Putin mwenyewe alitumia hadaa ya "special operation", kama tujuavyo special operation huwa shughuli ya siku chache, unapiga mabomu kwenye maeneo ya kimikakati kisha unatimiza lengo lako na kugeuza, kwa mfano angeishia kumega maeneo yanayomuunga mkono kisha maisha yaendelee.
Lakini badala ya special operation, amefanya full-scale military invasion, hata wanajeshi wengi wa Urusi walipigwa na butwaa maana hawakutegemea iwe hivi, waliokamatwa wote wanasema hilo moja kwamba hawakua wameandaliwa kisaikolojia wanakwenda kuvamia Ukraine mazima mazima, na kunao wanalia sana.
Uvamizi huu ungefaulu pakubwa kama rais wa sasa wa Ukraine angekua bonge la dikteta, wananchi wangepokea wanajeshi wa Urusi kwa vifijo na nderemo, ila sasa kidemokrasia Ukraine inaizidi Urusi, hivyo hapa inabidi kupambana dhidi ya raia wa Ukraine na wanajeshi wake. Unapovamia nchi inayotawaliwa na dikteta huwa rahisi, kwa mfano Tanzania ilipovamia Uganda, Waganda wengi hawakua wanamtaka Id Amin, walishukuru sana na kuna wengi walijiunga kwenye mapambano wakiwemo maelfu ya waasi waliokua wanaongozwa na Museveni na Tito Okello.
Putin kwenye huu ugomvi utamgharimu sana nje na nyumbani, pia ikumbukwe Ukraine na Urusi wana undugu, sio rahisi kwa wanajeshi wa Urusi kujitolea kizalendo hadi kufa kama walivyofanya dhidi ya Hittler. Ni kama leo hii Tanganyika iwatume wanajeshi kuvamia Zanzibar wafanye mauaji huko, wale Wazanzibari asilimia kubwa ukiondoa Waarabu, wengi ni Watanganyika waliovuka maji aidha enzi za utumwa au hivi majuzi, kila Mzanzibari mweusi ana asilia ya Tanganyika, utakuta ukifuata ukoo wake palipo makaburi ya mababu zake utakuta ni huko Unyamwezini, Usukumani n.k.
Urusi leo hii imepoteza hadhi hata kwa mataifa ya Uarabuni ambao hununua sana silaha zake, wengi wapo kimya wakishangaa hii aibu.