganya na kututisha na maneno mengi uongo uongo as if wote hapa ni watoto wadogo, kama mmezidiwa hoja ni kukaa pembeni tu! Mnatutisha na mavitabu yaliyoandikwa na ma-compromise, mtu unasoma kitabu ukurasa wa kwanza tu umeshaelewa kila kitu kitabu gani hicho?

- Waliotyaka kuandika vitabu vya ukweli si walufukuzwa au hujui? I mean wakuu wacheni tujadili taifa letu kama kawa!

William.
Muongo mkubwa wewe!
 
NasDaz
Harakati nyingi za kumtoa Idd Amin zilifanyika ndani ya Uganda; hii ilianza baada ya Idd Amin kufanya mauji ya askari wengi wa Uganda wenye asili ya makabila Lango na Acholi; tumeshakubaliana halikuwa kosa kwa Obote na wakimbizi wa Uganda kupokelewa Tanzania; na halikuwa kosa kwa waganda kujitetea dhidi ya Idd Amin. Idd Amin ndiye alikuwa na chokochoko za kutuma askari wake kuvuka mpaka alifanya hivyo mara kadhaa; hata alipoamua kutuvamia tulikuwa off guard hatukuwa na jeshi mpakani, brigedi kubwa ya jeshi ilikuwa Tabora sasa ikiwa Mwl. Nyerere alikuwa yeye ndiye mvamizi ni wazi Idd Amin hata mto Kagera asingefika; ilituchukua muda kukusanya askari na vifaa vya kijeshi sijui ulikuwa na umri gani wakati ule; Idd Amin ndiye aliyeitangazia dunia kuwa anaichukua Kagera; NasDaz mtu akikutia kidole cha ****** utamfanya nini? Kama ilikuwa hoja ni wakimbizi wa Uganda kuvuka mpaka na kufanya hujuma alichopaswa ni kupeleka malalamiko rasmi OAU na UN au kutuletea malalamiko rasmi; nilikugusia wakimbizi wa Rwanda na Burundi inaonyesha jinsi gani ulivyo na mapungufu; serikali ya Kagame imeshawahi kulalamika sana kuhusu vitendo vya wakimbizi kuvuka mpaka na kufanya hujuma Rwanda; vitendo hivyo si rahisi kuvidhibiti hata kama utaweka brigedi nzima bado wapo wakaopenya. Pamoja na maelewano yetu hafifu Kagame hakutuma jeshi kutuvamia; unapaswa kuelewa ni hawa madikteta wanaoingia madarakani kwa kupindua na kuendelea kuuwa raia zao siku zote kutakuwa na wanaowapinga.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Je vipi kuhusu Hitler si aliondolewa na majeshi ya NATO au, Hao Taliban wameondolewa na nani?..Nuriega, kina Milosovic na kadhalika. Iweje kweli jambo limetutokea sisi wenyewe na tukachukua jukumu la kulimaliza sisi wenyewe leo hii liwe swala la sheria na kufikiri wakati Idd Amin alivamia nchi yetu na kuua watu kibao huko Bukoba. Kapiga mabomu Mwanza nikiwa nimelala nyumba tatu tu toka pale yalipoangukia au sisi hatukuwa Watanzania kihivyo?..Hivi lini Ubinafsi wenu utakwisha na mkaweza kuyatazama maswlaa haya kwa mabana zaidi?

Mkandara,
Ni bahati mbaya sana huu mjadala umeukuta umefika mbali sana lakini itakuwa si vibaya ukipitia post za nyuma ili uone msingi wa kila mtu katika suala hili. Binafsi, nimeshatamka wazi kwamba kwa ilivyokuwa 1978 baada ya majeshi ya Amin kuvamia Tanzania, nasi hatukuwa na budi bali ni kuingia vitani. Hoja yangu ni kwamba hii vita ya 1978 ni matokeo tu ya chokochoko za huko nyuma. Historia inatuonesha kwamba, baada ya Amin kumpindua Obote wakati akiwa Singapore, Obote alikimbilia Tanzania baada ya kunyimwa hifadhi Kenya. Kwangu mimi, haikuwa kosa kwa Nyerere kumpa Obote hifadhi.

Baada ya Obote kuja Dar es salaam, maelfu ya wafuasi wake wa Uganda People's Congress wakavuka mpaka na kuja kuungana na Obote. Hadi hapo, Nyerere hakufanya kosa lolote kuwapokea wafuasi kwa sababu za kibinadamu.

