Vita vya Kagera: Nini chanzo? Kulikuwa na ulazima?

Vita vya Kagera: Nini chanzo? Kulikuwa na ulazima?

Tatizo la kusoma ughaibuni kukulia huko huko unarudi home kutaka vyeo, unapokosa cheo ndo unaanza kusoma historia ya tz.,
mambo ya zamani unayakumbuka leo,
mbona kuna mengi tu yaliyotokea baada ya Iddi amini dada.
 
tatizo la kusoma ughaibuni kukulia huko huko unarudi home kutaka vyeo, unapokosa cheo ndo unaanza kusoma historia ya tz.,
mambo ya zamani unayakumbuka leo,
mbona kuna mengi tu yaliyotokea baada ya iddi amini dada.

Hatimaye kala ban
 
Kuna watu tunacheza na mambo makubwa bila kutathimini athari zake. Hizi mada zinatakiwa ziletwe na watu wasafi kabisaa wasio na mawaa...wengine wetu kama tunajua tuna siri zetu ndani ya makabati, bora tukae kimya maana lazima tutaumbuka mbele ya safari.
 
ybf1979.jpg


Huyu tena nani anayeneemeka kuwatumikia wananchi wa bara la AFRIKA huko uthunguni?
 
Tatizo la kusoma ughaibuni kukulia huko huko unarudi home kutaka vyeo, unapokosa cheo ndo unaanza kusoma historia ya tz.,
mambo ya zamani unayakumbuka leo,
mbona kuna mengi tu yaliyotokea baada ya Iddi amini dada.

Hayo ambayo yalitokea baada ya Amin ni positive au negative?! Kama ni negative, sina haja nayo kwavile mengi nayafahamu; angalau kwa kusoma kupitia kwenye historia zisizopindishwa. Kama ni positive, kwa maana ya mambo mazuri kabisa; basi tushushie nondo hapa!!! Mie nipo katika kujifunza....!
 
I hope hii haikuwa ni awamu ya kwanza maana awamu ya kwanza. mambo mazuri yalianza baada ya awamu ya kwanza kuisha

Sahihisho: (Dag hakuwemo hapo)

Dag Hjalmar Agne Carl Hammarskjöld (29 July 1905 – 18 September 1961) was a Swedish diplomat, economist, and author. The second Secretary-General of the United Nations, he served from April 1953 until his death in a plane crash in September 1961. He is one of four people to have been awarded a posthumous Nobel Peace Prize.Hammarskjöld remains the only U.N. Secretary-General to die in office, and his death occurred en route to cease-fire negotiations. American President John F. Kennedy called Hammarskjöld "the greatest statesman of our century".
 
Acha upotoshaji usio na tija. Nani amesema Waganda hawakuwa na ruhusa ya kurudi kwao?! Ninachosema ni Waganda katika sura ya uanajeshi walioingia Uganda kutokea Tanzania na kwenda kufanya jaribio la mapinduzi na baada ya kushindwa kwa jaribio hilo wakarudi tena Tanzania. Kwa maana nyingine ni kwamba Tanzania ilihifadhi Waganda wanajeshi waliokuwa na lengo la kuipindua serikali ya Amin. Hilo halikubaliki hata kidogo….!!Suala la Tanzanaia kujihusisha na harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika ni suala lililokubalika kisheria. Na usizani kwamba Tanzania ilikurupuka tu from nowhere na kujiweka mbele kwenye suala la ukombozi bali Tanzania ilikuwa ndo Makao Makuu ya Kamati ya Ukombozi ambayo ilikuwa chini ya OAU ambao kama sikosei ilikuwa au iliwahi kuongozwa na Gen. Hasheem Mbita. Hivyo basi suala la Tanzania na ukombozi kusini mwa afrika ilikuwa ni kutekeleza wajibu wake kama Makao Makuu ya Kamati Ya Ukombozi na ndio maana wapigania uhuru kutoka nchoi mbalimbali walipewa hifadhi hapa na kuruhusiwa kuendesha harakati za ukombozi kutokea hapa.

