Analogia Malenga
Platinum Member
- Feb 24, 2012
- 5,292
- 10,842
Uwekezaji katika uchimbaji wa gesi na mafuta nchini Tanzania utaongezeka kwa Dola Bilioni 10 sawa na tsh. Trilioni 23.2. Awali, Tanzania na kampuni ya uchimbaji mafuta na gesi ili ya Equinor ASA na Shell Plc zilikubali kuwekeza Dola bilioni 30 sawa na Tsh. Trilioni 69.58 ambapo kutokana na mgogoro unaendelea mafuta na gesi vimeadimika hivyo wanatafuta vyanzo vipya.
Tanzania ina gesi zilizoko kwenye mita za ujazo trilioni57. Rais Samia Suluhu Hassan amesema mkataba wa kuanza uchimbaji unaweza kuisha Juni 2022 na uwekezaji ukaanza kwa wakati huo.
Kwa sasa Urusi ni mzalishaji mkubwa wa gesi na mafuta duniani, na kwa sababu ya vikwazo bei za mafuta na gesi zimepanda. Hivyo ni faida kwa Tanzania ambayo ina vyanzo vikubwa vya mafuta na gesi
Hata hivyo watafiti wameonesha Tanzania haiko vizuri kwenye mikataba yake kimataifa na mara nyingi huwa wanaishia kupoteza badala ya kufaidika na mafuta na gesi.
Kwa mkataba huu ambao ni lazima nchi zilizoendelea kuingia na Tanzania ni fursa ya Tanzania kuweka hadidu zitakazomfaidisha badala ya kumtafuna.
Rais amesema wapo katika marekebisho ya sheria ili kuvutia wawekezaji, hata hivyo ni suala muhimu kumuelekeza rais kuwa, kumvutia muwekezaji sio kusamehe kodi kwa wakati huu ambapo Tanzania inaweza kuwa 'Monopoly' na kutokana na ulazima wa mafuta na gesi uliopo.