Tatizo linaanzia pale baada ya Obote akisaidiwa na Nyerere kuendesha harakati za kijeshi dhidi ya Amin wakitokea Tanzania. Obote na wafuasi wake, kwa msaada wa Nyerere wakaitumia Tanzania kama military Training Ground ili waweze kwenda kufanya mapinduzi nchini Uganda. Na kweli ikatokea.....Waganda wakavuka mpaka na kuingia Uganda na kufanya jaribio lililoshindwa dhidi ya Amin. Baada ya kushindwa, walivuka mpaka na kurudi tena Tanzania. Lazima ufahamu kwamba serikali ya kijeshi ya Amin haikuwa dhaifu kama ile ya Kanali Bacar wa Commoro. Kwenda kumpindua Amin palihitaji maandalizi ya kutosha, ya kimkakati, kiuchumi na kijeshi. Hivyo, sina shaka yoyote kwamba watu wale kabla hawajavuka mpaka na kuingia Uganda tayari walishapata mafunzo na maandalizi ya kutosha. SWALI....maandalizi hayo walifanyia wapi kama sio Tanzania?!

Hivyo basi, kwavile Amin alishagundua kwamba Obote anatumia Tanzania kama uwanja wake wa maandalizi ya vita vya kumpindua yeye, there's no way kwamba Amin angekaa kimya. Hakuna kiongozi hata mmoja duniani ambae angekaa kimya hata baada ya kugundua jirani yake anafadhili maadui zake wenye lengo la kwenda kumtoa madarakani. Ikiwa viongozi wa kidini tu wanapigana kufa ama kupona kuyalinda madaraka yao, seuze hawa viongozi wa kidunia ambao always they fight for power?!

Hivyo basi, mauaji yaliyotokea Kagera ni matokeo tu....lazima tutafute kiini chake!! Hapa hakuna suala la chuki dhidi ya Nyerere wala nini lakini mapenzi yetu yasitufanye tujaribu kubadili nyekundu kuwa njano. Nyekundu itabaki nyekundu na njano itabaki kuwa njano. Haipendezi watu wanapo-criticise what happened kuwaona kwamba hao watu wana chuki na Nyerere....yaliyotokea zama zile ni somo ambalo tukijifanya hamnazo yanaweza kutokea tena. Watu watasema sana kwamba Nyerere alisukumwa zaidi na spirit yake dhidi ya freedom na haki....lakini siamini hata chembe kwamba kupinduliwa kule kwa Obote ingekuwa amepinduliwa Kenyatta Nyerere angefanya aliyofanya!

To cut story short, Vita vya Kagera ni matokeo ya chokochoko ambazo tulizengeneza sisi wenyewe kwa ajili ya ama kumtetea swahiba Obote au kuhakikisha tu Amin hakai madarakani.
 
wapendwa wanaJF,

msiwe mnajadili mambo na kusahau oficial records!

kama munataka kujua vizuri mambo ya mgogoro wa amini na tanzania, jitahidi kuperuzi records za OAU (au AU kwa sasa). hao waliushughulikia mgopgoro wa TZ na UG tangu mwanzoi hadi mwisho na kila kitu kiko documented! waziri wa foreign affairs alikuwa rais mstaafu Mkapa na mkifuatilia proceedings za OAU mtaona jinsi diplomasioa ya TZ ilivyojitahidi kuepusha vita lakini ikashindikana!

wanadiplomasia wote duniani wanakubaliana na ukweli kuwa "hakukuwa na njia nyingine yoyote ya kuihakikishia TZ usalama wake ila "kumchapa" amini! na kumuondoa uganda!

tanzania ililaziomika (licha ya kupingwa na "OAU"), kuingia vita ya kimataifa dhidi ya nchi nyingine "huru"! ya kiafrika! hili lilileta gumzo kubwa, lakini nyerere kwa ujasiri wake alisimama kidete na kusimamia vita hadi ushindi ulipopatikana!

ushindi huu, sio tu uliihakikishia TZ uhuru wake, bali pia uliihakikishia uganda amani ya kweli. rais wa sasa Museveni wa uganda ni moja ya matunda ya amani hiyo na ndiyo maana haachi kumtukuza mwal. nyerere!

nina siri nyingi sana za vita hii, kama ndg malecela anataka kujifunza basi, aendelee kujadili kwenye mada yake na mimi "nitammegea" yote niliyonayo bila uchoyo!

ila kwa kweli nimesikitishwa sana na uelewa wa mpendwa huyu juu ya masuala ya siasa kwa siku za hivbi karibini, hususani baada ya kushindwa ubunge wa EALC!!

Mungu wetu ni mkubwa na mwema sana na uaminifu wake wapita kizazi hata kizazi,

mbarikiwe sana wapendwa,

Glory to God!
 
Kwa hiyo official records ndio ukweli?
 
