Vita vya Ukraine; Wasichotuambia wazi

Elimu yote unayotoa hapo, imetokana na huyo aliyechora ramani ulizoweka. Sijui kama umeangalia maoni ya mchora ramani mwingine.
 
Elimu yote unayotoa hapo, imetokana na huyo aliyechora ramani ulizoweka. Sijui kama umeangalia maoni ya mchora ramani mwingine.
ndio, nimeweka zaidi ya ramani moja. Pia unaweza kugoogle zipo nyingi jibu lile lile
 
Vita sio suluhu, angeunda kikosi maalum cha intelijensia alafu akaharibu siasa za ukraine na kumuweka madarakani raisi wanaemtaka..ikibidi mrusi, ingechukua muda lakin angefanikiwa pakubwa sana...
Sasa hiv mambo magumu huko, askari wake wanakufa..vifaa vinaharibika..hasara tupu
 
sioni hili kufanyika siku mbili na jeshi lolote... Ukraine sio nchi ndogo
 
Kwa kweli mrusi kaonya na kuomba maongezi kwa miaka mingi, hadi kupata mkataba wa minsky ambapo kavumilia akiuona unabezwa na kuvunjwa. Sidhani alitaka vita kwanza kama suluhu
 
Kwa kweli mrusi kaonya na kuomba maongezi kwa miaka mingi, hadi kupata mkataba wa minsky ambapo kavumilia akiuona unabezwa na kuvunjwa. Sidhani alitaka vita kwanza kama
Angeunda kikosi akaweka raisi wake pale, mbona wenzake wamefanikiwa kumuweka zelensky,
Unaweka mgombea..
Unahack mifumo ya uchaguzi..
Mgombea wako alishinda, unaweka warusi kwenye system pale ukraine, mchezo umeisha
 
Kwenye mapambano ya ndani ya miji (towns) tayari askari wa Putin wanapokea kipigo cha haja, ndo sababu Putin anakodisha wapiganaji mamluki toka Uarabuni!!!


 

Hata atume wa wapi, huko wanakwenda kwenye machinjio, hamna kitu cha hatari uingie kwenye nchi ya watu ili uviziane nao kwenye mitaa yao, gheto zao...mbona mtakufa sana. Mitaa ambayo wenyeji hata wakifumba macho usiku wanajua pakuingilia na kutokea....
Unapishana na muuza nazi na maembe kumbe ni mjeda kwenye guta lake ameficha kifaa cha kubomoa kifaru.

Mmarekani vita vya Vietnam vilimshinda kwa ajili ya hili, walikua wanapita wakulima wakiwa kwenye shughuli zao za upanzi, ghafla hao wakulima unashangaa kila mmoja ana AK-47 mkononi wanafyatua risasi na makombora.
 
Ni mtoto mdogo tu anayeweza kufikiri kuwa Mrusi angemaliza mchezo kwa siku tatu!! Kumbuka kuwa Marekani akisaidiwa na nchi za ulaya Magharibi alishindwa kabisa kumaliza mchezo dhidi ya Taliban kwa zaidi ya miaka 15, hadi kuamua kukimbia!! Marekani alivamia Syria hadi leo ana kambi zake za kijeshi huko lakini ameshindwa klabisa kumaliza mchezo dhidi ya Rais Saad wa Syria takriban miaka 10 sasa!! Marekani na washirika wake wa NATO (isipokuwa Ufaransa) walivamia Iraq ya Sadam Hussein na hawakuweza kumaliza mchezo kwa miaka kadhaa japo baada ya miezi kadhaa Sadam Hussein aliuawa. Jaribu kuuliza Marekani alipoteza askari wangapi Iraq, Syria, Afghanistan nk. Huko mbali hata hapo Somalia!!
Kwa hiyo ni mtoto mchanga tu anayenyonya ndiye angeweza kudhani Urusi angemaliza mchezo kwa siku 3.
 
sioni hili kufanyika siku mbili na jeshi lolote... Ukraine sio nchi ndogo
Achilia mbali Ukraine hata Tanzania hapa hakuna anayeweza kuja na kuteka nchi yetu kwa siku mbili!! Kumbuka kuwa ndege na makombora huwa hazina uwezo wa kuteka nchi, bali jeshi la nchi kavu hususan askari wa miguu!! Kwa ngazi ya askari wa miguu hakuna tofauti kubwa ya nguvu na ujuzi miongoni mwa mataifa!! Ujue pia kuwa huwezi kuangamiza askari wengi kwa kutumia ndege na makombora. Hivyo huangamiza majumba, raia na miundombinu lakini si wanajeshi na silaha zao za mkononi!! Wewe piga mabomu lakini wako kwenye mahandaki wanakusubiri uingie mitaani!!! Ndiyo maana Marekani kawashindwa kabisa Taleban hadi kumwaga manyanga mchana kweupe!! Hali kadhalika hata Urusi yenyewe haitegemei kufikia lengo lake la kuipokonya silaha Ukraine kwa siku chacge tu! Hapa ni miezi kadhaa kama siyo miaka kadhaa!!
 