Na kuhusu kama uwepo wa Amin Kampala ilikuwa salama kwetu jibu ni kwamba ilikuwa salama hadi pale Tanzania ilipoamua kuitumia ardhi yake kama uwanja wa mafunzo wa watu waliokuwa wanampinga Amin. Maswali mengine uliyohoji sidhani kama yana msingi....!!!

Kwa sababu umeamua kujifumba macho ili usione naomba kumalizia kwa kusema kwamba, Cha msingi ni Kwamba alichokitaka Mwalimu kuwa kilikuwa, Idd Amin Aliondoka Kampala, Full Stop na baada ya hapo kama ni kweli baadhi yenu mnavyosema humu ndani kwamba alikuwa anasukumwa na dhamira ya kidini, basi pia ikawa hivyo chokochoko za viongozi au mataifa yanayoongozwa na viongozi wenye msimamo wa kiislamu nazo officially alizizima.
 
Kama nchi Tanzania tulikuwa na kila sababu ya kumchapa Nduli...

Kama alivyosema Mwalimu, "Sababu tunazo, nia tunayo na uwezo tunao." hakukuwa na sababu yoyote ya kumuacha Nduli achezee mipaka ya nchi yetu na kuwaua Watanzania ambao hawakuwa na hatia kila alipojisika kuvamia nchi yetu na Tanazania kama nchi kufumba macho na kuacha Watanzania wadhalilishwe kiasi kile.

RIP Mwalimu.
 
Facts about Uganda-Tanzania war

1. Source na mchokozi alikuwa Nyerere

2. Nyerere hakupata support ya wanachama wa OAU

3. Ilikuwa tabia ya Tanzania kuvamia nchi zingine, kabla ya hapo waliivamia Seychells..na OAU walikuwa kinyume na Tz.

4. Idd Amin hakuwa katili kama ilivyosemwa sana,leo kawalize waganda

5. mpaka 1983 USA walikuwa wanunuzi wakubwa wa kahawa uganda!

6. Idd Amin alifanyiwa ugadafi kwani alikuwa Lulu ya waafrika, mtu mwenye mind yake mwenyewe na asiyeogopa wamagharibi

7. leo hii Tanzania bado inaidai uganda kwa kumwondoa amin madarakani!! why?

8. Obote alijitayarisha kumpindua Amin akiwa Tanzania na Amin alimuwahi na kagera ilikuwa tu funika funika ukweli Nyerere alikuwa anaamuliwa amtoe kipenzi chake

9.athari za ile vita hazitaondoka Tanzania mpaka Uganda imalize deni!!!! mpaka sasa Uganda imeishailipa Tanzania Bilioni 120 Sh. zilizolipwa mara ya mwisho mwaka 2007

10. Tanzania ndio iliyomweka Lule awe rais na si Obote, kwani alikataliwa katakata na wananchi wake!

11. Ukiwa uganda slogan ni..Amin ameua elfu, Obote ameua makumi elfu...Museven ameua mamilioni! kupitia swaiba wake Kony!!

12. Idd Amin alimwona Nyerere kama mwanamke mrembo simply kwa sababu ya uwoga na kuelemea sana nchi za magharibii! ambao walipelekea Nyerere alazimishe muungano wa Zanzibar na Tanganyika, mmoja wa watu waliomdhihaki Nyerere ni Amin!!!

13. Kulikuwa na room ya mazungumzo kuzuia ile vita...kwa nn Nyerere hakuruhusu?



..............................


.............................

Hayo hapo ni NILIYOYAONA baada ya kupitia mapitio mbalimbali, movie mbalimbali, ikiwemo Last King of Scotland, nimeishi Uganda ikanifanya niwe na interest zaidi ya kumjua huyu jamaa......

ukweli ni kuwa donors wetu hawakutoa hata senti tano kusaidia ile vita

Ukija kwenye ulingo wa research na intelectualism...bado wanasema kuwa KULIKUWA NA MIXED MOTIVES AFTER 8 YEARS OF BAD RELATIONSHIP YA TZ na UG.......