- kama unataka kuongelea ufisadi then fungua thread yake, lakini kujaribu kuingiza hoja za propaganda hapa ndio ufisadi wenyewe, siamini kwamba Russia ilitusamehe madeni ya ile Vita, ambayo wao walikuwa wanauza silaha kwetu na kwa adui at the same time, tunaambiwa tulikuwa na Viongozi genius enzi hizo, lakini walikubali tukadanganywa na Russia wao wakiuza silaha huku na kule,

- Sasa leo tunawauliza was it fair kujiiingiza kwenye ile vita mpaka kufikia madeni yote tunayolipa mpaka leo? Mnasema ni propaganda, oooh maswali ya chuki za binafsi, REALLY?

William.

William
Soma report ya G8 summit Muskoka Canada 2010. Russia ilifuta 100% ya madeni kwa nchi maskini 16 duniani Tanzania ilikuwa ni mojawapo wa tulionufaika na uamuzi huo wa Russia, walitangaza azma hiyo 20007 na walitekeleza ahadi yao 2010; 2006 China walifuta 1/3 ya deni letu; kwa deni la vita limekwisha tujadili hili linalotukwamisha sasa hivi.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
NasDaz
Harakati nyingi za kumtoa Idd Amin zilifanyika ndani ya Uganda; hii ilianza baada ya Idd Amin kufanya mauji ya askari wengi wa Uganda wenye asili ya makabila Lango na Acholi; tumeshakubaliana halikuwa kosa kwa Obote na wakimbizi wa Uganda kupokelewa Tanzania; na halikuwa kosa kwa waganda kujitetea dhidi ya Idd Amin. Idd Amin ndiye alikuwa na chokochoko za kutuma askari wake kuvuka mpaka alifanya hivyo mara kadhaa; hata alipoamua kutuvamia tulikuwa off guard hatukuwa na jeshi mpakani, brigedi kubwa ya jeshi ilikuwa Tabora sasa ikiwa Mwl. Nyerere alikuwa yeye ndiye mvamizi ni wazi Idd Amin hata mto Kagera asingefika; ilituchukua muda kukusanya askari na vifaa vya kijeshi sijui ulikuwa na umri gani wakati ule; Idd Amin ndiye aliyeitangazia dunia kuwa anaichukua Kagera; NasDaz mtu akikutia kidole cha ****** utamfanya nini? Kama ilikuwa hoja ni wakimbizi wa Uganda kuvuka mpaka na kufanya hujuma alichopaswa ni kupeleka malalamiko rasmi OAU na UN au kutuletea malalamiko rasmi; nilikugusia wakimbizi wa Rwanda na Burundi inaonyesha jinsi gani ulivyo na mapungufu; serikali ya Kagame imeshawahi kulalamika sana kuhusu vitendo vya wakimbizi kuvuka mpaka na kufanya hujuma Rwanda; vitendo hivyo si rahisi kuvidhibiti hata kama utaweka brigedi nzima bado wapo wakaopenya. Pamoja na maelewano yetu hafifu Kagame hakutuma jeshi kutuvamia; unapaswa kuelewa ni hawa madikteta wanaoingia madarakani kwa kupindua na kuendelea kuuwa raia zao siku zote kutakuwa na wanaowapinga.

Chama
Gongo la Mboto DSM

Chama,
Sina shaka yoyote kwamba wewe hufahamu vizuri nini kilikuwa kinafanyika. Nyerere was VERY SMART MAN....hilo halina ubishi. Nyerere sio stupid. Nyerere asingeweza kuivamia Uganda pasipo na grounds za kufanya hivyo wakati haiba yake kimataifa ilikuwa kubwa na kuvutia. Kitu ambacho kilifanyika ni kuunda kikosi kidogo ambacho ni maalumu kwa ajili ya kwenda kumtekenya tekenya Amin. Kulikuwa na military training Handeni. Lengo hapa ilikuwa kumtia ghadhabu Amin ili a-react na ili Nyerere na Obote wapate sababu za kushambulia. Kwahiyo, kwa mtu mwerevu kama Nyerere asingeweka majeshi yake mpakani.

Hata hivyo, si kweli kwamba majeshi yalikuwa mbali kiasi hicho kwani ktk Mogadishu Accord ilikubaliwa kwamba majeshi ya nchi zote mbili yawe umbali wa at least 10 miles from common boarder na wakati uvamizi wa Amin unatokea majeshi yetu yalikuwa umbali wa kiasi cha maili 20 tu toka mto Kagera. Nyerere asingekuewa mpuuzi wa kutokuwa na stationed army wakati situation ilikuwa so intense.

