Vita vya yom-kippur kati ya Israel na waarabu 1973-1

Vita vya yom-kippur kati ya Israel na waarabu 1973-1

Echolima

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2007
Posts
3,824
Reaction score
2,079
Leo inatimia miaka 40 toka vita vya YOM-KIPPUR kuanza vita hii ilianza tarehe 06-10-1973 nchi za kiarabu zilijipanga vilivyo ili tu kurejesha ardhi zao walizopoteza katika vita vilivyovunja record ya Dunia vita vilivyopiganwa kati ya nchi za Ki-arabu na Israel kwa mda wa siku sita Mwaka 1967 na majeshi ya nchi za Ki-arabu kusalimu Amri na kuacha ardhi zao kutekwa na askari wao kwa mamia kupoteza maisha yao na Maelfu kutekwa.

Vita hii iliacha maumivu na makovu makubwa sana katika ulimwengu wa Kiarabu hata kupelekea nchi hizo hasa Misri na syria kuanza mikakati ya kukomboa ardhi zao zilizotekwa na Mjeshi ya Israel,kwa maana syria milima ya Ki-mbinu ya Golan ilikuwa imetekwa na kwa upande wa Misri ilipoteza Jangwa lote la sinai ikiwa pamoja na Mfereji wa Suez nchi hizi zilikuwa na machungu sana hasa ikichukuliwa kuwa nchi iliyowashinda ni ndogo sana hivyo mipango iliyofanywa mwaka 1973 ni kuzikomboa ardhi zilizotekwa baadaye kuifutilia mbali Israel katika uso wa Dunia.

Mipango ya kuivamia Israel ilipangwa ifanyike siku ya Jumamosi ambapo kulikuwa na sikukuu ya Kiyahudi inayojulikana kama YOM-KIPPUR,Siku hiyo Israel ilipata changamoto kubwa ambayo katika historia ya nchi hiyo Kivita haijawahi kutokea, maana siku hiyo Maelfu ya vifaru na Makumi elfu ya Majeshi na ndege za kijeshi zilifanya shambulizi la kushitukiza na kwa pamoja katika mipaka ya Israel ya kusini na kaskazini hii ilikuwa Ishara tosha kuwa Syria na Misri zilikuwa zinataka kurudisha ardhi zao zilizotekwa katika vita vya siku sita vya mwaka 1967.

CHANZO CHA VITA YA YOM-KIPPUR.
Baada ya Israel kushinda vita vya 1967 Israel ilipata ardhi kubwa ambayo ilipaswa kulindwa kwa gharama yoyote ili kupata Muafaka wa kisiasa kati ya nchi hiyo na nchi za Kiarabu kwa upande wa Misri Israel ilichukua Sinai na Suez canal hivyo Jeshi la Israel lilipata changamoto kubwa sana kulinda mpaka wote wa sinai na Mfereji wa Suez,Majeshi ya Israel yaliweka vituo vya ulinzi vilivyojulikana kama BAR-LEV line,na kwa upande wa Syria Israel ilichukua Milima ya Golan ambayo kwa Israel lilikuwa eneo jipya lililotakiwa kulindwa kwa nguvu zote maana Ki-Jeshi lilikuwa ni strategic la kimbinu sana Maana milima hiyo ya Golan iko kwenye mwinuko kwa hiyo eneo hilo likishikiliwa na Syria ina maana Majeshi ya Syria yana Uwezo wa kumiliki Kijeshi ndani ya Israel kilomita zaidi ya 25 na wakati huohuo Israel haingekuwa na uwezo wa kupata target Shabaha nzuri kupiga majeshi ya Syria yaliyoko kwenye milima hiyo ya Golan na ndiyo maana mpaka leo Israel haiwezi kuiachia milima hiyo maana kufanya hivyo ni sawa na kujitoa MHANGA kwa jeshi la Israel,Badala yake Inataka kuirudisha milima hiyo kwa kubadilisha na AMANI na Syria ili wawekeane mkataba wa AMANI na kutoshambuliana na Israel ili iweze kupata uhakika wa kutoshambuliwa toka milima hiyo ya Golan.