Ukija kwa wataalamu wa vita wanasema ilikuwa ni.....just war... WAR WAS MORALLY LEGITIMATE !!!

Ukija kwa Humanitarian watasema..why forces when we had opportunity ya kuongea nao

MY TAKE ITABAKI KUWA ....KAMA WEWE UNGEKUWA NYERERE AT THAT TIME, UNGEFANYA NINI?? Yes alimtetea rafiki yake ambaye walikuwa wasocialist lakini mwisho wa siku what would you do??




Pili shutuma za kutaka kupinduliwa na kambona na uvamizi wa kusini (msumbiji na kaskazini uganda) mwaka 72 na ambazo zilizosababisha Nyerere na Obote watengeneze Guirreilas wars sio siri ni ukweli mtupu uliomfanya Nyerere amalize mzizi wa Fitina mwaka 1978...

Huwa nasikia kichefuchefu mtu anapomtetea Nyerere kana kwamba ni mtume au malaika, this could be stupidity hasa unapompenda marehemu ambaye alikuwa mtu na alikosea sana

Nyerere is not and will never be a saint. Huwa nawaambia uwa Nyerere atajitetea yy mwenyewe, maan wa kizazi chake watakufa na maswali ya aina hii yataulizwa tu....andikeni vitabu mapema kuweka kila kitu sawa ila historia itasimama tu!

KWA HIYO KULIKUWA NA MIXED MOTIVES.......... KWENYE ILE VITA SAWA WILLY?

NINGEKUWA NYERERE NINGEFANYA KAMA YEYE TU-simply kwa sababu na mimi nataka kuheshimiwa, selfish, na hidden motives nyingi tu...why think of my citizen, tell them anything they will agree!!!! life is too short to wait for chances that will show who you are!!! especially when I take country as my house



ATAKAYESOMA HII PAPER HAPA CHINI ATAPATA MTAZAMO MPYA, KWANZA KUJUA IN DEEP, PILI SABABU TATU THEORIES MBALIMBALI.....za vita na ukweli.......Napenda paper za style hii ambazo ni well reserached, haziko biased na tatu ni educative


sipendi ubishi nionekane nampenda Nyerere au simpendi Nyerere ...factz ni nzuri sana, zinakuweka huru muda wote!! I will always take him as just anothe human who was stonger in things he stood for and weaker in the things he failed!!



http://www.unomaha.edu/itwsjr/ThirdXII/AchesonBrownTanzaniaVol12.pdf
 
W. J. Malecela,

Nadhani ulikuwa kijana Mzima Mwenye akili timamu wakati wa Matatizo kati ya Tanzania na Uganda, kama unakumbuka wakati huo East African Community ilikuwa hai, lakini Idd Amini bado alikuwa anafanya Mashambulizi ya hapa na pale Maeneo ya Mutukula, Maeneo hayo Wananchi ni Wakulima na pia ni Wafugaji, walijuwa wanashambuliwa na kuchukuliwa Mifugo yao au Mashamba yao kutibuliwa na Vifaru au saa nyingine wanajeshi wanavuka Mpaka wanafanya vitisho na kuondoka.

Na unakumbuka Nyerere alikuwa hafanyi chochote, Idd Amin alikuwa anamwita Nyerere Mwanamke wake, na Unakumbuka wakati mmoja alikuwa kwenye Ulingo wa boxing akasema atafungwa Mkongo wake wa kulia na Macho atatumia Mkono wa kulia kupambana na Nyerere ulingoni na bado atampiga mpaka atamuua.

Alikuwa na Kejeli nyingi, Sasa Idd Amin hakuwa mtu mzuri kwa Wananchi wake aliua karibia watu 400,000 nchini kwake tu, baadhi ya miili ya watu wake aliila.

Sasa Makamu wake wa Urais aliyeitwa General Mustafa Idrisa, alipata ajali ya Gari ya kiajabu ajabu na Unajua Idd Amin alikuwa na kawaida ya kuuwa wapinzani wake kwa kawaida za ajali ya Magari, General Idrisa alikuwa anaongoza Elite Battalion iliyokuwa inaitwa Simba Battalion, Simba Battalion commando wakakimbia wakavuka Mpaka wa Uganda wakaingia Tanzania.