Kuhusu suala la wakimbizi wa Rwanda, kwa mara nyingine upo off-guard! Kuna tofauti kubwa kati ya hao wakimbizi wa Rwanda unaowazungumzia na wakimbizi wa UPC. Na ndio maana unakuta sehemu zote nilizozungumza kuhusu wakimbizi wa UPC, hapo nimeihusisha na serikali....kwamba wakaimbizi wa UPC walikuwa wanapata msaada wa kijeshi toka serikali ya Tanzania na hao wa Rwanda sio! Alichokuwa anashutumu Kagame ni vile ambavyo tunashindwa kuwadhibiti wakimbizi waliopo kwenye makambi hadi wanafanikiwa kutoka makambini na kwenda kufanya vurugu Rwanda....lakini si kwa msaada wa serikali ya Tanzania. Na kimsingi, serikali ya Rwanda ilikuwa na haki ya kulalamika lakini hakuwa na haki ya kutushambulia ingawaje kama hali ingekuwa mbaya zaidi kiasi cha kutishia uhai wa serikali yake basi angekuwa na haki vile vile ya kuvuka mpaka na kuja kuwafagia huku huku lakini sio kuishambulia Tanzania. Hata kama si sheria, lakini katika kuhakikisha usalama wa nchi yake, nchi yeyote inaweza kufanya hivyo. Na hii inatokea kila uchao kwenye ukanda wetu. Kenya wamevuka mpaka na kuingia Somalia kwa lengo la kuitia adabu Al-Shabab...lakini hawakuingia Somalia kuipiga serikali ya Somalia. Hali hiyo pia imepata kutokea kati ya Rwanda na DRC, Uganda na DRC, Uganda na Sudani and vice versal! Kwahiyo kuwa makini na mifano yako. USICHANGANYE MAMBO!
 
Mkandara,
Ni bahati mbaya sana huu mjadala umeukuta umefika mbali sana lakini itakuwa si vibaya ukipitia post za nyuma ili uone msingi wa kila mtu katika suala hili. Binafsi, nimeshatamka wazi kwamba kwa ilivyokuwa 1978 baada ya majeshi ya Amin kuvamia Tanzania, nasi hatukuwa na budi bali ni kuingia vitani. Hoja yangu ni kwamba hii vita ya 1978 ni matokeo tu ya chokochoko za huko nyuma. Historia inatuonesha kwamba, baada ya Amin kumpindua Obote wakati akiwa Singapore, Obote alikimbilia Tanzania baada ya kunyimwa hifadhi Kenya. Kwangu mimi, haikuwa kosa kwa Nyerere kumpa Obote hifadhi.

Baada ya Obote kuja Dar es salaam, maelfu ya wafuasi wake wa Uganda People's Congress wakavuka mpaka na kuja kuungana na Obote. Hadi hapo, Nyerere hakufanya kosa lolote kuwapokea wafuasi kwa sababu za kibinadamu.

Tatizo linaanzia pale baada ya Obote akisaidiwa na Nyerere kuendesha harakati za kijeshi dhidi ya Amin wakitokea Tanzania. Obote na wafuasi wake, kwa msaada wa Nyerere wakaitumia Tanzania kama military Training Ground ili waweze kwenda kufanya mapinduzi nchini Uganda. Na kweli ikatokea.....Waganda wakavuka mpaka na kuingia Uganda na kufanya jaribio lililoshindwa dhidi ya Amin. Baada ya kushindwa, walivuka mpaka na kurudi tena Tanzania. Lazima ufahamu kwamba serikali ya kijeshi ya Amin haikuwa dhaifu kama ile ya Kanali Bacar wa Commoro. Kwenda kumpindua Amin palihitaji maandalizi ya kutosha, ya kimkakati, kiuchumi na kijeshi. Hivyo, sina shaka yoyote kwamba watu wale kabla hawajavuka mpaka na kuingia Uganda tayari walishapata mafunzo na maandalizi ya kutosha. SWALI....maandalizi hayo walifanyia wapi kama sio Tanzania?!

Hivyo basi, kwavile Amin alishagundua kwamba Obote anatumia Tanzania kama uwanja wake wa maandalizi ya vita vya kumpindua yeye, there's no way kwamba Amin angekaa kimya. Hakuna kiongozi hata mmoja duniani ambae angekaa kimya hata baada ya kugundua jirani yake anafadhili maadui zake wenye lengo la kwenda kumtoa madarakani. Ikiwa viongozi wa kidini tu wanapigana kufa ama kupona kuyalinda madaraka yao, seuze hawa viongozi wa kidunia ambao always they fight for power?!

