Vita ya Aleppo inaanza tena

Vita ya Aleppo inaanza tena

Acha ujinga hivyo ni vita ya kimaslahi kati ya mataifa makubwa kwa sababu Syria ipo kwenye eneo la kimkakati hakuna uhusiano wowote na dini.
Mbona Urusi na Ukraine wanauwana na wote ni waothodox lakini hujawahi kuhusisha mgogoro wao na dini?
Hivi nyinyi waisilam walisha wafanya nini mbona mmejaa vinyongo dhidi yao?
Ukisema ubishane na watu wa hivyo utakaukiwa nishati mwili.
Wewe ukimuona mtu analeta udini mu ignore tu mkuu.
Achana naye.
 
Mkuu Uturuki ndo muhusika mkuu kwa hichi kinacho endelea sasa ,maana waasi anao waunga mkono ndo wahusika wakuu wa mashambulizi yanayo endelea japo kuna makundi mengine madogo.
Turkey, Israel na USA wote lao Moja hapo syria.ila nimefurahi Russia amenimwagia moto wa kutosha usiku wa kuamkia leo hawa waasi hawana maisha marefu wameanza kulia kuwa Russia ana commit war crimes
 
Ntaandika kwa key points

1. Netanyahu alichukizwa na Assad kutorosha silaha za hizbollah kupitia Syria zilikua zikitoka Iran na Urusi. Hili limesemwa kwenye press ya mwisho ya netanyau kabla ya cease fire kama unataka references itafute hio press, ambapo Netanyahu kamtishia maneno mawili Assad mwanzo kanwambia litakukuta la Nasrallah maana umecheza na moto

2. Netanyahu anataka kuhakikisha anafunga njia ya silaha kumfikia hzb kwa kudisturb root yake huko Syria hivyo akafanya cease fire na Hizbollah kwa siku 60 ili azuie kabisa hio root, ndio maana baada ya cease fire Jio yake kaactivate makundi HTS,Isil na mengine kumvuruga Assad.

3. Mrusi ana maslahi yake Syria, Iran ana maslahi yake Syria mojawapo ni kulinda makundi yake wote hao Iran na Russia wana mkataba na Assad wa kuwepo pale.

4. Sasa Mturuki nae kuingiza kundi lake pale anakiwasha ndani ya Syria ambapo Iran kalalamika Mturuki kafata nini na hana makubaliano yoyote na serikali ya Assad, Mturuki pale ana interest zake nadhani ni kulinda biashara zake na Israel

5. Mgogoro huu unakuzwa na Israel na Marekani kwa malengo ya kupata amani yao kwa kuisolate gaza na lebanon ili Israeli aishi kwa amani kama wanavyofikiri wao wakidhani Iran haelewi kinachoendelea, Iran yeye anaendelea kuranda randa na karata yake ya kushambulia Israel kama kulipa kisasi siku akiona mambo yamemuelemea ndio maana katulia kwanza
Israel ujanja mwingi mbele kiza Arab spring waliratibu wao wakidhani wakishawatawanya nchi za kiarabu wataishi kwa amani lakini leo bado wapo matatizoni
 
Vita nchini Lebanon ilipokuwa inaelekea mwisho, mzozo mwingine mkubwa umezuka Mashariki ya Kati - au labda si mpya sana. Waasi wa Syria wanaopinga serikali wameanzisha mashambulizi ya haraka dhidi ya jiji kubwa zaidi nchini, Aleppo. Tayari wanadhibiti vijiji kadhaa na wameendelea hadi barabara kuu ya Damascus-Aleppo.

Kwa mara ya kwanza tangu 2020, mapigano makali yamezuka nchini Syria. Vikosi vya serikali vinatoa upinzani dhaifu. Waasi wanasonga mbele kwa kasi, na vikosi vya Assad vimeshindwa kuwazuia, vikijiondoa vyenyewe maeneo

Wakati wa mapigano karibu na Aleppo, mshauri wa kijeshi wa Iran, Jenerali wa IRGC Kiyumars Pourhashemi, aliuawa. Shughuli mpya za waasi zimechochewa na kushindwa kwa Hezbollah na Israeli na kupelekwa tena kwa vikosi vya Urusi vilivyokuwa syria Ukraine. Dikteta wa Syria Bashar al-Assad amepanda ndege haraka kwenda Urusi kwa mashauriano na Putin.

Kulingana na ripoti ambazo hazijathibitishwa, makumi ya wanajeshi wa Urusi kutoka kwa "PMC ya Wagner" wameuawa wakati wa mashambulizi ya waasi, na baadhi , ya silaha na usafiri wa Urusi zimekamatwa. Waasi wanabomoa picha za Bashar al-Assad na alama zinazohusishwa na Urusi. Wametangaza kuwa maadui wao wakuu ni WaIrani na Warusi, wanaounga mkono utawala wa Assad.

View attachment 3165135
Kobazi huwa wanawaza ugaidi masaa 24
 
lazima tushangae inakuaje waislam kwa waislam wapigane? Hao waothodox wa urusi na ukraine wanabondana kutokana na mmoja kuwa upande wa magharibi akitumiwa kumdhoofisha mwenzake. Urusi hataki ukuda huo anaamua kumuadhibu ndugu yake kwa kukaribisha maadui karibu yake
Kwa nini Ukraine wawe vibaraka wa Marekani na si Urusi ambao ni waothodox wenzao? tunarudi pale pale ni masilahi ndo yamefanya ndugu hawa wagombane.

Mbona hujawahi kujiuliza kuwa ni kwann Venezuela na Cuba ni maadui wakubwa wa Marekani ambao ni wakatoliki wenzao?
Ulisha wahi kujiuliza ni kwanini China na Vietnam ni maadui wakati wote ni mabudha?
Ulisha wahi kujiuliza ni kwanini Bangladesh ilitengana na paksitani hali yakuwa wote ni waisilam?

Linapo kuja suala la masilahi ya wana siasa mambo ya sijui undugu , sijui dini ,sijui kabila huwa ni takataka kwake,mwana siasa kumuua hata baba na mama yake kwa ajili ya madaraka ni kitu cha kawaida.
 
sisi waafrika tusikubali kuchonganishwa na nchi zetu kuwa viwanja vya mapambano ya nchi zenye nguvu kuoneshana ubabe kwa majaribio ya silaha zao mpya za kisasa
Ukipenda sana kula vyao matokeo yake ndo kama hayo
 
Back
Top Bottom