Idd Amin aliposikia hayo hakufurahishwa na alisha kuwa anaivamia Maeneo ya mara kwa mara kwahiyo akaenda akaivamia tema Mutukula na kuichukua na kuweka Bendera ya Uganda na kutangaza kuwa hiyo Sehemu ni Mali ya Uganda akaitembelea aliporudi Kampala akatangaza Vita dhidi ya Tanzania.

Tanzania ikaenda OAU, wakagoma kuongelea hiyo issue na pia kugoma kumuambia Idd Amin arudishe ardhi ya Tanzania, akapeleka UN na unakumbuka wakati huo Rais alikuwa Jimmy Carter alisha wekea Uganda visingiti vya kiuchumi, UN hawakuongelea ombi la Tanzania; OAU sababu haikuongelea ombi la Tanzania ni kwa Sababu Nyerere aliunga Mkono Mapinduzi ya Sychelles iliyomweka Madarakani Albert Rene.

Kwahiyo, Ilibidi ipigane imuondoe Nduli Idd Amin kutoka Mutukula na pia Uganda sababu hakuna Msaada toka mataifa yoyote, ndio bila vita uchumi wetu ungekuwa bora zaidi ya nchi yoyote Africa, ndio tulinunua silaha kwa bei za rushwa yaani Mara mbili ya bei ya kawaida na ndio iliyotutupa kwenye Umasikini na kumfanya Nyerere kujiuzulu kuliko kupokea machungu ya IMF na World Bank; Yeah Uganda ilitulipa kidogo kidogo walimaliza deni 2007.

Kuhusu Obote, Nyerere hakuikomboa Uganda Sababu ya Obote, Nyerere alimpenda sana Yusuf Lule awe Rais wa Uganda, lakini wakati ule wananchi wa Uganda bado walikuwa na kumbukumbu na Obote alivyokuwa kiongozi bora, hawakujua baada ya miaka mingi uraiani amejenga maadui wengi mmoja wao ni Yoweri Museveni walikuwa wanaongea Mjini Moshi lakini Obote alikuwa na chuki ndani kwa ndani.

Kwahiyo Nyerere hakuikomboa Uganda kwa sababu ya Obote; ni kwa Manufaa ya Watanzania; Wananchi wa Uganda ndio waliomchagua Obote.
 
Last edited by a moderator:
sio wewe hata mi nimejifunza mengi saana, ila nimeugundua Kuwa negative side Nyerere inafichwa sana Sijui kwa nini but he also a failure in some areas
Pukudu,

Sidhani kuwa ni kweli kuna kuficha negative side.

Ili mtu athibitike kuwa ni mhalifu ni lazima yawepo madai, yathibitike bila shaka na hukumu itolewe.

Kinachotokea katika baadhi ya thread ni 'short cut'. Nyerere anaandikiwa shitaka la neno moja bila kujengewa hoja. Hukumu inatolewa hapo hapo. Hii inafanywa kwa nia na makusudi mengi. Wapo waathirika wa siasa za Nyerere,wapo wanaodhani ili wapande daraja lazima wazue uongo n.k. Hicho ndicho wengine wanakipinga na wala si kuficha historia

Mfano, utasoma thread, Nyerere alishiriki mauaji ya Lumumba, Nyerere alikuwa chanzo chamauaji ya kimbari Rwanda na Burundi, Nyerere hakuwapenda wasukuma na waanglikan n.k. Kwa bahati mbaya haya yote hayajengewi maelezo ya kina ila yanahitimishwa kwa maneno 'policy zake zimeshindwa' ni 'mtu mbaya sana' n.k.

Well,hata ikiwa kuna ukweli lakini basi onyesha ukweli ulipo kwanza halafu toa hukumu kulingana na ukweli.