Hivyo basi, mauaji yaliyotokea Kagera ni matokeo tu....lazima tutafute kiini chake!! Hapa hakuna suala la chuki dhidi ya Nyerere wala nini lakini mapenzi yetu yasitufanye tujaribu kubadili nyekundu kuwa njano. Nyekundu itabaki nyekundu na njano itabaki kuwa njano. Haipendezi watu wanapo-criticise what happened kuwaona kwamba hao watu wana chuki na Nyerere....yaliyotokea zama zile ni somo ambalo tukijifanya hamnazo yanaweza kutokea tena. Watu watasema sana kwamba Nyerere alisukumwa zaidi na spirit yake dhidi ya freedom na haki....lakini siamini hata chembe kwamba kupinduliwa kule kwa Obote ingekuwa amepinduliwa Kenyatta Nyerere angefanya aliyofanya!

To cut story short, Vita vya Kagera ni matokeo ya chokochoko ambazo tulizengeneza sisi wenyewe kwa ajili ya ama kumtetea swahiba Obote au kuhakikisha tu Amin hakai madarakani.
Mkuu nimewasoma sana kabla sijaingia hapa na pengine labda unachukulia kutoziona likes zangu, lakini naelewa vizuri sana mnachodai nyie kutuweka ktk hatia wakati haikuwa hivyo hata kidogo.

Kwanza kabisa Idd Amin hakuivamia Tanzania kwa sababu ya Obote hilo sii kweli hata kidogo isipokuwa Idd Amin mwenyewe aliamini kwamba Bukoba ni sehemu ya Uganda. Na historia itakwambia wazi kwamba waliotakla kumpindua Idd Amin mwaka 1972 walikuwa watu wa kusini mashariki wenye asili ya Acholi na Walang ambao kama unakumbuka vizuri Idd Amin alitaka kuzipiga na Kenya kwanza kbala yetu. Akawaua sana hawa watu ikisemekana ni wafuasi wa Obote, binafsi sijui kwa nini walimfuata Obote.

Hivyo, hata Obote mwenyewe ambaye alikimbilia Tanzania mbona aliondolewa na kundi la wanajeshi waliokuwa Tanzania kina Mseveni? mbona Obote hakuivamia Tanzania wakati alijua wazi kwamba hata sisi tulikuwa tumemchoka. Idd Amin na Nyerere picha zilikkuwa haziendi kwa sababu the guy alitaka yeye kuwa rais wa EAC, the man to be reckoned with. Pingamizi pale alikuwa Nyerere tu. Huyu jamaa alikuwa na dream yake sawa na Ghadaff kuamini kuamini uwezo wao mkubwa ktk utawala. na alitaka ku prove that kwa Waganda na Afrika nzima ndio maana akawafukuza wahindi na hata kuwabebesha wazungu kiti chake kama lipizo la utumwa kwa babu zake. The guy was phycal...yaani zimepitiliza.

Idd Amin alipendwa sana na Waganda hasa baada ya kumpa heshima zote Kabaka Mutesa na aliwapenda wananchi wake, na watu walimwona mjinga sana alipowapa wananchi wake kuchukua mali za Wahindi wakati ule lakini leo hii ni Uganda peke yake ktk nchi zote za Afrika mashariki Waganda ndio wanaendesha uchumi wa nchi yao. Waganda kwa makabila yao ndio wawekezaji ktk miradi mingi ya kitaifa maana Utajirisho japokuwa unaweza kuwa wa kijinga kama wa Idd Amin na haupo vitabuni lakini matokeo yake leo hii Uganda is almost self reliant na Waganda wenyewe ndio matajiri na wanaendelsha miradi yao. Kwa hilo Waganda watamheshimu mwendawazimu yule haki kiyama.
 
Kwa hiyo official records ndio ukweli?

mpendwa,

najua "official records" zinaweza kuwa si za kweli!

sas tujuze wewe ukweli ni upi?

nakusubiri tujadili,

ubarikiwe sana ,

Glory to God!
 
wapendwa wanaJF,

msiwe mnajadili mambo na kusahau oficial records!

kama munataka kujua vizuri mambo ya mgogoro wa amini na tanzania, jitahidi kuperuzi records za OAU (au AU kwa sasa). hao waliushughulikia mgopgoro wa TZ na UG tangu mwanzoi hadi mwisho na kila kitu kiko documented! waziri wa foreign affairs alikuwa rais mstaafu Mkapa na mkifuatilia proceedings za OAU mtaona jinsi diplomasioa ya TZ ilivyojitahidi kuepusha vita lakini ikashindikana!

wanadiplomasia wote duniani wanakubaliana na ukweli kuwa "hakukuwa na njia nyingine yoyote ya kuihakikishia TZ usalama wake ila "kumchapa" amini! na kumuondoa uganda!

