Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Baada ya vita vikali vya Israel kwa kutumia jeshi la anga na vifaru,vita halisi walivyokuwa wakivisubiri Hamas vitakavyowatoa jasho na kamasi Israel vimeanza.vita hivyo vinaweza vikavuta zaidi muda wa mapigano kati ya mwamba huyo na wapiganaji ambao muda mwengine wakiwa vitani huamua kuvaa suruali za adidas na malapa
Vita hivyo japo Israel tangu mwanzo waliviogopa lakini kwa vile wameshavivulia nguo ni lazima waviogelee.Vita vyenyewe ni vya kupigana mtaa kwa mtaa ndani ya magofu na majumba yaliyohamwa ya jiji la Gaza.
Kuonesha kwamba bado Hamas wapo Gaza na wana nguvu na nidhamu za hali ya juu chini ya viongozi wao,Wanamgambo hao siku ya tatu ya kubadilishana mateka kwa wafungwa wa kipalestina Hamas waliibuka katikati ya Gaza kwenye uwanja wa mashujaa na kukabidhi mateka wa Israel,
Mbali na tukio hilo Hamas pia ilitaka tukio la mwisho la kukabidhiana mateka iwe ni wafungwa wa kipalestina kwa maiti za askari wa IDF waliokufa vitani.Kitendo hicho kiliikasirisha mno Israel na hivyo kukataa mpango huo.
Matukio ya kuitangaza Hamas huwa yanaikasirisha Israel kiasi kwamba kule ukingo wa mashariki wafungwa wa kipalestina wakishaachiwa basi ni marufuku kwa ndugu zao kusherehekea kwa kukushanyika na kuwapokea kwa sauti au kwa mabango.