Baada ya vita vya 1967 Msri na Syria zilianza kujenga majeshi yao ili waweze kukomboa ardhi zao zilizotekwa, Nchi hizo zilihitaji zana za kivita zaa kisasa ili kuweza kummaliza adui yao Israel walihitaji sana kupata silaha toka Urusi wakati huo USSR Walihitaji kupata Ndege aina ya MIG na vifaru aina ya T-62 Vilevile makombora ya kuangushia ndege aina ya SA-2,3,6 na SA-7 pamoja na silaha za kubomolea Vifaru aina ya SAGGER ANT-TANK GUIDED MISSILES.

Kufikia mwezi October 1972 Rais wa misri wakati huo Anwar Sadat aliwahi kuongea na makamanda wake kuhusu kuishambulia israel na ilipofikia mwezi may 1973 vyombo vya kijasusi vya Israel vilikuwa vimepata habari kuwa Misri itaishambulia Israel kupitia mfereji wa Suez Misri walikuwa wanajua kuwa kama Misri itaishambulia Israel basi Syria nayo ingejiunga na kuishambulia Israel kutokea Kaskazini. Vilevile Israel walidaganyika kuwa Misri itaishambulia Israel mara tu itakapopokea ndege aina ya MIG-23 na SCUD-D toka Urusi Jeshi la Israel lilijua kuwa Misri haijapokea silaha hizo toka Urusi hivyo iliamini Misri haiwezi kuanzisha vita hivyo kabla ya kupokea silaha hizo toka Urusi.

Mwezi May na Mwezi August 1973 Majeshi ya Misri yalifanya mazoezi makubwa ya kijeshi katika eneo la mpaka na Israel,Israel nayo ilipoona hivyo ilianza kukusanya askari wake kwa maandalizi ya vita lakini baada ya pale hakukuwa na harakati zingine za kijeshi katika eneo hilo la mpaka hivyo Jeshi la Israel liliona kuwa hiyo ilikuwa kawaida tu yaani waliona kama yalikuwa mazoezi ya kawaida tu.

Septemba 25,1973 Mfalme hussein wakati huo alikutana na waziri mkuu wa Israel wakati huo Mama Gold Meir wakati huo Mfalme Hussein alishakutana na Rais Sadat na Assad wa Syria na alimwonya waziri mkuu wa Israel kuhusiana na kukalia eneo la Syria la milima ya Golan na Sinai eneo la Misri,Baada ya kumalizika kikao hicho na Mfalme Hssein waziri mkuu wa Israel pamoja na waziri wa ulinzi wa Israel wakati huo MOSHE DAYAN pamoja na vyombo vya Kijasusi vya Israel waligundua moja kwa moja kuwa Misri ingewashambulia wakati wowote.

Masaa machache tu kabla ya Misri kuishambulia Israel tarehe 06-10-1973 waziri mkuu Golda Meir na waziri wa Ulinzi Moshe Dayan na Mkuu wa utawala jeshini Gen.David Elazar kwa pamoja waliamua kuwaita wanajeshi wa anga wale wa akiba na wale wa vifaru wale wa akiba maana walijua hapo sasa vita haiepukiki.

Kabla ya vita siku hiyo majeshi ya pande zote mbili yalikuwa na zana zilizokuwa zinakisiwa kuwa hivi:

ISRAEL MAADUI ZAKE
Ndege za kivita 358 Ndege za kivita 998
Vifaru 2100 Vifaru 4350
Meli za kivita 37 Meli za kivita 137

Ilipofika saa nane kamili mchana majeshi ya Msri na yale ya Syria yalianza kumimina makombora kuelekea katika sehemu zilizokuwa zinakaliwa na Israel,Misri na Syria zilichagua siku ya jumanosi maana ilikuwa ni sikukuu ya kiyahudi ya YOM KIPPUR waliona siku hiyo wayahudi wote huwa wanasherehekea hivyo ilikuwa upenyo mzuri sana kwao.