tanzania ililaziomika (licha ya kupingwa na "OAU"), kuingia vita ya kimataifa dhidi ya nchi nyingine "huru"! ya kiafrika! hili lilileta gumzo kubwa, lakini nyerere kwa ujasiri wake alisimama kidete na kusimamia vita hadi ushindi ulipopatikana!

ushindi huu, sio tu uliihakikishia TZ uhuru wake, bali pia uliihakikishia uganda amani ya kweli. rais wa sasa Museveni wa uganda ni moja ya matunda ya amani hiyo na ndiyo maana haachi kumtukuza mwal. nyerere!

nina siri nyingi sana za vita hii, kama ndg malecela anataka kujifunza basi, aendelee kujadili kwenye mada yake na mimi "nitammegea" yote niliyonayo bila uchoyo!

ila kwa kweli nimesikitishwa sana na uelewa wa mpendwa huyu juu ya masuala ya siasa kwa siku za hivbi karibini, hususani baada ya kushindwa ubunge wa EALC!!

Mungu wetu ni mkubwa na mwema sana na uaminifu wake wapita kizazi hata kizazi,

mbarikiwe sana wapendwa,

Glory to God!
Ms Judith,

Acha mbwembwe kwamba una siri nyingi juu ya Vita vya Kagera....zitoe hizo siri hapa tuzione.

Am very sorry kusema wazi kwamba unapotosha ukweli, ama kwa makusudi au kwa kutofahamu ingawaje umejigamba kwamba unafahamu siri nyingi. Ukweli kuhusu diplomasia ni kwamba Nyerere alikuwa hataki kabisa kufanya diplomasia na Amin...!!!! Nyerere aliamini kwamba Amin alimwondoa madarakani kiongozi halali wa Uganda ambae wakati wote Obote alipokuwa Tanzania, aliendelea kutambulika kama kiongozi halali wa Uganda. Na kukuthibitishia kwamba Nyerere alikuwa hataki kukaa meza moja na Amin, ni pale aliposusia sherehe za mapinduzi ya Somalia ambazo zilifanyika less than two weeks tangu kusainiwa makubaliano ya amani (Mogadishu Accord) kati ya Tanzania na Amin. Nyerere alilazimika kusaini makubaliano hayo kutokana na pressure alizikuwa anapata. Na kwa kuonesha kwamba aliyasaini shingo upande ndio maana alisusia sherehe hizo kwavile tu Amin nawe alikuwa ni miongoni mwa watu ambao wangehuhudhuria.

Mfano wa pili wa kuonesha kwamba Nyerere alikuw ahataki kukaa meza moja na Amin ni pale aliposusia Mkutano wa OAU ambao Amin nae angekuwepo. Nyerere alitoa sharti kwa OAU ni lazima imlaani Amin lakini OAU hawakufanya hivyo. Hivyo, si kweli kwamba Tanzania ilijitahidi sana kufanya diplomasia lakini ilishindikana. Akilini mwa Nyerere, Amin alikuwa ni jambazi tu asiyestahjili kufanya nae mazungumzo. Ni kama ilivyo siku hizi mataifa ya magharibi wanavyowachukulia magaidi!
 
Last edited by a moderator:
Nakumbuka Mwalimu Nyerere alisema wakati ule kwamba,''Safari hii akitushambulia tena mapigano hayataishia mpakani,tutakwenda mpaka Kampala,tunataka Amin aelewe hivyo'' Kwa hiyo ilikuwa kama ni adhabu kwa mtu aliyekuwa anafanya makosa tena na tena.
Halafu kumbuka kulikuwa na abuses nyingi katika serikali ya Amin. Wapinzani wake walikuwa wanapata 'VIP' treatment,ndivyo jinsi Amin alivyokuwa anaiita torture.
 
- Chama saafi sana sasa unaongea hoja: HOWEVER tizama mimi ninakuja hapa kutoa maoni yangu bila kujali anybody, niaamini JF kazi yetu inatakiwa kuwa kukosoa, kukosoa kila kiongozi hakuna wa kumbakisha wala kumuogopa, maneno ya agenda na propaganda siyajui, mimi umeona ninaposhambuliwa personal, huwa ninatumia fursa hiyo kujiweka vizuri na public kwa sababu ninajaribu kumuonyesha aliyerusha matusi hana FACTS, wala haelewi anachosema, lakini sio kumjibu matusi na vitisho kama mnavyofanya!

