Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Katika vita vya silaha taifa la Marekani limetia hasara kubwa maeneo mengi duniani na hawajawahi kushinda hata sehemu moja.
Wamepigana Afghanistan na hatimae wakashindwa na kukimbia mbio nyingi.Iraq nako ni kama hivyo.Libya mpaka balozi wa Marekani aluliwa ubalozi wao ulipochomwa moto.
Ukienda Ukraine na Gaza pamoja na silaha nyingi za teknolojia za kisasa kupelekwa hakuna mafanikio yoyote zaidi ya aibu na kufilisika.
Upande wa Venezual na Korea kaskazini na Iran ni maneno tu lakini hawana wanachoweza kufanya kuondosha tawala hizo.Hata upande wa Syria yule raisi mzembe Bashar hawakuweza kumng'oa mpaka wasyria wenyewe walipofanya hivyo.
Sasa Trump amerudi madarakani na wazimu wake wa vita vya kibiashara ambavyo inaonekana havijali marafiki na washirika wake wala majirani pia.
Marekani imeshaanza vita vya kibiashara na Canada na Mexico ambao ni majrani inayopakana nao.Wote hao wamekaza kamba kama Hamas hawajaonesha nia ya kukimbia.
Korea kusini na Japan nao ambao ni washirika na wapambe wakubwa wa Marekani wameanza kulalamikia vita vya kibiashara vya Trump wakisema na wao vitawaathiri kama vitaendelea kwa kasi hii.
Nchi za Ulaya ni wapambe wakubwa na wa miaka mingi wa Marekani kupitia NATO.
Raisi Donald Trump amesema hata Europe nayo itapata sehemu yake ya vikwazo vya kiuchumi isipokuwa Uiengereza tu.