Kwa upande wa Sinai majeshi ya Msri yaliweza kuvuka mfereji wa Suez kupitia sehem tano tofauti na kwa upande wa mizinga Misri iliweza kukipiga kituo cha wanaanga wa Israel waliokuwa Refidim katika jangwa la sinai na vikosi vingine vya mizinga vya Israel vilishasmbuliwa na mizinga ya Misri,na kufikia saa 11 jioni maelfu ya Wanajeshi wa misri walikuwa wamefika upande na kulikamata eneo lote la mashariki mwa mfereji wa Suez na wakati wa usiku vikosi vya vifaru vilivuka mfereji wa Suez hapo ndipo hali ya uwanja wa vita ilibadirika kabisa kwa Israel uwepo wa askari wa miguu wa Israel na mizinga yao hakukuweza kuyasimamisha majeshi ya Misri. Division ya 252 na Brigedi ya 14 ya kikosi cha vifaru viliadhirika vibaya sana asilimia kubwa ya vifaru vyao vilikuwa vimeangamizwa na silaha aina ya SAGGER ANT-TANK GUIDED MISSILES toka Misri.

Jeshi la anga la Israel lilipoitwa ili kudhibiti majeshi ya Misri,Ndege hizo zilijikuta zinaangushwa na mizinga ya kuangushia ndege, Misri iliweza kuzitungua ndege za Israel kiasi cha kuzimalizia uwezo wa kushambulia na baada ya kujipanga vizuri na kujua namna ya kukwepa makombora ya kuangushia ndege aina ya SA-7 ndege za Israel ziliweza kuziangamiza helcopter zilizokuwa zimebeba Makamandoo wa misri na kuweza kuzitungua ndege 7 aina ya MIG kwenye uwanja wa mapambano. mapambano hayo yalifanyika kusini mwa mfereji wa Suez ndege hizo ziliangushwa na ndege za Israel aina ya PHANTOM.

Kwa upande wa milima ya Golani majeshi ya Syria yaliweza kusonga mbele huku mizinga na vifaru pamoja na askari wa miguu waliweza kumiminia mizinga,risasi majeshi ya Israel kwa saa nzima mfululizo wakati huo Israel ilikuwa na Brigedi mbili za vifaru Division ya 36th ndiyo ilikuwa mstari wa mbele na Brigedi 188th nayo ilikuwa na jukumu la kulinda sehemu ya kusini ya mlima wa Golani na Brigedi ya 7th ilikuwa na jukumu la kulinda sehemu ya kaskazin mwa mlima Golan hivyo vifaru vya Israel havikuweza kuvishambulia vikosi vya Syria sababu havikuwa kwenye RANGE ya kuweza kushambuliwa.

Mapigano ya vifaru yalianza tu siku hiyo baada ya jua kuzama majeshi ya Syria yaliweza kupenya ngome za Majeshi ya Israel kwa kuwa walikuwa wanatumia NIGHT-VISION viona usiku hivyo vilisaidia sana majeshi ya vifaru vya Syria vifaru vya Israel vilivyokuwa upande wa kaskazini havikuweza kufua dafu mbele ya vikosi vya Syria,vifaru vya Syria viliweza kushika sehemu ya kusini mwa mlima Golan na ilipofika asubuhi ya tarehe 07-10-1973 vifaru zaidi ya 600 vilikuwa vimeingia ndani ya ardhi ya Israel na vilikimbilia kwenda kulishika Daraja mhimu la nto Jordan na kambi ya kijeshi ya Nafar,Israel pia ilipoteza mlima wa HELMON ambao ulikuwa wa kimbinu strategic nao uliangukia mikononi mwa majeshi ya Syria hili lilikuwa pigo kubwa kwa majeshi ya Israel.