Unaongeleaje vita ya 1978 bila kuangalia mlolongo wa matukio tangu mwaka 70, 72 n.k.?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mkandara
Waganda hawakuwa na mapenzi na Idd Amin walikuwa na hofu wakati wa utawala wa Amin ilikuwa ummpende yeye ama uuliwe; Amin alishajijengea utamaduni wa kuua wapinzani wake aliauwa mamia ya askari wanye kutoka makabila ya Acholi Lango, aliuuwa Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana, gavana wa benki kuu, waziri wake mkuu; kwa ujumla waganda walitawaliwa na hofu na si mapenzi.

Chama
Gongo la Mboto DSM
chama,

Nalewa sana lakini kama utajiingiza ktk siasa za kumpinga. Ukiwa mwananchi huru unayetaka kuibadilisha nchi toka fikra za kutawaliwa na kuabudu wageni lazima ungepmenda Idd Amin na hata Ghadaff. hawa watu walionekana wabaya kwa sababu sii rahisi kumlazimisha mtu kutofanya mabaya. Leo hii ukiweka sheria ya kwamba hakuna kijana (teenager) ambaye yuko shule anaruhusiwa kufanya ngono utaonekana Dikteta na wananchi wako kuiihsi kwa woga japokuwa wote hawa wanakubaliana na hoja ya kwamba vijana wadogo na ngono huwapotezea muda wa kuelimika.

Kwa hiyo Idd Amin aliwaendesha waganda kwa sababu kwanza hakutaka kabisa kusikia Ufisadi, hakutaka kusikia udhoofu wa kiongozi ambaye kaomba madaraka kisha akayachezea. Yule Askofu naye kosa alofanya ni kuingilia siasa kama wanavyofanya viongozi wetu wa dini nyumbani. Unajua wapo viongozi hawawezi kubeba shutuma hizi zinapojaribu kujenga Udini ama Ukabila. Mwa mfano Kagame amepiga marufuku kabisa mijadala inayozungumzia vita ama chuki baina ya Wahutu na Watusi ukionekana unatiwa ndani, sasa nadhani ni vizuri kwetu sisi kuelewa anachokifanya.

Hata Marekani kwenyewe miaka ya 60 hadi mwanzo wa 80s ilikuwa marufuku kuonekana na kitabu, gazeti au nyaraka zozo te za Ukomunist na ukionekana unatiwa ndani. Hivi sasa maswala ya Alqaeda ukiwa support unaitwa gaidi. Mbali na hivyo wapo watu walofungwa maisha kwa kutetea Ukomunist wakati ule, hivyo inategemea na malengo ya nchi, ukikiuka malengo hayo sheria inafanya kazi yake bila kujali wewe utatafsiri vipi.
 
Last edited by a moderator:
Zakumi,

Let me help our friend Chama in one aspect. It is true that Amin's army was better equipped. But his army was basically mechanized. That meant the vifarus had to go on tarmac while our infantry was on foot and could fight in matoke farms.

Actually that is what happened to the Libyans. While they depended on tarmac roads we were able to ambush them from the bushes. Most of the military equipments brought in by Libyans were captured by us.
Jasusi,

I will be back with data. Let me read some materials.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mkandara;
Amin alikuwa ni Dikteta wapo wachache ambao walinufaika na utawala wake hao lazima walimpenda; lakini mganda wa kawaida hakuna aliyempenda na hii ndio ilichangia anguko lake kirahisi; hofu iliwatawala waganda; hata kama kiongozi unapingwa na viongozi wa dini tendo halijustify uwauwe wapinzani wako. Hivi Mkandara inakuingia akilini kusema Askofu alifanya kosa kukemea mauji yaliyokuwa yakifanywa na Idd Amin?