Mlizima channels za Russia ili mtulishe matangopoli. Mmechelewa sana. Nani kakudananya mrusi a apigana vita Ukraine?? Kaishasema mala nyingi tu kuwa anafanya operation ndogo tu ya kijeshi.
 
wewe MK254 nikuulize: Nyie wakenya mlimaliza mchezo wenu na Alshabaab kwa siku tatu?? Hadi sasa ni miaka tayari lakini bado hajamalizana na Alshabaab!!! Utawezaje kudhani kuwa Urusi ishinde vita kwa siku tatu?? Marekani ndiye gwiji la kuvamia mataifa mbali mbali kijeshi katika historia ya dunia, je kuna mahali alivamia na kumaliza mchezo kwa siku 3 (pamoja na kwamba husaidiwa na makoloni yake ya ulaya magharibi)!! Kumbuka marekani ilivyovamia Iraq, Syria, Vietnum, Afghanistan Somalia na kote huko iliambulia kipigo cha mbwa mwizi hadi kukimbia mchana kweupe (mfano wa karibu ni huko Afghanistan alivyowakimbia Taliban!)
 

Putin mwenyewe alitumia hadaa ya "special operation", kama tujuavyo special operation huwa shughuli ya siku chache, unapiga mabomu kwenye maeneo ya kimikakati kisha unatimiza lengo lako na kugeuza, kwa mfano angeishia kumega maeneo yanayomuunga mkono kisha maisha yaendelee.

Lakini badala ya special operation, amefanya full-scale military invasion, hata wanajeshi wengi wa Urusi walipigwa na butwaa maana hawakutegemea iwe hivi, waliokamatwa wote wanasema hilo moja kwamba hawakua wameandaliwa kisaikolojia wanakwenda kuvamia Ukraine mazima mazima, na kunao wanalia sana.

Uvamizi huu ungefaulu pakubwa kama rais wa sasa wa Ukraine angekua bonge la dikteta, wananchi wangepokea wanajeshi wa Urusi kwa vifijo na nderemo, ila sasa kidemokrasia Ukraine inaizidi Urusi, hivyo hapa inabidi kupambana dhidi ya raia wa Ukraine na wanajeshi wake. Unapovamia nchi inayotawaliwa na dikteta huwa rahisi, kwa mfano Tanzania ilipovamia Uganda, Waganda wengi hawakua wanamtaka Id Amin, walishukuru sana na kuna wengi walijiunga kwenye mapambano wakiwemo maelfu ya waasi waliokua wanaongozwa na Museveni na Tito Okello.

Putin kwenye huu ugomvi utamgharimu sana nje na nyumbani, pia ikumbukwe Ukraine na Urusi wana undugu, sio rahisi kwa wanajeshi wa Urusi kujitolea kizalendo hadi kufa kama walivyofanya dhidi ya Hittler. Ni kama leo hii Tanganyika iwatume wanajeshi kuvamia Zanzibar wafanye mauaji huko, wale Wazanzibari asilimia kubwa ukiondoa Waarabu, wengi ni Watanganyika waliovuka maji aidha enzi za utumwa au hivi majuzi, kila Mzanzibari mweusi ana asilia ya Tanganyika, utakuta ukifuata ukoo wake palipo makaburi ya mababu zake utakuta ni huko Unyamwezini, Usukumani n.k.

Urusi leo hii imepoteza hadhi hata kwa mataifa ya Uarabuni ambao hununua sana silaha zake, wengi wapo kimya wakishangaa hii aibu.
 
Tugawane tenda ya propaganda mzee, hata mie uongo nauweza.
 
Yale yalikua makubaliano sio mkataba, mataifa hukubaliana na pia kuvunja makubaliano kila mmoja anabaki na hamsini zake, Tanzania na Kenya ni mfano hai.


Mnapokubaliana inakuwa vipi??
 
Mnapokubaliana inakuwa vipi??

Makubaliano huwa hayana uzito kihivyo, na mataifa mengi duniani yana makubaliano, uruhusu niingize kwako sukari na mimi nitaruhusu uuze kwangu kuku na maisha yaende, tukubaliane usijiunge kwenye muungano fulani ila na mimi kama fadhila nitakulinda au hata kukusaidia kiuchumi.
Sasa ukifika mahali upate ukakasi kwenye hayo makubaliano unayatupa kuleee!!!!!

Mkataba ni tofauti maana mnatia saini kabisa na wanakuwemo mashahidi wa pande zote mbili na humo kwenye mkataba kuna kipengee nini kifanyike pale yeyote atakiuka masharti.
 


Kwahiyo Makubaliano signed ndio mkataba??-- na yale unsigned sio mkataba??, na mkataba ndio wa kuheshimu na makubaliano bila signed na mashahidi hayahitaji kuheshimiwa au hayahitaji malalamiko kabla hayajavunjwa??!!.
 
Kwahiyo Makubaliano signed ndio mkataba??-- na yale unsigned sio mkataba??, na mkataba ndio wa kuheshimu na makubaliano bila signed na mashahidi hayahitaji kuheshimiwa au hayahitaji malalamiko kabla hayajavunjwa??!!.

Umejaza maneno ambayo sijayasema, labda huna uwezo wa kuelewa haya mavitu iwe najisumbua bure.
 
Umejaza maneno mbayo sijayasema, labda huna uwezo wa kuelewa haya mavitu iwe najisumbua bure.
Poleni sana wayuklein kwa kupigwa , Na nyie lipen mashambilizi huko Moscow kwani hamna vifaa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…