- Lets say mimi nime-specialize na mapungufu ya policies za MWalimu, kwa nini na wewe usi-specialize na mapungufu ya policies za Rais wa sasa, badala yake unaleta maneno ya propaganda hakuna hapa hizo hapa, mimi ninakata ishus tu sina cha nani wala nani, kama kuna anyeijhisi kwamba nina personal problems naye then waombeni utawala wa JF kuwa na limiti ya uwezo wa mtu hapa kufikiria, asiruhusiwe kufikiria mapungufu ya policies za MWalimu!

- I mean mbona sasa hizi kurasa tatu za mwisho tunajadili ishus na kinaeleweka kabisa kinachozungumzwa, kwa nini haumkuanza hivi toka mwanzo, I mean bravo people naona sasa tunaanza kukata ishu kama JF style. Kwamba Mwalimu aliamaliza madeni ndio kwanza leo ninasikia kwa mara ya kwanza.

- Mimi sipo hapa JF kujadili mazuri kihivyo, nipo hapa kukosoa kwanza kama for that ninavunja sheria yoyote ya JF then nitaacha kuchangia, lakini otherwise mwendo ni ule ule mdundo, mnanishngaza sana kwamba ninaanzisha thread ambayo hamuipendi, lakini mnakuja kulalamika na kuigeuza another story huo sio ustaarabu, jamani tuwacheni tukate ishus hapa msitutishe na vitabu uchwara wala hoja uchwara, kama thread ni mbaya iwache au omba mods waifute, akilni wacheni vitisho na mikwara jamani!!

William.

William
1. Nakujibu kwenye hizo red ili tuwe mstari mmoja kama hoja ni kujadili viongozi hiyo ni haki yako kabisa lakini itakuwa si busara kuwalazimisha wachangiaji wakubaliane na hoja zako; umesema vizuri sana hakuna kiongozi wa kumbakisha hilo pia nakubaliana na wewe labda nikukumbushe katika historia ya Tanzania tunao wanasiasa mahiri kama Mzee John Malecela usimsahau tuletee hoja zake ziwe nzuri ama mbaya tuzijadili.
2. Agenda unayo hukuamka tu na kuanza kuandika unayoyaona mabaya kuhusu Mwl. Nyerere; propaganda unazofanya kujijenga kisiasa hizo zitakuharibia; watanzania wanelewa Mwl. Nyerere aliwafanyia kitu gani; na kama suala ni kujadili maovu kuna maovu mangapi yanaendelea kufanyika mbona huyaleti ili tuyadili? Willima binafsi siamini kwenye personal attacks naamini hoja mara nyingi nimekuwa nikipingana na watu wasio na hoja na ambao wameelekeza personal attacks kwako; hapa tunajibizana kwa hoja.
3. Ningependa ufafanue vitisho ulivyofanyiwa ili pia navyo tuvijadili.
William usijaribu kupotosha ukweli sikusema Mwalimu alimaliza madeni; soma tena nilichoandika usibadili maana ya nilichoandika.
4.Si kweli kama tumeichukia thread yako; tunaichangia ili kuelemishana JF ni kama debate club tunajibishana kwa hoja hakuna vitisho na mikwara.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Ms Judith,
Acha mbwmbwe kwamba una siri nyingi juu ya Vita vya Kagera....zitoe hizo siri hapa tuzione.
Am very sorry kusema wazi kwamba unapotosha ukweli, ama kwa makusudi au kwa kutofahamu ingawaje umejigamba kwamba unafahamu siri nyingi. Ukweli kuhusu diplomasia ni kwamba Nyerere alikuwa hataki kabisa kufanya diplomasia na Amin...!!!! Nyerere aliamini kwamba Amin alimwondoa madarakani kiongozi halali wa Uganda ambae wakati wote Obote alipokuwa Tanzania, aliendelea kutambulika kama kiongozi halali wa Uganda. Na kukuthibitishia kwamba Nyerere alikuwa hataki kukaa meza moja na Amin, ni pale aliposusia sherehe za mapinduzi ya Somalia ambazo zilifanyika less than two weeks tangu kusainiwa makubaliano ya amani (Mogadishu Accord) kati ya Tanzania na Amin. Nyerere alilazimika kusaini makubaliano hayo kutokana na pressure alizikuwa anapata. Na kwa kuonesha kwamba aliyasaini shingo upande ndio maana alisusia sherehe hizo kwavile tu Amin nawe alikuwa ni miongoni mwa watu ambao wangehuhudhuria.