Kwa upande wa majini majeshi ya Israel yaliweza kuziangamiza boat zilizokuwa zinabeba makombora za Syria na miji yote iliyokuwa inazunguka milima ya Golan wakazi wake waliondolewa na majeshi ya Israel.na baada ya siku 18 Majeshi ya Israel yaliweza kujijenga upya na kuchukua tena eneo lote la milima ya Golan na mlima Hermon

INAENDELEA…………
 
its important to remember, aliyekua mkuu wa military intelligence kipindi hicho alipuuzia taarifa za majasusi wa front line waliokua Syria, Lebanon, Jordan na Egypt ambao waliripoti kwamba kulikua na alerting evacuation ya diplomats wa Russia na china kutoka kwenye balozi zao kwenye nchi hizo kurudi makwao..., hii pia kwenye intelligence ilikua ni indicator something massive was about to happen, lakini alipuuzia
 
Ukweli hata hio vita Israel hakupigana peke yake Saddat alisema kila walipokuwa wakipigana na Israel, walikutana na majeshi ya Italy, Uingereza, USA na mataifa mengi tu wako upande kuwasaidia Israel

Infamous Assassinations: Anwar Sadat (Documentary)by .... We did not fight Israel alone, there are nine ...

 
Last edited by a moderator:
Kwa upande wa milima ya Golan peke yake vifaru vya Israel vilipambana na vifaru 1400 vya Syria na kwa upande wa Misri eneo la mfereji wa Suez Wanajeshi wa Israel 500 waliweza kupambana na wanajeshi 80,000 wa Misri.

Israel wakati huo ilipata msaada wa kijeshi toka Marekani pia ilipewa nyaraka mhimu zenye upelezi na nyaraka zilizokuwa zinaonyesha kuhusu ndege ya kipelelezi ya Marekani SR-71 Blackbird ndege ambayo iliweza kuwaonyesha ni wapi walipo askari wengi wa Misri maana ndege hiyo ilikuwa inaruka kipindi chote cha vita hiyo kwa msaada wa ndege hiyo Wanajeshi wa Israel waliweza kuvishinda vikosi vya Misri waliona sehemu inayoelekea Ismailia haikuwa na askari wa kutosha hivyo walipeleka huko vikosi vya vifaru na kuweza kuvishinda vikosi hivyo na kuanza safari ya kuelekea Cairo kirahisi sana.

Kwa Upande wa Misaada ya kijeshi Misri na Syria zilipata misaada kutoka katika nchi za kiarabu kama Ifuatavyo;
- Iraq yenyewe ilituma kikosi cha ndege za kivita aina ya Hunter jet fighter kwa majeshi ya Misri miezi michache kabla ya vita kuanza vilevile Iraq ilitoa ndege za kirusi aina ya Mig na askari wa miguu 18,000
- Saudi Arabia pamoja na Kuwait wao walifadhiri vita hivi pamoja na saudi Arabia kutoa askari wa miguu 3,000 ambao walipigana vita. Libya nayo ilitoa ndege za kivita aina ya Mirage zilizotengenezwa Ufaransa vilevile Libya ilitoa Dola za kimarekani Bilion moja ili kuliunda upya jeshi la Misri na kununuli zana za kivita za kisasa toka Urusi.
- Nchi nyingine zilizosaidia Misri na Syria katika vita hivi ni pamoja na Tunisia,Sudan, Morocco na Jordan pia ilituma Brigedi mbili za vifaru na vikosi viwili vya Mizinga kusaidia Syria.

Majeshi ya Israel katika mapambano hayo mwanzoni ilionekana kuzidiwa sana katika viwanja vyote vya mapigano na ilipofika 08-10-1973 Israel iliwaita askari wote wa akiba na kuwapeleka kushambulia katika jangwa la Sinai siku hiyo walifanikiwa kuyarudisha nyuma Majeshi ya Misri na kuvuka mfereji wa Suez kusini mwa mji wa Ismailia hapo Majeshi ya Israel yaliweza kusonga Mbele kupitia Barabara ya Suez kwenda Cairo Majeshi hayo ya Israel yaliweza kusonga mbele kuelekea Cairo mpaka walibakiza maili 65 kufika Cairo.

