Wadogo zangu kama mnapenda starehe basi jifunzeni kunywa bia, kutizama filamu Kali, kusikiliza mziki mzuri, kwenda club siyo kwenda kwenye huo upuuzi sijui fiesta sijui wasafi nini kwanini nasema hivyo
Tasnia ya burudani ya matamasha Tanzania yangu ianze kukuwa na kupata wadau huu ni mwaka wa ishirini sasa ajabu wadau hao wamatamasha na wasanii hawataki kubadilika yani jambo uliloliona miaka kumi iliyopita kwenye tamasha furani ndio hill hill pamoja na kukuwa kwa sayansi na teknolojia bado wadau hawa wanageuza watanzania wajinga
Wanaandaa matamasha promosheni kibao ukienda kwenye tamasha ujinga ule ule play back nyingi, wasanii hawana ubunifu stejini yani mambo ni Yale Yale
Ndio maana nawashauri mnywe bia, muende club ina maana siku ukimis bata zuri unatafuta kiwanja kizuri kwenye DJ mzuri unaenda kufurahi, siyo kwenda kusimama uwanjani uku unambiwa piga kelele maua sana anapanda unakuwa na hamu kuona itajuwaje akiimba ule wimbo, gafla unaishiwa pozi maana atakachokifanya jukwaani utatamani ashuke usikilize wimbo tu.