Mfano wa pili wa kuonesha kwamba Nyerere alikuw ahataki kukaa meza moja na Amin ni pale aliposusia Mkutano wa OAU ambao Amin nae angekuwepo. Nyerere alitoa sharti kwa OAU ni lazima imlaani Amin lakini OAU hawakufanya hivyo. Hivyo, si kweli kwamba Tanzania ilijitahidi sana kufanya diplomasia lakini ilishindikana. Akilini mwa Nyerere, Amin alikuwa ni jambazi tu asiyestahjili kufanya nae mazungumzo. Ni kama ilivyo siku hizi mataifa ya magharibi wanavyowachukulia magaidi!

mpendwa,

naamini unajua maana ya "juhudi za kidiplomasia"

sasa, naomba tuzungumze vizuri, baada ya OAU (OAU kwa sasa) kukataa kumlaani amin, nini kiklifuatia, na nani alishinda?

je unajua kuwa tanzania (nyerere) ilikosana na OAU kwa sababu ya amini? kati ya msimamo wa tanzania na msimamo wa OAU dhidi ya amini, ni upi ilishinda?

naomba nitajie vita moja ambayo nchi yoyote duniani imewahi kupigana dhidi ya nchi nyingine (iliyosaidiwa na nchi kadhaa nyingine) na nchi isiyokuwa na msaada ikashinda!

napenda kukuambia kuwa hakuna nchi yenye heshima kubwa AU na UN kuishinda Tanzania!!

majira yetu haya, yangekuwaje sasa, utumwa wa nchi NYERERE ameukomesha!!

ubarikiwe sana mpendwa

Glory to Gpd!
 
NasDaz
Nakubaliana na wewe Nyerere alikuwa ni mtu smart sana basi pia tukubaliane kuwa Amin alikuwa mtu stupid sana

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Idd Amin hakuwa mjinga hivyo bali tamaa yake ya madaraka na ndoto kama za Ghadaff ndizo zilimponza, lakini alipendwa kuliko viongozi wote wa Uganda.
 
Nakumbuka Mwalimu Nyerere alisema wakati ule kwamba,''Safari hii akitushambulia tena mapigano hayataishia mpakani,tutakwenda mpaka Kampala,tunataka Amin aelewe hivyo'' Kwa hiyo ilikuwa kama ni adhabu kwa mtu aliyekuwa anafanya makosa tena na tena.
Halafu kumbuka kulikuwa na abuses nyingi katika serikali ya Amin. Wapinzani wake walikuwa wanapata 'VIP' treatment,ndivyo jinsi Amin alivyokuwa anaiita torture.

mpendwa Andrew,

nimejulishwa kuwa wewe ni mwana wa kwanza wa kiume wa mwalimu!

hata hivyo, nataka kujadili kwa uhuru na uwazi uzalendo wa mwalimu kuhusuiana na vita ya kagera dhidi ya nduli idd amini.

niharakishe kusema kuwa vita ile ililaaniwa sana na OAU kwa kuwa mwalimu alionaekana anaamrisha vita dhidi ya nchi nyingine "huru" ya kiafrika na OAU ilikataa kutoa msaada na ikaenda mbali hata kukataa kuiunga mkono tanzania katika shinikizo lake la kumtaka amini na majeshi yake kuondoka katika mpaka wa tanzania bila masharti! wakati mwalimu akimuona amini sawa na jambazi, OAU walikuwa "wakimtambua" lakini mwalimu kwa msimamo na ujasiri, alianzisha vita!

na mwisho wa vita ile:

1. tanzania (kupitia mwalimu) iliitawala uganda kwa kitambo. mwalimu akiwateua na kuwaondoa madarakani marais wa uganda wakati wowote asiporidhishwa na utendajki wao wa kazi! (rejeeni kesi za marekani na iraq baada ya saddam hussein)

2. OAU ilimheshimu mwalimu kuiliko kiongozi mwingine yoyote wa nchi yoyote duniani! manake hata bila msaada wake (OAU) mwalimu alishinda vita dhidi ya amini aliyesaidiewa na jumuia yote ya kiislamu duniani!!

3. waislamu kote duniani walihitimisha kuwa, mwalimu ni mpinga "uislamu" kwa kuwa "alimchapa" amini aliyekuwa muislamu na kumuondoa madarakani, akiififisha ndoto ya waislamu kuifanya afrika mashariki eneo la kushamiri serikali za kiislamu!!

marehemu gadafi, alipatwa kihoro si cha kitoto!!

natumaini mmenipata vizuri wapendwa,

mbarikiwe sana na Bwana wapendwa,

Glory to God!
 
mpendwa,

najua "official records" zinaweza kuwa si za kweli!

sas tujuze wewe ukweli ni upi?

nakusubiri tujadili,

ubarikiwe sana ,

Glory to God!

Je kwenye official documents kunaonyesha kuwa kulikuwa na nia ya kumrudisha Obote? Lakini analysis zote zinaonyesha kuwa baada ya vita juhudi kubwa zilifanyika kumrudisha Obote madarakani.
 
Back
Top Bottom