Kwa upande wa Syria Majeshi ya Israel yalipata mafanikio katika milima ya Golan ambapo Majeshi ya Syria yaliweza kurudishwa nyuma na Israel iliweza kuzikamata tena sehemu zilizokuwa zimetekwa na Syria wakitumia Barabara inayotoka Tiberia kwenda Damascus Majeshi ya Israel yalibakiza maili 35 kufika mji mkuu wa Syria.

Tarehe 24-10-1973 juhudi za kusimamisha mapigano zilianzishwa na Umoja wa mataifa na Umoja wa mataifa ulituma walinda Amani katika sehemu kulikokuwa kuna mapigano na kufikia kati ya mwezi January na March 1974 Israel na Misri zilikuwa zimeweka mkataba wa kusimamisha mapigano kwenye eneo la Mfereji wa Suez hapa Israel iliweza kubaki na kulidhibiti eneo la Kimbinu (strategic) katika Jangwa la Sinai ambalo majeshi yake yanaweza kuona kwa mbali nakuweza kuzuia kama mapigano yatazuka tena katika eneo hilo.

Katika milima ya Golan askari wa kulinda Amani 1200 waliwekwa huko mwezi May 1974 na kuweka eneo lisilo la kijeshi kati ya Israel na Syria.Henry kissenger ndiye aliyekuwa anayaongoza mazungumzo hayo ya Amani,kufikia September 1975 Misri na Israel waliwekeana mkataba wa Amani na kuahidi kumaliza tofauti zao Kisiasa na si Kijeshi na hii ilipelekea kuanzishwa Mazungumzo yaliyokuja kujulikana kama Mazungumzo ya Camp David.

Rais wa Misri Anwar Sadat alipoona Majeshi ya Israel yanaelekea Cairo hakika aliona mambo yanaenda kuwa Magumu hasa akiangalia nguvu waliyotumia na misaada waliyopewa na nchi za kiarabu aliamua kwa Moyo mmoja kuachana na nchi zingine ili tu iwepo Amani maana wametumia nguvu lakini hata chembe ya kurudia ardhi yao haionekani basi kaamua tu kuunga mkono juhudi za kusimamisha mapigano maana hata kama angekataa huku Majeshi ya Israel yalikuwa yanasonga mbele kuelekea mji mkuu Cairo Anwar Sadat aliamuakuachana na vita na kuanza kutafuta suluhu ya kusimamisha mapigano baadaye waliweka mkataba wa Amani na Israel
Rais Anwar Sadat alionekana kama Msaliti na aliweza kuuliwa na waislamu wenye siasa kali mwaka 1981Lakini atakumbukwa sana hasa kwa juhudi zake za kutafuta Amani hasa alipoona Juhudi za Vita hazileta matunda kaamua kufanya njia Mmbadala ya Amani

What did Israel get out of the Yom Kippur War?
Pamoja na kupata mafanikio kwa kuyarudisha nyuma majeshi ya Misri na Syria yaliyokuwa yameingia katika eneo lao la ulinzi, Israel haikufanya vizuri katika vita hivi kwa kuwa ilikuwa vigumu kukabili viwanja viwili vya mapigano vyenye askari wengi kuliko vyao
Askari wapelelezi hawakufanya kaziyao vizuri ilionekana kama walikua wame-yadharau majeshi ya Misri kulikuwa na ishara za wazi kuonyesha kuwa Misri itawashambulia lakini hawakutilia maanani.

Askari wa Israel wale wa akiba hawakuitwa kwa wakati maana walianza kukusanywa tarehe 8-10-1973 hivyo wangeitwa mapema huenda Historia ingesoma vingine.

The war also served as a salutary lesson to the Arab nations that surrounded Israel in that initial victories had to be built on. The failure of the Egyptian and Syrian forces to defeat Israel pushed Sadat towards adopting a diplomatic approach. It also encouraged some Palestinians to more extreme actions. On the diplomatic front, the Camp David talks took place while the actions of the PLO became more violent.

