Natty Bongoman
JF-Expert Member
- Oct 10, 2008
- 403
- 191
waUkraine na waRus wameishi pamoja kwa amani hadi mshinikizo wa mmarekani na wenzake wa ulaya magharibi - wakaanza kubeza na kuwaonea waRus tokea 2014 kiukatili sana... waUkraine (viongozi) na washinikizaji hadi wakaruhusu kundi la NATIONALIST (wabaguzi wenye itikadi za hitler) kuchochea ubaguzi, ukatili na kutenda matendo mabaya...
Umetambua vile hawatuambii kuhusu hii jamii kubwa ya asili ya kirusi nchini Ukraine? Kwa sababu inatuonyesha kumbe mrusi ana sababu nzuri za kuingia Ukraine.
Siamini waUkraine walio wengi wanakubaliana na siasa za Zelensky akishirikiana na wamagharibi na kundi la kina Hitler. Hitler alitesa na kuua waUkraine wengi vita vya 2 vya dunia - hadi mrusi alipomwaga damu nyingi kuwakomboa. Haileti mantiki raia walio wengi Ukraine wakawa na moyo wa kuwageuka warusi kama tunavotangaziwa na wamagharibi. Mbona karibu nusu nchi ni wa asili ya kirusi? Ni porojo na propaganda tunatangaziwa na wamagharibi ili tuingie mkenge. Wananchi walio wengi Ukraine wamekuwa wanawaogopa wale wanajeshi vichwa hitler manake wameumiza na kuua wapinzani wa sera zao. Kwa hiyo kupiga kelele nchini Ukraine wanaogopa sio kwamba wanaunga mkono kindakindaki.
Putin aliomba mazungumzo, akaonya, wakasaini MINSKY mkataba lkn viongozi wa Ukraine kwa shinikizo la wanje wakaubeza mkataba. Kila majaribio yalivofeli, na vile Putin anajua wanje hawawajali waUkraine ila wanajali kupata nchi ili wawe karibu na adui yao mrusi - kaamua kutatua tatizo pia kukomboa warusi.
Je Putin ilitakiwa asitetee wananchi wake? ana makosa gani?
Je raisi wa Ukraine hana makosa kukubali uchochezi, kuruhusu waasi wa kihitler kuwa wanajeshi na mdomo wake kuwaonea warusi nchini Ukraine?
Mimi naona Zelensky alikuwa mjinga kusahau historia yao na warusi na kukubali kushawishika kijinga
Je huyu raisi
SABABU KUU NAHISI:
- mafreemason lengo kuu ni kutawala dunia ya serikali na itikadi moja, kisia ni ipi inayosukumizwa dunia nzima siku hizi. Mrusi na mchina ni vikwazo kwa sababu ili lengo litimie inatakiwa wabaki wababe pekee yao.
- kuna hasira za kuboronga na kushindwa kule Afghanistan, Syria, Iraq, Iran, .... kwa sababu ya mrusi kwa njia moja ama nyingine.
- waliamua labda kipumbavu kwamba mrusi hana nguvu ama atatulia tu baada ya urusi kubwa kuvunjika... walimkadiria ovyo putin... katoa jibu ambalo hawakutegemea na sasa kwa sababu za sifa na ujeuri hawatakubali kushindwa bila kuvuruga sifa za mrusi duniani... vita vya propaganda ndio silaha waliobakiwa nayo