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Waberoya;
Baada ya kuisoma link uliyoweka Nyerere hakuwa na kosa vita ilikuwa sahihi; ukweli hakuna cha ajabu aliyoyafanya Nyerere ndiyo yanayofanyika sasa hivi; ni kweli vita vimetutia gharama bali gharama ya kumwacha Amin abakie madarakani ingekuwa kubwa zaidi. Ni raisi mpumbavu tu ndiye angeweza kumvumilia Amin.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Mkuu Mkandara;
Amin alikuwa ni Dikteta wapo wachache ambao walinufaika na utawala wake hao lazima walimpenda; lakini mganda wa kawaida hakuna aliyempenda na hii ndio ilichangia anguko lake kirahisi; hofu iliwatawala waganda; hata kama kiongozi unapingwa na viongozi wa dini tendo halijustify uwauwe wapinzani wako. Hivi Mkandara inakuingia akilini kusema Askofu alifanya kosa kukemea mauji yaliyokuwa yakifanywa na Idd Amin?

Chama
Gongo la Mboto DSM


Uganda imekaa kikabila sana, kuna kanda watampenda na kuna kanda watamchukia!! Lakini issue ya kuwa alikuwa dictator ilikuwa published sana na waingereza. Nenda kwao kaskazini mashariki sema hayo uliyosema utashangaa utakavyotukanwa mkuu!!


Idd Amin hakuwapenda na hakuwa tayari kuwafuata wazungu na ndio siri ya kuitwa hivyo, alichofanya idd amin ni sawa kabisa na viongozi wengine wengi wa kipindi kile..miaka ya 60,70

It will interest you even Nyerere some publications called him dictator!!


Nyerre had a deep passion for change and hatred toward imperialism. He helped to lead his country to independence in the late 1950's, early 1960's, laying a foundation for his country even before he became official president and dictator. Julius Nyerere- Tanzania


The death of Julius Nyerere, African independence leader and longtime dictator of Tanzania, evoked a flood of encomiums worldwide. The praise is misplaced. Nyerere's approach devastated much of postcolonial Africa (Forbes, 1999).
http://archive.lib.msu.edu/DMC/African%20Journals/pdfs/political%20science/volume8n1/ajps008001004.pdf



Nimekupa mifano tu mkuu, nimekaa uganda na ninaweza kukueleza mengi ya huko, Stop calling Amin a dictator, just because you studied that in history does mean so!! just because western propaganda it does mean so!! waingereza ndio walimuita sana Amin baada ya kuwafanyia yale mambo!!! USA at that very time mnamwita amin dicator bado walikuwa na mahusiano mazuri sana ya kibiashara, please find in literature!!






 
Waberoya;
Baada ya kuisoma link uliyoweka Nyerere hakuwa na kosa vita ilikuwa sahihi; ukweli hakuna cha ajabu aliyoyafanya Nyerere ndiyo yanayofanyika sasa hivi; ni kweli vita vimetutia gharama bali gharama ya kumwacha Amin abakie madarakani ingekuwa kubwa zaidi. Ni raisi mpumbavu tu ndiye angeweza kumvumilia Amin.

Chama
Gongo la Mboto DSM

sawa nashukuru kama umeielewa
 
Kwa sababu umeamua kujifumba macho ili usione naomba kumalizia kwa kusema kwamba, Cha msingi ni Kwamba alichokitaka Mwalimu kuwa kilikuwa, Idd Amin Aliondoka Kampala, Full Stop na baada ya hapo kama ni kweli baadhi yenu mnavyosema humu ndani kwamba alikuwa anasukumwa na dhamira ya kidini, basi pia ikawa hivyo chokochoko za viongozi au mataifa yanayoongozwa na viongozi wenye msimamo wa kiislamu nazo officially alizizima.

Watu wote wasio na hoja ukimbilia kwenye hoja mbovu kama hizo za udini....!!! Huo ndo upofu wa watu wasio na hoja za msingi na badala yake kukimbilia kujificha kwenye hoja zinazochefua kama hizo za udini. Unavyosema "baadhi yenu" ina maana nami ni mmoja wao...hebu onesha angalau mstari wangu mmoja achilia mbali post mzima ambayo nimehusisha suala la udini kama msukumo wa Nyerere. Ni aibu, narudia ni aibu...kukosa hoja halafu kukimbilia kwamba huo ni udini, chuki na upuuzi mwingine kama huo. Narudia, onesha angalau mstari mmoja ambao nimehusisha na suala la udini.
 
Back
Top Bottom