Why didn't the Arab nations build on their initial successes?
Clearly, the use of intelligence massively benefited the Israelis. However, as in 1948, the Arab nations did not fight as one unit. Their command structure was not unified and each fighting unit (in the Sinai and the Golan Heights) acted as individual units. With up to nine different nationalities involved on the Arab side, mere co-ordination would have been extremely difficult.

Secondly, the Israelis had to work to one simple equation: if they lost, the state of Israel would cease to exist. Therefore, for Israel it was a fight to the finish – literally "death or glory". If the various Arab nations lost, they could survive for another day.
 
Kwa upande wa milima ya Golan peke yake vifaru vya Israel vilipambana na vifaru 1400 vya Syria na kwa upande wa Misri eneo la mfereji wa Suez Wanajeshi wa Israel 500 waliweza kupambana na wanajeshi 80,000 wa Misri...

Mbona hutaki kutaja kuwa Jeshi la Israel lilisaidiwa na US,UK, France na Italy...kama wakuu walivyoeleza...?Au habari hii umekopy na kupest kutoka vyanzo vya Israel..ambavyo haviwezi kukiri kusaidiwa?
 
Mbona hutaki kutaja kuwa Jeshi la Israel lilisaidiwa na US,UK, France na Italy...kama wakuu walivyoeleza...?Au habari hii umekopy na kupest kutoka vyanzo vya Israel..ambavyo haviwezi kukiri kusaidiwa?
Dunia nzima wanafahamu wazi Israel hawezi kuwapiga warabu bila msada wa USA na Europe.

Kuna watu bado wana akili zile zilizo pitwa na wakati, eti Israel alipiga warabu katika mda wa siku sita, wakati USA ndo aliomba warabu wasimamishe vita.

Kuna watu wanafikiria warabu wa 1967 ndo wa 2013, hawafahamu bado kuna nchi za kiarabu sasa hivi wanatengenza part za ndege za kivita, na wengine wana tengeneza drone.

Mrusi atanunua drone karibu kutoka UAE.

http://www.thenational.ae/news/uae-...rtshttp://www.youtube.com/watch?v=C8pxz-W6m1k

Russia to buy Drones from the UAE - Defense Update - Military Technology & Defense News


Katika dunia ya sasa mwenye nguvu ni yule mwenye pesa, Israel anaweza kupigwa kwa pesa tu za warabu yeye na USA.
 
Dunia nzima wanafahamu wazi Israel hawezi kuwapiga warabu bila msada wa USA na Europe.

Kuna watu bado wana akili zile zilizo pitwa na wakati, eti Israel alipiga warabu katika mda wa siku sita, wakati USA ndo aliomba warabu wasimamishe vita.

Kuna watu wanafikiria warabu wa 1967 ndo wa 2013, hawafahamu bado kuna nchi za kiarabu sasa hivi wanatengenza part za ndege za kivita, na wengine wana tengeneza drone.

Mrusi atanunua drone karibu kutoka UAE.

http://www.thenational.ae/news/uae-...rtshttp://www.youtube.com/watch?v=C8pxz-W6m1k

Russia to buy Drones from the UAE - Defense Update - Military Technology & Defense News


Katika dunia ya sasa mwenye nguvu ni yule mwenye pesa, Israel anaweza kupigwa kwa pesa tu za warabu yeye na USA.

Hapo kwenye blue,
Angalia vizuri historia inasemaje. Waarabu walipigwa mpaka maeneo yao makubwa yakatekwa.

Within six days, Israel had won a decisive land war. Israeli forces had taken control of the Gaza Strip and the Sinai Peninsula from Egypt, the West Bank and East Jerusalem from Jordan, and the Golan Heights from Syria.

Source: Six-Day War - Wikipedia, the free encyclopedia

400px-Six_Day_War_Territories.svg.png
 
Hii ndiyo hasara ya kushinda kwenye vijiwe vya ghahawa.

Dunia nzima wanafahamu wazi Israel hawezi kuwapiga warabu bila msada wa USA na Europe.

Kuna watu bado wana akili zile zilizo pitwa na wakati, eti Israel alipiga warabu katika mda wa siku sita, wakati USA ndo aliomba warabu wasimamishe vita.

Kuna watu wanafikiria warabu wa 1967 ndo wa 2013, hawafahamu bado kuna nchi za kiarabu sasa hivi wanatengenza part za ndege za kivita, na wengine wana tengeneza drone.

Mrusi atanunua drone karibu kutoka UAE.

http://www.thenational.ae/news/uae-...rtshttp://www.youtube.com/watch?v=C8pxz-W6m1k

Russia to buy Drones from the UAE - Defense Update - Military Technology & Defense News


Katika dunia ya sasa mwenye nguvu ni yule mwenye pesa, Israel anaweza kupigwa kwa pesa tu za warabu yeye na USA.
 
Hii ndiyo hasara ya kushinda kwenye vijiwe vya ghahawa.

Mkuu Ngongo
Mimi huwa natembelea sana hivyo vijiwe. Huwa nasikitika kuona kuwa kuna watu wanajizushia stories za kujipa MATUMAINI halafu wanazikomalia mpaka watu wengine wanaziamini kuwa ndio ukweli. It is so sad.
 
Last edited by a moderator:
bila kusahau enzi hizo kiteknolojia RUSSIA/USSR walikua na vifaru bora kuliko USA. Sasa hapo aidha ni miujiza au waarab hawajui kupigana vita maana wao ndo walikua na vifaa vya kirusi
 
bila kusahau enzi hizo kiteknolojia RUSSIA/USSR walikua na vifaru bora kuliko USA. Sasa hapo aidha ni miujiza au waarab hawajui kupigana vita maana wao ndo walikua na vifaa vya kirusi
Mimi bado sijafahamu kwani Israel walisema wanadanganya wale walio sema USA alitusaidia kwenye vita.

Hapo wenye akili mbona wameisha jua wazi, siku zote mwizi anawahi kujitetea hajaiba.

Na kama ulisaidiwa lazima useme hujasaidiwa, na kusema wengine wanazua uwongo.
 
Soma vizuri nimeelezea Israel ilisaidiwa Marekani Iliweza kupata msaada wa hali na mali na Misri na Syria nao walipata msaada wa Hali na Mali toka nchi za kiaraabu na nimeeleza kwa kirefu,Kwa Dunia hii hakuna nchi inayoweza kuingia vitani na nchi nyingine bila Msaada toka nchi nyingine lakini pamoja na yote hayo Mjanja anaonekana kwenye MEDANI au kwenye uwanja wa VITA kupewa msaada si sababu maana hata nchi ya Misri na Syria nazo zilipata msaada kama kawaida.
Mbona hutaki kutaja kuwa Jeshi la Israel lilisaidiwa na US,UK, France na Italy...kama wakuu walivyoeleza...?Au habari hii umekopy na kupest kutoka vyanzo vya Israel..ambavyo haviwezi kukiri kusaidiwa?
 
Kama una uwezo Badilisha HISTORIA isomeke jinsi wewe unavyotaka ama kweli wahenga walisema Kuku mgeni hakosi kamba mguuni.
Dunia nzima wanafahamu wazi Israel hawezi kuwapiga warabu bila msada wa USA na Europe.

Kuna watu bado wana akili zile zilizo pitwa na wakati, eti Israel alipiga warabu katika mda wa siku sita, wakati USA ndo aliomba warabu wasimamishe vita.

Kuna watu wanafikiria warabu wa 1967 ndo wa 2013, hawafahamu bado kuna nchi za kiarabu sasa hivi wanatengenza part za ndege za kivita, na wengine wana tengeneza drone.

Mrusi atanunua drone karibu kutoka UAE.

http://www.thenational.ae/news/uae-...rtshttp://www.youtube.com/watch?v=C8pxz-W6m1k

Russia to buy Drones from the UAE - Defense Update - Military Technology & Defense News


Katika dunia ya sasa mwenye nguvu ni yule mwenye pesa, Israel anaweza kupigwa kwa pesa tu za warabu yeye na USA.
 
Invisible tunaomba msaada wa kuiwekea hii thread mtiririko na kuedit kidogo ili isomeke vizuri.Jamaa kajitahidi kutiririka vizuri ila mpangilio wa uandishi ndio taabu kidogo.
 
Last edited by a moderator:
Kwa maneno yako hayo unataka ubadiri HISTORIA isomeke kuwa Waarabu walishinda vita vya 1967?????
Warabu wao watashinda vita vyote vinavyo kuja ndo sababu ukaona Israel anaomba nchi za kiarbu zipigwe na USA, anajua yeye haziwezi.
 
Soma vizuri nimeelezea Israel ilisaidiwa Marekani Iliweza kupata msaada wa hali na mali na Misri na Syria nao walipata msaada wa Hali na Mali toka nchi za kiaraabu na nimeeleza kwa kirefu,Kwa Dunia hii hakuna nchi inayoweza kuingia vitani na nchi nyingine bila Msaada toka nchi nyingine lakini pamoja na yote hayo Mjanja anaonekana kwenye MEDANI au kwenye uwanja wa VITA kupewa msaada si sababu maana hata nchi ya Misri na Syria nazo zilipata msaada kama kawaida.
Nchi za kiarabu hazisaidiwi na taifa lingine, wanajisaidia wao kwa wao tu.


Israel ndo anaye saidiwa na taifa lingine sio la ki Israel.

Kilio cha wenzako wanavyo ogopa kikosi tu cha kiarabu, magazeti yao yanajaribu kujidai wao wamba lakini wanaogopa, ukweli ndio huo.

Erdan: Hezbollah Has 200,000 New Rockets, and the Same Goal

Israel's enemies now aim to instill fear and chaos rather than to conquer land. Israel's job is to stop them, minister says.
AAFont Size

By Maayana Miskin First Publish: 10/9/2013, 10:37 AM



381671.jpg
Hamas terrorists train for rocket attacks
Israel news photo: Flash 90

Israel's enemies are taking a new approach to warfare, and Israel must be ready, Minister of Home Front Defense Gilad Erdan said Tuesday, speaking at a conference at Bar Ilan University.
"Our enemies have abandoned the idea of conquering territory in the land of Israel. What remains is their desire to defeat Israel by threatening the homefront," he explained.
The preparations Israel's enemies have made clearly show that their aim in a future battle would be to attack civilians and civilian infrastructure, he said.
Hezbollah in particular has focused on stockpiling missiles and increasing their accuracy, Erdan said. The group now has over 200,000 rockets, he warned, "Every tenth house in Lebanon has either a rocket launcher, or ammunition in storage."
A future battle would likely be similar to the Second Lebanon War, but on a larger scale, he said, "Three weeks in which thousands of rockets are fired at the Israeli homefront, at the entire country."
Hezbollah would use its most accurate rockets carefully, he said. "They'll try to aim those where it would do the most harm to daily life," he said.
This new style of battle – a war of terror targeting the civilian population – has radically changed the importance of the Home Front, Erdan said. The homefront was once important in times of war due to its ability to produce goods that were needed on the battlefront, he said.
"Today, the importance of the homefront has increased dramatically, and is almost equal to that of the IDF on the battlefront," he declared. "It's a completely different way of thinking."
Israel's enemies plan to defeat Israel by breaking its citizens' spirit, he said. Israel's job is not to let them do that.
"My job, and that of my ministry, is to bring the Home Front to a level of preparedness… to create an apparatus that ensures that whatever happens, we will continue to function," he said. Daily life must continue, and will continue, even if Israel comes under attack, he stated.
Erdan noted that while he sees Hezbollah's massive rocket arsenal as a "realistic scenario," he does not believe that Israel's enemies will use chemical weapons.
 
Back
Top Bottom